Asubuhi moja ya mwezi Oktoba yenye joto, nilishuka kutoka kwenye treni ya usiku Mandalay, mji mkuu wa kifalme wa zamani wa Burma, sasa Myanmar. Kwenye mtaa, nikakutana na kundi la wanaume ambao ni wakorofi wakiwa wamesimama pembeni ya baiskeli zao. Mmoja kati yao akanifuata na kujitolea kunionesha maeneo. Bei aliyoitaja ilikuwa ni ya kushangaza. Ilikuwa ni kidogo kuliko ambayo ningetumia kununua chokoleti nyumbani. Nikapanda kwenye baiskeli yake, na akaanza kutuendesha polepole kwenye makasri na mahekalu. Wakati anaendesha, akaniambia jinsi alivyokuja mjini kutoka kijijini kwake. Alikuwa na digrii ya hisabati. Ndoto yake ilikuwa awe mwalimu. Hakika maisha ni magumu kwenye udikteta wa kijeshi, kwa sasa, hii ilikuwa ni namna pekee ya kujipatia kipato. Mara nyingi usiku, aliniambia, alilala kwenye guta yake ili kusudi apate wateja wa kwanza wa treni ya usiku. Punde si punde, tukagundua kwamba kwa namna fulani tuna mengi ya kufanana -- wote tulikuwa kwenye miaka ya 20, sote tulikuwa tunavutiwa na tamaduni za kigeni -- mpaka akanikaribisha nyumbani. Tukatoka kwenye mtaa wenye watu wengi, na tukaanza kupita kwenye njia zenye mabonde na kona nyingi Kulikuwa na nyumba zilizo bomoka kila sehemu. Kwakweli sikujua nilipokuwepo, na nikagundua kua chochote kinaweza kunitokea sasa. Ninaweza ibiwa au leweshwa au kibaya zaidi. Hamna ambaye angejua. Mwishowe, akasimama na akanipeleka kwenye kibanda, ambacho kilikuwa na chumba kimoja tu kidogo. Kisha akainama chini, kwenye kitanda chake. Kitu ndani yangu kikaganda. Nikawa nasubiri nione atavuta nini. Mwishowe akatoa boksi. Ndani yake kulikuwa na barua zote alizowahi kupokea kutoka kwa wageni wa nchi za nje, na baadhi zao alikuwa amebandika picha ndogo zisizo na rangi zilizochoka za marafiki zake wapya wa kigeni. Hivyo tulivyoagana usiku ule, nikagundua kua amenionyesha pia siri ya kwenye kusafiri, ambayo ni kufanya kitu bila uwoga, kusafiri ndani vile vile na nje, kwenda sehemu ambazo usingeenda vinginevyo, kufanya usiyoyafahamu, usichokielewa, hata uwoga. Nyumbani, ni hatari kirahisi kujiona tupo juu ya mambo. Nje kwenye dunia, unakumbushwa kila saa kwamba haupo na hauwezi kufikia kwenye mwisho wa mambo pia. Kila sehemu, "Watu wanatamani kutulia," Ralph Waldo Emerson alitukumbusha, "lakini mara nyingi tunapokuwa hatujatulia ndipo kuna tumaini kwetu." Kwenye hili kongamano, tumebahatika sana kusikia mawazo mapya ya kustaajabisha na vumbuzi na kweli, kuhusu njia zote ambazo maarife yanasukumwa mbele sana. Lakini kuna hatua, maarifa yanaondoka. Na huo ndio muda ambao maisha yako yanaamua kweli: unapata upendo; unapoteza rafiki; taa zinazimika. Na ni hapo, ambapo ukiwa umepotea, au huelewi au umepoteza matumaini, ndipo unapogundua wewe ni nani. Siamini kama ujinga ni starehe. Sayansi imefanya maisha yetu yang'ae zaidi, marefu zaidi na yenye afya zaidi. Na ninawashukuru sana walimu walionifundisha kanuni za fizikia, na kunielekeza kwamba tatu mara tatu ni tisa. Naweza kuhesabu hiyo kwa vidole vyangu. muda wowote wa usiku au mchana. Lakini mwanahisabati akiniambia hio ukitoa mara tatu ukitoa tatu ni tisa, hiyo ni aina ya mantiki inayoonekana kama uaminifu. Tofauti ya maarifa, kwa maneno mengine, sio lazima iwe ujinga. Inaweza ikawa mshangao. Au maajabu. Uwezekano. Na kwenye maisha yangu, nimegundua ni vile nisivyovijua