Jinsi ya kuokoa dunia(au wewe mwenyewe) kutokana mikutano mibaya.
-
0:01 - 0:03Pata picha hii:
-
0:03 - 0:04Ni Jumatatu asubuhi,
-
0:04 - 0:05upo ofisini,
-
0:05 - 0:07unakaa sawa kwa ajili ya kuanza siku ya kazi,
-
0:07 - 0:09na mtu uliyekutana nae wakati upo jengo la chini,
-
0:09 - 0:11anaingia kwenye kijiofisi chako
-
0:11 - 0:13na kuiba kiti chako.
-
0:13 - 0:14Hasemi neno lolote ---
-
0:14 - 0:15anaondoka nacho tu.
-
0:15 - 0:18Hakupi sababu yoyote ni kwa nini amechukua kiti chako
-
0:18 - 0:20na kuacha viti vyote vilivyopo katika jengo hilo
-
0:20 - 0:22Hatambui kwamba utahitaji kiti chako
-
0:22 - 0:24ili kukamilisha kazi siku ya leo.
-
0:24 - 0:25Hutapigania
-
0:25 - 0:28Utamfata yule mtu katika kijiofisi chake
-
0:28 - 0:30na kusema "Kwanini uchukue kiti changu?"
-
0:30 - 0:36Ni jumanne asubuhi na upo ofisini,
-
0:36 - 0:38na mualiko wa kikao unajitokeza katika kalenda yako.
-
0:38 - 0:41(Vicheko)
-
0:41 - 0:43Na ni kutoka kwa mwanamama unayemfahamu kiasi kutoka jengo la chini,
-
0:43 - 0:47na kichwa cha habari kinaongelea miradi ambayo ulishawahi kuisikia kwa ufupi tu.
-
0:47 - 0:48Lakini hakuna ajenda.
-
0:48 - 0:52Hakuna taarifa ni kwanini umealikwa katika mkutano huo.
-
0:52 - 0:56Na bado unakubali kuhudhuria mkutano huo, na unaenda.
-
0:56 - 1:00Na baada ya mkutano huu usio na maana kuisha,
-
1:00 - 1:00unarudi katika kijiofisi chako,
-
1:00 - 1:02na usimama na kusema,
-
1:02 - 1:05"Natamani ningerudishiwa masaa mawili niliyopoteza,
-
1:05 - 1:07kama ninavyotamani kurudishiwa kiti changu"
-
1:07 - 1:08(Vicheko)
-
1:08 - 1:09Kila siku, tunawaruhusu wafanyakazi wenzetu,
-
1:09 - 1:13ambao, ni watu wazuri sana,
-
1:13 - 1:15kutuibia.
-
1:15 - 1:19Na ninaongelea vitu muhimu sana zaidi ya hata samani za ofisini.
-
1:19 - 1:22Naongelea kuhusu muda. Muda wako.
-
1:22 - 1:24Kiukweli, Naamini ya kwamba
-
1:24 - 1:27tupo katikati ya janga la kiulimwengu
-
1:27 - 1:32la ugonjwa mpya ambao ni hatari sana unaofahamika kama MAS:
-
1:32 - 1:34Mindless Accept Syndrome( Ugonjwa wa kukubali jambo bila kuhoji linahusu nini).
-
1:34 - 1:36(Vicheko)
-
1:36 - 1:39Dalili za msingi za MAS
-
1:39 - 1:43ni kukubali mualiko wa kikao pale tu unaoonekana katika kalenda yako.
-
1:43 - 1:44(Vicheko)
-
1:44 - 1:48Ni jambo lisilo la hiari, baada ya hapo....
-
1:48 - 1:51"Inabidi niondoke, nachelewa kwenye kikao"(Vicheko)
-
1:51 - 1:53Vikao ni muhimu, sawa?
-
1:53 - 1:56Na umoja ni funguo ya mafanikio katika kampuni yoyote.
-
1:56 - 2:00Na kikao kinachoendeshwa vizuri kitaleta mafanikio chanya.
-
2:00 - 2:01Lakini katika utandawazi
-
2:01 - 2:04na upana wa teknolojia ya mawasiliano,
-
2:04 - 2:05vile tunavyofanya kazi
-
2:05 - 2:09kumebadilika kwa kiasi kikubwa sana katika miaka michache iliyopita.
-
2:09 - 2:12Na tumekuwa wa ovyo. (Vicheko)
-
2:12 - 2:15Na tumekuwa wa ovyo si kwa sababu watu wengine hawawezi kuongoza kikao vizuri,
-
2:15 - 2:18ni kwa sababu ya MAS,
-
2:18 - 2:22ambalo ni gonjwa tulilonalo.
