Simulizi letu la ubakaji na maridhiano
-
0:00 - 0:03[Majadiliano yana lugha na maelezo ya ukatili wa kijinsia
-
0:03 - 0:05Mtazamaji anatahadharishwa]
-
0:05 - 0:08Tom Stranger: Mwaka 1996,
nilipokuwa nina miaka 18, -
0:08 - 0:11Nilipata fursa ya kusoma nchi ngeni,
-
0:12 - 0:16La kushangaza mimi ni mzaliwa wa Australia anayependa baridi ya haswa,
-
0:16 - 0:21hivyo nilikuwa na furaha na njonzi
nilipopanda ndege kwenda Iceland, -
0:21 - 0:24baada ya kuwaaga wazazi wangu na ndugu.
-
0:25 - 0:28Nilikaribishwa katika familia nzuri ya wana Iceland
-
0:28 - 0:29ambao walinichukua katika matembezi,
-
0:29 - 0:32na kunisaidia kuielewa lugha ya tuni ya wana Iceland.
-
0:33 - 0:36Mwanzo nilipambana na hisia za kutamani kurudi nyumbani
-
0:36 - 0:38Baada ya shule, nilicheza mchezo wa kuteleza juu ya barafu
-
0:38 - 0:40na kulala sana.
-
0:40 - 0:44Masaa mawili ya Kemia katika lugha ambayo bado hujaielewa,
-
0:44 - 0:46inaweza kukuweka kulala vizuri.
-
0:46 - 0:47(Vicheko)
-
0:49 - 0:51Mwalimu wangu ilipendekeza
nishiriki katika igizo shuleni, -
0:51 - 0:54ilinijumuike na wengine shuleni.
-
0:54 - 0:57Hata kama sikuwa sehemu ya igizo,
-
0:57 - 0:59hapo nilikutana na Thordis.
-
0:59 - 1:02Tulifurahia simulizi letu la penzi la ujanani,
-
1:02 - 1:04tulikula wote mchana, ili tu kushika mikono
-
1:04 - 1:06na kutembea jiji la Reykjavík.
-
1:07 - 1:10Nilikutana na familia yake,
naye alikutana na marafiki zangu. -
1:11 - 1:13Tulikuwa katika urafiki karibia zaidi ya mwezi
-
1:13 - 1:16wakati shule iliandaa sherehe ya Krismasi
-
1:18 - 1:21Thordis Elva: Nilikuwa miaka 16
na nimekutana penzi langu la kwanza. -
1:22 - 1:24Kwenda pamoja kwa sherehe ya Krismasi
-
1:24 - 1:26Ilikuwa uthibitisho wa uhusiano wetu,
-
1:26 - 1:29na nilijisikia kama msichana mwenye bahati sana duniani.
-
1:29 - 1:32Sio tena mtoto, lakini mwanamke.
-
1:33 - 1:35mkakamavu katika upevu wangu mpya,
-
1:35 - 1:39Niliamini kuwa kujaribu kunywa
kilo kwa mara ya kwanza, -
1:39 - 1:42ulikuwa uamuzi mbaya.
-
1:42 - 1:43Niliumwa sana,
-
1:43 - 1:45kupoteza fahamu na kutojielewa
-
1:45 - 1:48katika misukosuko ya kutapika.
-
1:48 - 1:51Walinzi walitaka kuniitia gari la wagonjwa,
-
1:51 - 1:54lakini Tom aliatokea kuwa mkombezi wangu,
-
1:54 - 1:56na kuwaambia atanipeleka nyumbani.
-
1:57 - 1:58Ilikuwa kama simulizi za vichimbakazi,
-
1:59 - 2:00mikono yake yenye nguvu ikinishikilia,
-
2:00 - 2:03kuniweka katika usalama wa kitanda changu.
-
2:04 - 2:08Lakini shukrani yang kwake iligeuka haraka kuwa woga
-
2:08 - 2:13aliponivua nguo na kupanda juu yangu.
-
2:13 - 2:15nilikuwa nimepata fahamu,
-
2:15 - 2:18lakini mwili wangu ulikuwa bado
dhaifu mno kupambana, -
2:18 - 2:20na maumivu yalikuwa makali.
-
2:21 - 2:23Nilidhani nimegawanywa mara mbili.
