Je tunaweza kuzuia mwisho wa Dunia?
-
0:00 - 0:03Miaka kumi iliyopita, niliandika kitabu
nilichokipa jina -
0:03 - 0:06"Karne yetu ya mwisho?" Alama ya kuuliza.
-
0:06 - 0:09Wachapishaji wa kitabu hiki waliondoa
alama ya kuuliza. (Vicheko) -
0:09 - 0:11Wachapishaji wa Marekani
walibadili jina -
0:11 - 0:15na kuwa "Lisaa Letu la Mwisho".
-
0:15 - 0:19Wamarekani hupenda kuridhishwa haraka na
kinyume. -
0:19 - 0:20(Vicheko)
-
0:20 - 0:22Na ujumbe wangu ulikuwa huu:
-
0:22 - 0:26Dunia yetu imekuwepo kwa karne milioni 45,
-
0:26 - 0:28lakini hii hapa ni maalumu ---
-
0:28 - 0:31ni ya kwanza ambayo jamii moja, yetu,
-
0:31 - 0:34ina mustakabali wa sayari mikononi mwake.
-
0:34 - 0:36Zaidi karibia ya historia yote ya Dunia,
-
0:36 - 0:38vitisho vimetoka kwenye mazingira,
-
0:38 - 0:42magonjwa, mitetemeko ya ardhi na
mengine mengi -- -
0:42 - 0:47lakini kuanzia sasa, hatari kubwa
inatoka kwetu. -
0:47 - 0:50Na sasa sio matisho tu ya nuklia;
-
0:50 - 0:52kwenye dunia yetu iliyoungana,
-
0:52 - 0:55kuvunjika kwa mitandao kunaweza
sambaa duniani; -
0:55 - 0:59usafiri wa anga unaweza kusambaza magonjwa
dunia nzima ndani ya siku; -
0:59 - 1:03na mitandao ya kijamii inaweza kusambaza
vitisho na uzushi -
1:03 - 1:06kihalisi kama kasi ya mwanga.
-
1:06 - 1:09Tunagombana sana kuhusu matatizo madogo --
-
1:09 - 1:13uwezekano wa ndege kudondoka,
kemikali kwenye chakula, -
1:13 - 1:15dozi ndogo za mionzi, na kadhalika --
-
1:15 - 1:18lakini sisi na wakuu wetu wa siasa
-
1:18 - 1:22tupo kwenye kukana kuhusu hali za majanga.
-
1:22 - 1:25Bahati nzuri mabaya hayajatokea bado.
-
1:25 - 1:28Kweli, pengine hayatatokea.
-
1:28 - 1:31Lakini kama tukio lina maafa makubwa,
-
1:31 - 1:34linastahili kupewa faida kubwa
-
1:34 - 1:38kulinda dhidi yake, hata kama
inaweza isitokee, -
1:38 - 1:42kama tunavyotoa bima ya moto kwenye
nyumba yetu. -
1:42 - 1:47Kama sayansi inavyoleta nguvu kubwa
na ahadi, -
1:47 - 1:51upande wa chini unazidi kuogopesha pia.
-
1:51 - 1:53Tunazidi kuwa dhaifu na waoga,
-
1:53 - 1:55Ndani ya miongo michache,
-
1:55 - 1:57mamilioni watakuwa na uwezo,
-
1:57 - 2:00wa kutumia vibaya bioteknolojia inayokua,
-
2:00 - 2:04Kama wanavyotumia teknolojia vibaya leo.
-
2:04 - 2:07Freeman Dyson, kwenye mazungumzo ya TED,
-
2:07 - 2:11aliona kuwa huko mbeleni watoto
wataweza kutengeneza viumbe hai -
2:11 - 2:14kama ambavyo kizazi chake
kilivyocheza na seti za kemia. -
2:15 - 2:18Hii inaweza kuwa sayansi ya kubuniwa
zaidi, -
2:18 - 2:21lakini tuna amini itatokea hata kwa kiasi,
-
2:21 - 2:24mazingira yetu na hata viumbe vyetu
-
2:24 - 2:28hawataweza kuishi muda mrefu
bila kubadilika, -
2:28 - 2:31Mfano, kuna wanamazingira wengi
wa msimamo mkali, -
2:31 - 2:34wanaomini kua itafaa kwa sayari yetu,
-
2:34 - 2:37kwa Gaia, kama kutakuwa na binadamu
wachache. -
2:37 - 2:40Nini kitatokea kama watu hawa wakifuzu
-
2:40 - 2:42ufundi wa kibiolojia za sanisia
-
2:42 - 2:45ambao utasambaa ifikapo mwaka 2050?
