Ukweli 12 niliojifunza kupitia maisha na uandishi
-
0:01 - 0:04Chumba cha mjukuu wangu mwenye miaka saba kipo karibu na changu
-
0:05 - 0:06mara nyingi huamka asubuhi
-
0:06 - 0:08na kusema,
-
0:08 - 0:10"Unajua, leo inaweza kuwa siku bora kuliko zote. "
-
0:11 - 0:13Na mara nyingine, usiku wa manane,
-
0:13 - 0:16huita kwa sauti za woga
-
0:16 - 0:19"Nana, utaumwa na kufa siku moja?"
-
0:19 - 0:24Nadhani hili linasema mengi kwangu na watu wengi ninaowajua,
-
0:24 - 0:27kwamba sisi ni mchanganyiko
wa matarajio yenye furaha -
0:27 - 0:28na hofu.
-
0:29 - 0:33Hivyo, siku chache kabla ya kutimiza miaka 61, nilitafakari
-
0:33 - 0:37nikaamua kukusanya orodha ya kila kitu ninachojua.
-
0:38 - 0:41Kuna ukweli mchache sana katika utamaduni wetu,
-
0:41 - 0:44na ni vizuri tuwe na uhakika na mambo machache.
-
0:45 - 0:48Kwa mfano, umri wangu sio 47 tena,
-
0:49 - 0:52Ingawa ndio umri ninaojisikia,
-
0:52 - 0:54au umri ningependa kufikiri niko.
-
0:55 - 0:58Rafiki yangu Paulo alisema katika miaka yake ya 70
-
0:58 - 1:01kwamba alihisi kama kijana mwenye matatizo mengi tu.
-
1:01 - 1:05(Vicheko)
-
1:05 - 1:08Nafsi yetu ya kweli ipo nje ya muda na sehemu
-
1:08 - 1:09lakini nikiangalia nyaraka,
-
1:09 - 1:13Naweza, kwa kweli, kuona kwamba nilizaliwa mwaka wa 1954
-
1:13 - 1:16Hisia zangu binafsi zipo nje ya muda na sehemu.
-
1:16 - 1:18Haina umri.
-
1:18 - 1:22Nina kila umri ambao nimewahi kuwa,na wewe pia,
-
1:22 - 1:24Ingawa siwezi kuepuka kusema,
-
1:24 - 1:27kwamba ingesaidia kama nisingefuata
-
1:27 - 1:30kanuni za huduma ya ngozi za miaka ya 60,
-
1:30 - 1:33ambayo ilihusisha kuota jua kama iwezekanavyo
-
1:33 - 1:36nikijisiliba mafuta ya mtoto
-
1:36 - 1:40na kumeremeta chini ya foii ya aluminium
-
1:40 - 1:42(Vicheko)
-
1:42 - 1:44Nilijisikia uhuru sana, ingawa,
nilbidi kuutizama ukweli -
1:44 - 1:48kwamba sikuwa tena katika miaka ya mwisho ya rika la kati,
-
1:48 - 1:52hivyo niliamua kuandika
kila kitu nilichojua. -
1:52 - 1:55Siku hizi watu wamejisikia wameelemewa,
-
1:55 - 1:58na huniuliza ukweli ni upi.
-
1:58 - 2:05Hivyo, natumaini orodha ya vitu ninavzo fahamu kwau fasaha
-
2:05 - 2:08itatoa misingi ya uendeshaji
-
2:08 - 2:11kwa mtu yeyote anayehisi
kuelemewa au kuchanganyikiwa. -
2:12 - 2:14Namba moja:
-
2:14 - 2:18Jambo la kwanza na ukweli kabisa ni kwamba ukweli wote ni kitendawili.
-
2:18 - 2:22Maisha yana thamani, na zawadi nzuri sana kupita maelezo,
-
2:22 - 2:27na haiwezekani kutelezeka kwa kiumbe cha mwili.
-
2:27 - 2:28Imekuwa uwiano mbaya sana
-
2:28 - 2:32kwa wale ambao tulizaliwa nyeti sana.
-
2:32 - 2:35Ni vigumu sana na ni ajabu
kwamba wakati mwingine tunajiuliza -
2:35 - 2:36kama tunataniwa.
