Miaka kumi iliyopita, niliandika kitabu nilichokipa jina "Karne yetu ya mwisho?" Alama ya kuuliza. Wachapishaji wa kitabu hiki waliondoa alama ya kuuliza. (Vicheko) Wachapishaji wa Marekani walibadili jina na kuwa "Lisaa Letu la Mwisho". Wamarekani hupenda kuridhishwa haraka na kinyume. (Vicheko) Na ujumbe wangu ulikuwa huu: Dunia yetu imekuwepo kwa karne milioni 45, lakini hii hapa ni maalumu --- ni ya kwanza ambayo jamii moja, yetu, ina mustakabali wa sayari mikononi mwake. Zaidi karibia ya historia yote ya Dunia, vitisho vimetoka kwenye mazingira, magonjwa, mitetemeko ya ardhi na mengine mengi -- lakini kuanzia sasa, hatari kubwa inatoka kwetu. Na sasa sio matisho tu ya nuklia; kwenye dunia yetu iliyoungana, kuvunjika kwa mitandao kunaweza sambaa duniani; usafiri wa anga unaweza kusambaza magonjwa dunia nzima ndani ya siku; na mitandao ya kijamii inaweza kusambaza vitisho na uzushi kihalisi kama kasi ya mwanga. Tunagombana sana kuhusu matatizo madogo -- uwezekano wa ndege kudondoka, kemikali kwenye chakula, dozi ndogo za mionzi, na kadhalika -- lakini sisi na wakuu wetu wa siasa tupo kwenye kukana kuhusu hali za majanga. Bahati nzuri mabaya hayajatokea bado. Kweli, pengine hayatatokea. Lakini kama tukio lina maafa makubwa, linastahili kupewa faida kubwa kulinda dhidi yake, hata kama inaweza isitokee, kama tunavyotoa bima ya moto kwenye nyumba yetu. Kama sayansi inavyoleta nguvu kubwa na ahadi, upande wa chini unazidi kuogopesha pia. Tunazidi kuwa dhaifu na waoga, Ndani ya miongo michache, mamilioni watakuwa na uwezo, wa kutumia vibaya bioteknolojia inayokua, Kama wanavyotumia teknolojia vibaya leo. Freeman Dyson, kwenye mazungumzo ya TED, aliona kuwa huko mbeleni watoto wataweza kutengeneza viumbe hai kama ambavyo kizazi chake kilivyocheza na seti za kemia. Hii inaweza kuwa sayansi ya kubuniwa zaidi, lakini tuna amini itatokea hata kwa kiasi, mazingira yetu na hata viumbe vyetu hawataweza kuishi muda mrefu bila kubadilika, Mfano, kuna wanamazingira wengi wa msimamo mkali, wanaomini kua itafaa kwa sayari yetu, kwa Gaia, kama kutakuwa na binadamu wachache. Nini kitatokea kama watu hawa wakifuzu ufundi wa kibiolojia za sanisia ambao utasambaa ifikapo mwaka 2050? Kipindi hicho, matisho mengine ya sayansi ya kubuniwa yanaweza kugeuka kweli: roboti za kijinga kujiongoza zenyewe, au mtandao unaotumia akili yake yenyewe unatutisha sote. Je, tutaweza kujikinga na hizi hatari kwa sheria? Itabidi tujaribu, lakini hizi biashara zina ushindani mkubwa, zipo dunia nzima, na zinasukumwa na mbinu za biashara, kwa kila kinachoweza kufanyika, kitafanyika mahali, bila kujali sheria zinasema nini. Ni kama sheria za madawa -- tunajaribu kuzipunguza, lakini hatuwezi. Na kijiji cha dunia kitakua na wajinga wa kijiji, nao watakua na masafa ya dunia. Kama nilivyosema kwenye kitabu changu, tutakuwa na mwendo mtata kwenye hii karne. Kunaweza kuwa na vikwazo kwenye jamii yetu -- kweli, asilimia 50 ya vikwazo zikali. Lakini kuna matukio ya maana yanayoweza kuwa mabaya zaidi, matukio yanayoweza kutoa maisha yote? Pale punje mpya chochezi iikija mtandaoni, badhi ya watu walijiuliza kwa bidii, vinaweza kuharibu dunia, au mbaya zaidi, kuharibu kabisa mfumo wa anga? Bahati nzuri, tuliweza kujihakikishia. Mimi na wenzangu tulisema kua asili imefanya majaribio kama hayo mara zilioni tayari, kutumia kugongana kwa miali ya anga. Lakini wanasayansi wanatakiwa wawe makini kuhusu majaribio yanayotengeneza hali bila uhakiki kwenye dunia ya halisi. Wanabiolojia wanatakiwa kuepuka kuachia uharibifu muhimu wa vimelea vilivyoundwa kijenetiki. Na pia, karaha yetu ya kipekee kwenye hatari ya mafaa makubwa inatokana na swali hili kubwa la msingi, nalo ni; Zingatia hali mbili. Hali A inaua asilimia 90 ya binadamu. Hali B inaua asilimia 100. Je B ni mbaya kiasi gani kuliko A? Baadhi watasema ni asilimia 10 mbaya zaidi. Idadi ni asilimia 10 zaidi. Lakini nasema kua B ni mbaya zaidi. Kama mwanafalaki, siamini binadamu ni mwisho wa hadithi. Ni miaka bilioni tano mpaka jua liripuke, na ulimwengu ungeendelea kuwepo, kwahiyo mageuzi ya binadamu wa baadae, hapa duniani na kwingineko mbali, inaweza kuwa ndefu kama harakati ya Darwinian iliyokuja kwetu, na nzuri zaidi. Na kweli, mageuzi ya mbeleni yatatokea kwa haraka zaidi, kwenye kipimo cha mda cha teknolojia, sio wa uchaguzi wa asili. Kwahiyo tupo katika mwanga wa hicho kipimo, kutokupokea hata hatari moja kati ya billioni ambayo kupotea kwa binadamu kutasababisha huu uwezekano mkubwa. Baadhi ya hali ambazo zilionyesha kua kweli zingekua sayansi ya kubuniwa, lakini nyingine zinaweza kuwa ni za kweli. Ni msemo muhimu kua vile visivyozoeleka sio sawa na vinavyoshindikana, na ndio maana, sisi katika Chuo cha Cambridge, tunaanda kitivo cha kujifunza jinsi ya kuepuka hizi hatari kubwa. Inaonekana ni ya maana kwa watu wachache kuwaza kuhusu haya mafaa yanayoweza kutokea. Na tunahitaji msaada wote tutakaopata kwa wengine, sababu sote ni wahudumu wa, kidoti cha bluu kwenye ulimwengu huu mkubwa, sayari yenye karne milioni 50 mbele yake. Kwa hiyo tusiharibu mustakabali wetu. Na ningependa kumalizia na nukuu kutoka kwa mwanasayansi mashuhuri aitwae Peter Medawar. nanukuu "Kengengele zinazolia kwa binadamu ni kama zile za mifugo ya Alpine. Zimefungwa shingoni mwetu wenyewe, na ni juu yetu kama hazitatengeneza mfuatano mzuri wa sauti." Asanteni sana. (Makofi)