Fahad Al-Attiya: Nchi isiyokuwa na maji
-
0:01 - 0:04Salaam alaikum
-
0:04 - 0:05Karibuni Doha.
-
0:05 - 0:09Mimi ndio muhusika wa usalama wa chakula nchi hii.
-
0:09 - 0:11Hii ni kazi yangu kwa miaka miwili ijayo,
-
0:11 - 0:13kutengeneza mpango mkuu,
-
0:13 - 0:17na kwa miaka kumi ijayo kuupendekeza
-
0:17 - 0:19na watu wengine wengi,
-
0:19 - 0:23Lakini kwanza,nahitaji kukuhadithia,hii ni hadithi yangu,
-
0:23 - 0:27kuhusu nchi hii mliyopo leo
-
0:27 - 0:31Kwa uhakika,wengi wenu mmekula milo mitatu leo,
-
0:31 - 0:35nahisi mtaendelea kula tena baada ya hii shughuli.
-
0:35 - 0:40Tuangalie sasa ni vipi Quatar ilikuwa katika mwaka 1940?
-
0:40 - 0:44Tulikuwa watu kama 11,000 tunaoishi hapa.
-
0:44 - 0:51Hakukuwa na maji.Hakukuwa an nishati,mafuta,magari,vyote hivo havikuwepo.
-
0:51 - 0:52Watu wengi walioishi hapa
-
0:52 - 0:55waliishi vijiji vya pwani,kuvua,
-
0:55 - 1:01au walikuwa watu wa kuhamahama ambao walitembea kutafuta maji.
-
1:01 - 1:04Uzuri wote huu unauona haukuwepo.
-
1:04 - 1:09Hakukuwa na jiji kama uonavyo leo Doha au Dubai au Abu Dhabi au Kuwait au Riyadh.
-
1:09 - 1:12Haikuwa kwamba walishidwa kuendeleza miji.
-
1:12 - 1:14Malighafi hazikuwepo kuweza kuendeleza.
-
1:14 - 1:17Na unaweza kuona muda wa watu kuishi ulikuwa mfupi.
-
1:17 - 1:19Watu wengi walifariki katika miaka 50
-
1:19 - 1:23Twende sasa ukurasa wa pili:wakati wa mafuta.
-
1:23 - 1:261939,hapo ndipo mafuta yaligundulika.
-
1:26 - 1:31Kwa bahati mbaya,hayakutumika vya kutosha kibiashara
-
1:31 - 1:33mpaka vita ya pili ya dunia.
-
1:33 - 1:35Ilifanya nini?
-
1:35 - 1:38Ilibadilisha muonekano wa nchi,kama unavyoona na kushuhudia.
-
1:38 - 1:42Na ilifanya wale watu wote waliokuwa wakizunguka jangwa..
-
1:42 - 1:45kutafuta maji,kutafuta chakula,
-
1:45 - 1:50wakijaribu kuwatunza wanyama wao..wakaepata maendeleo
-
1:50 - 1:52Unaweza kuona ni ajabu,
-
1:52 - 1:55lakini katika familia yangu tuna lafudhi tofauti.
-
1:55 - 1:59Mama yangu ana asili ambayo ni tofauti na baba yangu,
-
1:59 - 2:04wote tupo idadi inayofikia watu 300,000 tunaoishi katika nchi moja.
-
2:04 - 2:08Kuna lafudhi kama tano au sita katika nchi hii ninapoongea mpaka sasa.
-
2:08 - 2:12Kuna mtu husema"Kivipi?Inawezekanaje kutokea?
-
2:12 - 2:14Kwa kuwa tuliishi tukiwa tumetawanyika.
-
2:14 - 2:19Hatukuishi katika sehemu ya pamoja sana kwa sababu hatukuwa na malighafi.
-
2:19 - 2:22Na malighafi zilipokuja,mafuta,
-
2:22 - 2:26tukaanza kutengeneza teknolojia ya hali ya juu
-
2:26 - 2:29na kuwaleta watu pamoja kwa sababu tulihitaji kukusanyika.
-
2:29 - 2:32Watu walianza kufahamiana.
-
2:32 - 2:36Na tukagundua kulikuwa na tofauti ya asili.
-
2:36 - 2:38Hiyo ilikuwa ukurasa wa pili:wakati wa mafuta.
-
2:38 - 2:41Tuangalie leo.
-
2:41 - 2:45Inawezekana hiki ndicho wengi mnachojua kuhusu Doha.
-
2:45 - 2:47Idadi ya watu ikoje leo?
-
2:47 - 2:49ni watu milioni moja na laki saba.
-
2:49 - 2:52Hiyo ni katika kipindi kisichozidi miaka 60.
