1 00:00:01,272 --> 00:00:02,649 Pata picha hii: 2 00:00:02,649 --> 00:00:03,742 Ni Jumatatu asubuhi, 3 00:00:03,742 --> 00:00:04,861 upo ofisini, 4 00:00:04,861 --> 00:00:06,615 unakaa sawa kwa ajili ya kuanza siku ya kazi, 5 00:00:06,615 --> 00:00:09,437 na mtu uliyekutana nae wakati upo jengo la chini, 6 00:00:09,437 --> 00:00:11,273 anaingia kwenye kijiofisi chako 7 00:00:11,273 --> 00:00:12,675 na kuiba kiti chako. 8 00:00:12,675 --> 00:00:13,917 Hasemi neno lolote --- 9 00:00:13,917 --> 00:00:15,305 anaondoka nacho tu. 10 00:00:15,305 --> 00:00:17,788 Hakupi sababu yoyote ni kwa nini amechukua kiti chako 11 00:00:17,788 --> 00:00:19,899 na kuacha viti vyote vilivyopo katika jengo hilo 12 00:00:19,899 --> 00:00:22,041 Hatambui kwamba utahitaji kiti chako 13 00:00:22,041 --> 00:00:23,582 ili kukamilisha kazi siku ya leo. 14 00:00:23,582 --> 00:00:24,979 Hutapigania 15 00:00:24,979 --> 00:00:27,866 Utamfata yule mtu katika kijiofisi chake 16 00:00:27,866 --> 00:00:30,215 na kusema "Kwanini uchukue kiti changu?" 17 00:00:30,215 --> 00:00:35,819 Ni jumanne asubuhi na upo ofisini, 18 00:00:35,819 --> 00:00:38,028 na mualiko wa kikao unajitokeza katika kalenda yako. 19 00:00:38,028 --> 00:00:40,753 (Vicheko) 20 00:00:40,753 --> 00:00:42,709 Na ni kutoka kwa mwanamama unayemfahamu kiasi kutoka jengo la chini, 21 00:00:42,709 --> 00:00:46,514 na kichwa cha habari kinaongelea miradi ambayo ulishawahi kuisikia kwa ufupi tu. 22 00:00:46,514 --> 00:00:48,197 Lakini hakuna ajenda. 23 00:00:48,197 --> 00:00:52,023 Hakuna taarifa ni kwanini umealikwa katika mkutano huo. 24 00:00:52,023 --> 00:00:55,889 Na bado unakubali kuhudhuria mkutano huo, na unaenda. 25 00:00:55,889 --> 00:01:00,006 Na baada ya mkutano huu usio na maana kuisha, 26 00:01:00,006 --> 00:01:00,499 unarudi katika kijiofisi chako, 27 00:01:00,499 --> 00:01:02,008 na usimama na kusema, 28 00:01:02,008 --> 00:01:04,671 "Natamani ningerudishiwa masaa mawili niliyopoteza, 29 00:01:04,671 --> 00:01:06,674 kama ninavyotamani kurudishiwa kiti changu" 30 00:01:06,674 --> 00:01:08,180 (Vicheko) 31 00:01:08,180 --> 00:01:09,328 Kila siku, tunawaruhusu wafanyakazi wenzetu, 32 00:01:09,328 --> 00:01:12,965 ambao, ni watu wazuri sana, 33 00:01:12,965 --> 00:01:14,632 kutuibia. 34 00:01:14,632 --> 00:01:18,710 Na ninaongelea vitu muhimu sana zaidi ya hata samani za ofisini. 35 00:01:18,710 --> 00:01:21,739 Naongelea kuhusu muda. Muda wako. 36 00:01:21,739 --> 00:01:24,392 Kiukweli, Naamini ya kwamba 37 00:01:24,392 --> 00:01:26,877 tupo katikati ya janga la kiulimwengu 38 00:01:26,877 --> 00:01:31,917 la ugonjwa mpya ambao ni hatari sana unaofahamika kama MAS: 39 00:01:31,917 --> 00:01:34,190 Mindless Accept Syndrome( Ugonjwa wa kukubali jambo bila kuhoji linahusu nini). 