Return to Video

Msingi Wa Kuzidisha

  • 0:01 - 0:03
    Tujifunze kuzidisha
  • 0:03 - 0:08
    ZIDISHA
  • 0:08 - 0:12
    Ninadhani njia mwafaka kabisa ya kufanya chochote ni kufanya mifano
  • 0:12 - 0:14
    kisha jadili maswali haya na kujaribu
  • 0:14 - 0:16
    Kubaini maana ya mifano hii
  • 0:16 - 0:21
    Katika mfano wa kwanza, tujaribu kuzidisha mbili mara tatu
  • 0:21 - 0:25
    Kwa sasa labda walijua jibu ujumulishapo tatu na mbili
  • 0:25 - 0:27
    Mbili jumulisha na tatu
  • 0:27 - 0:28
    Ambapo jibu ni tano
  • 0:28 - 0:31
    kama ungetaka choto cha gwaride, ungefikiria
  • 0:31 - 0:35
    ningekuwa na mbili, kwa mfano magenta mbili
  • 0:35 - 0:37
    Rangi hii- cherries
  • 0:37 - 0:42
    Nami nataka kujumlisha na maembe matatu.
  • 0:42 - 0:45
    Kwa jumla, ninayo matunda mangapi?
  • 0:45 - 0:48
    Na ungesema, moja, mbili, tatu, nne, tano.
  • 0:48 - 0:55
    ama bidhalika, tungekuwa na laini ya namba,
  • 0:55 - 0:58
    nawe labda…Hauhitaji gwaride hili, lakini haidhuru.
  • 0:58 - 1:01
    Haidhuru kutomea dhana hii
  • 1:01 - 1:10
    Na kama hii ni sufuri,moja, mbili, tatu, nne na tano.
  • 1:10 - 1:14
    Ukiwa kwa nambari mbili upande wa kulia wa sufuri na kwa ujumla,
  • 1:14 - 1:18
    Tukielekea upande wa chanya, tunaelekea upande wa kulia
  • 1:18 - 1:20
    Na kama ungeiongezea tatu, ungesonga
  • 1:20 - 1:22
    Nafasi tatu kuelekea upande wa kulia.
  • 1:22 - 1:26
    Kama ningesema, kama ningesonga mara tatu kuelekea
  • 1:26 - 1:27
    Upande wa kulia, nitafikia wapi?
  • 1:27 - 1:30
    Moja, mbili, tatu
  • 1:30 - 1:31
    Ninafikia nambari tano
  • 1:31 - 1:35
    Kwa hivyo tukitumia njia yoyote kati ya mbili tulizotumia awali, utaelewa kuwa ukijumlisha mbili na tatu, jibu ni tano.
  • 1:35 - 1:38
    Sasa ni nini jibu la kuzidisha mbili mara tatu?
  • 1:38 - 1:42
    Njia rahisi ya kufikiria kuzidisha ama uzidisho
  • 1:42 - 1:47
    wa kitu nj njia rahisi kujumlisha,na kurudia vile mara nyingi
  • 1:47 - 1:50
    Itakuwa tatanishi kidogo
  • 1:50 - 1:52
    Hautajumlisha mbili na tatu
  • 1:52 - 1:53
    Utajumulisha
  • 1:53 - 1:56
    na kwa hakika kunazo njia mbili za kuifikiria
  • 1:56 - 2:00
    Hautajumlisha mbili na tatu
  • 2:00 - 2:01
    Hiyo yamaanisha nini?
  • 2:01 - 2:08
    Naam, inamaanisha utajumlisha mbili kwa mbili kwa mbili.
  • 2:08 - 2:09
    Sasa nambari tatu ilipotelea mwapi?
  • 2:09 - 2:13
    aam, tunazo nambari mbili ngapi hapa?
  • 2:13 - 2:17
    Hebu tuone, ninayo nambari mbili (moja), ninazo nambiri mbili tena(mbili)
  • 2:17 - 2:19
    Na ninazo nambari mbili (tatu)
  • 2:19 - 2:20
    Nahesahu nambiri hizi hapa
  • 2:20 - 2:22
    kama nilivyoyahesabu Maembe hapo mbeleni
  • 2:22 - 2:24
    Nilikuwa na maembe moja, mbili na tatu
  • 2:24 - 2:27
    Ninayo mbili mara moja, mbili na mara tatu
  • 2:27 - 2:34
    Sasa hii tatu inanionyesha idadi ya nambari mbili nitakazo kuwa nazo
  • 2:34 - 2:36
    Sasa, ukizidisha mbili mara tatu, utapata nini?
