Return to Video

Jinsi mbio za magari zinavyoweza kuwasaidia watoto wachanga?

  • 0:00 - 0:03
    Mbio za magari ni biashara ya zamani ya kufurahisha
  • 0:03 - 0:05
    Tunatengeneza gari jipya kila mwaka,
  • 0:05 - 0:07
    halafu tunatumia msimu wote
  • 0:07 - 0:10
    kujaribu kuelewa ni nini ambacho tumekijenga
  • 0:10 - 0:13
    kuifanya iwe bora zaidi, na kuifanya iende kasi zaidi.
  • 0:13 - 0:16
    halafu mwaka unaofuata, tunaanza upya.
  • 0:16 - 0:21
    Gari lililo mbele yako
  • 0:21 - 0:24
    chesisi inaundwa na vifaa mbalimbali takribani 11,000
  • 0:24 - 0:27
    Injini vingine 6000,
  • 0:27 - 0:30
    vya elektroniki takriban 8500
  • 0:30 - 0:34
    kwa hiyo kuna vitu kama 25,000 hivi vinavyoweza kuharibika.
  • 0:34 - 0:39
    kwa umakini wa hali ya juu ni muhimu sana katika mbio za magari
  • 0:39 - 0:42
    Kitu kingine kuhusu mbio za magari hasa ya langa langa
  • 0:42 - 0:44
    ni kwamba kila wakati tunabadilisha gari.
  • 0:44 - 0:47
    Kila wakati tunajaribu kulifanya bora zaidi.
  • 0:47 - 0:50
    Kila baada ya wiki mbili, tunakuwa tunatengeneza
  • 0:50 - 0:54
    vifaa vipya 5000 kwa ajili ya kuweka katika gari.
  • 0:54 - 0:56
    asilimia 5 mpaka 10 ya gari la mbio.
  • 0:56 - 1:00
    linabadilishwa kila baada ya wiki mbili.
  • 1:00 - 1:02
    Kwa hiyo tunafanyaje haya yote?
  • 1:02 - 1:06
    Tunaanza na gari la mashindano,
  • 1:06 - 1:10
    Tuna vifaa vya kupima mambo mbalimbali vingi sana.
  • 1:10 - 1:12
    katika gari la mashindano mbele
  • 1:12 - 1:15
    kuna vifaa vya kupima mambo mbalimbali kama 120 linapoenda mashindanoni.
  • 1:15 - 1:19
    vinapima vitu mbalimbali katika gari
  • 1:19 - 1:21
    Taarifa zinawekwa katika kumbukumbu. tunatunza kumbukumbu
  • 1:21 - 1:24
    500 mbalimbali za vitu mbalimbali,
  • 1:24 - 1:28
    vitu mbalimbali kuhusu afya ya gari na matukio
  • 1:28 - 1:33
    kuelezea mambo yanapoenda vibaya,
  • 1:33 - 1:35
    tunatuma taarifa hizi kwenda kitengo cha matengenezo
  • 1:35 - 1:40
    Kwa kutumia kifaa cha kupima taarifa mbalimbali
  • 1:40 - 1:43
    kila masaa mawili ya mbio,kila gari linatuma
  • 1:43 - 1:46
    namba 750 millioni
  • 1:46 - 1:49
    hiyo ni mara mbili ya maneno ambayo
  • 1:49 - 1:50
    tunazungumza katika maisha yetu
  • 1:50 - 1:53
    ni kiasi kikubwa cha taarifa.
  • 1:53 - 1:56
    lakini haitoshi tu, kuwa na taarifa na vipimo.
  • 1:56 - 1:58
    unahitaji kuwa na uwezo wa kuzifanyia kazi.
  • 1:58 - 2:00
    Kwa hiyo tumetumia muda mwingi na juhudi
  • 2:00 - 2:02
    kubadilisha taarifa kuwa hadithi
  • 2:02 - 2:05
    ili kuweza kueleza, hali ya injini,
  • 2:05 - 2:08
    Matairi yanachoka vipi,
  • 2:08 - 2:11
    mafuta yanatumikaje?
