Return to Video

Vitu tutumiavyo kila siku, historia ya kusikitisha

  • 0:01 - 0:02
    Hivi ni vitu rahisi au vya kawaida
  • 0:02 - 0:06
    saa,funguo,vitana,miwani.
  • 0:06 - 0:09
    Ni vitu ambavyo wahanga wa mauaji ya kimbari huko Bosnia
  • 0:09 - 0:12
    walivibeba katika safari yao ya mwisho.
  • 0:12 - 0:14
    Wote tunayafahamu haya mambo,
  • 0:14 - 0:16
    vitu vya kila siku.
  • 0:16 - 0:18
    Ukweli wa kwamba baadhi ya wahanga walibeba
  • 0:18 - 0:21
    vitu binafsi kama miswaki na dawa za meno
  • 0:21 - 0:23
    ni dalili ya wazi ioneshayo kwamba hawakuwa na wazo
  • 0:23 - 0:25
    ni kipi hasa kingeenda kuwatokea.
  • 0:25 - 0:28
    Katika hali ya kawaida, waliambiwa wataenda kubadilishwa
  • 0:28 - 0:30
    na wafungwa wa vita.
  • 0:30 - 0:32
    Hivi vitu vilikuja patikana
  • 0:32 - 0:35
    katika baadhi ya makaburi nchini mwangu,
  • 0:35 - 0:38
    mpaka sasa tunapoongea,wataalamu wa vinasaba wanafukua miili
  • 0:38 - 0:40
    katika makaburi yaliyogunduliwa,
  • 0:40 - 0:41
    miaka 20 baada ya vita.
  • 0:41 - 0:45
    Na inawezekana ni kiasi kikubwa sana kilichowahi kugunduliwa.
  • 0:45 - 0:48
    Katika miaka minne ya mtafaruku
  • 0:48 - 0:50
    uliowachanganya akili watu wa taifa la Bosnia mwanzoni mwa miaka ya 90,
  • 0:50 - 0:54
    takribani wananchi 30,000,wengi wao wakiwa raia wa kawaida,
  • 0:54 - 0:56
    walipotea,kudhaniwa kuuawa,
  • 0:56 - 0:58
    na wengine 100,000 waliuawa
  • 0:58 - 1:00
    wakati wa operesheni ya kivita
  • 1:00 - 1:01
    Wengi wao waliuawa
  • 1:01 - 1:03
    aitha siku za mwanzo za vita
  • 1:03 - 1:04
    au nyakati za mwishoni za wasiwasi,
  • 1:04 - 1:07
    upande wa umoja wa mataifa ulio salama mfano Srebrenica
  • 1:07 - 1:11
    uliposhikiliwa na jeshi la Serbia.
  • 1:11 - 1:13
    Taasisi ya uhalifu wa kimataifa
  • 1:13 - 1:14
    ilitoa namba ya hukumu
  • 1:14 - 1:17
    kwa uhalifu wa kukiuka haki za binadamu na mauaji ya kimbari.
  • 1:17 - 1:21
    Mauaji ya kimbari ni hali ya
  • 1:21 - 1:24
    kuleta ubaguzi wa rangi,kuvuruga siasa, hali ya kidini
  • 1:24 - 1:26
    au makabila
  • 1:26 - 1:29
    Kwa vile mauaji ya kimbari lengo lake ni kupoteza maisha ya watu.
  • 1:29 - 1:32
    Pia inaharibu mali zao,
  • 1:32 - 1:33
    urithi wao wa kitamaduni,
  • 1:33 - 1:37
    viashirio muhimu sana vitavyoonesha waliwahi kuwepo.
  • 1:37 - 1:39
    Mauaji ya kimbari sio kwa ajili ya kukatisha maisha ya watu tu;
  • 1:39 - 1:42
    ni hali ya kukana utambulisho.
  • 1:42 - 1:44
    Kuna ufahamu kwamba-
  • 1:44 - 1:46
    hakuna kitu kama uhalifu maridadi
  • 1:46 - 1:48
    Siku zote kutakuwa na mabaki ya wale waliofariki
  • 1:48 - 1:51
    ambayo ni imara kuliko miili yao iliyo rahisi kuharibika
  • 1:51 - 1:55
    na kumbukumbu zao ambazo zinafifia.
  • 1:55 - 1:57
    Vitu hivi vinawezwa kupatikana
  • 1:57 - 1:58
    katika baadhi ya makaburi,
  • 1:58 - 2:02
    hatua ya ukusanyaji wa vitu hivi ipo
  • 2:02 - 2:03
    katika hali ya kipekee
  • 2:03 - 2:07
    katika kutambua wale waliopotea katika mauaji,
  • 2:07 - 2:09
    mauaji ya kwanza katika udongo wa Ulaya
  • 2:09 - 2:11
    tangu wakati wa Holocaust.
  • 2:11 - 2:13
    Mwili hata mmoja hautakiwi ubaki haujapatikana
  • 2:13 - 2:15
    au kutotambuliwa.
  • 2:15 - 2:17
    Unapopatikana,
  • 2:17 - 2:20
    vile vitu vilivyokuwa na mwili huo
