Asubuhi moja ya mwezi Oktoba yenye joto,
nilishuka kutoka kwenye treni ya usiku
Mandalay,
mji mkuu wa kifalme wa zamani wa Burma,
sasa Myanmar.
Kwenye mtaa, nikakutana na kundi la
wanaume ambao ni wakorofi
wakiwa wamesimama pembeni ya baiskeli zao.
Mmoja kati yao akanifuata
na kujitolea kunionesha maeneo.
Bei aliyoitaja ilikuwa ni ya kushangaza.
Ilikuwa ni kidogo kuliko ambayo ningetumia
kununua chokoleti nyumbani.
Nikapanda kwenye baiskeli yake,
na akaanza kutuendesha polepole
kwenye makasri na mahekalu.
Wakati anaendesha, akaniambia jinsi
alivyokuja mjini kutoka kijijini kwake.
Alikuwa na digrii ya hisabati.
Ndoto yake ilikuwa awe mwalimu.
Hakika maisha ni magumu kwenye
udikteta wa kijeshi,
kwa sasa, hii ilikuwa ni namna
pekee ya kujipatia kipato.
Mara nyingi usiku, aliniambia,
alilala kwenye guta yake
ili kusudi apate wateja wa kwanza
wa treni ya usiku.
Punde si punde, tukagundua kwamba
kwa namna fulani
tuna mengi ya kufanana --
wote tulikuwa kwenye miaka ya 20,
sote tulikuwa tunavutiwa na
tamaduni za kigeni --
mpaka akanikaribisha nyumbani.
Tukatoka kwenye mtaa wenye watu wengi,
na tukaanza kupita kwenye njia zenye
mabonde na kona nyingi
Kulikuwa na nyumba zilizo bomoka
kila sehemu.
Kwakweli sikujua nilipokuwepo,
na nikagundua kua chochote
kinaweza kunitokea sasa.
Ninaweza ibiwa au leweshwa
au kibaya zaidi.
Hamna ambaye angejua.
Mwishowe, akasimama na akanipeleka
kwenye kibanda,
ambacho kilikuwa na chumba kimoja
tu kidogo.
Kisha akainama chini,
kwenye kitanda chake.
Kitu ndani yangu kikaganda.
Nikawa nasubiri nione atavuta nini.
Mwishowe akatoa boksi.
Ndani yake kulikuwa na barua zote
alizowahi kupokea
kutoka kwa wageni wa nchi za nje,
na baadhi zao alikuwa amebandika
picha ndogo zisizo na rangi zilizochoka
za marafiki zake wapya wa kigeni.
Hivyo tulivyoagana usiku ule,
nikagundua kua amenionyesha pia
siri ya kwenye kusafiri,
ambayo ni kufanya kitu bila uwoga,
kusafiri ndani vile vile na nje,
kwenda sehemu ambazo usingeenda
vinginevyo,
kufanya usiyoyafahamu,
usichokielewa,
hata uwoga.
Nyumbani, ni hatari kirahisi
kujiona tupo juu ya mambo.
Nje kwenye dunia, unakumbushwa
kila saa kwamba haupo
na hauwezi kufikia kwenye
mwisho wa mambo pia.
Kila sehemu, "Watu wanatamani kutulia,"
Ralph Waldo Emerson alitukumbusha,
"lakini mara nyingi tunapokuwa
hatujatulia
ndipo kuna tumaini kwetu."
Kwenye hili kongamano,
tumebahatika sana
kusikia mawazo mapya ya
kustaajabisha na vumbuzi
na kweli, kuhusu njia zote
ambazo maarife yanasukumwa
mbele sana.
Lakini kuna hatua, maarifa yanaondoka.
Na huo ndio muda
ambao maisha yako yanaamua kweli:
unapata upendo;
unapoteza rafiki;
taa zinazimika.
Na ni hapo, ambapo ukiwa umepotea,
au huelewi au umepoteza matumaini,
ndipo unapogundua wewe ni nani.
Siamini kama ujinga ni starehe.
Sayansi imefanya maisha yetu
yang'ae zaidi, marefu zaidi na yenye
afya zaidi.
Na ninawashukuru sana walimu
walionifundisha kanuni za fizikia,
na kunielekeza kwamba
tatu mara tatu ni tisa.
Naweza kuhesabu hiyo kwa vidole vyangu.
muda wowote wa usiku au mchana.
Lakini mwanahisabati akiniambia
hio ukitoa mara tatu
ukitoa tatu ni tisa,
hiyo ni aina ya mantiki inayoonekana
kama uaminifu.
Tofauti ya maarifa, kwa maneno mengine,
sio lazima iwe ujinga.
Inaweza ikawa mshangao.
Au maajabu.
Uwezekano.
Na kwenye maisha yangu, nimegundua
ni vile nisivyovijua
ndivyo ambavyo vimeninyanyua
na kunisukuma mbele zaidi
kushinda vile ninavyovijua.
