Return to Video

Tunawezaje kupima umbali angani? - Yuan-Sen Ting

  • 0:07 - 0:10
    Mwanga ndio kitu kilicho na kasi zaidi
    tunalojua.
  • 0:10 - 0:13
    Lina kasi sana tunapima umbali mkubwa sana
  • 0:13 - 0:16
    kutumia muda ambao mwanga hutumia
    kuisafiri.
  • 0:16 - 0:20
    Kwa mwaka mmoja, mwanga husafiri takriban
    maili bilioni sita,
  • 0:20 - 0:23
    umbali tunaoita mwaka mmoja wa mwanga.
  • 0:23 - 0:25
    Kukupa wazo la umbali huu,
  • 0:25 - 0:29
    mwezi, lililowachukua wanaanga wa Apollo
    siku nne kuifikia,
  • 0:29 - 0:32
    ni sekundi moja tu la mwanga kutoka dunia.
  • 0:32 - 0:37
    Wakati huo huo, nyota lililo karibu
    kupita jua letu ni Proxima Centauri,
  • 0:37 - 0:40
    umbali wa miaka ya mwanga 4.24.
  • 0:40 - 0:44
    Milky Way yetu iko kwenye mpango wa
    miaka ya mwanga 100,000 toka upande mmoja.
  • 0:44 - 0:47
    Galaksi iliyo karibu sana na yetu,
    Andromeda,
  • 0:47 - 0:50
    ni umbali wa takriban miaka ya mwanga
    millioni 2.5
  • 0:50 - 0:53
    Anga una upana mkubwa kushangaza.
  • 0:53 - 0:57
    Lakini ngoja, tuanjuaje ubali wa nyota na
    magalaksi?
  • 0:57 - 1:01
    Ata hivyo, tunapotazama anga,
    tuna mtazamo wa mielekeo miwili.
  • 1:01 - 1:05
    Ukielekeza kidole chako kwa nyota moja,
    huwezi kujua umbali wa nyota hio,
  • 1:05 - 1:09
    kwa hivyo wanaastrofysik wanajuaje?
  • 1:09 - 1:11
    Kwa vitu vilivyo karibu sana,
  • 1:11 - 1:15
    tunaweza kutumia dhana inayoitwa
    "trigonometric parallax".
  • 1:15 - 1:17
    Wazo hili ni rahisi sana.
  • 1:17 - 1:18
    Tufanye jaribio.
  • 1:18 - 1:21
    Elekeza gumba lako na ufumbe jicho lako
    la kushoto.
  • 1:21 - 1:25
    Sasa, fumbua jicho lako la kushoto na
    ufumbe jicho lako la kulia.
  • 1:25 - 1:27
    Itaonekana ni kama gumba lako limesonga,
  • 1:27 - 1:31
    wakati ambapo vitu vingine vilivyo mbali
    kwenye usuli vimebaki pale pale.
  • 1:31 - 1:34
    Wazo hilo linatumika tunapotazama nyota,
  • 1:34 - 1:38
    lakini nyota za mbali ziko na umbali
    mkubwa sana kuliko mkono wako,
  • 1:38 - 1:40
    na dunia sio kubwa sana,
  • 1:40 - 1:43
    kwa hivyo hata kama ungekuwa na darubini
    tofauti kwenye ikweta,
  • 1:43 - 1:46
    huautaona mbadiliko mkubwa wa nafasi.
  • 1:46 - 1:51
    Badala ya hivyo, tunatazama mabadiliko ya
    msimamo wa nyota baada ya miezi sita,
  • 1:51 - 1:56
    msimamo nusu wa mzunguko mmoja wa dunia
    kwa jua.
  • 1:56 - 1:59
    Tunapohesabu misimamo wa nyota kwenye
    msimu wa kiangazi,
  • 1:59 - 2:03
    na tena kwenye msimu wa majira ya baridi,
    ni kama kutazama na jicho lako jingine.
  • 2:03 - 2:05
    Nyota za karibu zinaonekana zimesongea
    kwenye usuli
  • 2:05 - 2:08
    wa nyota na galaksi na nyota zilizo mbali.
  • 2:08 - 2:13
    Lakini mbinu hii inatumika kwa vitu
    vilivyo chini ya miaka ya mwanga elfu.
  • 2:13 - 2:16
    Kupita galaksi yetu,
    umbali ni mkubwa sana
  • 2:16 - 2:21
    kiasi cha parallax ni ndogo sana
    kuchunguza na vyombo vyetu vyovyote.
  • 2:21 - 2:24
    Kwa hivyo kwa wakati huu inabidi tutumie
    mbinu nyingine
  • 2:24 - 2:27
    kutumia viashiria tunavyoita
    mishumaa ya kiwangogezi.
  • 2:27 - 2:32
    mishumaa ya kiwangogezi ni vile vitu
    ambavyo mwangaza wao
  • 2:32 - 2:34
    tunaujua vizuri sana.
  • 2:34 - 2:37
    Kwa mfano, kama unaujua mwangaza wa
    taa lako,
  • 2:37 - 2:41
    na umuulize rafiki yako alichukue hilo taa
    na atembee mbali na wewe,
  • 2:41 - 2:44
    unajua kiasi cha mwangaza utakayopata
    kutoka rafiki yako
  • 2:44 - 2:47
    itapungua na umbali.
  • 2:47 - 2:50
