Uzuri wa ambavyo hatutovijua
-
0:01 - 0:05Asubuhi moja ya mwezi Oktoba yenye joto,
-
0:05 - 0:07nilishuka kutoka kwenye treni ya usiku
-
0:07 - 0:09Mandalay,
-
0:09 - 0:12mji mkuu wa kifalme wa zamani wa Burma,
-
0:12 - 0:13sasa Myanmar.
-
0:14 - 0:18Kwenye mtaa, nikakutana na kundi la
wanaume ambao ni wakorofi -
0:18 - 0:22wakiwa wamesimama pembeni ya baiskeli zao.
-
0:22 - 0:23Mmoja kati yao akanifuata
-
0:23 - 0:25na kujitolea kunionesha maeneo.
-
0:27 - 0:29Bei aliyoitaja ilikuwa ni ya kushangaza.
-
0:30 - 0:34Ilikuwa ni kidogo kuliko ambayo ningetumia
kununua chokoleti nyumbani. -
0:34 - 0:37Nikapanda kwenye baiskeli yake,
-
0:37 - 0:43na akaanza kutuendesha polepole
kwenye makasri na mahekalu. -
0:44 - 0:49Wakati anaendesha, akaniambia jinsi
alivyokuja mjini kutoka kijijini kwake. -
0:49 - 0:52Alikuwa na digrii ya hisabati.
-
0:52 - 0:54Ndoto yake ilikuwa awe mwalimu.
-
0:54 - 0:59Hakika maisha ni magumu kwenye
udikteta wa kijeshi, -
0:59 - 1:03kwa sasa, hii ilikuwa ni namna
pekee ya kujipatia kipato. -
1:05 - 1:09Mara nyingi usiku, aliniambia,
alilala kwenye guta yake -
1:09 - 1:13ili kusudi apate wateja wa kwanza
wa treni ya usiku. -
1:16 - 1:19Punde si punde, tukagundua kwamba
kwa namna fulani -
1:19 - 1:21tuna mengi ya kufanana --
-
1:21 - 1:23wote tulikuwa kwenye miaka ya 20,
-
1:23 - 1:26sote tulikuwa tunavutiwa na
tamaduni za kigeni -- -
1:27 - 1:29mpaka akanikaribisha nyumbani.
-
1:30 - 1:34Tukatoka kwenye mtaa wenye watu wengi,
-
1:34 - 1:38na tukaanza kupita kwenye njia zenye
mabonde na kona nyingi -
1:38 - 1:40Kulikuwa na nyumba zilizo bomoka
kila sehemu. -
1:40 - 1:43Kwakweli sikujua nilipokuwepo,
-
1:44 - 1:48na nikagundua kua chochote
kinaweza kunitokea sasa. -
1:48 - 1:50Ninaweza ibiwa au leweshwa
-
1:50 - 1:52au kibaya zaidi.
-
1:52 - 1:53Hamna ambaye angejua.
-
1:54 - 1:58Mwishowe, akasimama na akanipeleka
kwenye kibanda, -
1:58 - 2:01ambacho kilikuwa na chumba kimoja
tu kidogo. -
2:02 - 2:04Kisha akainama chini,
-
2:04 - 2:06kwenye kitanda chake.
-
2:08 - 2:10Kitu ndani yangu kikaganda.
-
2:12 - 2:15Nikawa nasubiri nione atavuta nini.
-
2:15 - 2:18Mwishowe akatoa boksi.
-
2:19 - 2:24Ndani yake kulikuwa na barua zote
alizowahi kupokea -
2:24 - 2:26kutoka kwa wageni wa nchi za nje,
-
2:27 - 2:29na baadhi zao alikuwa amebandika
-
2:29 - 2:33picha ndogo zisizo na rangi zilizochoka
-
2:33 - 2:35za marafiki zake wapya wa kigeni.
