Salaam alaikum Karibuni Doha. Mimi ndio muhusika wa usalama wa chakula nchi hii. Hii ni kazi yangu kwa miaka miwili ijayo, kutengeneza mpango mkuu, na kwa miaka kumi ijayo kuupendekeza na watu wengine wengi, Lakini kwanza,nahitaji kukuhadithia,hii ni hadithi yangu, kuhusu nchi hii mliyopo leo Kwa uhakika,wengi wenu mmekula milo mitatu leo, nahisi mtaendelea kula tena baada ya hii shughuli. Tuangalie sasa ni vipi Quatar ilikuwa katika mwaka 1940? Tulikuwa watu kama 11,000 tunaoishi hapa. Hakukuwa na maji.Hakukuwa an nishati,mafuta,magari,vyote hivo havikuwepo. Watu wengi walioishi hapa waliishi vijiji vya pwani,kuvua, au walikuwa watu wa kuhamahama ambao walitembea kutafuta maji. Uzuri wote huu unauona haukuwepo. Hakukuwa na jiji kama uonavyo leo Doha au Dubai au Abu Dhabi au Kuwait au Riyadh. Haikuwa kwamba walishidwa kuendeleza miji. Malighafi hazikuwepo kuweza kuendeleza. Na unaweza kuona muda wa watu kuishi ulikuwa mfupi. Watu wengi walifariki katika miaka 50 Twende sasa ukurasa wa pili:wakati wa mafuta. 1939,hapo ndipo mafuta yaligundulika. Kwa bahati mbaya,hayakutumika vya kutosha kibiashara mpaka vita ya pili ya dunia. Ilifanya nini? Ilibadilisha muonekano wa nchi,kama unavyoona na kushuhudia. Na ilifanya wale watu wote waliokuwa wakizunguka jangwa.. kutafuta maji,kutafuta chakula, wakijaribu kuwatunza wanyama wao..wakaepata maendeleo Unaweza kuona ni ajabu, lakini katika familia yangu tuna lafudhi tofauti. Mama yangu ana asili ambayo ni tofauti na baba yangu, wote tupo idadi inayofikia watu 300,000 tunaoishi katika nchi moja. Kuna lafudhi kama tano au sita katika nchi hii ninapoongea mpaka sasa. Kuna mtu husema"Kivipi?Inawezekanaje kutokea? Kwa kuwa tuliishi tukiwa tumetawanyika. Hatukuishi katika sehemu ya pamoja sana kwa sababu hatukuwa na malighafi. Na malighafi zilipokuja,mafuta, tukaanza kutengeneza teknolojia ya hali ya juu na kuwaleta watu pamoja kwa sababu tulihitaji kukusanyika. Watu walianza kufahamiana. Na tukagundua kulikuwa na tofauti ya asili. Hiyo ilikuwa ukurasa wa pili:wakati wa mafuta. Tuangalie leo. Inawezekana hiki ndicho wengi mnachojua kuhusu Doha. Idadi ya watu ikoje leo? ni watu milioni moja na laki saba. Hiyo ni katika kipindi kisichozidi miaka 60. Wastani wa ukuaji w uchumi wetu ni asilimia 15 katika miaka mitano iliyopita. Tegemeo la kuishi limeongezeka hadi miaka 78. Matumizi ya maji yameongezeka hadi lita 430. Na hii ndo takwimu kubwa duniani. Kutoka kutokuwa na maji mpaka kutumia maji katika kiwango kikubwa duniani,kikubwa kuliko taifa lolote. Sijui kama hii ni matokeo ya ukosefu wa maji. Lakini ni kipi kinachonifurahisha kwenye hadithi niliyosimulia? Kinachofurahisha ni kwamba tunaendelea kukua asilimia 15 kila mwaka kwa miaka mitano bila maji. Sasa hiyo ni historia.Haijawahi tokea kabla ya historia. Miji yote iliharibika kwa sababu ya ukoseu wa maji. Hii ni historia iliyotengenezwa katika eneo hili. Sio miji tu ndo tunajenga, lakini miji yenye maono na watu ambao wanatamani kuwa wanasayansi,madaktari. Kujenga nyumba nzuri,kuwaleta wasanifu majengo,kutengeneza nyumba yangu. Hawa watu wanaamini kwamba sehemu hii unaweza kuishi wakati ilipokuwa haiwezekani. Lakini