  • 2:36 - 2:41
    Naam, nilichukua nambari mbili nikaiongezea nambari mbili zingine mara mbili
  • 2:41 - 2:43
    Kwa hivyo, mbili ukiongeza mbili ingine, jibu ni nne.
  • 2:43 - 2:47
    Nne ukiongeza mbili, jibu ni sita.
  • 2:47 - 2:48
    Sasa hiyo ni njia moja tu ya kuisuluhisha.
  • 2:48 - 2:52
    Kwa njia nyingine,
  • 2:52 - 2:56
    tungesema, badala ya kuongeza mbili kwa mbili mara tatu
  • 2:56 - 2:59
    Tungeongeza tatu nyingine kwa ya kwanza
  • 2:59 - 3:01
    Na najua labda imeanza kukuchanganyisha kidogo, lakini
  • 3:01 - 3:04
    Ukifanya mazoezi ziadi, utaelewa.
  • 3:04 - 3:07
    Sasa, swali hili hapa juu, nikiliandika tena..
  • 3:07 - 3:10
    Mbili mara tatu
  • 3:10 - 3:16
    Pia ingeandikwa kama: tatu mara mbili
  • 3:16 - 3:20
    Ambayo ni tau uongeze tatu
  • 3:20 - 3:22
    Na utashangaa—nambari mbili imepotelea wapi?
  • 3:22 - 3:24
    Unajua, nilikuwa na mbili mara tatu, na kila unapojumlisha,
  • 3:24 - 3:28
    unaona nina mbili, oh sijui hizi,sawa..nilisema
  • 3:28 - 3:30
    Cherries, lakini labda zingekuwa raspberries ama chochote kile!
  • 3:30 - 3:33
    Na tena nina vitu viwili, nina vitatu na vile viwili
  • 3:33 - 3:34
    Na vitatu havipotei
  • 3:34 - 3:37
    Na nazijumlisha nipate tatu!
  • 3:37 - 3:39
    Lakini hapa nasema kuwa mbili mara tatu ni kama
  • 3:39 - 3:40
    Tatu uongeze tatu.
  • 3:40 - 3:41
    Mbili ilienda wapi?
  • 3:41 - 3:44
    mbili, katika mandhari haya, inanionyesha
  • 3:44 - 3:49
    Ni mara gapi nitaongeza tatu kwa yenyewe
  • 3:49 - 3:55
    Lakini kinachofurahisha ni kuwa, bila kuzingatia namna
  • 3:55 - 3:58
    ninavyofasiri mbili mara tatu, naweza kuifasiri kuwa ni: Mbili uongeze mbili, uongeze mbili nyingine tena
  • 3:58 - 4:01
    ama uongeze mbili kwa yenyewe mara tatu.
  • 4:01 - 4:04
    Naweza kufasiri kwa njia hiyo ama naweza kuifasiri ni
  • 4:04 - 4:07
    Kuongeza tatu kwa yenyewe mara tatu.
  • 4:07 - 4:09
    Lakini, ukigundua majibu yanafanana
  • 4:09 - 4:11
    Ukijumlisha tatu na tatu utapata nini?
  • 4:11 - 4:14
    Utapata kuwa jibu pia ni sita
  • 4:14 - 4:17
    Na labda hii ni mara yako ya kwanza
  • 4:17 - 4:19
    Utapambana na kitu nadhifu
  • 4:19 - 4:21
    Wakati mwingine,bila kuzingatia njia utumiayo, bora
  • 4:21 - 4:25
    Iwe njia sawa, utapata jibu sahihi.
  • 4:25 - 4:27
    Sasa watu wawili wanaweza kuiwazia
  • 4:27 - 4:29
    bora wanaiwazia kwa njia sahihi,hesabu mbili tofauti
  • 4:29 - 4:34
    Lakini wanapata jibu sawa.
