Return to Video

Jinsi nilivyojifunza kuwasilisha maisha yangu nikiwa na Aspegaz

  • 0:01 - 0:03
    Leo ninataka kuzungumza nawe kuhusu ndoto.
  • 0:04 - 0:07
    nimekuwa mwota ndoto mzuri maisha yote,
  • 0:07 - 0:09
    na ni nzuri kuliko za kwenye filamu.
  • 0:09 - 0:11
    (kicheko)
  • 0:11 - 0:13
    zaidi ya kupaa, kupumua moto,
  • 0:13 - 0:16
    na kufanya wanaume wazuri
    watokee kwa ghafla ...
  • 0:16 - 0:18
    (kicheko)
  • 0:18 - 0:21
    Ninaweza kufanya vitu kama kusoma na
    kuandika muziki.
  • 0:21 - 0:25
    Cha kufurahisha ni kuwa niliandika
    habari yangu binafsi kwenda chuoni
  • 0:25 - 0:26
    nikiwa kwenye ndoto.
  • 0:26 - 0:29
    Na nilikubaliwa. Hivyo sawa.
  • 0:30 - 0:32
    Ninafikiri kwa namna ya picha.
  • 0:32 - 0:35
    Ninafikiri kwa picha, sio maneno.
  • 0:35 - 0:39
    Kwangu mimi, maneno ni kama
    lugha na hisia.
  • 0:40 - 0:42
    Kuna watu wengi kama mimi;
  • 0:42 - 0:44
    Nikola Tesla, kwa mfano,
  • 0:44 - 0:49
    ambaye anaweza kuona, kubuni,
    kupima na kutafuta suluhu kila kitu --
  • 0:49 - 0:53
    uvumbuzi wake wote --
    katika akili yake, kwa ufasaha.
  • 0:55 - 0:58
    Lugha ni kitu ambacho hakipo
    katika aina yetu, hata hivyo.
  • 0:58 - 1:00
    mimi ni mshamba kidogo,
  • 1:00 - 1:03
    kama toleo la beta la tafsiri ya Google.
  • 1:03 - 1:05
    (Kicheko)
  • 1:07 - 1:11
    Ubongo wangu una uwezo wa kuzingatia
    kwa hali ya juu kwenye vitu vinavyonivutia
  • 1:11 - 1:14
    Kwa mfano, niliwahi kuwa na mapenzi
    na hesabu za calculus
  • 1:14 - 1:17
    ambayo yalidumu kwa muda mrefu
    kuliko ndoa za watu maarufu.
  • 1:17 - 1:20
    (kicheko)
  • 1:21 - 1:23
    Kuna mambo mengine yasiyo ya kawaida
    kuhusu mimi.
  • 1:24 - 1:27
    utakuwa umegundua kuwa
    sina mawimbi
  • 1:27 - 1:28
    kwenye sauti yangu
  • 1:28 - 1:32
    Ndio mana watu
    hunichanganya mimi na GPS.
  • 1:32 - 1:35
    (Kicheko)
  • 1:36 - 1:40
    Hii inafanya mawasiliano kuwa changamoto,
    labda kama unahitaji maelekezo.
  • 1:40 - 1:44
    (kicheko)
  • 1:44 - 1:46
    Asante.
  • 1:46 - 1:50
    (Makofi)
  • 1:51 - 1:54
    Miaka michache iliyopita,
    nilipoanza kufanya mawasilisho,
  • 1:54 - 1:56
    Nilikwenda kupigwa shoti za kichwa
    kwa mara ya kwanza.
  • 1:57 - 2:00
    Mpiga picha aliniambia nijiweke kichafu.
  • 2:00 - 2:02
    (kicheko)
  • 2:02 - 2:05
    Sikuwa ninafahamu
    alichokuwa anamaanisha
  • 2:05 - 2:07
    (kicheko)
  • 2:07 - 2:09
    Akasema, "fanya kile kitu,
    unajua, kwa macho yako,
  • 2:09 - 2:11
    pale unapo washawishi wanaume."
  • 2:11 - 2:13
    "kitu gani?" nikauliza.
  • 2:14 - 2:15
    "unajua, macho".
  • 2:16 - 2:17
    Hivyo nikajaribu, kiukweli.
  • 2:17 - 2:19
    Ikatokea kitu kama hiki.
  • 2:19 - 2:22
    (kicheko)
  • 2:22 - 2:24
    Nikaonekana kama aliyekuwa anatafuta Waldo.
  • 2:25 - 2:27
    (kicheko)
  • 2:29 - 2:30
    Kuna sababu kuhusu hili,
  • 2:30 - 2:33
    kama ambavyo iko sababu ya Waldo kujificha.