-
2:37 - 2:42Imejazwa na wema na uzuri wa umbo,
-
2:42 - 2:44umasikini,
-
2:44 - 2:47Mafuriko na watoto na chunusi na Mozart,
-
2:47 - 2:49vyote vilibiringizwa pamoja.
-
2:50 - 2:52Sidhani ni mfumo mzuri.
-
2:52 - 2:55(Vicheko)
-
2:55 - 2:59Namba mbili: karibia kila kitu kitafanya kazi tena
-
2:59 - 3:01ukikichomoa kwa dakika chache --
-
3:01 - 3:04(Vicheko)
-
3:04 - 3:07(Makofi)
-
3:07 - 3:09hata na wewe.
-
3:11 - 3:14Tatu: karibia, hakuna chochote nje ya wewe
-
3:14 - 3:17kitakachokusaidia kwa njia yoyote ya kudumu,
-
3:17 - 3:19isipokuwa kama unasubiria kiungo.
-
3:20 - 3:25Huwezi kununua, kutekeleza au kuchumbia utulivu na amani.
-
3:25 - 3:29Huu ni kweli ya kutisha,
na ninauchukia. -
3:30 - 3:32Lakini ni kazi ya ndani,
-
3:32 - 3:35na hatuwezi kupanga amani
au uboreshaji wa kudumu -
3:35 - 3:37kwa ajili ya watu tunaowapenda duniani.
-
3:37 - 3:39Wanapaswa kutafuta njia yao wenyewe,
-
3:39 - 3:41majibu wenyewe.
-
3:41 - 3:44Huwezi kuenda pamoja na
watoto wako wakubwa -
3:44 - 3:49kwenye safari yao ya kishujaa.
-
3:49 - 3:51Unapaswa kuwaacha huru.
-
3:51 - 3:54Sio heshima kuwavunga.
-
3:55 - 3:57Na kama ni tatizo la mtu mwingine,
-
3:57 - 3:59labda hata wewe hauna jibu, pia.
-
3:59 - 4:00(Vicheko)
-
4:01 - 4:03Msaada wetu mara nyingi hausaidii.
-
4:04 - 4:06Msaada wetu mara nyingi ni sumu.
-
4:07 - 4:10Na msaada ni upande chanya wa udhibiti.
-
4:11 - 4:13Acha kusaidia sana.
-
4:13 - 4:17Usisambaze msaada wako na wema kwa kila mtu.
-
4:17 - 4:19(Vicheko)
-
4:19 - 4:21(Makofi)
-
4:21 - 4:23Hii inatuleta kwa namba nne:
-
4:23 - 4:27kila mtu amevunjika,
amevunjwa, ana wivu na hofu zake, -
4:27 - 4:30hata wanaoonekana kuwa pamoja zaidi.
-
4:30 - 4:32Wako kama wewe kuliko unavzoweza kuamini,
-
4:32 - 4:37hivyo usilinganisha undani wako na nje za watu wengine.
-
4:37 - 4:40Itakufanya ujisikie ovyo kuliko ulivyo tayari.
-
4:40 - 4:43(Vicheko)
-
4:44 - 4:48Pia, huwezi kuwaokoa, kurekebisha au kuwakomboa
-
4:48 - 4:50au kumpatia mtu yeyote busara.
-
4:50 - 4:53Kilichosaidia kupata nafuu na kukaa safi na madawa kwa miaka 30 iliyopita
-
4:53 - 4:56ilikuwa janga la tabia na fikra zangu.
-
4:56 - 4:58Hivyo niliomba msaada kwa marafiki,
-
4:58 - 5:00na nikamrudia muumbaji.
-
5:00 - 5:04Kifupisho kimoja cha Mungu ni "zawadi ya kukata tamaa,"
-
5:04 - 5:06M-U-N-G-U,
-
5:06 - 5:08Au kama rafiki yangu mmoja alivyoiweka,
-
5:08 - 5:13mwishoni nilikuwa nikipungukiwa kuliko nilivyoweza kupunguza viwango vyangu.
-
5:13 - 5:19(Vicheko)
-
5:19 - 5:21Kwa hiyo Mungu anaweza kumaanisha, katika kesi hii,
-
5:21 - 5:25"mimi kuishiwa na mawazo yoyote mazuri zaidi."