  • 4:34 - 4:35
    Na labda unauliza, Sal
  • 4:35 - 4:43
    Ni lini kuzidisha huku kutakuwa na umuhimu?
  • 4:43 - 4:44
    Na umuhimu wake ndio huu.
  • 4:44 - 4:47
    Wakati mwingine hurahisisha kuhesabu.
  • 4:47 - 4:52
    Na tuseme-..aah…
  • 4:52 - 4:57
    acha tutumie mfano wetu wa matunda
  • 4:57 - 5:00
    Tamthili ni tu unapofanaisha vitu.
  • 5:00 - 5:02
    Aahh…sawa sitaifafanua sana.
  • 5:02 - 5:04
    Mfano wetu wa matunda.
  • 5:04 - 5:05
    Tuseme kwa mfano nina limau
  • 5:05 - 5:07
    Wacha nichore mkole wa malimau
  • 5:07 - 5:09
    Nitayachora malimau haya katika zefe kila moja ikiwa na tatu
  • 5:09 - 5:15
    Sasa niko na moja, mbili, tatu-uummh basi…zitazisoma kwasababu..
  • 5:15 - 5:18
    Iyo itafichua jibu letu.
  • 5:18 - 5:21
    Ninachora tu zefe la malimau
  • 5:21 - 5:27
    Sasa, kama ningesema: uniambie malimau ngapi ninayo hapa
  • 5:27 - 5:29
    na kama ningefanya hivyo,
  • 5:29 - 5:31
    ungeendelea kuhesabu malimau yote
  • 5:31 - 5:34
    na haitakuchukua muda kusema kuwa: oh, kuna
  • 5:34 - 5:39
    Malimau -Moja, mbili, tatu, nne, tano, sita, saba, nane,tisa,kumi,kumi na moja, kumi na mbili…..ata kwanza
  • 5:39 - 5:40
    Nishawatobolea jibu!
  • 5:40 - 5:43
    Twajua kuwa kuna malimau kumi na mawili kule
  • 5:43 - 5:45
    lakini kuyo njia rahisi
  • 5:45 - 5:48
    na ya haraka ya kuhesabu Idadi ya malimau haya yote
  • 5:48 - 5:52
    Nikiuliza, kuna malemau mangapi katika kila zefe?
  • 5:52 - 5:57
    Na zefe ni kama malimau yaliyo kando kwa kando
  • 5:57 - 6:00
    Nadhai wafahamu zefe ni nini
  • 6:00 - 6:03
    Sitaki kuanza kueleza ni nini
  • 6:03 - 6:06
    Sasa malimau mangapi katika zefe moja?
  • 6:06 - 6:09
    Sawa, kunayo malimau matatu katika kila zefe
  • 6:09 - 6:12
    Na sasa wacha nikuulize swali jingine:
  • 6:12 - 6:16
    Kuna mazefe mangapi?
  • 6:16 - 6:21
    Ukiangalia, hili ni zefe la kwanza, hilki ni la pili
  • 6:21 - 6:27
    Hili ni la tatu,na hili ni la nne
  • 6:27 - 6:31
    Njia rahisi ya kuihesabu ni kusema, ninayo malimau matatu katika kila zefe
  • 6:31 - 6:32
    ambazo ni nne
  • 6:32 - 6:35
    Sasa tuseme tunayo malimau matatu katika kila zefe
  • 6:35 - 6:38
    Ninatumai sikuchanganyishi, lakini nafikira unaifurahia
  • 6:38 - 6:40
    Na kisha ninayo mazefe manne
  • 6:40 - 6:43
    Kwa hivyo nina malimau matatu mara nne
  • 6:43 - 6:46
    malimau matatu mara nne
  • 6:46 - 6:51
    Ambayo inafaa iafikiane na idadi ya malimau yote niliyo nayo- kumi na mawili.
  • 6:51 - 6:55
    na tu kufananisha na nilichofanya katika kujumlisha,
  • 6:55 - 6:56
    tutafakari.
  • 6:56 - 6:59
    nne mara tatu- kwa kawaida, .