-
2:24 - 2:25Ili kubaki timamu,
-
2:25 - 2:29nilihesabu sekunde kwenye saa yangu.
-
2:30 - 2:31Na tangu usiku huo,
-
2:31 - 2:37Nimejua kwamba kuna sekunde 7200 katika masaa mawili.
-
2:39 - 2:42Pamoja na kuchechmea na kulia kwa mawiki,
-
2:42 - 2:47tukio hili halikuwakilisha mawazo yangu kuhusu ubakaji kama nilivyoona kwenye TV.
-
2:47 - 2:49Tom hakuwa mwendawazimu mwenye silaha;
-
2:49 - 2:51alikuwa mpenzi wangu.
-
2:51 - 2:54Na haikutokea katika mahali pa ajabu,
-
2:54 - 2:56ilitokea katika kitanda changu mwenyewe.
-
2:57 - 3:00nilipotambua kwamba nimebakwa,
-
3:00 - 3:02alikuwa amemaliza masomo yake
-
3:02 - 3:04na kurudi kwao Australia.
-
3:05 - 3:08Hivyo nilijiambia kuwa hakuna maana kufuatilia kilichotokea.
-
3:08 - 3:09Na zaidi,
-
3:09 - 3:12ilibidi iwe kosa langu.
-
3:13 - 3:15Nilikulia katika dunia
ambapo wasichana hufundishwa -
3:15 - 3:17kwamba wakibakwa ni kwa sababu.
-
3:18 - 3:20sketi zao ni fupi mno,
-
3:20 - 3:23tabasamu zao kubwa mno,
-
3:23 - 3:25pumzi yao inanuka kileo.
-
3:26 - 3:29Nilikuwa na hatia ya mambo hayo yote,
-
3:29 - 3:31hivyo aibu ilibidi iwe yangu.
-
3:32 - 3:33Ilinichukua miaka kutambua
-
3:33 - 3:37kwamba jambo moja tu ilngeweza kuzuia mimi kubakwa,
-
3:37 - 3:39haikuwa sketi yangu,
-
3:39 - 3:41haikuwa tabasamu langu,
-
3:41 - 3:43haikuwa imani yangu ya kitoto.
-
3:44 - 3:48Kitu pekee ambacho kingeweza kuzuia kubakwa
-
3:48 - 3:50ni aliyenibaka --
-
3:50 - 3:52kama angejizuia.
-
3:53 - 3:55TS: Sina kumbukumbu nzuri ya siku ya pili
-
3:56 - 3:58athari ya kileo,
-
3:58 - 4:01utupu niliojaribu kukandamiza.
-
4:02 - 4:03Hakuna cha ziada.
-
4:04 - 4:06Lakini sikuenda kwa Thordis.
-
4:07 - 4:09Sasa, ni muhimu kusema
-
4:09 - 4:12kwamba sikuona tendo langu kwa ubaya wake..
-
4:13 - 4:16Neno "ubakaji" halikuwepo katika mawazo yangu kama ilivyotakiwa,
-
4:17 - 4:20sikujisulibisha kwa kumbukumbu ya usiku uliopita.
-
4:22 - 4:24Hata haikuwa mimi kukataa kwa fahamu,
-
4:24 - 4:27ila zaidi kuwa kukiri ukweli wowote ni haramu.
-
4:28 - 4:32Tafsiri yangu ya matendo yangu yalikanusha kutambua
-
4:33 - 4:35madhara nilyomfanyia Thordis.
-
4:36 - 4:38Kusema ukweli,
-
4:38 - 4:42Nilikemea kitendo chote siku za baadaye
-
4:43 - 4:44na wakati nilikuwa natenda.
-
4:45 - 4:50Niliukataa ukweli kwa kuJIshawishi
ilikuwa ngono sio ubakaji. -
4:51 - 4:55Na huu ni uongo umekuwa ukiniwinda.
-
4:56 - 4:58Niliachana na Thordis siku kadhaa baadaye,
-
4:58 - 5:00nilimuona mara kadhaa
-
5:00 - 5:02katika muda wangu uliobaki Iceland,
-
5:02 - 5:05nilijisikia vibaya na roho nzito kila wakati.
-
5:06 - 5:10Ndani, nilijua nimekosa vibaya mno.