-
5:26 - 5:30Wakati kurekebisha na kuokoa
na kujaribu kuokoa ni bure, -
5:30 - 5:33Kujitegemea na kujitunza ni quantum,
-
5:33 - 5:37na hujiangaza katika mazingira yako
-
5:37 - 5:38kama hewa safi.
-
5:38 - 5:41Ni zawadi kubwa kwa duniani.
-
5:41 - 5:46Watu wanapojibu kwa kusema,
"Mmh, mtizame anavyojisikia," -
5:46 - 5:49tabasamu tu kama vile Mona Lisa
-
5:49 - 5:52na kuwatengenezea kikombe cha chai.
-
5:53 - 5:57Kuonyesha upendo kikamilifu
kwa uzuzu wa mtu, ubinafsi, -
5:57 - 6:00ukimwa, usumbufu wako
-
6:00 - 6:01ni nyumbani.
-
6:01 - 6:03Ndipo amani ya dunia huanzia.
-
6:05 - 6:07Namba tano:
-
6:07 - 6:12chokoleti yenye asilimia 75 kakao sio kweli chakula.
-
6:12 - 6:16(Vicheko)
-
6:16 - 6:20Matumizi yake bora ni katika mitego ya nyoka
-
6:20 - 6:25au kusawazisha miguu ya viti vinavyotetema.
-
6:25 - 6:28Haikuwahi kumaanishwa kama chakula.
-
6:30 - 6:31Namba sita
-
6:31 - 6:35(Vicheko)
-
6:35 - 6:36Kuandika.
-
6:37 - 6:41Kila mwandishi unayemjua huanaandika rasimu mbaya za mwanzo,
-
6:41 - 6:43Lakini hutuliza kitako kwenye kiti.
-
6:43 - 6:45Hiyo ndio siri ya maisha.
-
6:45 - 6:48Hiyo labda ndio tofauti kuu
kati yako na wao. -
6:48 - 6:50Wanafanya tu.
-
6:50 - 6:52Wanafanya kwa makubaiano na wao wenyewe.
-
6:53 - 6:55Wanafanya katika deni la heshima yao.
-
6:55 - 6:58Wanasimulia hadithi kutokea kwao
-
6:58 - 7:00siku moja banda ya nyingine, kidogo kidogo.
-
7:00 - 7:02Kaka yangu alipokuwa darasa la nne,
-
7:02 - 7:06alitakiwa kuwasilisha insha juu ya ndege kesho yake,
-
7:06 - 7:09Na hakuanza bado.
-
7:09 - 7:13Basi baba akaketi naye na kitabu cha Audubon,
-
7:13 - 7:15karatasi, penseli na brads -
-
7:15 - 7:21kwa wale ambao mmekuwaa wadogo kidogo na mna kukumbuka brads -
-
7:21 - 7:24na akamwambia kaka yangu,
-
7:24 - 7:26"Chukua tu ndege kwa ndege, rafiki.
-
7:26 - 7:29Soma tu juu ya Mwari
-
7:29 - 7:33na kisha andika kuhusu Mwari kwa sauti yako mwenyewe.
-
7:33 - 7:36Na kisha soma kuhusu chickadee,
-
7:36 - 7:38na utuambie kwa sauti yako mwenyewe.
-
7:39 - 7:40Na kisha bata bukini. "
-
7:40 - 7:44Hivyo vitu viwili muhimu kuhusu kuandika ni: ndege kwa ndege
-
7:44 - 7:47na kwa kweli rasimu ovyo za mwanzo.
-
7:48 - 7:50Kama hujui uanzie wapi
-
7:50 - 7:53kumbuka unamiliki kila kitu kilichokutokea
-
7:53 - 7:54na unaweza kusimulia.
-
7:55 - 7:58Ikiwa watu walitaka uandike mazuri kuhusu wao,
-
7:58 - 8:00wangemudu tabia zao vizuri zaidi.
-
8:00 - 8:03(Vicheko)
-
8:03 - 8:06(Makofi)
-
8:07 - 8:10Utajisikia ovyo siku moja utakapoamka
-
8:10 - 8:12na hujaandika juu ya mambo
-
8:12 - 8:15yanazo anazokukereketa, unayotunza moyoni:
-
8:15 - 8:19hadithi zako, kumbukumbu,
maono na nyimbo - -
8:19 - 8:20Ukweli wako,
-
8:20 - 8:22mtizamo wako wa vitu -
-
8:22 - 8:24katika sauti yako mwenyewe.