40 00:01:34,190 --> 00:01:36,084 (Vicheko) 41 00:01:36,084 --> 00:01:38,785 Dalili za msingi za MAS 42 00:01:38,785 --> 00:01:42,705 ni kukubali mualiko wa kikao pale tu unaoonekana katika kalenda yako. 43 00:01:42,705 --> 00:01:43,975 (Vicheko) 44 00:01:43,975 --> 00:01:47,643 Ni jambo lisilo la hiari, baada ya hapo.... 45 00:01:47,643 --> 00:01:50,936 "Inabidi niondoke, nachelewa kwenye kikao"(Vicheko) 46 00:01:50,936 --> 00:01:53,323 Vikao ni muhimu, sawa? 47 00:01:53,323 --> 00:01:56,269 Na umoja ni funguo ya mafanikio katika kampuni yoyote. 48 00:01:56,269 --> 00:01:59,662 Na kikao kinachoendeshwa vizuri kitaleta mafanikio chanya. 49 00:01:59,662 --> 00:02:01,420 Lakini katika utandawazi 50 00:02:01,420 --> 00:02:03,735 na upana wa teknolojia ya mawasiliano, 51 00:02:03,735 --> 00:02:05,406 vile tunavyofanya kazi 52 00:02:05,406 --> 00:02:08,635 kumebadilika kwa kiasi kikubwa sana katika miaka michache iliyopita. 53 00:02:08,635 --> 00:02:11,842 Na tumekuwa wa ovyo. (Vicheko) 54 00:02:11,842 --> 00:02:15,382 Na tumekuwa wa ovyo si kwa sababu watu wengine hawawezi kuongoza kikao vizuri, 55 00:02:15,382 --> 00:02:17,855 ni kwa sababu ya MAS, 56 00:02:17,855 --> 00:02:21,970 ambalo ni gonjwa tulilonalo. 57 00:02:21,970 --> 00:02:27,117 Nina ushahidi kwa kuonesha MAS ni janga la ulimwengu. 58 00:02:27,117 --> 00:02:28,764 Ngoja nikwambie ni kwanini. 59 00:02:28,764 --> 00:02:33,036 Miaka michache iliyopita, niliweka video Youtube, na video hiyo, 60 00:02:33,036 --> 00:02:36,234 Nilionyesha aina zote za mikutano ya ovyo uliyowahi hudhuria. 61 00:02:36,234 --> 00:02:37,893 Ni ya muda wa dakika tano, 62 00:02:37,893 --> 00:02:41,084 na ina kila kitu tusichopenda kuhusu mikutano mibaya. 63 00:02:41,084 --> 00:02:44,427 Kuna muongoza kikao asiye na wazo ni jinsi gani ya kuongoza kikao. 64 00:02:44,427 --> 00:02:46,726 Kuna washiriki wasio wa wazo kwanini wapo katika mkutano huo. 65 00:02:46,726 --> 00:02:50,688 Kila kitu kinaenda ovyo. 66 00:02:50,688 --> 00:02:53,114 Na kila mtu anaondoka na hasira. 67 00:02:53,114 --> 00:02:54,903 Inafurahisha. 68 00:02:54,903 --> 00:02:56,486 (Vicheko) 69 00:02:56,486 --> 00:02:58,638 Tuangalie kwa harakaharaka. 70 00:02:58,638 --> 00:03:02,465 (Video) Lengo letu leo ni kukubaliana katika pendekezo muhimu sana. 71 00:03:02,465 --> 00:03:04,552 Kama kundi, tunatakiwa kuamua kama--- 72 00:03:04,552 --> 00:03:04,571 mlio 73 00:03:04,571 --> 00:03:08,690 Habari, nani kajiunga? 74 00:03:08,690 --> 00:03:13,910 Habari, ni mimi Joe. Leo nafanya kazi kutoka nyumbani. 75 00:03:13,910 --> 00:03:15,800 (Vicheko) 76 00:03:15,800 --> 00:03:18,868 Karibu Joe, asante kwa kujiunga nasi leo, ni vizuri. 77 00:03:18,868 --> 00:03:21,658 Nilikuwa nasema, tuna watu wengi tunaohitaji kuwa nao hapa, 78 00:03:21,658 --> 00:03:23,292 tuendelee 79 00:03:23,292 --> 00:03:25,722 na nitaanza kama ifuatavyo. 