-
2:45 - 2:48Kipindi hicho, matisho mengine ya sayansi
ya kubuniwa -
2:48 - 2:50yanaweza kugeuka kweli:
-
2:50 - 2:52roboti za kijinga kujiongoza zenyewe,
-
2:52 - 2:54au mtandao unaotumia akili yake yenyewe
-
2:54 - 2:57unatutisha sote.
-
2:57 - 3:00Je, tutaweza kujikinga na hizi
hatari kwa sheria? -
3:00 - 3:03Itabidi tujaribu, lakini hizi biashara
-
3:03 - 3:06zina ushindani mkubwa, zipo dunia nzima,
-
3:06 - 3:08na zinasukumwa na mbinu za biashara,
-
3:08 - 3:11kwa kila kinachoweza kufanyika,
kitafanyika mahali, -
3:11 - 3:13bila kujali sheria zinasema nini.
-
3:13 - 3:17Ni kama sheria za madawa -- tunajaribu
kuzipunguza, lakini hatuwezi. -
3:17 - 3:20Na kijiji cha dunia kitakua na
wajinga wa kijiji, -
3:20 - 3:23nao watakua na masafa ya dunia.
-
3:23 - 3:26Kama nilivyosema kwenye kitabu changu,
-
3:26 - 3:29tutakuwa na mwendo mtata kwenye hii karne.
-
3:29 - 3:32Kunaweza kuwa na vikwazo kwenye
jamii yetu -- -
3:32 - 3:36kweli, asilimia 50 ya vikwazo zikali.
-
3:36 - 3:39Lakini kuna matukio ya maana
-
3:39 - 3:41yanayoweza kuwa mabaya zaidi,
-
3:41 - 3:45matukio yanayoweza kutoa maisha yote?
-
3:45 - 3:48Pale punje mpya chochezi iikija mtandaoni,
-
3:48 - 3:49badhi ya watu walijiuliza kwa bidii,
-
3:49 - 3:52vinaweza kuharibu dunia, au mbaya zaidi,
-
3:52 - 3:54kuharibu kabisa mfumo wa anga?
-
3:54 - 3:58Bahati nzuri, tuliweza kujihakikishia.
-
3:58 - 4:00Mimi na wenzangu tulisema kua asili
-
4:00 - 4:02imefanya majaribio kama hayo
-
4:02 - 4:04mara zilioni tayari,
-
4:04 - 4:06kutumia kugongana kwa miali ya anga.
-
4:06 - 4:09Lakini wanasayansi wanatakiwa wawe makini
-
4:09 - 4:11kuhusu majaribio yanayotengeneza hali
-
4:11 - 4:14bila uhakiki kwenye dunia ya halisi.
-
4:14 - 4:17Wanabiolojia wanatakiwa kuepuka kuachia
uharibifu muhimu wa -
4:17 - 4:20vimelea vilivyoundwa kijenetiki.
-
4:20 - 4:24Na pia, karaha yetu ya kipekee
-
4:24 - 4:27kwenye hatari ya mafaa makubwa
-
4:27 - 4:30inatokana na swali hili kubwa la msingi,
-
4:30 - 4:32nalo ni;
-
4:32 - 4:34Zingatia hali mbili.
-
4:34 - 4:40Hali A inaua asilimia 90 ya binadamu.
-
4:40 - 4:43Hali B inaua asilimia 100.
-
4:43 - 4:46Je B ni mbaya kiasi gani kuliko A?
-
4:46 - 4:49Baadhi watasema ni asilimia 10 mbaya
zaidi. -
4:49 - 4:53Idadi ni asilimia 10 zaidi.
-
4:53 - 4:55Lakini nasema kua B ni mbaya zaidi.
-
4:55 - 4:58Kama mwanafalaki, siamini
-
4:58 - 5:01binadamu ni mwisho wa hadithi.