  • 2:33 - 2:37
    (kicheko)
  • 2:41 - 2:43
    Nina Aspega
  • 2:43 - 2:45
    aina ya usonji wenye uwezo mkubwa
  • 2:45 - 2:48
    ambayo inaharibu ujuzi wa kijamii
    ambao mtu anategemewa kuuonyesha.
  • 2:51 - 2:54
    Inafanya maisha kuwa magumu kwa namna nyingi,
  • 2:54 - 2:58
    na nilipokuwa nakuwa,
    nilipata ugumu kuishi na jamii.
  • 2:58 - 3:02
    Marafiki zangu walisema vichekesho,
    lakini sikuweza kuwaelewa.
  • 3:02 - 3:07
    Mashujaa wangu walikuwa George Carlin
    na Stephen Colbert --
  • 3:07 - 3:09
    na walinifundisha ucheshi.
  • 3:11 - 3:15
    Haiba yangu ikabadilika
    kutoka kuwa na aibu na wa ajabu
  • 3:15 - 3:18
    kuwa mtukutu na ninayesababisha dhoruba
  • 3:18 - 3:21
    Sina haja ya kusema,
    Sikuwa na marafiki wengi.
  • 3:22 - 3:24
    Lakini pia nilikuwa na hisia kali na
    hali za vitu.
  • 3:25 - 3:28
    Hisia ya maji kwenye ngozi yangu
    ilikuwa kama sindano na pini,
  • 3:28 - 3:31
    hivyo kwa miaka mingi, nilikataa kuoga.
  • 3:31 - 3:35
    ninakuhakikishia hali yangu ya usafi
    iko kwa viwango kwa sasa, hata hivyo.
  • 3:35 - 3:37
    (Kicheko)
  • 3:38 - 3:43
    Ilinibidi kufanya kazi kubwa kufika hapa,
    na wazazi wangu --
  • 3:43 - 3:48
    mambo kidogo yalikwenda mrama
    nilipodhalilishwa kingono na mtu wa rika langu,
  • 3:48 - 3:52
    na juu ya mambo yote,ilifanya
    hali mbaya kuwa mbaya zaidi.
  • 3:53 - 3:59
    Nikapaswa kusafiri maili 2000
    ndani ya nchi kupata matibabu,
  • 3:59 - 4:03
    lakini siku chache baada ya
    kupewa dawa mapya,
  • 4:03 - 4:05
    maisha yangu yakageuka kuwa
    kipindi cha mfu anayetembea.
  • 4:06 - 4:09
    Nikawa mtu wa ajabu na kikaanza
    kuona vitu ambavyo havipo.
  • 4:09 - 4:12
    kwamba maiti zilizooza
    zinanijia.
  • 4:13 - 4:16
    hatimaye familia yangu ikaninusuru,
  • 4:16 - 4:20
    lakini kwa wakati huo, nilipoteza
    paundi 19 katika wiki tatu,
  • 4:20 - 4:23
    pamoja na kuanza kuwa na tatizo
    la kupungukiwa damu,
  • 4:23 - 4:25
    na nilifikia kutaka kujiua.
  • 4:26 - 4:31
    Nilienda kwenye kituo kingine cha matibabu
    ambacho kilielewa machukizo yangu,
  • 4:31 - 4:35
    taabu yangu, na hofu yangu ya kijamii.
  • 4:35 - 4:38
    na walifahamu namna ya kunitibu,
    na nilipata msaada niliouhitaji.
  • 4:38 - 4:41
    Na baada ya miezi 18 ya kazi ngumu,
  • 4:41 - 4:44
    Nikaenda kufanya mambo ya ajabu.
  • 4:45 - 4:48
    Kitu kimojawapo kuhusu Aspegaz
    ni kwamba mara kwa mara,
  • 4:48 - 4:50
    hawa watu huwa wana
    utu wa ndani mtata sana,
  • 4:50 - 4:53
    na mimi ninajifahamu,
    nina haiba ya kuvutia sana,
  • 4:53 - 4:57
    maoni mazuri, na vitu vingi
    vinavyoendelea kwenye akili yangu.
  • 4:57 - 5:00
    Lakini kuna mwanya kati
    ya mahali hilo linasimama,
  • 5:00 - 5:03
    na jinsi ninavyowasilisha
    hayo kwa ulimwengu unaonizunguka.
  • 5:03 - 5:07
    Na hii inaweza kufanya
    mawasiliano ya kawaida kuwa na changamoto.
  • 5:08 - 5:11
    Sio sehemu nyingi zinaweza kuniajiri,
    kwa sababu ya ukosefu wa stadi za kijamii,
  • 5:11 - 5:14
    Ndio maana niliomba kazi Waffle House.