-
2:36 - 2:40Hivyo tulivyoagana usiku ule,
-
2:40 - 2:43nikagundua kua amenionyesha pia
-
2:43 - 2:45siri ya kwenye kusafiri,
-
2:45 - 2:47ambayo ni kufanya kitu bila uwoga,
-
2:47 - 2:50kusafiri ndani vile vile na nje,
-
2:50 - 2:52kwenda sehemu ambazo usingeenda
vinginevyo, -
2:53 - 2:55kufanya usiyoyafahamu,
-
2:56 - 2:57usichokielewa,
-
2:57 - 2:59hata uwoga.
-
3:00 - 3:03Nyumbani, ni hatari kirahisi
-
3:03 - 3:05kujiona tupo juu ya mambo.
-
3:06 - 3:10Nje kwenye dunia, unakumbushwa
kila saa kwamba haupo -
3:10 - 3:13na hauwezi kufikia kwenye
mwisho wa mambo pia. -
3:14 - 3:17Kila sehemu, "Watu wanatamani kutulia,"
-
3:17 - 3:19Ralph Waldo Emerson alitukumbusha,
-
3:19 - 3:22"lakini mara nyingi tunapokuwa
hatujatulia -
3:22 - 3:24ndipo kuna tumaini kwetu."
-
3:25 - 3:27Kwenye hili kongamano,
tumebahatika sana -
3:27 - 3:31kusikia mawazo mapya ya
kustaajabisha na vumbuzi -
3:31 - 3:33na kweli, kuhusu njia zote
-
3:33 - 3:36ambazo maarife yanasukumwa
mbele sana. -
3:37 - 3:40Lakini kuna hatua, maarifa yanaondoka.
-
3:41 - 3:42Na huo ndio muda
-
3:42 - 3:45ambao maisha yako yanaamua kweli:
-
3:46 - 3:48unapata upendo;
-
3:48 - 3:50unapoteza rafiki;
-
3:51 - 3:52taa zinazimika.
-
3:53 - 3:58Na ni hapo, ambapo ukiwa umepotea,
au huelewi au umepoteza matumaini, -
3:58 - 4:00ndipo unapogundua wewe ni nani.
-
4:02 - 4:06Siamini kama ujinga ni starehe.
-
4:06 - 4:09Sayansi imefanya maisha yetu
-
4:09 - 4:12yang'ae zaidi, marefu zaidi na yenye
afya zaidi. -
4:13 - 4:18Na ninawashukuru sana walimu
walionifundisha kanuni za fizikia, -
4:18 - 4:21na kunielekeza kwamba
tatu mara tatu ni tisa. -
4:22 - 4:25Naweza kuhesabu hiyo kwa vidole vyangu.
-
4:25 - 4:27muda wowote wa usiku au mchana.
-
4:29 - 4:30Lakini mwanahisabati akiniambia
-
4:30 - 4:34hio ukitoa mara tatu
ukitoa tatu ni tisa, -
4:34 - 4:39hiyo ni aina ya mantiki inayoonekana
kama uaminifu. -
4:41 - 4:44Tofauti ya maarifa, kwa maneno mengine,
sio lazima iwe ujinga. -
4:45 - 4:46Inaweza ikawa mshangao.
-
4:46 - 4:48Au maajabu.
-
4:48 - 4:49Uwezekano.
-
4:50 - 4:54Na kwenye maisha yangu, nimegundua
ni vile nisivyovijua -
4:54 - 4:56ndivyo ambavyo vimeninyanyua
na kunisukuma mbele zaidi -
4:56 - 4:59kushinda vile ninavyovijua.
-
5:00 - 5:02Ni pia vile nisivyovijua
-
5:02 - 5:05vilivyonileta karibu na kila mtu
anaenizunguka. -
5:07 - 5:09Kwa Novemba nane mfululizo, hivi karibuni,
-
5:09 - 5:13nimesafiri kila mwaka kupitia
Japan na Dalai Lama. -
5:14 - 5:17Na kitu ambacho alikuwa anasema kila siku
-
5:17 - 5:21ambacho kilionekana kuwapa watu
suluhisho na tumaini -
5:21 - 5:23ilikuwa ni "sijui."