  • 2:20 - 2:21
    wakati wa mauaji
  • 2:21 - 2:23
    vinasafishwa kwam makini,kufanyiwa uchunguzi,
  • 2:23 - 2:26
    kuwekwa kati makundi na kisha kutunzwa.
  • 2:26 - 2:29
    Maelfu ya vitu hivi yamewekwa katika mifuko myeupe ya plastiki
  • 2:29 - 2:31
    kama ile unayoona katika tume ya uchunguzi wa uhalifu unaohusisha mauaji.
  • 2:31 - 2:34
    Vitu hivi vinatumika kawa ajili ya utambuzi wa vinasaba
  • 2:34 - 2:36
    ili kutambua wahanga,
  • 2:36 - 2:40
    lakini pia vinatumika kama uthibitisho muhimu sana katika vinasaba
  • 2:40 - 2:42
    kwenye majaribu ya mauaji yanayoendelea.
  • 2:42 - 2:45
    Wale waliookoka huwa wanaitwa mara kwa mara
  • 2:45 - 2:47
    kujaribu kutambua vitu hivi,
  • 2:47 - 2:50
    lakini kuangalia kwa macho ya kawaida ni ngumu kidogo,
  • 2:50 - 2:54
    ni hatua ambayo haina uhakika sana na inaumiza.
  • 2:54 - 2:57
    Mara baada ya wataalamu wa vinasaba, madaktari na wanasheria
  • 2:57 - 2:58
    wanapomalizana na hivi vitu
  • 2:58 - 3:01
    vinabaki yatima kwa kuachwa tu.
  • 3:01 - 3:04
    Vingi huaribiwa,amini usiamini,
  • 3:04 - 3:06
    au vinawekwa,
  • 3:06 - 3:08
    mbali ambapo haviwezi kufikiriwa tena.
  • 3:08 - 3:11
    Miaka michache iliyopita niliamua
  • 3:11 - 3:13
    kupiga picha kila kitu kilichofukuliwa
  • 3:13 - 3:15
    ili niweze kutengeneza maktaba ya picha
  • 3:15 - 3:19
    ili wale waliokoka waweze kuona kwa urahisi.
  • 3:19 - 3:23
    Kama msimulia hadithi, ningependa kurudisha kitu kwa jamii.
  • 3:23 - 3:25
    Ninapenda kwenda mbali zaidi katika kufikiri na kutenda ili kuongeza ufahamu.
  • 3:25 - 3:28
    Katika hili, mtu anaweza
  • 3:28 - 3:29
    kutambua vitu hivi
  • 3:29 - 3:32
    au picha zinaweza kubaki
  • 3:32 - 3:36
    muda mrefu sana, bila kusumbuliwa na kumbukumbu sahihi
  • 3:36 - 3:38
    ya yale yaliyotokea.
  • 3:38 - 3:40
    Kupiga picha kunahusisha kuelewa hisia za wengine,
  • 3:40 - 3:43
    na vitu hivi vinahusisha sana hisia za wengine.
  • 3:43 - 3:45
    Mimi ni kama kifaa katika swala hili,
  • 3:45 - 3:47
    mtaalamu wa vinasaba, kama ukipenda,
  • 3:47 - 3:50
    na matokeo yake ni picha ambayo ipo karibu sana
  • 3:50 - 3:52
    na kuwa nyaraka.
  • 3:52 - 3:56
    Pale watu wote waliopotea waligundulika,
  • 3:56 - 3:57
    miili yao inayooza katika makaburi yao
  • 3:57 - 4:00
    na hivi vitu vya kila siku vyote vitabaki.
  • 4:00 - 4:02
    Katika urahisi,
  • 4:02 - 4:04
    vitu hivi ni agano la mwisho
  • 4:04 - 4:05
    katika utambulisho wa wahanga,
  • 4:05 - 4:07
    ukumbusho wa mwisho ambao utadumu
  • 4:07 - 4:09
    na kuonyesha kwamba watu hawa waliwahi kuwepo.
  • 4:09 - 4:12
    Asante sana
  • 4:12 - 4:15
    (Makofi)
Title:
Vitu tutumiavyo kila siku, historia ya kusikitisha
Speaker:
Ziyah Gafic
Description:

Ziyah Gafic anapiga picha vitu tunavyotumia kila siku-saa, viatu, miwani. Lakini vitu hivi vinaonekana ni vya kawaida; vilifukuliwa kutoka katika makaburi ya watu waliokufa kutokana na vita ya Bosnia. Gafic, ambaye ni mshiriki wa TED na mkazi wa Sarajevo, amepiga picha kila kitu kilichotoka katika makaburi yale na kisha kutengeneza maktaba ya kudumu ya utambulisho wa watu waliofariki katika vita hivyo.

more » « less
Video Language:
English
Team:
closed TED
Project:
TEDTalks
Duration:
04:32

Swahili subtitles

Revisions