-
8:24 - 8:26Hicho pekee ndicho unachokubui kutupatia,
-
8:26 - 8:29Hiyo ndiyo sababu ulizaliwa.
-
8:30 - 8:35Saba: kuchapishwa na mafanikio ya ubunifu ya muda mfupi
-
8:35 - 8:37ni kitu ambacho unapaswa kuponywa kutoka.
-
8:38 - 8:41Vinaua watu wengi kama visivo.
-
8:41 - 8:43Vitakuumiza, kukuharibu na kukubadilisha
-
8:43 - 8:45kwa njia ambazo huwezi kufikiria.
-
8:46 - 8:49Watu dhilifu na waovu kuliko wote niliowahi kujua
-
8:49 - 8:52ni waandishi wa kiume walioandika vitabu vilivyo uza vizuri mno.
-
8:53 - 8:57Na bado, tukurudia namba moja, kwamba ukweli wote ni kitendawili,
-
8:57 - 9:00Pia ni muujiza kupata kazi yako kuchapishwa,
-
9:00 - 9:03Ili hadithi zako zisomwe na kusikika.
-
9:03 - 9:05Jaribu tu kujitahidi polepole na fantasia
-
9:05 - 9:08ambayo itakuponya,
-
9:08 - 9:12itajaza mashimo ya chizi ya Uswisi ndani yako.
-
9:12 - 9:14haiwezekani.
-
9:14 - 9:15haitokuwa.
-
9:15 - 9:17Lakini uandishi unaweza.
-
9:17 - 9:20Pia unaweza kuimba kwenye kwaya
au bendi. -
9:20 - 9:24Pia uchoraji au ufugaji wa ndege
-
9:24 - 9:27au kukuza mbwa wazee ambao hakuna mtu mwingine anataka.
-
9:29 - 9:32Ya nane: familia.
-
9:33 - 9:36Familia ni ngumu, ngumu, ngumu,
-
9:36 - 9:39haijalishi namna gani tunaipenda au wavyotushangaza.
-
9:39 - 9:42Tena, rudia namba moja
-
9:42 - 9:43(Vicheko)
-
9:43 - 9:47Katika mikusanyiko ya familia ambapo ghafla hujisikia kuua au kujiua --
-
9:47 - 9:48(Vicheko)
-
9:48 - 9:50Kumbuka kwamba katika hali zote,
-
9:50 - 9:56Ni muujiza kwamba yeyote kati yetu hasa, alizaliwa.
-
9:57 - 9:58Dunia ni shule ya msamaha.
-
9:58 - 10:01Inaanza kwa kujisamehe,
-
10:01 - 10:04na kisha unaweza pia kuanza kusamehe watu mezani.
-
10:05 - 10:08Hivyo unaweza kufanya kazi hio katika hali tulivu.
-
10:08 - 10:11(Vicheko)
-
10:11 - 10:13William Blake aliposema kuwa tuko hapa
-
10:13 - 10:16kujifunza kuhimili miale ya upendo,
-
10:16 - 10:20alijua kwamba familia yako itakuwa sehemu kubwa ya hili,
-
10:20 - 10:23Hata unapotaka kukimbia, kupiga kelele kwa ajili ya kimaisha chako.
-
10:24 - 10:26Lakini ninakuahidi uko tiyari.
-
10:26 - 10:30Unaweza, Sindereli, unaweza,
-
10:30 - 10:32Na utashangaa.
-
10:33 - 10:35Tisa: chakula.
-
10:36 - 10:39Jaribu kufanya vizuri zaidi.
-
10:39 - 10:41Nadhani unajua ninachmaanisha.
-
10:41 - 10:45(Vicheko)
-
10:51 - 10:52Namba 10 --
-
10:52 - 10:55(Vicheko)
-
10:55 - 10:56neema.
-
10:56 - 11:00Neema ni WD-40 ya kiroho,
-
11:00 - 11:01Au mabawa ya maji.
-
11:01 - 11:07Fumbo la neema ni kwamba Mungu anapenda Henry Kissinger na Vladimir Putin
-
11:07 - 11:08na mimi
-
11:08 - 11:13sawa kama anavyompenda mjukuu wako mpya.