-
2:52 - 2:58Wastani wa ukuaji w uchumi wetu ni asilimia 15 katika miaka mitano iliyopita.
-
2:58 - 3:00Tegemeo la kuishi limeongezeka hadi miaka 78.
-
3:00 - 3:05Matumizi ya maji yameongezeka hadi lita 430.
-
3:05 - 3:09Na hii ndo takwimu kubwa duniani.
-
3:09 - 3:11Kutoka kutokuwa na maji
-
3:11 - 3:16mpaka kutumia maji katika kiwango kikubwa duniani,kikubwa kuliko taifa lolote.
-
3:16 - 3:20Sijui kama hii ni matokeo ya ukosefu wa maji.
-
3:20 - 3:26Lakini ni kipi kinachonifurahisha kwenye hadithi niliyosimulia?
-
3:26 - 3:29Kinachofurahisha ni kwamba tunaendelea kukua
-
3:29 - 3:36asilimia 15 kila mwaka kwa miaka mitano bila maji.
-
3:36 - 3:41Sasa hiyo ni historia.Haijawahi tokea kabla ya historia.
-
3:41 - 3:45Miji yote iliharibika kwa sababu ya ukoseu wa maji.
-
3:45 - 3:47Hii ni historia iliyotengenezwa katika eneo hili.
-
3:47 - 3:49Sio miji tu ndo tunajenga,
-
3:49 - 3:54lakini miji yenye maono na watu ambao wanatamani kuwa wanasayansi,madaktari.
-
3:54 - 3:58Kujenga nyumba nzuri,kuwaleta wasanifu majengo,kutengeneza nyumba yangu.
-
3:58 - 4:04Hawa watu wanaamini kwamba sehemu hii unaweza kuishi wakati ilipokuwa haiwezekani.
-
4:04 - 4:06Lakini kwa sababu ya teknolojia.
-
4:06 - 4:12Brazil ina kiasi cha mvua kwa milimita 1782 kwa mwaka.
-
4:12 - 4:15Quatar ina 74,na tuna ukuaji kiasi hicho.
-
4:15 - 4:17Swali ni kivipi?
-
4:17 - 4:20Tunawezaje kuendela hivi?
-
4:20 - 4:22Hatuna maji kabisa.
-
4:22 - 4:29kwa sababu ya mashine kubwa ya kutoa chumvi kwenye maji.
-
4:29 - 4:33Nishati ni kitu kikubwa hapa.Imebadilisha kila kitu.
-
4:33 - 4:37Ni ambacho kinakitoa toka ardhini,tunaunguza tani na tani,
-
4:37 - 4:40wengi wenu mmekitumia kuja Doha.
-
4:40 - 4:43Hilo ni ziwa letu,kama unaweza kuona.
-
4:43 - 4:45Huo ni mto wetu.
-
4:45 - 4:51Hivyo ndivyo inavotokea mpaka kutumia na kufaidi maji.
-
4:51 - 4:57Hii ni teknolojia nzuri sana ambayo eneo hili linayo,kuondoa chumvi katika maji
-
4:57 - 4:59Je,hatari ni zipi?
-
4:59 - 5:01Unaogopa sana?
-
5:01 - 5:05Naweza kusema,ukiangalia ukweli kiujumla,
-
5:05 - 5:08utagundua,unatakiwa kuwa na mashaka.
-
5:08 - 5:10Kuna hitaji la kukua,ukuaji wa idadi ya watu.
-
5:10 - 5:13Tumekuwa bilioni saba miezi michache iliyopita.
-
5:13 - 5:17Na hiyo idadi pia inahitaji chakula.
-
5:17 - 5:20Na kuna makisio kwamba tutakuwa bilioni tisa kwa mwaka 2050.
-
5:20 - 5:23Kwa hiyo nchi ambayo haina maji
-
5:23 - 5:26inakuwa na wasiwasi kipi kitachotokea nje ya mipaka yake.
-
5:26 - 5:29Kuna kubadilisha ulaji.
-
5:29 - 5:33Kwa kuongezeka katika hali ya juu ya maisha,
-
5:33 - 5:35pia wanabadilisha ulaji wao.
-
5:35 - 5:38Wanaanza kula kula sana nyama na vinginevyo.
-
5:38 - 5:40Kwa upande mwingine,uzalishaji unaporomoka
-
5:40 - 5:43kwa sababu ya mabadiliko ya tabia ya nchi na sababu nyinginezo.
-
5:43 - 5:48Na inatakiwa mtu atambue lini hili tatizo litakuja kutokea.
-
5:48 - 5:52Hii ni hali hapa Quatar,kwa wale wasiojua.
-
5:52 - 5:55Tuna siku mbili tu za utunzaji maji.
