Miaka kumi iliyopita, niliandika kitabu
nilichokipa jina
"Karne yetu ya mwisho?" Alama ya kuuliza.
Wachapishaji wa kitabu hiki waliondoa
alama ya kuuliza. (Vicheko)
Wachapishaji wa Marekani
walibadili jina
na kuwa "Lisaa Letu la Mwisho".
Wamarekani hupenda kuridhishwa haraka na
kinyume.
(Vicheko)
Na ujumbe wangu ulikuwa huu:
Dunia yetu imekuwepo kwa karne milioni 45,
lakini hii hapa ni maalumu ---
ni ya kwanza ambayo jamii moja, yetu,
ina mustakabali wa sayari mikononi mwake.
Zaidi karibia ya historia yote ya Dunia,
vitisho vimetoka kwenye mazingira,
magonjwa, mitetemeko ya ardhi na
mengine mengi --
lakini kuanzia sasa, hatari kubwa
inatoka kwetu.
Na sasa sio matisho tu ya nuklia;
kwenye dunia yetu iliyoungana,
kuvunjika kwa mitandao kunaweza
sambaa duniani;
usafiri wa anga unaweza kusambaza magonjwa
dunia nzima ndani ya siku;
na mitandao ya kijamii inaweza kusambaza
vitisho na uzushi
kihalisi kama kasi ya mwanga.
Tunagombana sana kuhusu matatizo madogo --
uwezekano wa ndege kudondoka,
kemikali kwenye chakula,
dozi ndogo za mionzi, na kadhalika --
lakini sisi na wakuu wetu wa siasa
tupo kwenye kukana kuhusu hali za majanga.
Bahati nzuri mabaya hayajatokea bado.
Kweli, pengine hayatatokea.
Lakini kama tukio lina maafa makubwa,
linastahili kupewa faida kubwa
kulinda dhidi yake, hata kama
inaweza isitokee,
kama tunavyotoa bima ya moto kwenye
nyumba yetu.
Kama sayansi inavyoleta nguvu kubwa
na ahadi,
upande wa chini unazidi kuogopesha pia.
Tunazidi kuwa dhaifu na waoga,
Ndani ya miongo michache,
mamilioni watakuwa na uwezo,
wa kutumia vibaya bioteknolojia inayokua,
Kama wanavyotumia teknolojia vibaya leo.
Freeman Dyson, kwenye mazungumzo ya TED,
aliona kuwa huko mbeleni watoto
wataweza kutengeneza viumbe hai
kama ambavyo kizazi chake
kilivyocheza na seti za kemia.
Hii inaweza kuwa sayansi ya kubuniwa
zaidi,
lakini tuna amini itatokea hata kwa kiasi,
mazingira yetu na hata viumbe vyetu
hawataweza kuishi muda mrefu
bila kubadilika,
Mfano, kuna wanamazingira wengi
wa msimamo mkali,
wanaomini kua itafaa kwa sayari yetu,
kwa Gaia, kama kutakuwa na binadamu
wachache.
Nini kitatokea kama watu hawa wakifuzu
ufundi wa kibiolojia za sanisia
ambao utasambaa ifikapo mwaka 2050?
Kipindi hicho, matisho mengine ya sayansi
ya kubuniwa
yanaweza kugeuka kweli:
roboti za kijinga kujiongoza zenyewe,
au mtandao unaotumia akili yake yenyewe
unatutisha sote.
Je, tutaweza kujikinga na hizi
hatari kwa sheria?
Itabidi tujaribu, lakini hizi biashara
zina ushindani mkubwa, zipo dunia nzima,
na zinasukumwa na mbinu za biashara,
kwa kila kinachoweza kufanyika,
kitafanyika mahali,
bila kujali sheria zinasema nini.
Ni kama sheria za madawa -- tunajaribu
kuzipunguza, lakini hatuwezi.
Na kijiji cha dunia kitakua na
wajinga wa kijiji,
nao watakua na masafa ya dunia.
Kama nilivyosema kwenye kitabu changu,
tutakuwa na mwendo mtata kwenye hii karne.
Kunaweza kuwa na vikwazo kwenye
jamii yetu --
kweli, asilimia 50 ya vikwazo zikali.
Lakini kuna matukio ya maana
yanayoweza kuwa mabaya zaidi,
matukio yanayoweza kutoa maisha yote?
Pale punje mpya chochezi iikija mtandaoni,
badhi ya watu walijiuliza kwa bidii,
vinaweza kuharibu dunia, au mbaya zaidi,
kuharibu kabisa mfumo wa anga?
Bahati nzuri, tuliweza kujihakikishia.
Mimi na wenzangu tulisema kua asili
imefanya majaribio kama hayo
mara zilioni tayari,
kutumia kugongana kwa miali ya anga.
Lakini wanasayansi wanatakiwa wawe makini
kuhusu majaribio yanayotengeneza hali
bila uhakiki kwenye dunia ya halisi.
Wanabiolojia wanatakiwa kuepuka kuachia
uharibifu muhimu wa
vimelea vilivyoundwa kijenetiki.
Na pia, karaha yetu ya kipekee
kwenye hatari ya mafaa makubwa
inatokana na swali hili kubwa la msingi,
nalo ni;
Zingatia hali mbili.
Hali A inaua asilimia 90 ya binadamu.
Hali B inaua asilimia 100.
Je B ni mbaya kiasi gani kuliko A?
Baadhi watasema ni asilimia 10 mbaya
zaidi.
Idadi ni asilimia 10 zaidi.
Lakini nasema kua B ni mbaya zaidi.
Kama mwanafalaki, siamini
binadamu ni mwisho wa hadithi.
Ni miaka bilioni tano mpaka jua liripuke,
na ulimwengu ungeendelea kuwepo,
kwahiyo mageuzi ya binadamu wa baadae,
hapa duniani na kwingineko mbali,
inaweza kuwa ndefu kama harakati
ya Darwinian
iliyokuja kwetu, na nzuri zaidi.
Na kweli, mageuzi ya mbeleni
yatatokea kwa haraka zaidi,
kwenye kipimo cha mda cha teknolojia,
sio wa uchaguzi wa asili.
Kwahiyo tupo katika mwanga wa
hicho kipimo,
kutokupokea hata hatari moja kati
ya billioni
ambayo kupotea kwa binadamu kutasababisha
huu uwezekano mkubwa.
Baadhi ya hali ambazo zilionyesha
kua kweli zingekua sayansi ya
kubuniwa,
lakini nyingine zinaweza kuwa ni za kweli.
Ni msemo muhimu kua vile visivyozoeleka
sio sawa na vinavyoshindikana,
na ndio maana, sisi katika Chuo cha
Cambridge,
tunaanda kitivo cha kujifunza jinsi ya
kuepuka
hizi hatari kubwa.
Inaonekana ni ya maana kwa watu wachache
kuwaza kuhusu haya mafaa yanayoweza
kutokea.
Na tunahitaji msaada wote tutakaopata
kwa wengine,
sababu sote ni wahudumu wa,
kidoti cha bluu kwenye ulimwengu huu
mkubwa,
sayari yenye karne milioni 50 mbele yake.
Kwa hiyo tusiharibu mustakabali wetu.
Na ningependa kumalizia na nukuu
kutoka kwa mwanasayansi mashuhuri aitwae
Peter Medawar.
nanukuu "Kengengele zinazolia kwa binadamu
ni kama zile za mifugo ya Alpine.
Zimefungwa shingoni mwetu wenyewe,
na ni juu yetu kama hazitatengeneza
mfuatano mzuri wa sauti."
Asanteni sana.
(Makofi)