1 00:00:00,000 --> 00:00:03,321 Huu ni mjadala wa kweli wa masaa mawili nilioutoa kwa wanafunzi wa sekondari, 2 00:00:03,345 --> 00:00:04,596 unakatiza kwa dakika tatu. 3 00:00:04,620 --> 00:00:07,261 Na yote yalianza siku moja nikiwa kwenye ndege, nikielekea TED, 4 00:00:07,285 --> 00:00:08,579 miaka saba iliyopita. 5 00:00:08,603 --> 00:00:12,976 Na katika siti iIiyopo pembeni yangu alikuwapo mwanafunzi wa sekondari, kijana, 6 00:00:13,000 --> 00:00:15,007 alitokea katika familia masikini sana. 7 00:00:15,483 --> 00:00:17,976 Na alitaka kujitengenezea maisha, 8 00:00:18,000 --> 00:00:20,039 akaniuliza swali rahisi. 9 00:00:20,063 --> 00:00:22,008 Alisema, "Ni nini husababisha mafanikio?" 10 00:00:22,032 --> 00:00:23,411 Na nilijisikia vibaya sana, 11 00:00:23,435 --> 00:00:25,896 kwa sababu sikuweza kumpa jibu zuri. 12 00:00:25,920 --> 00:00:27,976 Hivyo nilitoka kwenye ndege, na kuja TED. 13 00:00:28,000 --> 00:00:31,730 Na nikafikiri, lahaula, niko miongoni mwa watu wenye mafanikio! 14 00:00:31,754 --> 00:00:34,365 Kwa nini nisiwaulize wao nini kiliwasaidia kufanikiwa, 15 00:00:34,389 --> 00:00:36,103 na kuwaelimisha watoto? 16 00:00:36,817 --> 00:00:40,426 Hivyo, miaka saba, mahojiano 500 baadaye, 17 00:00:40,450 --> 00:00:43,390 nitawaambia nini hasa hupelekea mafanikio 18 00:00:43,414 --> 00:00:44,779 yanayowasukuma wanaTED. 19 00:00:45,367 --> 00:00:46,976 Na jambo la kwanza ni shauku. 20 00:00:47,787 --> 00:00:50,319 Freeman Thomas anasema, "Ninaendeshwa na shauku yangu." 21 00:00:50,763 --> 00:00:53,223 WanaTED hufanya yote kwa sababu ya upendo; hawafanyi kwa ajili ya fedha. 22 00:00:53,247 --> 00:00:56,731 Carol Coletta anasema, "Ningelipa mtu kufanya ninachofanya. " 23 00:00:56,755 --> 00:00:58,166 Na jambo la kushangaza ni: 24 00:00:58,190 --> 00:01:00,381 ukifanya kwa upendo, pesa huja hata hivyo. 25 00:01:00,866 --> 00:01:03,976 Kazi! Rupert Murdoch aliniambia, "Yote ni kazi ngumu. 26 00:01:04,000 --> 00:01:07,083 Hakuna kitu kinakuja kwa urahisi. Lakini ninaifurahia kazi yangu. " 27 00:01:07,107 --> 00:01:09,977 Amesema furaha? Rupert? Ndiyo! 28 00:01:10,001 --> 00:01:11,477 (Vicheko) 29 00:01:11,501 --> 00:01:14,247 WanaTED hufurahia kazi zao. Na hufanya kazi kwa bidii. 30 00:01:14,271 --> 00:01:17,224 Niligundua, sio workaholics. Ni workafrolics. 31 00:01:17,248 --> 00:01:18,838 (Vicheko) 32 00:01:18,862 --> 00:01:19,919 Vyema! 33 00:01:19,943 --> 00:01:20,944 (Makofi) 34 00:01:20,968 --> 00:01:24,314 Alex Garden anasema, "Ili kufanikiwa, weka jitihada katika kitu kimoja 35 00:01:24,338 --> 00:01:25,584 na kuwa mtaalamu kwenye hilo." 36 00:01:25,608 --> 00:01:28,450 Hakuna mazingaombwe; ni mazoezi, mazoezi, mazoezi. 37 00:01:28,474 --> 00:01:29,493 Na ni lengo. 38 00:01:29,517 --> 00:01:31,251 Norman Jewison aliniambia, 39 00:01:31,275 --> 00:01:34,267 "Nadhani huhusiana na kujishughulisha na jambo moja. " 40 00:01:34,773 --> 00:01:35,838 Na kukazana! 