Angela Lee Duckworth:Ufunguo wa Mafanikio? Uvumilivu na Shauku.
-
0:01 - 0:03Nilipokuwa na miaka 27
-
0:03 - 0:06niliacha kazi ya kuchukua muda sana kama mshauri wa utawala
-
0:06 - 0:11kufanya kazi inayochukua muda zaidi sana ya kufundisha.
-
0:11 - 0:14Nilienda kufundisha hisabati, watoto wa darasa la saba.
-
0:14 - 0:16Katika shule ya serikali ya New York.
-
0:16 - 0:19Na kama Mwalimu yeyote, niliandaa majaribio na mitihani.
-
0:19 - 0:21Nilitoa pia mazoezi ya nyumbani
-
0:21 - 0:24Kazi ziliporudishwa, nikafanya mahesabu ya alama walizopata.
-
0:24 - 0:29Kilichonishangaza ni kuwa I.Q haikuwa tofauti pekee
-
0:29 - 0:33kati ya wanafunzi wanaofanya vizuri sana na wale waliofanya vibaya sana.
-
0:33 - 0:35Baadhi ya wale wazuri sana
-
0:35 - 0:38hawakuwa na I.Q za juu sana.
-
0:38 - 0:42walikuwa hawafanyi vizuri sana.
-
0:42 - 0:44na hii ikanifanya nifikiri.
-
0:44 - 0:47Vitu unavyohitaji kujifunza darasa la saba
-
0:47 - 0:51ni kweli vigumu kama: uwiano,desimali,
-
0:51 - 0:52eneo la msambamba.
-
0:52 - 0:55lakini dhana hizi sio ngumu,
-
0:55 - 0:59na niliamini kuwa wanafunzi wangu
-
0:59 - 1:02wanaweza kujifunza vitu hivi
-
1:02 - 1:05kama wakijituma kwa bidii.
-
1:05 - 1:07Baada ya miaka kadhaa ya kufundisha,
-
1:07 - 1:11nilipata hitimisho kuwa tunachohitaji katika elimu
-
1:11 - 1:14ni ufahamu mzuri zaidi wa wanafunzi na usomaji
-
1:14 - 1:17kwa kuangalia upande wa uhimizaji
-
1:17 - 1:20kwa kuangalia upande wa kisaikolojia
-
1:20 - 1:24Katika elimu,kitu tunachokipima vizuri
-
1:24 - 1:30ni I.Q, lakini vipi kama kufanikiwa shuleni na katika maisha
-
1:30 - 1:32inategemea zaidi
-
1:32 - 1:36ya uwezo wako wa kusoma haraka na kirahisi?
-
1:36 - 1:38Nikaondoka darasani,
-
1:38 - 1:42na nikaenda katika masomo ya uzamili ili kuwa mwanasaikolojia
-
1:42 - 1:44nikaanza kujifunza kuhusu watoto na watu wazima
-
1:44 - 1:47katika mazingira magumu mbalimbali,
-
1:47 - 1:49na katika kila utafiti swali langu lilikuwa,
-
1:49 - 1:52ni nani ambaye amefanikiwa hapa na kwa nini?
-
1:52 - 1:56Timu yangu ya watafiti na mimi tulienda katika chuo cha kijeshi cha West Point.
-
1:56 - 1:58Tulijaribu kutabiri makadeti gani
-
1:58 - 2:02watakaa katika mafunzo na wale ambao watashindwa na mafunzo
-
2:02 - 2:04Tukaenda shindano la taifa la kutamka herufi
-
2:04 - 2:07na kutabiri watoto gani wataendelea mpaka
-
2:07 - 2:10mwisho wa shindano.