-
5:01 - 5:04Ni miaka bilioni tano mpaka jua liripuke,
-
5:04 - 5:07na ulimwengu ungeendelea kuwepo,
-
5:07 - 5:09kwahiyo mageuzi ya binadamu wa baadae,
-
5:09 - 5:11hapa duniani na kwingineko mbali,
-
5:11 - 5:14inaweza kuwa ndefu kama harakati
ya Darwinian -
5:14 - 5:17iliyokuja kwetu, na nzuri zaidi.
-
5:17 - 5:20Na kweli, mageuzi ya mbeleni
yatatokea kwa haraka zaidi, -
5:20 - 5:22kwenye kipimo cha mda cha teknolojia,
-
5:22 - 5:24sio wa uchaguzi wa asili.
-
5:24 - 5:28Kwahiyo tupo katika mwanga wa
hicho kipimo, -
5:28 - 5:32kutokupokea hata hatari moja kati
ya billioni -
5:32 - 5:34ambayo kupotea kwa binadamu kutasababisha
-
5:34 - 5:36huu uwezekano mkubwa.
-
5:36 - 5:38Baadhi ya hali ambazo zilionyesha
-
5:38 - 5:40kua kweli zingekua sayansi ya
kubuniwa, -
5:40 - 5:43lakini nyingine zinaweza kuwa ni za kweli.
-
5:43 - 5:46Ni msemo muhimu kua vile visivyozoeleka
-
5:46 - 5:49sio sawa na vinavyoshindikana,
-
5:49 - 5:51na ndio maana, sisi katika Chuo cha
Cambridge, -
5:51 - 5:55tunaanda kitivo cha kujifunza jinsi ya
kuepuka -
5:55 - 5:57hizi hatari kubwa.
-
5:57 - 6:00Inaonekana ni ya maana kwa watu wachache
-
6:00 - 6:02kuwaza kuhusu haya mafaa yanayoweza
kutokea. -
6:02 - 6:05Na tunahitaji msaada wote tutakaopata
kwa wengine, -
6:05 - 6:08sababu sote ni wahudumu wa,
-
6:08 - 6:11kidoti cha bluu kwenye ulimwengu huu
mkubwa, -
6:11 - 6:14sayari yenye karne milioni 50 mbele yake.
-
6:14 - 6:17Kwa hiyo tusiharibu mustakabali wetu.
-
6:17 - 6:19Na ningependa kumalizia na nukuu
-
6:19 - 6:22kutoka kwa mwanasayansi mashuhuri aitwae
Peter Medawar. -
6:22 - 6:26nanukuu "Kengengele zinazolia kwa binadamu
-
6:26 - 6:28ni kama zile za mifugo ya Alpine.
-
6:28 - 6:30Zimefungwa shingoni mwetu wenyewe,
-
6:30 - 6:33na ni juu yetu kama hazitatengeneza
-
6:33 - 6:35mfuatano mzuri wa sauti."
-
6:35 - 6:38Asanteni sana.
-
6:38 - 6:40(Makofi)
- Title:
- Je tunaweza kuzuia mwisho wa Dunia?
- Speaker:
- Sir Martin Rees
- Description:
-
Baada ya mwisho wa dunia, binadamu hawapo, inaonekana kama kitu cha sayansi ya kubuniwa ya TV na filamu. Lakini katika maelezo haya mafupi na ya kushangaza, Lord Martin Rees anatuuliza tuwaze maafa yanayoweza kutukumba-- ya asili na ya kutengenezwa yanayoweza kufanya binadamu wote watoweke. Kama binadamu anayefuatilia vizuri yanayoendelea, anauliza: Ni kitu gani kibaya zaidi kinaweza kutokea?
- Video Language:
- English
- Team:
- closed TED
- Project:
- TEDTalks
- Duration:
- 06:52
Nelson Simfukwe approved Swahili subtitles for Can we prevent the end of the world? | ||
Doris Mangalu accepted Swahili subtitles for Can we prevent the end of the world? | ||
Doris Mangalu edited Swahili subtitles for Can we prevent the end of the world? | ||
Doris Mangalu edited Swahili subtitles for Can we prevent the end of the world? | ||
Doris Mangalu edited Swahili subtitles for Can we prevent the end of the world? | ||
Julieth Mbeyella edited Swahili subtitles for Can we prevent the end of the world? | ||
Julieth Mbeyella edited Swahili subtitles for Can we prevent the end of the world? | ||
Julieth Mbeyella edited Swahili subtitles for Can we prevent the end of the world? |