-
11:13 - 11:14Embu fikiria.
-
11:14 - 11:16(Vicheko)
-
11:16 - 11:19Harakati ya neema ndio kinachotubadilisha, hutuponya
-
11:19 - 11:21na huponya ulimwengu wetu.
-
11:21 - 11:25Kuita neema, sema, "Nisaidie,"
na kisha jiandae. -
11:25 - 11:28Neema hukukuta wewe mahali ulipo,
-
11:28 - 11:30lakini haikuachi itakapokukuta.
-
11:30 - 11:34Na neema haitofanana na Casper zimwi rafiki,
-
11:34 - 11:35kwa bahati mbaya.
-
11:35 - 11:38Lakini simu itapiga au barua itakuja
-
11:38 - 11:39Na kisha dhidi ya vikwazo vyote,
-
11:39 - 11:42utapata ucheshi wako kuhusu mwenyewe tena.
-
11:43 - 11:46Kicheko kweli ni utakatifu wenye kaboni.
-
11:47 - 11:50Inatusaidia kupumua tena na tena
-
11:50 - 11:52Na kujipa tena,
-
11:52 - 11:55Na hutupa imani katika maisha na wengine.
-
11:56 - 12:00Na kumbuka - daima neema huja mwishoni.
-
12:02 - 12:05Eleven: Mungu anamaanisha wema tu.
-
12:05 - 12:07Hata haiogopeshi.
-
12:07 - 12:12Ina maana ya kimungu au upendo,
kimaarifa -
12:12 - 12:15au, kama tulivyojifunza kutoka kwa "Deteriorata" mkuu
-
12:15 - 12:17"keki ya kikosmiki."
-
12:18 - 12:21Jina jema la Mungu ni: "Sio mimi."
-
12:22 - 12:25Emerson alisema mtu mwenye furaha zaidi duniani
-
12:25 - 12:29ni anayejifunza ibada kutoka kwa mazingira.
-
12:29 - 12:32Hivyo nenda nje na angalia juu.
-
12:32 - 12:36Mchungaji wangu alisema unaweza kutega nyuki ndani ya glasi bila kufunika
-
12:36 - 12:38kwa sababu hawaangalii juu,
-
12:38 - 12:43hivyo wanatembea tu kwa huzuni na kuingia ndani ya glasi.
-
12:43 - 12:45Nenda nje. Tazama juu
-
12:45 - 12:46Siri ya maisha.
-
12:47 - 12:49Na hatimaye: kifo.
-
12:50 - 12:52Namba 12.
-
12:53 - 12:54Wow na yikes.
-
12:55 - 13:00Ni vigumu kuhimili kifo cha watu wachache tunaowapenda kwa dhati.
-
13:00 - 13:03Kamwe huwezi kusahau hasara hizi, haijalishi utamaduni unasemaje,
-
13:03 - 13:05hautakiwi.
-
13:05 - 13:10Sisi wakristo tunapenda kufikiria kifo kama mabadiliko makubwa ya anwani,
-
13:10 - 13:15Lakini katika hali yoyote, mtu huishi tena katika moyo wako
-
13:15 - 13:17usipoufunga na sili.
-
13:17 - 13:20Kama Leonard Cohen alisema, "Kuna nyufa katika kila kitu,
-
13:20 - 13:22na ndio jinsi mwanga unavyoingia.
-
13:22 - 13:25Na ndivyo tunavyojisikia wapendwa wetu wakiwa hai tena.
-
13:27 - 13:31Pia, watu watakufanya ucheke kwa nguvu
-
13:31 - 13:34katika mida isio sahihi,
-
13:34 - 13:36na hiyo ndiyo habari njema.
-
13:36 - 13:41Lakini kutokuwepo kwao pia utakuacha na ndoto mbaya na ukimisi nyumbani daima
-
13:41 - 13:46Huzuni na marafiki, muda na machozi
vitakuponya kwa kiasi fulani. -
13:46 - 13:50Machozi yatakuosha na kukubatiza
na kukuhidrati na kukurutubisha -
13:50 - 13:52na ardhi unayotembelea.
-
13:52 - 13:55Unajua kitu cha kwanza Mungu amwambia Musa?