-
2:10 - 2:11Tuliwatafiti walimu wapya
-
2:11 - 2:15wanaofanya kazi katika maeneo magumu sana, tukiuliza
-
2:15 - 2:17walimu gani wataendelea kuwepo wakifundisha
-
2:17 - 2:19mpaka mwisho wa mwaka wa masomo,
-
2:19 - 2:22na kati yao,yupi atakuwa amefanikiwa
-
2:22 - 2:25kuongeza uwezo wa kimasomo wa wanafunzi wake?
-
2:25 - 2:28Tulishirikiana na kampuni binafsi, tukiuliza
-
2:28 - 2:30kati ya watu kadhaa wa masoko ni yupi atakayeendelea kuwa kazini?
-
2:30 - 2:33na yupi atapata pesa nyingi zaidi?
-
2:33 - 2:35katika mazingira hayo mbalimbali,
-
2:35 - 2:38kitu kimoja kiliibuka
-
2:38 - 2:40kama kiashiria muhimu cha mafanikio.
-
2:40 - 2:43haikuwa uwezo wa kufikiri.
-
2:43 - 2:48haikuwa mwonekano wa kuvutia,afya nzuri na haikuwa I.Q
-
2:48 - 2:50ilikuwa ni uvumilivu na shauku
-
2:50 - 2:55ni shauku na uvumilivu wa malengo ya muda mrefu.
-
2:55 - 2:57ni kuwa na stamina.
-
2:57 - 3:01ni kung'ang'ania kila siku,
-
3:01 - 3:05si kwa wiki moja, si kwa mwezi mmoja,
-
3:05 - 3:08lakini ni kwa miaka, ma kufanya kazi kwa bidii
-
3:08 - 3:11na kufanya maisha yako ya baadaye kuwa kitu halisi.
-
3:11 - 3:16ni kuishi maisha kama mbio ndefu za marathon na sio mbio fupi.
-
3:16 - 3:19Miaka michache iliyopita nilianza, kujifunza kuhusu hali hii
-
3:19 - 3:21katika shule za serikali za mji wa Chicago.
-
3:21 - 3:23niliwaomba maelfu ya wanafunzi wa sekondari
-
3:23 - 3:25kujibu dodoso kuhusu hali hii
-
3:25 - 3:27baadae nikasubiri zaidi ya mwaka mmoja
-
3:27 - 3:29kuangalia ni nani atakayehitimu.
-
3:29 - 3:32inaonekana watoto wenye shauku na uvumilivu huu sana
-
3:32 - 3:35walikuwa na nafasi kubwa zaidi ya kuhitimu,
-
3:35 - 3:39hata pale nilipolinganisha vigezo mbalimbali,
-
3:39 - 3:41vigezo kama kipato cha familia,
-
3:41 - 3:44matokeo ya mitihani ya kupima uwezo,
-
3:44 - 3:47hata watoto walivyojisikia salama wakiwa shuleni.
-
3:47 - 3:50Kwa hiyo si tu katika chuo cha Westpoint au shindano la taifa la kutamka herufi
-
3:50 - 3:53shauku na uvumilivu huu unapokuwa na maana,lakini shuleni,
-
3:53 - 3:57zaidi sana kwa watoto walio hatarini kuacha masomo.
-
3:57 - 4:00Kwangu kitu cha kushangaza kuhusu shauku na uvumilivu huu
-
4:00 - 4:02ni jinsi tusivyofahamu mengi kuhusu hali hii
-
4:02 - 4:05jinsi kidogo sana sayansi inavyojua, kuhusu kuijenga.
-
4:05 - 4:07Kila siku, wazazi na walimu wananiuliza,
-
4:07 - 4:09"Ninaijengaje hali hii ndani ya watoto"?
-
4:09 - 4:13nifanyeje kuwafundisha watoto umuhimu wa kazi?
-
4:13 - 4:16nifanyeje kuwamasisha kwa muda mredu zaidi?"
-
4:16 - 4:20Jibu ni kuwa sijui.(vicheko)
-
4:20 - 4:23nachojua ni kuwa kipaji hakikusaidii kuwa na hali hii.