  • 5:14 - 5:19
    (Kicheko)
  • 5:20 - 5:24
    Waffle House ni mgahawa wa
    masaa 24 ---
  • 5:24 - 5:26
    (Kicheko)
  • 5:26 - 5:29
    (Makofi)
  • 5:29 - 5:31
    Asante --
  • 5:31 - 5:33
    ambapo unaweza kuagiza hasi brown
  • 5:33 - 5:36
    kwa namna nyingi ambavyo
    mtu anaweza kutupa mzoga wa binadamu ...
  • 5:36 - 5:38
    (kicheko)
  • 5:38 - 5:42
    imekatwa, ina pilipili, imewekwa topin,
    iko vipande, na imefunikwa.
  • 5:42 - 5:44
    (kicheko)
  • 5:44 - 5:46
    Kama taratibu za kijamii zinavyoweka,
  • 5:46 - 5:49
    unatakiwa kwenda Waffle House
    mida isiyo ya kawaida usiku tu.
  • 5:49 - 5:51
    (kicheko)
  • 5:51 - 5:55
    Hivyo siku moja, saa 8 alfajiri, nilikuwa
    naongea na muhudumu, nikamuuliza,
  • 5:55 - 5:58
    "nikitu gani cha ajabu kimewahi kukutokea
    katika kazi yako?"
  • 5:59 - 6:02
    Na akaniambia wakati mmoja,
    mwanaume aliingia akiwa uchi kabisa.
  • 6:02 - 6:03
    (kicheko)
  • 6:04 - 6:06
    Nikasema "vyema! niweke mimi
    kwenye zamu ya makaburini!"
  • 6:06 - 6:09
    (kicheko)
  • 6:09 - 6:12
    Sina haja ya kusema,
    Waffle House hawakuniajiri.
  • 6:14 - 6:18
    Hivyo kwa habari ya kuwa na Aspegaz,
    inaweza kuonekana kama tatizo,
  • 6:18 - 6:20
    na wakati mwingine ni
    maumivu halisi ya kitako,
  • 6:20 - 6:22
    lakini pia ni kinyume chake.
  • 6:22 - 6:26
    Ni zawadi, na inaniruhusu mimi
    kuwaza kiuvumbuzi.
  • 6:27 - 6:34
    Nikiwa na miaka 19, nilishinda shindano
    la utafiti, katika tafiti yangu ya miamba maji,
  • 6:34 - 6:35
    Na nikaishia kuzungumza
  • 6:35 - 6:37
    Katika kongamano la UN
    la utofauti wa kibayolojia,
  • 6:37 - 6:39
    nikiwasilisha utafiti huu.
  • 6:39 - 6:41
    (Makofi)
  • 6:41 - 6:42
    Asante.
  • 6:42 - 6:47
    (Makofi)
  • 6:47 - 6:51
    Na nikiwa na miaka 22, ninajiangaa
    kumaliza chuo,
  • 6:51 - 6:55
    na ni mwanzilishi-mwenza wa kampuni
    ya kibayoteki inayoitwa AutismSees.
  • 6:56 - 6:57
    (Makofi)
  • 6:57 - 6:59
    Asante.
  • 6:59 - 7:01
    (Makofi)
  • 7:01 - 7:04
    Lakini ukizingatia yale niliyofanya
    ili kufika hapa:
  • 7:04 - 7:10
    wataalamu 25, kukusea vipimo 11,
    na miaka ya maumivu na kiwewe.
  • 7:11 - 7:14
    Nimetumia muda mwingi kuwaza
    kama kuna njia nzuri zaidi,
  • 7:14 - 7:18
    Na ninadhani ipo:
    teknolojia ya kusaidia-usonji.
  • 7:19 - 7:21
    Teknolojia hii
    itafanya kazi muhimu
  • 7:21 - 7:23
    katika kuwasaidia watu
    wenye tatizo la usonji,
  • 7:23 - 7:25
    au ASD.
  • 7:26 - 7:31
    podium ya programu, iliyoachiliwa
    na kampuni yangu, AutismSees,
  • 7:31 - 7:37
    inauwezo wa kuchunguza kibinafsi
    na kusaidia kuendeleza ujuzi wa mawasiliano.
  • 7:37 - 7:42
    Zaidi ya hapo, inafuatilia
    kutizama kwa macho kupitia kamera
  • 7:42 - 7:48
    na inaigiza mazungumzo ya halaiki
    na uzoefu wa mahojiano ya kazi.
  • 7:49 - 7:51
    Na hivyo labda siku moja,
    Waffle House wanaweza kuniajiri,
  • 7:51 - 7:53
    Baada ya kuifanyia mazoezi kwa muda.