-
5:11 - 5:14Lakini bila kukusudia, nilikandamiza kumbukumbu yote
-
5:14 - 5:16ilikusahau kabisa.
-
5:18 - 5:20Kilichofuata ni miaka tisa
-
5:20 - 5:23ya "Kuukana na kuukimbia ukweli."
-
5:24 - 5:28Nilipopata nafasi ya kutambua
uhalisi wa unyama niliotenda, -
5:29 - 5:31sikuweza kustahamili.
-
5:32 - 5:34Nilihekaheka, iwe kwa
-
5:34 - 5:36matumizi ya madawa,
-
5:36 - 5:37kutafuta hatari
-
5:37 - 5:41au kukandamika hisia zangu,
-
5:41 - 5:43Nilikataa kukaa tuli na kimya.
-
5:45 - 5:46Na sauti hiyo,
-
5:46 - 5:49nilitafakari katika sehemu nyingine za maisha yangu
-
5:49 - 5:52ili kujenga picha ya mimi ni nani.
-
5:53 - 5:54Nilikuwa surfer,
-
5:54 - 5:56mwanafunzi wa sayansi za jami,
-
5:56 - 5:58rafiki kwa watu wema,
-
5:58 - 6:00kaka mpendwa na mwana,
-
6:00 - 6:02kiongozi wa burudani za nje ,
-
6:02 - 6:03na hatimaye, mfanyakazi wa mambo ya vijana.
-
6:04 - 6:08Nilshikilia imani kuwa sikuwa mtu mbaya.
-
6:09 - 6:12Sikudhani nilikuwa na ukatili katika mifupa yangu.
-
6:12 - 6:14Nilidhani nilikuwa tofauti.
-
6:15 - 6:16Katika malezi yangu,
-
6:16 - 6:19upendo wa familia na jamaa,
-
6:20 - 6:22watu wa karibu walikuwa wakarimu na wakweli
-
6:22 - 6:23katika heshima yao kwa wanawake.
-
6:25 - 6:30Ilinichukua muda mrefu kuangalia kona ya kiza changu,
-
6:30 - 6:31na kujiuliza maswali hayo.
-
6:34 - 6:36TE: Miaka tisa tangu ile sherehe ya Krismasi,
-
6:36 - 6:38Nilikuwa nina miaka 25,
-
6:38 - 6:40ninaelekea kuchanganyikiwa.
-
6:41 - 6:45thamani yangu ilizikwa na usiri
-
6:45 - 6:48ulionitenga kutoka kwa kila mtu niliyemjali,
-
6:48 - 6:51na chuki na hasira
-
6:51 - 6:53niliyoelekeza kwangu mwenyewe.
-
6:54 - 6:56Siku moja, nilitoka nje
kwa hasira na machozi -
6:56 - 6:58baada ya kugombana na mpendwa,
-
6:58 - 7:00na kuingia katika café,
-
7:00 - 7:02ambapo niliomba kalamu.
-
7:03 - 7:04Daima nilikuwa daftari pamoja nami,
-
7:05 - 7:08nikidai ilikuwa ni kwa ajili ya kuandika mawazo mapya,
-
7:08 - 7:13lakini ukweli ni kwamba nilihitaji
daima kuriaria, -
7:13 - 7:14kwa sababu katika wakati wa utulivu,
-
7:14 - 7:17nilijikuta nikihesabu sekunde tena.
-
7:18 - 7:23Lakini siku hiyo, nilistaajabu
jinsi maneno yalitoka kwenye kalamu yangu, -
7:23 - 7:26kuandika barua muhimu maishani
-
7:26 - 7:28kwa Tom.
-
7:28 - 7:32Pamoja na nakala ya ukatili alionitendea,
-
7:32 - 7:35maneno, "Nataka kutafuta msamaha"
-
7:35 - 7:37yalinishangaa,
-
7:37 - 7:39kunishangaza mimi hasa.
-
7:40 - 7:44Lakini ndani, niligundua hio
Ilikuwa ni njia ya kujikomboa mateso yangu, -
7:44 - 7:48kwa sababu, bila kujali kama alistahili msamaha wangu au la,
-
7:48 - 7:51mimi nilistahili amani.
-
7:51 - 7:54Kipindi changu cha aibu kimefika kikomo.