-
5:55 - 5:58Tunaagiza asilimia 90 ya chakula chetu,
-
5:58 - 6:01na tunalima chini ya asilimia moja ya ardhi yetu.
-
6:01 - 6:04Idadi ndogo ya wakulima ambayo tunayo
-
6:04 - 6:07wameondolewa katika taratibu zao za ulimaji
-
6:07 - 6:13kwa sababu ya soko huria na ushindani, n.k.
-
6:13 - 6:16Kwa hiyo tunakumbana na hatari
-
6:16 - 6:23Hatari hizi zimeathiri uendeleaji wa taifa hili
-
6:23 - 6:26Swali ni kwamba,je kuna suluhisho?
-
6:26 - 6:28Kuna ufumbuzi wa uhakika?
-
6:28 - 6:30Kiukweli upo.
-
6:30 - 6:34Hii inaonesha nyaraka zipatazo 1000 za kiufundi
-
6:34 - 6:37ambazo tulikuwa tunafanyia kazi katika miaka miwili iliyopita.
-
6:37 - 6:38Tuanze na maji.
-
6:38 - 6:42Tunajua fika...niliwaonyesha mapema..kwamba tunahitaji hii nishati.
-
6:42 - 6:45Kwa hiyo kama tutahitaji nishati,ni aina ipi?
-
6:45 - 6:47nishati inayoisha?mafuta ghafi?
-
6:47 - 6:50Au tutumie kitu kingine?
-
6:50 - 6:53Tunayo faida ya kulinganisha kutumia aina nyingine ya nishati?
-
6:53 - 6:57Nahisi wote mnafahamu kwamba tuna siku 300 za jua.
-
6:57 - 7:03Kwa tunaweza tumia hii nishati kutupa maji tunayohitaji.
-
7:03 - 7:08Kwa hiyo tunaweza kuweka 1800 megawati za umeme jua
-
7:08 - 7:11kuzalisha milioni 3.5 za ujazo za maji.
-
7:11 - 7:13Na hayo ni maji mengi.
-
7:13 - 7:15Hayo maji yataenda kwa wakulima,
-
7:15 - 7:17na wakulima wataweza kumwagilia mazao yao,
-
7:17 - 7:21wataweza kuihudumia jamii kwa chakula
-
7:21 - 7:23Lakini kwa ajili ya kuhimili upande huu
-
7:23 - 7:27kwa sababu hii ni mipango,hii ni mipango tunayotekeleza
-
7:27 - 7:29pia tunatakiwa tuendeleze upande mwingine
-
7:29 - 7:35kusimamia mifumo,elimu ya hali ya juu,tafiti na maendeleo,
-
7:35 - 7:40vinwanda,teknolojia,kutengeneza teknolojia kwa matumizi,na mwisho masoko.
-
7:40 - 7:46Lakini kipi kinarahisha na kuwezesha,ni sheria,sera,utaratibu.
-
7:46 - 7:48Bila hivi hatuwezi kufanya chochote.
-
7:48 - 7:50Kwa hiyo hiki ndicho tunachopanga kufanya.
-
7:50 - 7:53Ndani ya miaka miwili tunaweza kuwa tumekamilisha mipango hii
-
7:53 - 7:55na kuongelea kuitekeleza.
-
7:55 - 8:02Lengo letu kuu ni kuwa jiji la kimilenia,kama majiji mengine ya kimilenia
-
8:02 - 8:09Instanbul,Rome,London,Paris,Damascus,Cairo.
-
8:09 - 8:13Tuna miaka 60 tu,lakini tunataka kuishi milele
-
8:13 - 8:18kama jiji,kuishi kwa amani.
-
8:18 - 8:20Asante sana.
-
8:20 - 8:24(makofi)
- Title:
- Fahad Al-Attiya: Nchi isiyokuwa na maji
- Speaker:
- Fahad Al-Attiya
- Description:
-
Fikiri kuhusu nchi ambayo ina umeme mwingi sana -- mafuta na gesi,Mwanga wa jua,upepo(na pesa) --lakini imepungukiwa na huduma muhimu kwa ajili ya maisha: Maji. Mhandisi wa miundo mbinu Fahad Al-Attiya anaongelea njia zisizotegemewa ambazo taifa dogo la Mashariki ya Kati la Qatar linatumia kutengeneza mfumo wake wa usambazaji wa maji.
- Video Language:
- English
- Team:
- closed TED
- Project:
- TEDTalks
- Duration:
- 08:46
Joachim Mangilima approved Swahili subtitles for A country with no water | ||
Joachim Mangilima accepted Swahili subtitles for A country with no water | ||
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for A country with no water | ||
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for A country with no water | ||
Nelson Simfukwe added a translation |