Siri 8 za mafanikio
-
0:00 - 0:03Huu ni mjadala wa kweli wa masaa mawili nilioutoa kwa wanafunzi wa sekondari,
-
0:03 - 0:05unakatiza kwa dakika tatu.
-
0:05 - 0:07Na yote yalianza siku moja nikiwa kwenye ndege, nikielekea TED,
-
0:07 - 0:09miaka saba iliyopita.
-
0:09 - 0:13Na katika siti iIiyopo pembeni yangu
alikuwapo mwanafunzi wa sekondari, kijana, -
0:13 - 0:15alitokea katika familia masikini sana.
-
0:15 - 0:18Na alitaka kujitengenezea maisha,
-
0:18 - 0:20akaniuliza swali rahisi.
-
0:20 - 0:22Alisema, "Ni nini husababisha mafanikio?"
-
0:22 - 0:23Na nilijisikia vibaya sana,
-
0:23 - 0:26kwa sababu sikuweza kumpa jibu zuri.
-
0:26 - 0:28Hivyo nilitoka kwenye ndege, na kuja TED.
-
0:28 - 0:32Na nikafikiri, lahaula, niko miongoni mwa watu wenye mafanikio!
-
0:32 - 0:34Kwa nini nisiwaulize wao
nini kiliwasaidia kufanikiwa, -
0:34 - 0:36na kuwaelimisha watoto?
-
0:37 - 0:40Hivyo, miaka saba,
mahojiano 500 baadaye, -
0:40 - 0:43nitawaambia nini hasa hupelekea mafanikio
-
0:43 - 0:45yanayowasukuma wanaTED.
-
0:45 - 0:47Na jambo la kwanza ni shauku.
-
0:48 - 0:50Freeman Thomas anasema,
"Ninaendeshwa na shauku yangu." -
0:51 - 0:53WanaTED hufanya yote kwa sababu ya upendo;
hawafanyi kwa ajili ya fedha. -
0:53 - 0:57Carol Coletta anasema, "Ningelipa
mtu kufanya ninachofanya. " -
0:57 - 0:58Na jambo la kushangaza ni:
-
0:58 - 1:00ukifanya kwa upendo,
pesa huja hata hivyo. -
1:01 - 1:04Kazi! Rupert Murdoch aliniambia, "Yote ni kazi ngumu.
-
1:04 - 1:07Hakuna kitu kinakuja kwa urahisi.
Lakini ninaifurahia kazi yangu. " -
1:07 - 1:10Amesema furaha? Rupert? Ndiyo!
-
1:10 - 1:11(Vicheko)
-
1:12 - 1:14WanaTED hufurahia kazi zao.
Na hufanya kazi kwa bidii. -
1:14 - 1:17Niligundua, sio workaholics. Ni workafrolics.
-
1:17 - 1:19(Vicheko)
-
1:19 - 1:20Vyema!
-
1:20 - 1:21(Makofi)
-
1:21 - 1:24Alex Garden anasema, "Ili kufanikiwa, weka jitihada katika kitu kimoja
-
1:24 - 1:26na kuwa mtaalamu kwenye hilo."
-
1:26 - 1:28Hakuna mazingaombwe;
ni mazoezi, mazoezi, mazoezi. -
1:28 - 1:29Na ni lengo.
-
1:30 - 1:31Norman Jewison aliniambia,
-
1:31 - 1:34"Nadhani huhusiana na kujishughulisha na jambo moja. "
-
1:35 - 1:36Na kukazana!
-
1:36 - 1:38Daudi Gallo anasema, "Jisukume.
-
1:38 - 1:41Kimwili, kiakili,
unapaswa kujisukuma, kujisukuma, kujisukuma." -
1:41 - 1:44Unahitaji kujisukuma kutoka katika aibu na mashaka.