-
7:56 - 7:58Kabla ya kutuma barua,
-
7:58 - 8:00nilijitayarisha kwa kila aina
ya majibu hasi, -
8:00 - 8:04kuliko vote:
sikutarajia kupata jibu lolote. -
8:05 - 8:08Tokeo ambalo sikujiandaa tu
-
8:08 - 8:10ndilo nililopata-
-
8:10 - 8:15barua ya kukiri kutoka Tom, iliyojaa majuto.
-
8:16 - 8:20Yeye pia alikuwa amefungwa katika ukimya.
-
8:20 - 8:24Na huo ndio mwanzo wa mawasiliano ya yetu yaliyodumu miaka nane
-
8:24 - 8:27Mungu anajua haikuwa rahisi kamwe,
-
8:27 - 8:29lakini daima ukweli.
-
8:30 - 8:33Nilitua dhulma yote niliyobeba,
-
8:33 - 8:37na yeye, kwa moyo wote
alikiri alichofanya. -
8:37 - 8:40Mabadilishano yetu yakawa jukwaa la
-
8:40 - 8:42kuchambua matokeo ya usiku ule,
-
8:42 - 8:45na ilikuwa kila kitu,
kutoka maneno yaliyoumiza -
8:45 - 8:47hadi uponyaji kupita maelezo.
-
8:48 - 8:52Na bado, haikuwa kunipa amani.
-
8:52 - 8:56Labda kwa sababu barua pepe haikua binafsi ya kutosha,
-
8:56 - 8:58labda kwa sababu ni rahisi kuwa jasiri
-
8:58 - 9:02wakati unajificha nyuma ya kompyuta upande wa pili wa dunia
-
9:02 - 9:04Lakini tulianza mjadala
-
9:04 - 9:08niliyohisi ni lazima kuchunguza kikamilifu.
-
9:08 - 9:10Hivyo, baada ya miaka nane ya kuandikiana,
-
9:10 - 9:14na karibia miaka 16 tangia usiku ule,
-
9:14 - 9:18nilikwamua ujasiri kupendekeza:
-
9:18 - 9:19kwamba tukutane uso kwa uso
-
9:19 - 9:22kuongelea historia yetu na kumalizana kabisa.
-
9:25 - 9:28TS: Kijiografia, Iceland na Australia zipo hivi.
-
9:29 - 9:31Katikati, ni Afrika Kusini.
-
9:32 - 9:35Tuliamua kukutana mji wa Cape Town,
-
9:35 - 9:37kwa wiki moja.
-
9:38 - 9:42mji wenyewe ulikuwa ni uthibitisho fika kwa mazingira
-
9:42 - 9:45ya kufikia maridhiano
na msamaha. -
9:46 - 9:48Hakuna mahali pengine ambapo uponyaji wa mahusiano yamejaribiwa
-
9:49 - 9:50kama nchini Afrika Kusini.
-
9:51 - 9:55Kama taifa, Afrika Kusini walitaka
kuishi katika ukweli wa historia, -
9:55 - 9:57na kuwasikiliza maelezo ya historia yake.
-
9:59 - 10:03Kujua hii tu, athari ya Cape Town iliongezeka kwetu .
-
10:04 - 10:05Katika kipindi cha wiki hio,
-
10:05 - 10:08tulisimuliana hadithi ya maisha yetu kwa kila mmoja,
-
10:08 - 10:11kuanzia manzo hai mwisho.
-
10:11 - 10:14Na kuchambua historia yetu wenyewe.
-
10:16 - 10:18Tulifuata sera kali ya kuwa wakweli,
-
10:18 - 10:21hii ilimaanisha kujiweka wazi,
-
10:21 - 10:23uwazi kuhusu kasoro na mapungufu yetu.
-
10:24 - 10:26Kulikuwa na kukiri,
-
10:26 - 10:29na wakati ambapo sote hatukuweza kudhania kabisa
-
10:29 - 10:31maaumivu ya mwingine.
-
10:32 - 10:37Madhara ya ukatili wa kijinsia
yalisemwa kwa sauti na hisia, -
10:37 - 10:39uso kwa uso.
-
10:40 - 10:41Wakati mwingine,
-
10:42 - 10:44tuligundua ubayana uliyongezeka,
-
10:45 - 10:50na hata vicheko visivyotarajiwa
lakini vilitukomboa . -
10:51 - 10:53Ki ukweli,
-
10:53 - 10:56tulijitahidi kusikilizana kwa makini.
