Pata picha hii: Ni Jumatatu asubuhi, upo ofisini, unakaa sawa kwa ajili ya kuanza siku ya kazi, na mtu uliyekutana nae wakati upo jengo la chini, anaingia kwenye kijiofisi chako na kuiba kiti chako. Hasemi neno lolote --- anaondoka nacho tu. Hakupi sababu yoyote ni kwa nini amechukua kiti chako na kuacha viti vyote vilivyopo katika jengo hilo Hatambui kwamba utahitaji kiti chako ili kukamilisha kazi siku ya leo. Hutapigania Utamfata yule mtu katika kijiofisi chake na kusema "Kwanini uchukue kiti changu?" Ni jumanne asubuhi na upo ofisini, na mualiko wa kikao unajitokeza katika kalenda yako. (Vicheko) Na ni kutoka kwa mwanamama unayemfahamu kiasi kutoka jengo la chini, na kichwa cha habari kinaongelea miradi ambayo ulishawahi kuisikia kwa ufupi tu. Lakini hakuna ajenda. Hakuna taarifa ni kwanini umealikwa katika mkutano huo. Na bado unakubali kuhudhuria mkutano huo, na unaenda. Na baada ya mkutano huu usio na maana kuisha, unarudi katika kijiofisi chako, na usimama na kusema, "Natamani ningerudishiwa masaa mawili niliyopoteza, kama ninavyotamani kurudishiwa kiti changu" (Vicheko) Kila siku, tunawaruhusu wafanyakazi wenzetu, ambao, ni watu wazuri sana, kutuibia. Na ninaongelea vitu muhimu sana zaidi ya hata samani za ofisini. Naongelea kuhusu muda. Muda wako. Kiukweli, Naamini ya kwamba tupo katikati ya janga la kiulimwengu la ugonjwa mpya ambao ni hatari sana unaofahamika kama MAS: Mindless Accept Syndrome( Ugonjwa wa kukubali jambo bila kuhoji linahusu nini). (Vicheko) Dalili za msingi za MAS ni kukubali mualiko wa kikao pale tu unaoonekana katika kalenda yako. (Vicheko) Ni jambo lisilo la hiari, baada ya hapo.... "Inabidi niondoke, nachelewa kwenye kikao"(Vicheko) Vikao ni muhimu, sawa? Na umoja ni funguo ya mafanikio katika kampuni yoyote. Na kikao kinachoendeshwa vizuri kitaleta mafanikio chanya. Lakini katika utandawazi na upana wa teknolojia ya mawasiliano, vile tunavyofanya kazi kumebadilika kwa kiasi kikubwa sana katika miaka michache iliyopita. Na tumekuwa wa ovyo. (Vicheko) Na tumekuwa wa ovyo si kwa sababu watu wengine hawawezi kuongoza kikao vizuri, ni kwa sababu ya MAS, ambalo ni gonjwa tulilonalo. Nina ushahidi kwa kuonesha MAS ni janga la ulimwengu. Ngoja nikwambie ni kwanini. Miaka michache iliyopita, niliweka video Youtube, na video hiyo, Nilionyesha aina zote za mikutano ya ovyo uliyowahi hudhuria. Ni ya muda wa dakika tano, na ina kila kitu tusichopenda kuhusu mikutano mibaya. Kuna muongoza kikao asiye na wazo ni jinsi gani ya kuongoza kikao. Kuna washiriki wasio wa wazo kwanini wapo katika mkutano huo. Kila kitu kinaenda ovyo. Na kila mtu anaondoka na hasira. Inafurahisha. (Vicheko) Tuangalie kwa harakaharaka. (Video) Lengo letu leo ni kukubaliana katika pendekezo muhimu sana. Kama kundi, tunatakiwa kuamua kama--- mlio Habari, nani kajiunga? Habari, ni mimi Joe. Leo nafanya kazi kutoka nyumbani. (Vicheko) Karibu Joe, asante kwa kujiunga nasi leo, ni vizuri. Nilikuwa nasema, tuna watu wengi tunaohitaji kuwa nao hapa, tuendelee na nitaanza kama ifuatavyo. Lengo letu leo ni kukubaliana katika