-
1:44 - 1:46Goldie Hawn anasema,
"Siku zote nilikuwa na mashaka. -
1:46 - 1:48Sikuwa na ujuzi wakutosha;
Sikukuwa na kipaji cha kutosha. -
1:48 - 1:50Sikufikiri ningeweza kufanikiwa."
-
1:50 - 1:52Daima si rahisi kujisukuma,
-
1:52 - 1:54na ndiyo maana tuna mama.
-
1:54 - 1:55(Vicheko)
-
1:55 - 1:57(Makofi)
-
1:57 - 2:00Frank Gehry aliniambia,
-
2:00 - 2:01"Mama yangu alinisukuma."
-
2:01 - 2:03(Vicheko)
-
2:03 - 2:04Tumikia!
-
2:04 - 2:07Sherwin Nuland anasema,
"Ilikuwa ni fursa kutumikia kama daktari." -
2:08 - 2:10Watoto wengi wanataka kuwa mamilionea.
-
2:10 - 2:11Jambo la kwanza ninalosema ni:
-
2:12 - 2:13"Sawa, vizuri huwezi kujihudumia mwenyewe;
-
2:13 - 2:16unapaswa kutumikia wengine
kitu cha thamani. -
2:16 - 2:18Kwa sababu hiyo ndiyo njia
watu hupata utajiri. " -
2:19 - 2:20Mawazo!
-
2:20 - 2:23MwanaTED Bill Gates anasema, "Nilikuwa na wazo:
-
2:23 - 2:26kuanzisha kampuni ya kwanza ya programu za mikro-kompyuta."
-
2:26 - 2:28Ningependa kusema ni wazo zuri sana.
-
2:28 - 2:31Na hakuna miujiza katika ubunifu
wa mawazo mapya -- -
2:31 - 2:33ni kufanya baadhi ya mambo rahisi sana.
-
2:33 - 2:35Na ninatoa ushahidi mwingi.
-
2:35 - 2:36Stahimili!
-
2:37 - 2:38Joe Kraus anasema,
-
2:38 - 2:40"Ustahimilifu ni sababu namba
moja ya mafanikio yetu. " -
2:41 - 2:44Unahitaji kustahimili unapofeli. Unahitaji kustahimili misukosuko!
-
2:44 - 2:48Ambayo ni "Kukosolewa,
Kukataliwa, Watu ovyo na Presha." -
2:48 - 2:51(Vicheko)
-
2:51 - 2:54Hivyo, jibu kwa swali hili ni rahisi:
-
2:54 - 2:57Lipa dola 4,000 na uje kwenye TED.
-
2:57 - 2:58(Vicheko)
-
2:58 - 3:01Au ukishindwa hilo, fanya
mambo haya nane - na niamini, -
3:01 - 3:04haya ni mambo makuu nane
ambayo huleta mafanikio. -
3:04 - 3:07Asanteni wanaTED
kwa mahojiano yenu yote! -
3:07 - 3:10(Makofi)
- Title:
- Siri 8 za mafanikio
- Speaker:
- Richard St. John
- Description:
-
Kwa nini watu wanafanikiwa? Je, ni kwa sababu wana akili? Au ni bahati tu? Wala. Mchambuzi Richard St. John anatoa muhtasari wa miaka ya mahojiano katika dakika 3 kuhusu siri halisi za mafanikio.
- Video Language:
- English
- Team:
- closed TED
- Project:
- TEDTalks
- Duration:
- 03:13
Nelson Simfukwe approved Swahili subtitles for 8 secrets of success | ||
Nelson Simfukwe accepted Swahili subtitles for 8 secrets of success | ||
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for 8 secrets of success | ||
Sophia Mwema edited Swahili subtitles for 8 secrets of success | ||
Sophia Mwema edited Swahili subtitles for 8 secrets of success | ||
Sophia Mwema edited Swahili subtitles for 8 secrets of success | ||
Sophia Mwema edited Swahili subtitles for 8 secrets of success | ||
Sophia Mwema edited Swahili subtitles for 8 secrets of success |