-
2:22 - 2:27Nina ushahidi kwa kuonesha MAS ni janga la ulimwengu.
-
2:27 - 2:29Ngoja nikwambie ni kwanini.
-
2:29 - 2:33Miaka michache iliyopita, niliweka video Youtube, na video hiyo,
-
2:33 - 2:36Nilionyesha aina zote za mikutano ya ovyo uliyowahi hudhuria.
-
2:36 - 2:38Ni ya muda wa dakika tano,
-
2:38 - 2:41na ina kila kitu tusichopenda kuhusu mikutano mibaya.
-
2:41 - 2:44Kuna muongoza kikao asiye na wazo ni jinsi gani ya kuongoza kikao.
-
2:44 - 2:47Kuna washiriki wasio wa wazo kwanini wapo katika mkutano huo.
-
2:47 - 2:51Kila kitu kinaenda ovyo.
-
2:51 - 2:53Na kila mtu anaondoka na hasira.
-
2:53 - 2:55Inafurahisha.
-
2:55 - 2:56(Vicheko)
-
2:56 - 2:59Tuangalie kwa harakaharaka.
-
2:59 - 3:02(Video) Lengo letu leo ni kukubaliana katika pendekezo muhimu sana.
-
3:02 - 3:05Kama kundi, tunatakiwa kuamua kama---
-
3:05 - 3:05mlio
-
3:05 - 3:09Habari, nani kajiunga?
-
3:09 - 3:14Habari, ni mimi Joe. Leo nafanya kazi kutoka nyumbani.
-
3:14 - 3:16(Vicheko)
-
3:16 - 3:19Karibu Joe, asante kwa kujiunga nasi leo, ni vizuri.
-
3:19 - 3:22Nilikuwa nasema, tuna watu wengi tunaohitaji kuwa nao hapa,
-
3:22 - 3:23tuendelee
-
3:23 - 3:26na nitaanza kama ifuatavyo.
-
3:26 - 3:30Lengo letu leo ni kukubaliana katika pendekezo muhimu sana.
-
3:30 - 3:32Kama kundi, tunatakiwa kuamua kama---
-
3:32 - 3:33mlio
-
3:33 - 3:35(Vicheko)
-
3:35 - 3:37Habari, nani kajiunga nasi?
-
3:37 - 3:42Hapana? nilidhani nimesikia mlio. (Vicheko)
-
3:42 - 3:44Si jambo geni?
-
3:44 - 3:46si jambo geni kwangu pia.
-
3:46 - 3:48Wiki zilizopita baada ya kuiweka katika mtandao,
-
3:48 - 3:50watu 500,000 kutoka nchi mbalimbali,
-
3:50 - 3:52Namaanisha nchi nyingi mbalimbali
-
3:52 - 3:53waliangalia video hii.
-
3:53 - 3:57Na miaka mitatu baadaye, bado inaendelea kuangalia karibuni mara elfu moja katika kila mwezi.
-
3:57 - 3:59Inakaribia kufika milioni sasa hivi.
-
3:59 - 4:01Na kiukweli, baadhi ya makampuni makubwa duniani,
-
4:01 - 4:03ambayo huwa unayasikia ila sitayataja,
-
4:03 - 4:06wameomba ruhusa yangu ili kutumia video hii katika mafunzo ya kuajiri wafanyakazi wapya
-
4:06 - 4:11kuwafundisha waajiriwa wapya jinsi ya kutofanya mikutano katika kampuni zao.
-
4:11 - 4:12Na kama namba---
-
4:12 - 4:15watu wameangalia mara milioni na inatumika na makampuni yote haya
-
4:15 - 4:18hicho sio kigezo tosha cha kuonyesha tuna tatizo la kiulimwengu katika kundesha mikutano,
-
4:18 - 4:20kuna maoni mengi sana, maelfu
-
4:20 - 4:21yaliyotolewa katika mtandao.
-
4:21 - 4:24baada ya video kuonekana.
-
4:24 - 4:26Maelfu ya watu waliandika vitu kama,
-
4:26 - 4:27"Mungu wangu, hivyo ndivyo siku yangu ilivyokuwa leo"
-
4:27 - 4:28"Hivyo ndivyo maisha yangu ya kazini yanavyokuwa kila siku"
-
4:28 - 4:31"Haya ni maisha yangu"
-
4:31 - 4:32Bwana mmoja aliandika,
-
4:32 - 4:33"Inafurahisha kwa sababu ni kweli.
-
4:33 - 4:35Ukweli wa kuhuzunisha na kuumiza.
-
4:35 - 4:37Imenifanya nicheke mpaka nikaanza kulia.
-
4:37 - 4:39Nikalia na kulia na kulia zaidi."