-
5:24 - 5:26"Nini kitatokea Tibet?"
-
5:27 - 5:30"Lini tutapata amani duniani?"
-
5:31 - 5:33"Ipi ni njia sahihi ya kulea watoto?"
-
5:34 - 5:37"Kiukweli," anasema huyu mtu mwenye
busara, -
5:37 - 5:38"Sijui."
-
5:40 - 5:44Mshindi wa tuzo ya Nobeli,
mwanauchumi Daniel Kahneman -
5:44 - 5:48ametumia zaidi ya miaka 60 sasa
akichunguza tabia za binadamu, -
5:48 - 5:50na muafaka wake ni
-
5:50 - 5:55kua huwa tunajiamini sana na kile
tunachodhani tunakijua -
5:55 - 5:57kuliko tunavyotakiwa kuwa.
-
5:57 - 5:59Tunakuwa, kama anavyosema,
-
5:59 - 6:04na "uwezo usio na kikomo wa
kupuuzia ujinga wetu." -
6:05 - 6:10Tunajua -- nanukuu -- timu yetu
itaenda kushinda wikiendi hii, -
6:10 - 6:12na tunakumbuka tu hayo maarifa
-
6:12 - 6:15mara chache tukiwa sahihi.
-
6:16 - 6:18Mara nyingi, tunakuwa gizani.
-
6:19 - 6:23Na hapo ndipo hisia za kweli zipo.
-
6:25 - 6:28Unajua mpenzi wako
atakachokua anafanya kesho? -
6:29 - 6:30Je unataka kujua?
-
6:32 - 6:34Wazazi wetu sote
kama watu wanavyowaita, -
6:34 - 6:36Adam na Hawa,
-
6:36 - 6:40wasigeweza kufa, alimradi waliendelea kula
kutoka kwenye mti wa uzima. -
6:41 - 6:43Ila punde walivyoanza kula
-
6:43 - 6:45kutoka kwenye mti wa maarifa,
ya mema na mabaya, -
6:45 - 6:47wakaanguka kutoka kwenye weupe wao.
-
6:48 - 6:51Wakajawa na aibu na uwoga,
-
6:51 - 6:52wakajitambua.
-
6:53 - 6:55Na wakajifunza,
kwa kuchelewa, pengine, -
6:55 - 6:58kwamba kwa kweli kuna vitu
tunahitaji kuvijua, -
6:58 - 7:02lakini kuna vingi, vingi zaidi
ambavyo ni bora visichunguzwe. -
7:04 - 7:06Sasa, nilivyokuwa mtoto,
-
7:06 - 7:09nilijua vyote, bila shaka.
-
7:09 - 7:14Nilitumia miaka 20 darasani
nikikusanya mawazo, -
7:14 - 7:16na nilikuwa kweli
kwenye biashara ya habari, -
7:16 - 7:18nikiandika makala ya gazeti la Time.
-
7:19 - 7:24Nikasafiri kwenda Japan kwa mara ya kwanza
kwa muda wa wiki mbili na nusu, -
7:24 - 7:28na nikarudi na insha ya karatasi 40
-
7:28 - 7:31ikielezea kila kitu kuhusu
nyumba za ibada za Japan, -
7:31 - 7:34mitindo yake, michezo yake ya besiboli,
-
7:34 - 7:36nafsi yake.
-
7:37 - 7:40Lakini chini ya hayo yote,
-
7:40 - 7:43kitu ambacho sikuweza elewa
-
7:43 - 7:47kiliniongoza kwa sababu
nisizoweza kuwaelezea bado, -
7:48 - 7:51mpaka nikaamua kwenda kuishi Japan.
-
7:52 - 7:55Na sasa ambapo nimekuwa kule kwa miaka 28,
-
7:55 - 7:58siwezi kuwaelezea mengi kabisa
-
7:58 - 7:59kuhusu nyumbani kwangu.