-
10:57 - 11:03Na hali halisi yetu binafsi ziliwasilihwa kwa uhalisia wake
-
11:03 - 11:06kwamba hatukuweza kufanya lolote
kuliko kurahisha uzito wa nafsi. -
11:09 - 11:13TE: Kutaka kulipiza kisasi
ni hisia ya kawaida kama binadamu -- -
11:13 - 11:14ya kiasili, hata.
-
11:15 - 11:17Nilichotaka kufanya kwa miaka yote
-
11:17 - 11:21ni kumdhuru Tom kama alivyoniumiza.
-
11:22 - 11:25Lakini sikupata njia ya kutoa chuki na hasira yangu,
-
11:25 - 11:27sina hakika kama ningekuwa nasimama hapa leo.
-
11:28 - 11:32Hivyo siyo kusema kwamba sikuwa na mashaka yangu njiani.
-
11:33 - 11:36Ndege ilipotua Cape Town,
-
11:36 - 11:38Nakumbuka kufikiri,
-
11:38 - 11:42"Kwa nini sikujipatia mtaalamu na chupa ya vodka
-
11:42 - 11:44kama mtu wa kawaida? "
-
11:44 - 11:47(Vicheko)
-
11:47 - 11:51Wakati mwingine, utafiti wetu
wa uelewa Cape Town -
11:51 - 11:53ulionekana kama jitihada isiyowezekana,
-
11:53 - 11:55na nilitaka kukata tu tamaa
-
11:55 - 11:57na kurudi nyumbani kwa mume wangu mpenzi, Vidir,
-
11:57 - 11:58na mtoto wetu.
-
12:00 - 12:02Lakini licha ya matatizo yetu,
-
12:02 - 12:07safari hii ilileta hisia ya ushindi
-
12:07 - 12:10kwamba mwanga umeshinda giza,
-
12:11 - 12:15kwamba kitu chema kinaweza kujengwa kutoka kwa magofu.
-
12:17 - 12:18Nilisoma mahali fulani
-
12:18 - 12:22kwamba unapaswa kujaribu na kuwa mtu uliyehitaji ulipokuwa mtoto.
-
12:22 - 12:23Na nilipokuwa kijana,
-
12:23 - 12:27Ningependa kujua kwamba aibu haikuwa yangu,
-
12:27 - 12:30kwamba kuna matumaini baada ya kubakwa,
-
12:30 - 12:31kwamba unaweza hata kupata furaha,
-
12:31 - 12:33kama niliyonayo na mume wangu leo.
-
12:34 - 12:38Ndiyo maana niliaanza kuandika niliporudi kutoka Cape Town,
-
12:38 - 12:41kitabu na mwandishi mwenzangu Tom,
-
12:41 - 12:44kwamba tuna imani kinaweza kuwa msaada kwa pande zote mbili,
-
12:44 - 12:47aliyetendwa na kutenda.
-
12:47 - 12:49Vinginevyo,
-
12:49 - 12:53ni hadithi tulipaswa kusikia tulipokuwa vijana.
-
12:55 - 12:57Kutokana na hali ya hadithi yetu,
-
12:57 - 12:59Najua maneno ambayo huambatana nayo -
-
13:00 - 13:02muathirika, mbakaji --
-
13:03 - 13:05na majina yanayotumika kuapanga dhana,
-
13:05 - 13:09lakini wanaweza pia huvua utu katika vidokezo yanavyomaanisha.
-
13:10 - 13:12Mtu anapoonyeshwa kama muathirika,
-
13:12 - 13:17ni rahisi sana kumpuuza kama bidhaa mbovu,
-
13:17 - 13:19fedheha,
-
13:19 - 13:20isiyo na thamani.
-
13:21 - 13:23Na vivyo hivyo, mara moja mtu
anapoitwa mbakaji, -
13:23 - 13:26ni rahisi zaidi kumuita zimwi -
-
13:27 - 13:28mnyama.