ndivyo ambavyo vimeninyanyua na kunisukuma mbele zaidi kushinda vile ninavyovijua. Ni pia vile nisivyovijua vilivyonileta karibu na kila mtu anaenizunguka. Kwa Novemba nane mfululizo, hivi karibuni, nimesafiri kila mwaka kupitia Japan na Dalai Lama. Na kitu ambacho alikuwa anasema kila siku ambacho kilionekana kuwapa watu suluhisho na tumaini ilikuwa ni "sijui." "Nini kitatokea Tibet?" "Lini tutapata amani duniani?" "Ipi ni njia sahihi ya kulea watoto?" "Kiukweli," anasema huyu mtu mwenye busara, "Sijui." Mshindi wa tuzo ya Nobeli, mwanauchumi Daniel Kahneman ametumia zaidi ya miaka 60 sasa akichunguza tabia za binadamu, na muafaka wake ni kua huwa tunajiamini sana na kile tunachodhani tunakijua kuliko tunavyotakiwa kuwa. Tunakuwa, kama anavyosema, na "uwezo usio na kikomo wa kupuuzia ujinga wetu." Tunajua -- nanukuu -- timu yetu itaenda kushinda wikiendi hii, na tunakumbuka tu hayo maarifa mara chache tukiwa sahihi. Mara nyingi, tunakuwa gizani. Na hapo ndipo hisia za kweli zipo. Unajua mpenzi wako atakachokua anafanya kesho? Je unataka kujua? Wazazi wetu sote kama watu wanavyowaita, Adam na Hawa, wasigeweza kufa, alimradi waliendelea kula kutoka kwenye mti wa uzima. Ila punde walivyoanza kula kutoka kwenye mti wa maarifa, ya mema na mabaya, wakaanguka kutoka kwenye weupe wao. Wakajawa na aibu na uwoga, wakajitambua. Na wakajifunza, kwa kuchelewa, pengine, kwamba kwa kweli kuna vitu tunahitaji kuvijua, lakini kuna vingi, vingi zaidi ambavyo ni bora visichunguzwe. Sasa, nilivyokuwa mtoto, nilijua vyote, bila shaka. Nilitumia miaka 20 darasani nikikusanya mawazo, na nilikuwa kweli kwenye biashara ya habari, nikiandika makala ya gazeti la Time. Nikasafiri kwenda Japan kwa mara ya kwanza kwa muda wa wiki mbili na nusu, na nikarudi na insha ya karatasi 40 ikielezea kila kitu kuhusu nyumba za ibada za Japan, mitindo yake, michezo yake ya besiboli, nafsi yake. Lakini chini ya hayo yote, kitu ambacho sikuweza elewa kiliniongoza kwa sababu nisizoweza kuwaelezea bado, mpaka nikaamua kwenda kuishi Japan. Na sasa ambapo nimekuwa kule kwa miaka 28, siwezi kuwaelezea mengi kabisa kuhusu nyumbani kwangu. Ambayo ni nzuri, sababu inamaanisha kila siku ninagundua kitu kipya. na kwenye hiyo harakati, kuangalia pembeni na kuona mamia na maelfu ya vitu nisingeweza kujua. Maarifa ni zawadi kubwa sana. Lakini maarifa ya uwongo yanaweza kua hatari kuliko ujinga. Kuwaza kwamba unamjua mpenzi wako au adui yako inaweza kua ya hila zaidi kuliko kukubali kwamba hautowajua. Kila asubuhi Japan, ua likiwaka kwenye nyumba yetu ndogo, inanichukua maumivu mengi kutokuangalia utabiri wa hali ya hewa, sababu nikiangalia, akili yangu itajawa na mawazo, na itasumbuka hata kama siku ikiwa angavu. Nimekuwa mwandishi kwa miaka 34 sasa. Na kitu kimoja ambacho nimejifunza ni kua mabadiliko huja pale nisipoyapangilia, pale ambapo sijui nini kinafuata, pale ambapo siwezi kuwaza kua ni mkubwa kuliko kila kitu kinachonizunguka. Na hio ni kweli pia kwenye upendo au kwenye wakati wa majanga. Ghafla, tumerudi kwenye ile guta tena na tunaruka mitaa mikubwa yenye taa; na tunakumbushwa, kweli, kwenye kanuni ya kwanza ya safari na hivyo, ya maisha: una nguvu tu kama uwezo wako wa kujisalimisha. Mwishowe, pengine, kuwa binadamu ni muhimu zaidi kuliko kuwa kwenye kujua kikamilifu. Asanteni. (Makofi)