  • 7:53 - 7:55
    (kicheko)
  • 7:57 - 8:03
    Na moja ya kitu kizuri zaidi
    ni kuwa nimetumia Podium
  • 8:03 - 8:08
    kunisaidia kujiandaa kwa leo,
    na imekuwa ya msaada mkubwa.
  • 8:08 - 8:09
    Lakini ni zaidi ya hapo.
  • 8:09 - 8:11
    Kuna la zaidi laweza kufanyika.
  • 8:12 - 8:15
    Kwa watu wenye ASD --
  • 8:15 - 8:20
    Imekuwa ikidhaniwa
    kuwa wavumbuzi wengi wa kisayansi,
  • 8:20 - 8:25
    watafiti, wasanii
    na wahandisi wanayo;
  • 8:25 - 8:31
    kama, mfano, Emily Dickinson,
    Jane Austen, Isaac Newton, and Bill Gates
  • 8:31 - 8:32
    ni baadhi ya mifano.
  • 8:32 - 8:34
    Lakini tatizo linalokuwepo
  • 8:34 - 8:38
    ni kuwa haya maoni mazuri
    mara nyingi hayawezi shirikishwa
  • 8:38 - 8:40
    kama kuna ukinzani wa mawasiliano.
  • 8:41 - 8:46
    Na hivyo watu wengi wenye usonji
    wanapitwa bila kuonekana kila siku,
  • 8:46 - 8:48
    na pia wanachukuliwa faida yao.
  • 8:49 - 8:56
    Hivyo ndoto yangu kwa watu wenye usonji
    ni kubadilisha hiyo,
  • 8:56 - 8:59
    na kuondoa ukinzani
    unaowazuia wao kufanikiwa.
  • 9:00 - 9:02
    Sababu moja wapo ninayopendelea
    kuota ndoto
  • 9:02 - 9:05
    ni kwasababu inaniruhusu kuwa huru,
  • 9:05 - 9:09
    bila kuhukumiwa na jamii
    na kupata madhara halisi.
  • 9:10 - 9:13
    Ninapopaa juu ya mandhari
    ninazozitengeneza kwenye akili yangu,
  • 9:13 - 9:14
    Ninakuwa na amani.
  • 9:15 - 9:17
    Niko huru na hukumu,
  • 9:17 - 9:19
    na ninaweza kufanya chochote nitakacho, unafahamu?
  • 9:19 - 9:24
    ninatengeneza na Brad Pitt,
    na Angelina hajali kabisa kuhusu hilo.
  • 9:24 - 9:26
    (Kicheko)
  • 9:28 - 9:32
    Lakini lengo la teknolojia ya
    usaidizi-usonji ni kubwa zaidi ya hilo,
  • 9:32 - 9:33
    na muhimu zaidi.
  • 9:34 - 9:38
    Lengo langu ni kubadili mitazamo ya watu
  • 9:38 - 9:43
    kuhusu usonji na watu wenye
    Aspegaz yenye uwezo mkubwa
  • 9:43 - 9:47
    kwa sababu kuna vitu vingi wanawezafanya.
  • 9:47 - 9:50
    Ninamaanisha, angalia
    Temple Grandin, kwa mfano.
  • 9:50 - 9:55
    Na kwa kufanya hivyo, tunaruhusu watu
    kushirikisha vipaji vyao kwa ulimwengu
  • 9:55 - 9:58
    na kufanya ulimwengu usonge mbele.
  • 9:58 - 10:01
    kwa kuongeza, tunawapa ujasiri
    kufuatilia ndoto zao
  • 10:01 - 10:03
    katika ulimwengu halisi, na wakati halisi.
  • 10:03 - 10:04
    Asanteni.
  • 10:04 - 10:08
    (Makofi)
  • 10:08 - 10:09
    Asante.
  • 10:09 - 10:13
    (Makofi)
Title:
Jinsi nilivyojifunza kuwasilisha maisha yangu nikiwa na Aspegaz
Speaker:
Alix Generous
Description:

Alix Generous ni mwanamke mdogo mwenye maoni milioni na moja - amefanya sayansi ya kushinda tuzo, amesaidia kutengeneza teknolojia na anaongea kwa utani mzuri( utamuona). Ana Aspegaz, aina ya usonji unaoweza kuharibu ujuzi wa kawaida wa kijamii unaohitajika kuwasiliana, na amefanya kazi ngumu kwa miaka kujifunza namna ya kushirikisha mawazo yake kwa ulimwengu. Katika haya mazungumzo ya kufurahisha, ya kibinafsi, anaelezea hadithi yake - na maono yake kwa nyenzo itakayosaidia watu wengi kuwasilisha maoni yao makubwa.

more » « less
Video Language:
English
Team:
closed TED
Project:
TEDTalks
Duration:
10:26

Swahili subtitles

Revisions