80 00:03:25,722 --> 00:03:29,840 Lengo letu leo ni kukubaliana katika pendekezo muhimu sana. 81 00:03:29,840 --> 00:03:32,405 Kama kundi, tunatakiwa kuamua kama--- 82 00:03:32,405 --> 00:03:32,537 mlio 83 00:03:32,537 --> 00:03:35,161 (Vicheko) 84 00:03:35,161 --> 00:03:37,184 Habari, nani kajiunga nasi? 85 00:03:37,184 --> 00:03:41,993 Hapana? nilidhani nimesikia mlio. (Vicheko) 86 00:03:41,993 --> 00:03:43,629 Si jambo geni? 87 00:03:43,629 --> 00:03:45,606 si jambo geni kwangu pia. 88 00:03:45,606 --> 00:03:47,662 Wiki zilizopita baada ya kuiweka katika mtandao, 89 00:03:47,662 --> 00:03:50,463 watu 500,000 kutoka nchi mbalimbali, 90 00:03:50,463 --> 00:03:52,103 Namaanisha nchi nyingi mbalimbali 91 00:03:52,103 --> 00:03:53,287 waliangalia video hii. 92 00:03:53,287 --> 00:03:56,641 Na miaka mitatu baadaye, bado inaendelea kuangalia karibuni mara elfu moja katika kila mwezi. 93 00:03:56,641 --> 00:03:58,608 Inakaribia kufika milioni sasa hivi. 94 00:03:58,608 --> 00:04:00,616 Na kiukweli, baadhi ya makampuni makubwa duniani, 95 00:04:00,616 --> 00:04:02,526 ambayo huwa unayasikia ila sitayataja, 96 00:04:02,526 --> 00:04:06,421 wameomba ruhusa yangu ili kutumia video hii katika mafunzo ya kuajiri wafanyakazi wapya 97 00:04:06,421 --> 00:04:10,670 kuwafundisha waajiriwa wapya jinsi ya kutofanya mikutano katika kampuni zao. 98 00:04:10,670 --> 00:04:12,155 Na kama namba--- 99 00:04:12,155 --> 00:04:14,536 watu wameangalia mara milioni na inatumika na makampuni yote haya 100 00:04:14,536 --> 00:04:18,062 hicho sio kigezo tosha cha kuonyesha tuna tatizo la kiulimwengu katika kundesha mikutano, 101 00:04:18,062 --> 00:04:19,839 kuna maoni mengi sana, maelfu 102 00:04:19,839 --> 00:04:21,459 yaliyotolewa katika mtandao. 103 00:04:21,459 --> 00:04:23,647 baada ya video kuonekana. 104 00:04:23,647 --> 00:04:25,621 Maelfu ya watu waliandika vitu kama, 105 00:04:25,621 --> 00:04:27,475 "Mungu wangu, hivyo ndivyo siku yangu ilivyokuwa leo" 106 00:04:27,475 --> 00:04:27,615 "Hivyo ndivyo maisha yangu ya kazini yanavyokuwa kila siku" 107 00:04:27,615 --> 00:04:30,597 "Haya ni maisha yangu" 108 00:04:30,597 --> 00:04:31,527 Bwana mmoja aliandika, 109 00:04:31,527 --> 00:04:33,066 "Inafurahisha kwa sababu ni kweli. 110 00:04:33,066 --> 00:04:34,973 Ukweli wa kuhuzunisha na kuumiza. 111 00:04:34,973 --> 00:04:36,691 Imenifanya nicheke mpaka nikaanza kulia. 112 00:04:36,691 --> 00:04:39,441 Nikalia na kulia na kulia zaidi." 