-
4:39 - 4:41(Vicheko)
-
4:41 - 4:43Bwana huyu alisema,
-
4:43 - 4:48"Maisha yangu mpaka siku nastaafu au umauti utaponikuta"
-
4:48 - 4:49Kuna misemo mingi
-
4:49 - 4:51na inahuzunisha sana.
-
4:51 - 4:54Ujumbe mmoja ambao unapatikana katika maoni yote haya
-
4:54 - 4:56ni imani kwamba hatuna nguvu
-
4:56 - 4:58ya kufanya kitu chochote kingine zaidi ya kwenda kwenye vikao
-
4:58 - 5:00na kukumbana na haya mambo yanayotokea katika vikao vinavyoongozwa ovyo
-
5:00 - 5:03na kesho tena kukutana katika mikutano hiyohiyo.
-
5:03 - 5:06Lakini ukweli ni huu, si kwamba hatuna nguvu kabisa.
-
5:06 - 5:09Kiukweli, tiba ya MAS ipo katika mikono yetu.
-
5:09 - 5:11Katika vidole vyetu, kiuhalisia.
-
5:11 - 5:14Ni kitu ninachoita No MAS
-
5:14 - 5:16(Vicheko)
-
5:16 - 5:17Ambapo ninakumbuka kihispania changu wakati nipo sekondari,
-
5:17 - 5:22ilimaanisha, "Imetosha, zuia kuendelea"
-
5:22 - 5:24Na hivi ndivyo No MAS inavyofanya kazi. Ni rahisi sana.
-
5:24 - 5:28Kabla ya yote, mara nyingine utapoalikwa katika mkutano
-
5:28 - 5:30ambao hauna maelezo yoyote ya kutosha,
-
5:30 - 5:32bonyezo kitufe cha kupata maelezo ya kikao hicho!
-
5:32 - 5:35Ni sawa, unaruhusiwa na ndo maana kimewekwa pale.
-
5:35 - 5:36Ni baada ya kitufe cha kukubali kujiunga na kikao.
-
5:36 - 5:40Kipo pale kukufanya wewe usikubali moja kwa moja.
-
5:40 - 5:44Halafu, wasiliana na mtu aliyekualika katika kikao hicho.
-
5:44 - 5:46Waambie umefurahishwa sana kusaidia kazi yao
-
5:46 - 5:48waulize ni lipi lengo hasa la kikao
-
5:48 - 5:52na uwaambie unahitaji kujifunza ni vipi unaweza kusaidia katika wao kufikia malengo yao.
-
5:52 - 5:54Na kama tutafanya hivi mara kwa mara,
-
5:54 - 5:55na kufanya kwa heshima,
-
5:55 - 5:57watu wataanza kufikiria zaidi kidogo
-
5:57 - 6:00ni jinsi gani ya kuandaa mikutano kwa ufanisi zaidi.
-
6:00 - 6:03Na itakufanya kufikiria zaidi unapotaka kukubali.
-
6:03 - 6:06Watu wataanza kutuma ajenda. Fikiria!
-
6:06 - 6:10Au hawatokuwa na kikao kwa njia ya simu cha watu 12 wakiongelea kuhusu jambo
-
6:10 - 6:13wakati wanaweza kutumiana barua pepe na kumaliza ajenda kirahisi.
-
6:13 - 6:18Watu wataanza kubadili tabia zao kwa sababu umebadili ya kwako.
-
6:18 - 6:21Na watarudisha kiti chako pia. (vicheko)
-
6:21 - 6:23hakuna MAS!
-
6:23 - 6:24Asante.
-
6:24 - 6:25(Makofi).
- Title:
- Jinsi ya kuokoa dunia(au wewe mwenyewe) kutokana mikutano mibaya.
- Speaker:
- David Grady
- Description:
-
Tatizo la mikutano mibaya, isiyo fanisi na iliyo na watu wengi --- inayopelekea wafanyakazi kufanya kazi vibaya. David ana wazo ni jinsi gani ya kuliondoa tatizo hili.
- Video Language:
- English
- Team:
- closed TED
- Project:
- TEDTalks
- Duration:
- 06:34
Joachim Mangilima approved Swahili subtitles for How to save the world (or at least yourself) from bad meetings | ||
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for How to save the world (or at least yourself) from bad meetings | ||
Joachim Mangilima accepted Swahili subtitles for How to save the world (or at least yourself) from bad meetings | ||
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for How to save the world (or at least yourself) from bad meetings | ||
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for How to save the world (or at least yourself) from bad meetings | ||
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for How to save the world (or at least yourself) from bad meetings | ||
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for How to save the world (or at least yourself) from bad meetings | ||
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for How to save the world (or at least yourself) from bad meetings |