41 00:01:36,235 --> 00:01:38,223 Daudi Gallo anasema, "Jisukume. 42 00:01:38,247 --> 00:01:40,889 Kimwili, kiakili, unapaswa kujisukuma, kujisukuma, kujisukuma." 43 00:01:40,913 --> 00:01:43,524 Unahitaji kujisukuma kutoka katika aibu na mashaka. 44 00:01:43,548 --> 00:01:45,976 Goldie Hawn anasema, "Siku zote nilikuwa na mashaka. 45 00:01:46,000 --> 00:01:48,096 Sikuwa na ujuzi wakutosha; Sikukuwa na kipaji cha kutosha. 46 00:01:48,120 --> 00:01:49,663 Sikufikiri ningeweza kufanikiwa." 47 00:01:50,264 --> 00:01:52,303 Daima si rahisi kujisukuma, 48 00:01:52,327 --> 00:01:54,415 na ndiyo maana tuna mama. 49 00:01:54,439 --> 00:01:55,439 (Vicheko) 50 00:01:55,439 --> 00:01:57,000 (Makofi) 51 00:01:57,000 --> 00:01:59,976 Frank Gehry aliniambia, 52 00:02:00,000 --> 00:02:01,370 "Mama yangu alinisukuma." 53 00:02:01,394 --> 00:02:02,608 (Vicheko) 54 00:02:02,632 --> 00:02:03,648 Tumikia! 55 00:02:04,427 --> 00:02:07,466 Sherwin Nuland anasema, "Ilikuwa ni fursa kutumikia kama daktari." 56 00:02:08,093 --> 00:02:10,203 Watoto wengi wanataka kuwa mamilionea. 57 00:02:10,227 --> 00:02:11,477 Jambo la kwanza ninalosema ni: 58 00:02:11,501 --> 00:02:13,403 "Sawa, vizuri huwezi kujihudumia mwenyewe; 59 00:02:13,427 --> 00:02:15,664 unapaswa kutumikia wengine kitu cha thamani. 60 00:02:15,688 --> 00:02:18,225 Kwa sababu hiyo ndiyo njia watu hupata utajiri. " 61 00:02:19,074 --> 00:02:20,099 Mawazo! 62 00:02:20,123 --> 00:02:22,976 MwanaTED Bill Gates anasema, "Nilikuwa na wazo: 63 00:02:23,000 --> 00:02:25,976 kuanzisha kampuni ya kwanza ya programu za mikro-kompyuta." 64 00:02:26,000 --> 00:02:27,976 Ningependa kusema ni wazo zuri sana. 65 00:02:28,000 --> 00:02:30,976 Na hakuna miujiza katika ubunifu wa mawazo mapya -- 66 00:02:31,000 --> 00:02:33,335 ni kufanya baadhi ya mambo rahisi sana. 67 00:02:33,359 --> 00:02:34,976 Na ninatoa ushahidi mwingi. 68 00:02:35,291 --> 00:02:36,405 Stahimili! 69 00:02:36,799 --> 00:02:37,800 Joe Kraus anasema, 70 00:02:37,824 --> 00:02:40,418 "Ustahimilifu ni sababu namba moja ya mafanikio yetu. " 71 00:02:40,832 --> 00:02:44,374 Unahitaji kustahimili unapofeli. Unahitaji kustahimili misukosuko! 72 00:02:44,398 --> 00:02:47,913 Ambayo ni "Kukosolewa, Kukataliwa, Watu ovyo na Presha." 73 00:02:47,937 --> 00:02:50,703 (Vicheko) 74 00:02:50,727 --> 00:02:54,446 Hivyo, jibu kwa swali hili ni rahisi: 75 00:02:54,470 --> 00:02:56,595 Lipa dola 4,000 na uje kwenye TED. 76 00:02:56,619 --> 00:02:57,812 (Vicheko) 77 00:02:57,836 --> 00:03:00,574 Au ukishindwa hilo, fanya mambo haya nane - na niamini, 78 00:03:00,598 --> 00:03:03,818 haya ni mambo makuu nane ambayo huleta mafanikio. 79 00:03:03,842 --> 00:03:06,561 Asanteni wanaTED kwa mahojiano yenu yote! 80 00:03:06,585 --> 00:03:09,585 (Makofi)