  • 6:59 - 7:02
    ukilitaja neno nne mara tatu
  • 7:02 - 7:05
    unaliona kama picha akilini
  • 7:05 - 7:07
    Mimi naona nne mara tatu
  • 7:07 - 7:09
    Kwa hivyo tatu mara nne
  • 7:09 - 7:12
    Tatu uongeze tatu na uongeze tatu nyingine
  • 7:12 - 7:13
    Tukifanya hivyo tunapata
  • 7:13 - 7:15
    twapata kuwa tatu ukiongeza tatu nyinine, jibu ni sita
  • 7:15 - 7:17
    Sita ukiongezea tatu unapata tisa.
  • 7:17 - 7:20
    Tisa ukiongezea tatu utapata kumi na mbili
  • 7:20 - 7:24
    a tulisoma hapo awali, katika sehemu awali ya video hii,
  • 7:24 - 7:27
    tulijifunza kuwa kuzidisha huku
  • 7:27 - 7:30
    kwaweza kufasiriwa
  • 7:30 - 7:33
    Kuwa ni tatu mara nne
  • 7:33 - 7:35
    Unaweza ukabadilisha mtindo
  • 7:35 - 7:37
    na hii ndio moja ya njia muhimu
  • 7:37 - 7:42
    Na ya kufurahisha sana, kwa hakika ni kama hulka za kuzidisha
  • 7:42 - 7:47
    Lakini hii pia ingeweza kuandikwa kama nne mara tatu
  • 7:47 - 7:50
    Ambayo nine uongeze nne, uongeze nne nyingine
  • 7:50 - 7:52
    Unaongeze nne kwa yenyewe mara tatu
  • 7:52 - 7:55
    Nne ukijumlisha na nne unapata nane
  • 7:55 - 7:58
    Nane ukijumlisha na nne nyingine unapata kumi na mbili
  • 7:58 - 8:03
    Marekani, huwa tunasema nne mara tatu,
  • 8:03 - 8:05
    lakini unajua, nimekutana
  • 8:05 - 8:08
    na watu wengi ambao wamesoma sana
  • 8:08 - 8:10
    Katika mfumo wa Kiingereza
  • 8:10 - 8:14
    Na mara nyingi wataiita nne( tatu) ama tatu (nne)
  • 8:14 - 8:16
    Ni rahisi kuelewa kutumia njia hii
  • 8:16 - 8:17
    Haieleweki kirahisi unaposikia mara ya kwanza
  • 8:17 - 8:19
    lakini wataiandika hesabu hii
  • 8:19 - 8:21
    ama watasema
  • 8:21 - 8:23
    nne (tatu) ni ngapi?
  • 8:23 - 8:25
    na wakisema nne( tatu) wanamaanisha kuwa:
  • 8:25 - 8:28
    nne( tatu) ni nini?
  • 8:28 - 8:32
    sasa hii ni tatu ya kwanza, ya pili, ya tatu na ya nne.
  • 8:32 - 8:34
    Sasa, nne(tatu) ni nini? Ukizijumlisha?
  • 8:34 - 8:35
    Jibu ni kumi na mbili.
  • 8:35 - 8:38
    Pia ungesema, tatu(nne) ni nini?
  • 8:38 - 8:41
    Wacha niiandike chini
  • 8:41 - 8:43
    Wacha niiandike kutumia rangi tofauti
  • 8:43 - 8:47
    Ambazo ni nne (tatu)
  • 8:47 - 8:49
    Namaanisha, kwa kawaida…ni nne (tatu)
  • 8:49 - 8:53
    na kama ningekuambia useme, au uandike nne (tatu) na ujumulishe
  • 8:53 - 8:53
    hili ndilo suluhisho
  • 8:53 - 8:56
    Na hiyo ni nne mara tatu
  • 8:56 - 8:57
    au tatu mara nne
  • 8:57 - 9:03
    Na hii ni- wacha niandike hii kutumia rangi tofauti
  • 9:03 - 9:09
    Ni tatu (nne)
  • 9:09 - 9:13
    Na pia ingeweza kuandikwa kama: Tatu mara nne
  • 9:13 - 9:16
    Na zote jibu ni kumi na mbili
  • 9:16 - 9:16
    Na saa hii labda unasemai
  • 9:16 - 9:19
    Ni hila nzuri sana Sal
  • 9:19 - 9:20
    uliyonifunz
  • 9:20 - 9:25
    lakini ilikuchukua muda mfupi sana kuyahesabu malimau haya
  • 9:25 - 9:27
    Kushinda kufanya hesabu hii
  • 9:27 - 9:30
    kwanza kabisa, hiyo tu ni kwa sasa kwa sababu ni mara yako ya kwanza kusomea kuzidisha.