Ni pia vile nisivyovijua
vilivyonileta karibu na kila mtu
anaenizunguka.
Kwa Novemba nane mfululizo, hivi karibuni,
nimesafiri kila mwaka kupitia
Japan na Dalai Lama.
Na kitu ambacho alikuwa anasema kila siku
ambacho kilionekana kuwapa watu
suluhisho na tumaini
ilikuwa ni "sijui."
"Nini kitatokea Tibet?"
"Lini tutapata amani duniani?"
"Ipi ni njia sahihi ya kulea watoto?"
"Kiukweli," anasema huyu mtu mwenye
busara,
"Sijui."
Mshindi wa tuzo ya Nobeli,
mwanauchumi Daniel Kahneman
ametumia zaidi ya miaka 60 sasa
akichunguza tabia za binadamu,
na muafaka wake ni
kua huwa tunajiamini sana na kile
tunachodhani tunakijua
kuliko tunavyotakiwa kuwa.
Tunakuwa, kama anavyosema,
na "uwezo usio na kikomo wa
kupuuzia ujinga wetu."
Tunajua -- nanukuu -- timu yetu
itaenda kushinda wikiendi hii,
na tunakumbuka tu hayo maarifa
mara chache tukiwa sahihi.
Mara nyingi, tunakuwa gizani.
Na hapo ndipo hisia za kweli zipo.
Unajua mpenzi wako
atakachokua anafanya kesho?
Je unataka kujua?
Wazazi wetu sote
kama watu wanavyowaita,
Adam na Hawa,
wasigeweza kufa, alimradi waliendelea kula
kutoka kwenye mti wa uzima.
Ila punde walivyoanza kula
kutoka kwenye mti wa maarifa,
ya mema na mabaya,
wakaanguka kutoka kwenye weupe wao.
Wakajawa na aibu na uwoga,
wakajitambua.
Na wakajifunza,
kwa kuchelewa, pengine,
kwamba kwa kweli kuna vitu
tunahitaji kuvijua,
lakini kuna vingi, vingi zaidi
ambavyo ni bora visichunguzwe.
Sasa, nilivyokuwa mtoto,
nilijua vyote, bila shaka.
Nilitumia miaka 20 darasani
nikikusanya mawazo,
na nilikuwa kweli
kwenye biashara ya habari,
nikiandika makala ya gazeti la Time.
Nikasafiri kwenda Japan kwa mara ya kwanza
kwa muda wa wiki mbili na nusu,
na nikarudi na insha ya karatasi 40
ikielezea kila kitu kuhusu
nyumba za ibada za Japan,
mitindo yake, michezo yake ya besiboli,
nafsi yake.
Lakini chini ya hayo yote,
kitu ambacho sikuweza elewa
kiliniongoza kwa sababu
nisizoweza kuwaelezea bado,
mpaka nikaamua kwenda kuishi Japan.
Na sasa ambapo nimekuwa kule kwa miaka 28,
siwezi kuwaelezea mengi kabisa
kuhusu nyumbani kwangu.
Ambayo ni nzuri,
sababu inamaanisha kila siku
ninagundua kitu kipya.
na kwenye hiyo harakati,
kuangalia pembeni na kuona
mamia na maelfu ya vitu
nisingeweza kujua.
Maarifa ni zawadi kubwa sana.
Lakini maarifa ya uwongo
yanaweza kua hatari kuliko ujinga.
Kuwaza kwamba unamjua mpenzi wako
au adui yako
inaweza kua ya hila zaidi
kuliko kukubali kwamba hautowajua.
Kila asubuhi Japan, ua likiwaka kwenye
nyumba yetu ndogo,
inanichukua maumivu mengi
kutokuangalia utabiri wa hali ya hewa,
sababu nikiangalia,
akili yangu itajawa na mawazo,
na itasumbuka
hata kama siku ikiwa angavu.
Nimekuwa mwandishi kwa miaka 34 sasa.
Na kitu kimoja ambacho nimejifunza
ni kua mabadiliko huja pale
nisipoyapangilia,
pale ambapo sijui nini kinafuata,
pale ambapo siwezi kuwaza kua ni mkubwa
kuliko kila kitu kinachonizunguka.
Na hio ni kweli pia kwenye upendo
au kwenye wakati wa majanga.
Ghafla, tumerudi kwenye ile guta tena
na tunaruka mitaa mikubwa yenye taa;
na tunakumbushwa, kweli,
kwenye kanuni ya kwanza ya safari
na hivyo, ya maisha:
una nguvu tu kama uwezo
wako wa kujisalimisha.
Mwishowe, pengine,
kuwa binadamu
ni muhimu zaidi
kuliko kuwa kwenye kujua kikamilifu.
Asanteni.
(Makofi)