    Kwa hivyo kufananisha kiasi cha
    mwanga utakayopata
  • 2:50 - 2:52
    na mwangaza wa taa ile,
  • 2:52 - 2:55
    unaweza kujua umbali wa rafiki yako.
  • 2:55 - 2:58
    Kwa somo la falaki, taa lako linakua
    aina spesheli ya nyota
  • 2:58 - 3:01
    inayoitwa "cepheid variable".
  • 3:01 - 3:03
    Nyota hizi hazina msimamo wa kindani,
  • 3:03 - 3:07
    kama baluni inayofutuka na kutoa hewa.
  • 3:07 - 3:11
    Na kwa ajili kufutuka na kupoteza hewa
    inarekebisha mwangaza wao,
  • 3:11 - 3:15
    tunaweza kuhesabu mwanga wao kwa kuhesabu
    muda wa mzunguko huo,
  • 3:15 - 3:19
    na nyota zilizo na mwanga nyingi na
    zinazobadilika polepole.
  • 3:19 - 3:22
    Kwa kufananisha mwangaza wa nyota hizi
  • 3:22 - 3:24
    kwa mwangaza tuliohesabu kwa mbinu hii,
  • 3:24 - 3:27
    tunagundua umbali wao.
  • 3:27 - 3:30
    Kwa bahati mbaya, huu sio mwisho
    wa hadithi.
  • 3:30 - 3:35
    Tunaweza kutazama nyota zilizo takriban
    miaka milioni arubaini ya nyota pekee,
  • 3:35 - 3:38
    Baada ya hapo, hazionekani vizuri.
  • 3:38 - 3:41
    Kwa bahati nzuri tunayo aina nyingine ya
    mshumaa:
  • 3:41 - 3:44
    ya umaarufu aina ya "1a supernova".
  • 3:44 - 3:50
    "Supernovae", milipuko mikubwa ndio moja
    wa njia ambazo nyota hufa.
  • 3:50 - 3:52
    Milipuko hii ina mwangaza sana,
  • 3:52 - 3:55
    inashinda mwangaza wa galaksi zilipo.
  • 3:55 - 3:58
    Kwa hivyo tunaposhindwa kuona nyota
    moja-moja ya galaksi,
  • 3:58 - 4:01
    bado tunaweza kuona "supernovae"
    zinapotokea.
  • 4:01 - 4:05
    Na aina ya "type 1a supernovae" inaweza
    kutumika kama mishumaa
  • 4:05 - 4:09
    kwa ajili zilizo na mwanga mkubwa sana
    hufifia polepole kushinda zile dhaifu.
  • 4:09 - 4:11
    Kwa kuelewa uhusiano huu
  • 4:11 - 4:13
    kati ya mwanga na kiwango cha kufifia,
  • 4:13 - 4:16
    tunaweza kutumia "supernovae"kupata umbali
  • 4:16 - 4:19
    wa bilioni kadhaa ya
    miaka ya mwanga.
  • 4:19 - 4:24
    Lakini ni nini umuhumu wa kutazama vitu
    vilivyo mbali nasi?
  • 4:24 - 4:27
    Basi kumbuka kasi ambao mwangaza husafiri.
  • 4:27 - 4:31
    Kwa mfano, mwangaza wa jua unachukua
    dakika nane kutufikia,
  • 4:31 - 4:37
    kumaanisha kuwa mwangaza tunaouona sasa
    hivi ni picha ya jua dakika 8 zilizopita
  • 4:37 - 4:38
    Unapoiangalia "Big Dipper",
  • 4:38 - 4:42
    unaangalia jinsi ilivyokuwa
    miaka 80 iliyopita.
  • 4:42 - 4:43
    Na galaksi zisizoonekana
    vyema?
  • 4:43 - 4:46
    Zina umbali wa mamilioni ya miaka
    ya mwangaza .
  • 4:46 - 4:49
    Imezichukua mamilioni ya miaka kutufikia.
  • 4:49 - 4:55
    Kwa hivyo ulimwengu wenyewe kwa njia, ina
    mashine ya wakati.
  • 4:55 - 4:59
    Tunapotazama mbali zaidi,
    tunagundua ulimwengu mchanga zaidi.
  • 4:59 - 5:02
    Wanaastrofysiks hujaribu kusoma historia
    ya ulimwengu,
  • 5:02 - 5:06
    na kugundua lini na wapi tunapotoka.
  • 5:06 - 5:11
    Ulimwengu unaendelea kututumia habari
    kwa njia ya mwangaza.
  • 5:11 - 5:14
    Kilichobaki ni sisi kuisimbua.
Title:
Tunawezaje kupima umbali angani? - Yuan-Sen Ting
Description:

Anagalia somo lote hapa: http://ed.ted.com/lessons/how-do-we-measure-distances-in-space-yuan-sen-ting

Tunapoangalia anga, tunaona muonekano wa usawa. Sasa je wanaanga wanajuaje umbali wa nyota kutoka duniani? Yuan-Sen Ting anatuonyesha jinsi vitu kama mishumaa vinavyoweza kusaidia kupima umbali wa vitu vilivyo mbali sana kutoka duniani.

Somo na Yuna-Sen Ting. Michoro na TED-Ed.

more » « less
Video Language:
English
Team:
closed TED
Project:
TED-Ed
Duration:
05:30

Swahili subtitles

Revisions