  • 9:30 - 9:34
    Lakini ambacho utagundua ni kuwa
  • 9:34 - 9:35
    kuna kuzidisha na kuzidisha kwingi
  • 9:35 - 9:39
    na sitaki kulitumia hilo neno mara nyingi katika video ya kuzidisha
  • 9:39 - 9:42
    - ambapo kila zefe la malimau
  • 9:42 - 9:43
    badala ya kuwa na tatu,
  • 9:43 - 9:44
    pengine kila zefe lina malimau mia moja!
  • 9:44 - 9:48
    Labda kuna mazefe mia moja!
  • 9:48 - 9:50
    na itakuchukua milele kuhesabu malimau yote haya
  • 9:50 - 9:52
    Na papa hapa ndipo umuhimu wa kuzidisha unajitokeza.
  • 9:52 - 9:57
    Hata kama wakati huu hatutasomea jinsi ya kuzidisha mia moja mara mia moja
  • 9:57 - 9:59
    sasa,kitu moja ninataka kukushika nayo na ni
  • 9:59 - 10:00
    Kama hila
  • 10:00 - 10:04
    namkumbuka dada yangu ili tu kujaribu kuonyesha uhodari wake
  • 10:04 - 10:07
    kunishinda nilipokuwa katika shule ya chekechea naye akiwa darasa la tatu.
  • 10:07 - 10:13
    Alikuwa akisema, Sal, nini jibu la tatu mara moja?
  • 10:13 - 10:15
    na ningesema, kwa sababu akili yangu ingesema
  • 10:15 - 10:16
    Hiyo ni kama tatu uongeze moja
  • 10:16 - 10:20
    Na ningemjibu kuwa tatu ongeze moja unapata nne.
  • 10:20 - 10:20
    Kisha ningesema tatu mara moja…
  • 10:20 - 10:24
    Hiyo pia lazima iwe nne
  • 10:24 - 10:26
    Naye angesema: La, mjinga! Jibu ni tatu!
  • 10:26 - 10:27
    Na nilikuwa nashangaa hiyo ingewezekanaje?
  • 10:27 - 10:31
    jinsi gani tatu mara namba nyingine ibakie tatu?
  • 10:31 - 10:33
    Hebu fikiria maana.
  • 10:33 - 10:39
    Waweza kuifasiri kam tatu(moja)
  • 10:39 - 10:40
    Hizi tatu(moja) ni nini?
  • 10:40 - 10:45
    Hiyo ni moja uongeze moja kasha uongeze moja nyingine ya tatu.
  • 10:45 - 10:46
    Ambayo ni tatu.
  • 10:46 - 10:49
    Vilevile ungeifasiri kuwa ni tatu mara moja.
  • 10:49 - 10:51
    Tatu mara moja unapata nini?
  • 10:51 - 10:54
    Ni rahisi sana
  • 10:54 - 10:55
    Jibu ni tatu tu.
  • 10:55 - 10:56
    Hiyo ni tatu moja
  • 10:56 - 11:00
    Unawezaje kuandika hii kama tatu moja?
  • 11:00 - 11:02
    ndio maana chochote mara moja
  • 11:02 - 11:04
    ama moja mara chochote
  • 11:04 - 11:06
    ni hicho chochote!
  • 11:06 - 11:08
    Inamaanisha tatu mara moja ni tatu.
  • 11:08 - 11:10
    Moja mara tatu ni tatu.
  • 11:10 - 11:14
    Na wajua, ningesema mia moja mara moja
  • 11:14 - 11:17
    ni mia moja.
  • 11:17 - 11:21
    Pia ningesema moja mara thelathini na tisa
  • 11:21 - 11:23
    ni thelathini na tisa
  • 11:23 - 11:27
    Na natarajia umezoea nambari kubwa kama hizi kwa sasa.