pendekezo muhimu sana. Kama kundi, tunatakiwa kuamua kama--- mlio (Vicheko) Habari, nani kajiunga nasi? Hapana? nilidhani nimesikia mlio. (Vicheko) Si jambo geni? si jambo geni kwangu pia. Wiki zilizopita baada ya kuiweka katika mtandao, watu 500,000 kutoka nchi mbalimbali, Namaanisha nchi nyingi mbalimbali waliangalia video hii. Na miaka mitatu baadaye, bado inaendelea kuangalia karibuni mara elfu moja katika kila mwezi. Inakaribia kufika milioni sasa hivi. Na kiukweli, baadhi ya makampuni makubwa duniani, ambayo huwa unayasikia ila sitayataja, wameomba ruhusa yangu ili kutumia video hii katika mafunzo ya kuajiri wafanyakazi wapya kuwafundisha waajiriwa wapya jinsi ya kutofanya mikutano katika kampuni zao. Na kama namba--- watu wameangalia mara milioni na inatumika na makampuni yote haya hicho sio kigezo tosha cha kuonyesha tuna tatizo la kiulimwengu katika kundesha mikutano, kuna maoni mengi sana, maelfu yaliyotolewa katika mtandao. baada ya video kuonekana. Maelfu ya watu waliandika vitu kama, "Mungu wangu, hivyo ndivyo siku yangu ilivyokuwa leo" "Hivyo ndivyo maisha yangu ya kazini yanavyokuwa kila siku" "Haya ni maisha yangu" Bwana mmoja aliandika, "Inafurahisha kwa sababu ni kweli. Ukweli wa kuhuzunisha na kuumiza. Imenifanya nicheke mpaka nikaanza kulia. Nikalia na kulia na kulia zaidi." (Vicheko) Bwana huyu alisema, "Maisha yangu mpaka siku nastaafu au umauti utaponikuta" Kuna misemo mingi na inahuzunisha sana. Ujumbe mmoja ambao unapatikana katika maoni yote haya ni imani kwamba hatuna nguvu ya kufanya kitu chochote kingine zaidi ya kwenda kwenye vikao na kukumbana na haya mambo yanayotokea katika vikao vinavyoongozwa ovyo na kesho tena kukutana katika mikutano hiyohiyo. Lakini ukweli ni huu, si kwamba hatuna nguvu kabisa. Kiukweli, tiba ya MAS ipo katika mikono yetu. Katika vidole vyetu, kiuhalisia. Ni kitu ninachoita No MAS (Vicheko) Ambapo ninakumbuka kihispania changu wakati nipo sekondari, ilimaanisha, "Imetosha, zuia kuendelea" Na hivi ndivyo No MAS inavyofanya kazi. Ni rahisi sana. Kabla ya yote, mara nyingine utapoalikwa katika mkutano ambao hauna maelezo yoyote ya kutosha, bonyezo kitufe cha kupata maelezo ya kikao hicho! Ni sawa, unaruhusiwa na ndo maana kimewekwa pale. Ni baada ya kitufe cha kukubali kujiunga na kikao. Kipo pale kukufanya wewe usikubali moja kwa moja. Halafu, wasiliana na mtu aliyekualika katika kikao hicho. Waambie umefurahishwa sana kusaidia kazi yao waulize ni lipi lengo hasa la kikao na uwaambie unahitaji kujifunza ni vipi unaweza kusaidia katika wao kufikia malengo yao. Na kama tutafanya hivi mara kwa mara, na kufanya kwa heshima, watu wataanza kufikiria zaidi kidogo ni jinsi gani ya kuandaa mikutano kwa ufanisi zaidi. Na itakufanya kufikiria zaidi unapotaka kukubali. Watu wataanza kutuma ajenda. Fikiria! Au hawatokuwa na kikao kwa njia ya simu cha watu 12 wakiongelea kuhusu jambo wakati wanaweza kutumiana barua pepe na kumaliza ajenda kirahisi. Watu wataanza kubadili tabia zao kwa sababu umebadili ya kwako. Na watarudisha kiti chako pia. (vicheko) hakuna MAS! Asante. (Makofi).