kwa sababu ya teknolojia. Brazil ina kiasi cha mvua kwa milimita 1782 kwa mwaka. Quatar ina 74,na tuna ukuaji kiasi hicho. Swali ni kivipi? Tunawezaje kuendela hivi? Hatuna maji kabisa. kwa sababu ya mashine kubwa ya kutoa chumvi kwenye maji. Nishati ni kitu kikubwa hapa.Imebadilisha kila kitu. Ni ambacho kinakitoa toka ardhini,tunaunguza tani na tani, wengi wenu mmekitumia kuja Doha. Hilo ni ziwa letu,kama unaweza kuona. Huo ni mto wetu. Hivyo ndivyo inavotokea mpaka kutumia na kufaidi maji. Hii ni teknolojia nzuri sana ambayo eneo hili linayo,kuondoa chumvi katika maji Je,hatari ni zipi? Unaogopa sana? Naweza kusema,ukiangalia ukweli kiujumla, utagundua,unatakiwa kuwa na mashaka. Kuna hitaji la kukua,ukuaji wa idadi ya watu. Tumekuwa bilioni saba miezi michache iliyopita. Na hiyo idadi pia inahitaji chakula. Na kuna makisio kwamba tutakuwa bilioni tisa kwa mwaka 2050. Kwa hiyo nchi ambayo haina maji inakuwa na wasiwasi kipi kitachotokea nje ya mipaka yake. Kuna kubadilisha ulaji. Kwa kuongezeka katika hali ya juu ya maisha, pia wanabadilisha ulaji wao. Wanaanza kula kula sana nyama na vinginevyo. Kwa upande mwingine,uzalishaji unaporomoka kwa sababu ya mabadiliko ya tabia ya nchi na sababu nyinginezo. Na inatakiwa mtu atambue lini hili tatizo litakuja kutokea. Hii ni hali hapa Quatar,kwa wale wasiojua. Tuna siku mbili tu za utunzaji maji. Tunaagiza asilimia 90 ya chakula chetu, na tunalima chini ya asilimia moja ya ardhi yetu. Idadi ndogo ya wakulima ambayo tunayo wameondolewa katika taratibu zao za ulimaji kwa sababu ya soko huria na ushindani, n.k. Kwa hiyo tunakumbana na hatari Hatari hizi zimeathiri uendeleaji wa taifa hili Swali ni kwamba,je kuna suluhisho? Kuna ufumbuzi wa uhakika? Kiukweli upo. Hii inaonesha nyaraka zipatazo 1000 za kiufundi ambazo tulikuwa tunafanyia kazi katika miaka miwili iliyopita. Tuanze na maji. Tunajua fika...niliwaonyesha mapema..kwamba tunahitaji hii nishati. Kwa hiyo kama tutahitaji nishati,ni aina ipi? nishati inayoisha?mafuta ghafi? Au tutumie kitu kingine? Tunayo faida ya kulinganisha kutumia aina nyingine ya nishati? Nahisi wote mnafahamu kwamba tuna siku 300 za jua. Kwa tunaweza tumia hii nishati kutupa maji tunayohitaji. Kwa hiyo tunaweza kuweka 1800 megawati za umeme jua kuzalisha milioni 3.5 za ujazo za maji. Na hayo ni maji mengi. Hayo maji yataenda kwa wakulima, na wakulima wataweza kumwagilia mazao yao, wataweza kuihudumia jamii kwa chakula Lakini kwa ajili ya kuhimili upande huu kwa sababu hii ni mipango,hii ni mipango tunayotekeleza pia tunatakiwa tuendeleze upande mwingine kusimamia mifumo,elimu ya hali ya juu,tafiti na maendeleo, vinwanda,teknolojia,kutengeneza teknolojia kwa matumizi,na mwisho masoko. Lakini kipi kinarahisha na kuwezesha,ni sheria,sera,utaratibu. Bila hivi hatuwezi kufanya chochote. Kwa hiyo hiki ndicho tunachopanga kufanya. Ndani ya miaka miwili tunaweza kuwa tumekamilisha mipango hii na kuongelea kuitekeleza. Lengo letu kuu ni kuwa jiji la kimilenia,kama majiji mengine ya kimilenia Instanbul,Rome,London,Paris,Damascus,Cairo. Tuna miaka 60 tu,lakini tunataka kuishi milele kama jiji,kuishi kwa amani. Asante sana. (makofi)