113 00:04:39,441 --> 00:04:41,073 (Vicheko) 114 00:04:41,073 --> 00:04:42,534 Bwana huyu alisema, 115 00:04:42,534 --> 00:04:47,611 "Maisha yangu mpaka siku nastaafu au umauti utaponikuta" 116 00:04:47,611 --> 00:04:49,011 Kuna misemo mingi 117 00:04:49,011 --> 00:04:50,810 na inahuzunisha sana. 118 00:04:50,810 --> 00:04:53,633 Ujumbe mmoja ambao unapatikana katika maoni yote haya 119 00:04:53,633 --> 00:04:56,174 ni imani kwamba hatuna nguvu 120 00:04:56,174 --> 00:04:58,075 ya kufanya kitu chochote kingine zaidi ya kwenda kwenye vikao 121 00:04:58,075 --> 00:05:00,453 na kukumbana na haya mambo yanayotokea katika vikao vinavyoongozwa ovyo 122 00:05:00,453 --> 00:05:02,542 na kesho tena kukutana katika mikutano hiyohiyo. 123 00:05:02,542 --> 00:05:05,683 Lakini ukweli ni huu, si kwamba hatuna nguvu kabisa. 124 00:05:05,683 --> 00:05:08,776 Kiukweli, tiba ya MAS ipo katika mikono yetu. 125 00:05:08,792 --> 00:05:10,977 Katika vidole vyetu, kiuhalisia. 126 00:05:10,977 --> 00:05:14,238 Ni kitu ninachoita No MAS 127 00:05:14,238 --> 00:05:16,468 (Vicheko) 128 00:05:16,468 --> 00:05:16,501 Ambapo ninakumbuka kihispania changu wakati nipo sekondari, 129 00:05:16,501 --> 00:05:21,657 ilimaanisha, "Imetosha, zuia kuendelea" 130 00:05:21,657 --> 00:05:24,409 Na hivi ndivyo No MAS inavyofanya kazi. Ni rahisi sana. 131 00:05:24,409 --> 00:05:27,606 Kabla ya yote, mara nyingine utapoalikwa katika mkutano 132 00:05:27,606 --> 00:05:30,453 ambao hauna maelezo yoyote ya kutosha, 133 00:05:30,453 --> 00:05:32,293 bonyezo kitufe cha kupata maelezo ya kikao hicho! 134 00:05:32,293 --> 00:05:34,743 Ni sawa, unaruhusiwa na ndo maana kimewekwa pale. 135 00:05:34,743 --> 00:05:36,252 Ni baada ya kitufe cha kukubali kujiunga na kikao. 136 00:05:36,252 --> 00:05:39,846 Kipo pale kukufanya wewe usikubali moja kwa moja. 137 00:05:39,846 --> 00:05:43,629 Halafu, wasiliana na mtu aliyekualika katika kikao hicho. 138 00:05:43,629 --> 00:05:46,215 Waambie umefurahishwa sana kusaidia kazi yao 139 00:05:46,215 --> 00:05:48,230 waulize ni lipi lengo hasa la kikao 140 00:05:48,230 --> 00:05:51,917 na uwaambie unahitaji kujifunza ni vipi unaweza kusaidia katika wao kufikia malengo yao. 141 00:05:51,917 --> 00:05:53,845 Na kama tutafanya hivi mara kwa mara, 142 00:05:53,845 --> 00:05:55,183 na kufanya kwa heshima, 143 00:05:55,183 --> 00:05:57,220 watu wataanza kufikiria zaidi kidogo 144 00:05:57,220 --> 00:05:59,682 ni jinsi gani ya kuandaa mikutano kwa ufanisi zaidi. 145 00:05:59,682 --> 00:06:02,534 Na itakufanya kufikiria zaidi unapotaka kukubali. 146 00:06:02,534 --> 00:06:05,794 Watu wataanza kutuma ajenda. Fikiria! 147 00:06:05,794 --> 00:06:09,542 Au hawatokuwa na kikao kwa njia ya simu cha watu 12 wakiongelea kuhusu jambo 148 00:06:09,542 --> 00:06:12,825 wakati wanaweza kutumiana barua pepe na kumaliza ajenda kirahisi. 149 00:06:12,825 --> 00:06:17,659 Watu wataanza kubadili tabia zao kwa sababu umebadili ya kwako. 150 00:06:17,659 --> 00:06:21,144 Na watarudisha kiti chako pia. (vicheko) 151 00:06:21,144 --> 00:06:22,519 hakuna MAS! 152 00:06:22,519 --> 00:06:23,959 Asante. 153 00:06:23,959 --> 00:06:25,106 (Makofi).