-
13:29 - 13:32Lakini ni jinsi gani tutaelewa
nini katika jamii -
13:32 - 13:33kinazalisha ukatili
-
13:33 - 13:38kama sisi kunataa kutambua
utu katika wale wanaoufanya? -
13:39 - 13:40
Na jinsi - -
13:40 - 13:42(Makofi)
-
13:42 - 13:47Na tunawezaje kuwawezesha waliopitia taabu kama hatuwathamini?
-
13:48 - 13:51Jinsi gani tunaweza kujadili ufumbuzi
kwa moja ya vitisho kubwa -
13:52 - 13:55katika maisha ya wanawake na watoto
duniani kote, -
13:55 - 13:59kama majina tunayotumia
ni sehemu ya tatizo? -
14:02 - 14:04TS: Nilichojifunza,
-
14:04 - 14:09matendo yangu usiku ule mwaka 1996
yalikuwa ya kibinafsi. -
14:10 - 14:12Nilijisikia kustahili mwili wa Thordis.
-
14:14 - 14:17Nilikuwa na misingi mizuri katika malezi na kijamii
-
14:17 - 14:19na mifano ya tabia usawa.
-
14:20 - 14:21Lakini katika tukio hilo,
-
14:21 - 14:23Nilichagua kufuata mifano mibaya.
-
14:24 - 14:27Ambayo wanawake walikuwa na thamani
ya chini , -
14:28 - 14:32na wanaume wana hati juu ya miili yao.
-
14:34 - 14:37Misukumo hii ilitokea nje kwangu.
-
14:38 - 14:40Ilikuwa mimi pekee katika chumba nifanya maamuzi,
-
14:40 - 14:42hakuna mtu mwingine.
-
14:43 - 14:45Unapokiri kosa
-
14:45 - 14:47na kweli kuchukua hatia kwa matendo yako,
-
14:48 - 14:51ninaamini mambo ya kushangaza yanaweza kutokea.
-
14:51 - 14:54Hiko nachoita kitendawili cha umiliki.
-
14:55 - 14:58Nilidhani ningeelemewa na uzito wa wajibu.
-
14:58 - 15:01Nilidhani cheti changu
cha ubinadamu kingechomwa moto. -
15:02 - 15:06Badala yake, nilipewa umiliki wa makosa yangu,
-
15:07 - 15:10na kutambua kwamba haikumiliki ukamilifu wa mimi ni nani.
-
15:11 - 15:13Kurahisisha,
-
15:13 - 15:17kitendo ulichofanya haliwezi kuwa Jumla ya nafsi na utu wako.
-
15:19 - 15:20Sauti katika kichwa changu zilikoma.
-
15:21 - 15:25Anasa ya kujihurumia iliyokuwa imekosa oksijeni,
-
15:25 - 15:29na kubadilishwa
na hewa safi ya kukubalika - -
15:31 - 15:35kukubalika kwamba nilimdhuru binadamu huyu wa ajabu anayesimama karibu na mimi;
-
15:35 - 15:41kukubalika kwamba mimi ni sehemu ya kundi kubwa la kutisha la wanaume
-
15:41 - 15:43ambao wamekuwa wakatili kwa wapenzi wao.
-
15:45 - 15:47Usidharau nguvu ya maneno.
-
15:48 - 15:53Kutubu kwa Thordis kwamba nilimbaka
ilibadili hiari yangu na mimi mwenyewe, -
15:53 - 15:54na pia na yeye.
-
15:56 - 15:57Lakini muhimu zaidi,
-
15:57 - 16:00lawama ilhamishwa kutoka kwa Thordis kwangu.
-
16:01 - 16:02Mara nyingi mno,
-
16:03 - 16:07wajibu ni ulitokana
kwa waathirika wa kike wa ukatili wa kijinsia, -
16:07 - 16:10na si kwa wanaume ambao kutunga yake.
-
16:11 - 16:12Mara nyingi mno,
-
16:12 - 16:17kuukana ukweli huwaacha wahusika mbali na ukweli.
-
16:19 - 16:22Kuna mazungumzo katika umma sasa,
-
16:22 - 16:25na kama watu wengi,
-
16:25 - 16:27tuna imanishwa na hamasa ndogo
-
16:27 - 16:30kwa majadiliano haya magumu
lakini muhimu. -
16:31 - 16:35Ninasikia wajibu kuongeza sauti zetu.
-
16:38 - 16:43TE: Tulichofanya sio formula tunayopendekeza kwa wengine.