-
13:56 - 13:59Anasema, "Vua viatu vyako."
-
13:59 - 14:03Kwa sababu hii ni ardhi takatifu, ushahidi wote unakanua hili.
-
14:03 - 14:06Ni vigumu kuamini, lakini ni jambo la ukweli kabisa nalojua .
-
14:06 - 14:10Unapokuwa mzee kidogo, kama mtoto mie,
-
14:10 - 14:14unatambua kifo ni takatifu kama kuzaliwa.
-
14:15 - 14:18Na hujali tena - bali uendelea na maisha yako.
-
14:18 - 14:23Karibu kila kifo ni rahisi na polepole
-
14:23 - 14:26pamoja na wapendwa wakikuzunguka
-
14:26 - 14:28kulingana na unavyohitaji.
-
14:28 - 14:29Hautokuwa peke yako.
-
14:31 - 14:34Watakusaidia kuvuka kwa chochote kinachokusubiri.
-
14:35 - 14:37Kama Ram Dass alisema,
-
14:37 - 14:38"Yote yakishasemwa na kutendwa,
-
14:39 - 14:42tunatembea tu katika nyumba ya kila mmoja wetu. "
-
14:43 - 14:45Nadhani nimemaliza,
-
14:45 - 14:47lakini kama nikifikiria kitu kingine chochote,
-
14:47 - 14:48Nitawajulisha.
-
14:48 - 14:49Ahsante.
-
14:49 - 14:51(Makofi)
-
14:51 - 14:52Ahsante.
-
14:52 - 14:54(Makofi)
-
14:54 - 14:56Nilishangaa sana nilipoulizwa kuja hapa,
-
14:56 - 14:59Kwa sababu sio eneo langu,
-
14:59 - 15:01Teknolojia au tarakibu au burudani.
-
15:01 - 15:05Yaani eneo langu ni imani na uandishi
-
15:05 - 15:08na huambatana pamoja.
-
15:08 - 15:09Na nilishangaa,
-
15:09 - 15:14Lakini waliniuliza niwasilishe majadiliano, na nilikubali.
-
15:14 - 15:16(Video) Kama hujui utaanzia wapi,
-
15:16 - 15:19kukumbuka kwamba unamiliki kila kitu kilichokutokea
-
15:19 - 15:20na una haki ya kusimulia.
-
15:20 - 15:23Anne Lamott: Watu wana hofu sana na kuhisi kweli wamepotea
-
15:23 - 15:25katika Amerika ya leo,
-
15:25 - 15:28na nilitaka tu kuwasaidia watu
kuuona ucheshi kuhusu hilo -
15:28 - 15:31na kutambua ni kiasi gani sio tatizo.
-
15:31 - 15:35Ukikuchukua hatua,
-
15:36 - 15:39chukua kweli hatua katika upendo, katika kirafiki,
-
15:39 - 15:42utabaki na hisia za upendo na urafiki.
- Title:
- Ukweli 12 niliojifunza kupitia maisha na uandishi
- Speaker:
- Anne Lamott
- Description:
-
Siku chache kabla ya kutimiza miaka 61, mwandishi Anne Lamott aliamua kuandika kuhusu kila kitu alichofahamu kwa hakika. Anazama katika mihangaiko ya mwanadamu anayeishi katika ulimwengu uliochanganika, wenye uzuri na hisia, unaompa hekima na ucheshi kuhusu familia, uandishi, maana ya Mungu, kifo na zaidi.
- Video Language:
- English
- Team:
- closed TED
- Project:
- TEDTalks
- Duration:
- 15:55
Joachim Mangilima approved Swahili subtitles for 12 truths I learned from life and writing | ||
Joachim Mangilima accepted Swahili subtitles for 12 truths I learned from life and writing | ||
Sophia Mwema edited Swahili subtitles for 12 truths I learned from life and writing | ||
Sophia Mwema edited Swahili subtitles for 12 truths I learned from life and writing | ||
Sophia Mwema edited Swahili subtitles for 12 truths I learned from life and writing | ||
Sophia Mwema edited Swahili subtitles for 12 truths I learned from life and writing | ||
Sophia Mwema edited Swahili subtitles for 12 truths I learned from life and writing | ||
Sophia Mwema edited Swahili subtitles for 12 truths I learned from life and writing |