-
4:23 - 4:26Taarifa zetu zinaonyesha wazi wazi
-
4:26 - 4:28kuwa wapo wengi wenye vipaji mbalimbali
-
4:28 - 4:32lakini wanshindwa kutimiza majukumu yao.
-
4:32 - 4:36na ukweli ni kwamba katika taarifa zetu,inaonyesha hakuna uhusiano
-
4:36 - 4:40wa aina yoyote na kipaji
-
4:40 - 4:44mpaka sasa,wazo zuri zaidi la kujenga hali hii kwa watoto nililolisikia
-
4:44 - 4:47ni kitu kinaitwa "ukuaji wa ufahamu."
-
4:47 - 4:50hili ni wazo liloanzishwa chuo kikuu cha Stanford
-
4:50 - 4:53na Carol Dweck, na ni imani kuwa
-
4:53 - 4:56uwezo wa kujifunza hauna mipaka,
-
4:56 - 4:59unaweza kubadilika kutokana na juhudi yako.
-
4:59 - 5:02Dr Dweck ameonyesha kuwa watoto wanaposoma na kujifunza
-
5:02 - 5:06kuhusu ubongo na jinsi unavyokua na kuongezeka
-
5:06 - 5:07unapokabiliana na changamoto,
-
5:07 - 5:11wanakuwa na nafasi kubwa ya kuvumilia wanaposhindwa,
-
5:11 - 5:14kwa kuwa hawaamini kuwa kushindwa
-
5:14 - 5:17kuwa ni hali ya kudumu.
-
5:17 - 5:21Kwa hiyo ukuaji wa ufahamu ni wazo zuri kwa kujenga hali hii.
-
5:21 - 5:23lakini tunahitaji zaidi.
-
5:23 - 5:24na hapa ndipo nitafunga maelezo yangu,
-
5:24 - 5:26kwa sababu ndipo tulipo.
-
5:26 - 5:28Hii ndiyo kazi iliyoko mbele yetu.
-
5:28 - 5:32Tunahitaji kuchukua mawazo yetu mazuri
-
5:32 - 5:34na kuyajaribu.
-
5:34 - 5:37Tunahitaji kupima kama tumefanikiwa,
-
5:37 - 5:41na tunahitaji kukubali kufeli,kutokuwa sahihi,
-
5:41 - 5:44kuanza upya na masomo tuliyojifunza.
-
5:44 - 5:47Kwa maneno mengine, tunahitaji kuwa na uvumilivu na shauku hii.
-
5:47 - 5:50kuwafanye watoto wetu kuwa na shauku na uvumilivu huu.
-
5:50 - 5:51Asante
-
5:51 - 5:56(Makofi)
- Title:
- Angela Lee Duckworth:Ufunguo wa Mafanikio? Uvumilivu na Shauku.
- Speaker:
- Angela Lee Duckworth
- Description:
-
Akiacha kazi ya hali ya juu sana ya ushauri, Angela Lee Duckworth alianza kazi ya kuwafundisha hisabati wanafunzi wa darasa la saba katika shuke ya serikali jijini New York.Mara moja aligundua kuwa IQ haikuwa sababu pekee inayotoafautisha wanafunzi wanaofanya vizuri na wale wasiofanya vizuri. Hapa anaeleza nadharia yake ya uvumulivu na shauku katika kufanya vitu kama kiashiria cha mafanikio.
- Video Language:
- English
- Team:
- closed TED
- Project:
- TEDTalks
- Duration:
- 06:12
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for The key to success? Grit | ||
Joachim Mangilima approved Swahili subtitles for The key to success? Grit | ||
Nelson Simfukwe accepted Swahili subtitles for The key to success? Grit | ||
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for The key to success? Grit | ||
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for The key to success? Grit | ||
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for The key to success? Grit | ||
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for The key to success? Grit | ||
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for The key to success? Grit |