-
16:43 - 16:49Hakuna mtu ana haki ya kuwaambia mtu mwingine namna ya kushughulikia maumivu yao
-
16:49 - 16:50au kosa lao mkuu.
-
16:51 - 16:54Kuvunja ukimya yako si rahisi kamwe,
-
16:54 - 16:56na kutegemea ni wapi katika dunia ulipo,
-
16:56 - 16:59inaweza hata kuwa ni kifo
kuzungumzia kuhusu ubakaji. -
17:00 - 17:04Nimetambua hata tukio baya la maisha yangu,
-
17:04 - 17:07bado ni ushahidi wa upendeleo kwangu,
-
17:07 - 17:10kwa sababu naweza kuzugumzia bila hofu ya unyanyapaa
-
17:10 - 17:12au hata kuuawa.
-
17:12 - 17:15Lakini pamoja na upendeleo wa kuwa na sauti
-
17:15 - 17:18huja wajibu wa kuitumia.
-
17:19 - 17:23Hiyo ni angalau mimi deni
langu kwa wenzangu wasiyoweza. -
17:25 - 17:28hadithi tuliyowasilisha ni ya kipekee,
-
17:28 - 17:33na bado ni ukatili wa kijinsia ni janga la kimataifa.
-
17:33 - 17:35Lakini haifai kuwa njia hivyo.
-
17:36 - 17:39Moja ya mambo nimeona muhimu
katika safari yangu ya uponyaji -
17:39 - 17:41ni kujielimisha kuhusu ukatili wa kijinsia.
-
17:41 - 17:44Na matokeo yake,
Nimekuwa nikisoma, kuandika -
17:44 - 17:47na kuzungumzia suala hili kwa zaidi ya muongo mmoja sasa,
-
17:47 - 17:49kwenda katika makongamano duniani kote.
-
17:49 - 17:51Katika uzoefu wangu,
-
17:51 - 17:56wanaohudhuria mijadala hayo
ni karibia wanawake pekee. -
17:57 - 18:04Lakini ni wakati tuache kuona
unyanyasaji wa kijinsia kama ya tatizo la wanawake tu. -
18:04 - 18:09(Makofi)
-
18:17 - 18:21Ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na wanaume
-
18:21 - 18:23unaofanywa na wanaume.
-
18:23 - 18:27Na bado sauti zao haziwakilishwi ipasavyo katika mjadala huu.
-
18:29 - 18:33Lakini sisi sote tunahitajika hapa.
-
18:34 - 18:38Fikiria mateso tunaweza kupunguza
-
18:38 - 18:42kama sisi alijitokeza uso suala hili kwa pamoja.
-
18:43 - 18:44Asanteni.
-
18:44 - 18:48(Makofi)
- Title:
- Simulizi letu la ubakaji na maridhiano
- Speaker:
- Thordis Elva, Tom Stranger
- Description:
-
Mwaka 1996, Elva Thordis alifurahia penzi la utotoni na Tom Stranger, mwanafunzi kutoka Australia. Baada ya sherehe ya Krismasi shuleni, Tom alimbaka Thordis, nahawakukutani baada ya miaka mingi. Katika majadiliano hayo ya ajabu, Elva na Stranger wanazungumzia miaka ya kuishi katika aibu na usiri, na kutualika kujadili changamoto ya hii kimataifa juu ya unyanyasaji wa kijinsia katika uaminifu mpya.
Kwa mjadala, tembelea go.ted.com/thordisandtom.
- Video Language:
- English
- Team:
- closed TED
- Project:
- TEDTalks
- Duration:
- 22:48
Joachim Mangilima approved Swahili subtitles for Our story of rape and reconciliation | ||
Joachim Mangilima accepted Swahili subtitles for Our story of rape and reconciliation | ||
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for Our story of rape and reconciliation | ||
Sophia Mwema edited Swahili subtitles for Our story of rape and reconciliation | ||
Sophia Mwema edited Swahili subtitles for Our story of rape and reconciliation | ||
Sophia Mwema edited Swahili subtitles for Our story of rape and reconciliation | ||
Sophia Mwema edited Swahili subtitles for Our story of rape and reconciliation | ||
Sophia Mwema edited Swahili subtitles for Our story of rape and reconciliation |