  • 11:27 - 11:28
    Sasa hiyo inavutia
  • 11:28 - 11:32
    Pia kunacho kitu kingine kinachovutia kuhusu kuzidisha.
  • 11:32 - 11:35
    Ni kama umezidisha mara sufuri
  • 11:35 - 11:38
    Na nitaanzia mfano unapojumlisha.
  • 11:38 - 11:41
    Tatu uongeze sufuri, natarajia unaifahamu
  • 11:41 - 11:42
    ni tatu
  • 11:42 - 11:44
    Kwa sababu siongezi chochote kwa tatu
  • 11:44 - 11:45
    Kama ninazo darabi tatu
  • 11:45 - 11:47
    na nikuongezee darabi sufuri
  • 11:47 - 11:49
    Bado una darabi tatu.
  • 11:49 - 11:50
    lakini tatu ni nini
  • 11:50 - 11:53
    au labda nimitumia nambari hii sana?
  • 11:53 - 11:54
    Wacha nibadilishe--
  • 11:54 - 11:59
    ini jibu ukizidisha nne mara sufuri?
  • 11:59 - 12:03
    Hii ni kama kusema sufuri mara nne
  • 12:03 - 12:09
    Sasa nini jibu la sufuri ukiongeza sufuri, uongeze sufuri,uongeze sufuri kisha uongeze sufiri nyingine?
  • 12:09 - 12:12
    Basi..jibu ni sufuri
  • 12:12 - 12:14
    Sawa? Sina chochote na nikijumulisha sufuri
  • 12:14 - 12:15
    sipati chochote!
  • 12:15 - 12:17
    Njia nyingine ya kuifasiri,
  • 12:17 - 12:19
    ninaweza kusema, nne mara sufuri.
  • 12:19 - 12:21
    Sasa nitaandikaje nne mara sufuri?
  • 12:21 - 12:23
    Naam, siandiki chochote, sivyo?
  • 12:23 - 12:24
    Kwa sababu nikiandika chochote
  • 12:24 - 12:27
    kwa mfano nikiandika nne-moja, na sina nne-sufuri
  • 12:27 - 12:28
    Hivi nikusema
  • 12:28 - 12:30
    Hii ni nne--
  • 12:30 - 12:31
    hebu niandike--
  • 12:31 - 12:36
    hi ni sufuri-nne
  • 12:36 - 12:41
    Naweza pia kuandika sufuri nne
  • 12:41 - 12:42
    Na sufuri nne ni nini?
  • 12:42 - 12:44
    Nitaacha pengo kubwa sana hapa
  • 12:44 - 12:44
    Kule, niliiandika:
  • 12:44 - 12:46
    Hakuna nambari nne yoyote hapa!
  • 12:46 - 12:48
    Inamaanisha kuna pengo kubwa sana.
  • 12:48 - 12:49
    Na huo ni mzaha mwingine
  • 12:49 - 12:51
    Inamaanisha chochote mara sufuri ni sufuri
  • 12:51 - 12:53
    Ningeandika nambari kubwa
  • 12:53 - 12:59
    kama 5,493,692
  • 12:59 - 13:02
    mara sufuri
  • 13:02 - 13:03
    Jibu ni nini?
  • 13:03 - 13:04
    Jibu ni sufuri
  • 13:04 - 13:05
    Na nikiuliza
  • 13:05 - 13:06
    nambari hii mara moja ni nini?
  • 13:06 - 13:08
    Sawa, ni namba ile ile tena
  • 13:08 - 13:12
    Na jibu la sufuri mara kumi na saba ni nini?
  • 13:12 - 13:15
    Tena, tunapata sufuri
  • 13:15 - 13:18
    Ala kuli hali, nimezungumza kwa muda mrefu.
  • 13:18 -
    Tuonane katika video ifuatayo!
Title:
Msingi Wa Kuzidisha
Description:

Mwanzo wa hesabu ya kuzidisha

more » « less
Video Language:
English
Duration:
13:20
Olengh edited Swahili subtitles for Basic Multiplication
Olengh edited Swahili subtitles for Basic Multiplication
Olengh added a translation

Swahili subtitles

Revisions