-
8:00 - 8:02Ambayo ni nzuri,
-
8:02 - 8:04sababu inamaanisha kila siku
ninagundua kitu kipya. -
8:04 - 8:06na kwenye hiyo harakati,
-
8:06 - 8:10kuangalia pembeni na kuona
mamia na maelfu ya vitu -
8:10 - 8:11nisingeweza kujua.
-
8:13 - 8:15Maarifa ni zawadi kubwa sana.
-
8:16 - 8:21Lakini maarifa ya uwongo
yanaweza kua hatari kuliko ujinga. -
8:22 - 8:25Kuwaza kwamba unamjua mpenzi wako
-
8:25 - 8:26au adui yako
-
8:27 - 8:28inaweza kua ya hila zaidi
-
8:28 - 8:31kuliko kukubali kwamba hautowajua.
-
8:32 - 8:36Kila asubuhi Japan, ua likiwaka kwenye
nyumba yetu ndogo, -
8:36 - 8:41inanichukua maumivu mengi
kutokuangalia utabiri wa hali ya hewa, -
8:41 - 8:42sababu nikiangalia,
-
8:42 - 8:46akili yangu itajawa na mawazo,
na itasumbuka -
8:46 - 8:48hata kama siku ikiwa angavu.
-
8:50 - 8:54Nimekuwa mwandishi kwa miaka 34 sasa.
-
8:55 - 8:58Na kitu kimoja ambacho nimejifunza
-
8:58 - 9:01ni kua mabadiliko huja pale
nisipoyapangilia, -
9:01 - 9:03pale ambapo sijui nini kinafuata,
-
9:03 - 9:08pale ambapo siwezi kuwaza kua ni mkubwa
kuliko kila kitu kinachonizunguka. -
9:09 - 9:11Na hio ni kweli pia kwenye upendo
-
9:12 - 9:14au kwenye wakati wa majanga.
-
9:15 - 9:18Ghafla, tumerudi kwenye ile guta tena
-
9:18 - 9:22na tunaruka mitaa mikubwa yenye taa;
-
9:22 - 9:26na tunakumbushwa, kweli,
kwenye kanuni ya kwanza ya safari -
9:26 - 9:28na hivyo, ya maisha:
-
9:29 - 9:34una nguvu tu kama uwezo
wako wa kujisalimisha. -
9:36 - 9:38Mwishowe, pengine,
-
9:38 - 9:39kuwa binadamu
-
9:39 - 9:41ni muhimu zaidi
-
9:41 - 9:44kuliko kuwa kwenye kujua kikamilifu.
-
9:45 - 9:46Asanteni.
-
9:46 - 9:53(Makofi)
- Title:
- Uzuri wa ambavyo hatutovijua
- Speaker:
- Pico Iyer
- Description:
-
Takribani miaka 30 iliyopita,Pico Iyer alisafiri kwenda Japan, akaipenda nchi na akahamia huko. Mfwatiliaji wa karibu wa roho ya binadamu, Iyer anasema kwamba sasa anaona anajua machache kuhusiana na Japan -- au, hakika, kuhusu chochote kile -- kama ambavyo alidhani anajua miongo mitatu iliyopita. Kwenye hii tafakari ya kishairi kuhusu hekima, Iyer anaelezea kuhusu uelewa unavyokuja na umri: kadri tunavyodhani tunajua, ndivyo tunagundua tunajua kidogo.
- Video Language:
- English
- Team:
- closed TED
- Project:
- TEDTalks
- Duration:
- 10:05
Nelson Simfukwe approved Swahili subtitles for The beauty of what we'll never know | ||
Doris Mangalu accepted Swahili subtitles for The beauty of what we'll never know | ||
Doris Mangalu edited Swahili subtitles for The beauty of what we'll never know | ||
Doris Mangalu edited Swahili subtitles for The beauty of what we'll never know | ||
Doris Mangalu edited Swahili subtitles for The beauty of what we'll never know | ||
Doris Mangalu edited Swahili subtitles for The beauty of what we'll never know | ||
Doris Mangalu edited Swahili subtitles for The beauty of what we'll never know | ||
Julieth Mbeyella edited Swahili subtitles for The beauty of what we'll never know |