  • 2:11 - 2:14
    hiyo yote inachukua taarifa
  • 2:14 - 2:18
    na kuzibadilisha kuwa maarifa tunayoweza kujifunza.
  • 2:18 - 2:21
    Sawa,kwa hiyo tuangalie kidogo kuhusu taarifa.
  • 2:21 - 2:23
    tuangalie kiasi kidogo cha taarifa kutoka
  • 2:23 - 2:26
    kwa mgonjwa wa miezi mitatu.
  • 2:26 - 2:30
    Huyu ni mtoto, na unachokiona hapa ni taarifa halisi,
  • 2:30 - 2:32
    na upande huu wa kulia,
  • 2:32 - 2:34
    mahali ambapo kila kitu kiaanza kuwa cha hatari,
  • 2:34 - 2:38
    ambapo mgonjwa anapata mshituko wa moyo.
  • 2:38 - 2:41
    inaonekana kuwa ni tukio lisilotabirika..
  • 2:41 - 2:45
    Hili lilikuwa ni shambulio la moyo ambalo hakuna mtu aliyeliona.
  • 2:45 - 2:48
    Lakini tunapoangalia taarifa pale,
  • 2:48 - 2:50
    tunaona vitu vinaanza kuwa
  • 2:50 - 2:54
    havieleweki kama dakika tano hivi kabla ya shambulio la la moyo.
  • 2:54 - 2:56
    Tunaona mabadiliko madogo
  • 2:56 - 2:58
    katika vitu kama mapigo ya moyo
  • 2:58 - 3:01
    hivi vilikuwa haviwezekani kugundulika na vipimo vya kawaida
  • 3:01 - 3:03
    ambazo zitatumika na taarifa
  • 3:03 - 3:06
    kwa hiyo swali, lilikuwa ni kwa nini hatukuweza kuona?
  • 3:06 - 3:09
    Je hili lilikuwa ni tukio la kutabirika?
  • 3:09 - 3:12
    je tunaweza kuangalia tabia za taarifa
  • 3:12 - 3:15
    ili kuweza kufanya vitu upya?
  • 3:15 - 3:18
    Kwa hiyo huyu ni mtoto,
  • 3:18 - 3:21
    umri sawa na gari la mbio jukwaani,
  • 3:21 - 3:23
    miezi mitatu.
  • 3:23 - 3:25
    Ni mgonjwa mwenye tatizo la moyo
  • 3:25 - 3:29
    Ukiangalia baadhi ya taarifa hapo juu,
  • 3:29 - 3:34
    mapigo ya moyo,oksijeni,upumuaji,
  • 3:34 - 3:37
    vyote sio sawa kwa mtoto wa kawaida,
  • 3:37 - 3:40
    lakini ni sawa kwa mtoto yule,
  • 3:40 - 3:44
    kwa hiyo moja kati ya changamoto tuliyo nayo katika huduma za afya,
  • 3:44 - 3:47
    Nawezaje kumwangalia mgonjwa mbele yangu
  • 3:47 - 3:50
    na kuwa na kitu maalum kwake
  • 3:50 - 3:52
    na kugundua mambo yanapoanza kubadilika,
  • 3:52 - 3:54
    mambo yanapoharibika?
  • 3:54 - 3:58
    Kwa sababu kama vile gari la mashindano,mgonjwa yeyote,
  • 3:58 - 4:00
    mambo yanapoharibika,unakuwa na muda mfupi
  • 4:00 - 4:02
    kuleta mabadiliko.
  • 4:02 - 4:05
    tulichofanya ni kuchukua mfumo wa taarifa
  • 4:05 - 4:08
    ambao unafanya kazi kila baada ya wiki mbili za mwaka
  • 4:08 - 4:11
    na kuufunga katika kompyuta za hospitali
  • 4:11 - 4:14
    katika hospitali ya watoto ya Birmingham.
  • 4:14 - 4:16
    Tulisafirisha taarifa kutoka katika vifaa vya vitandani
  • 4:16 - 4:18
    katika wodi ya watoto mahututi
  • 4:18 - 4:22
    ili tuweze kuona taarifa kwa wakati huo huo
  • 4:22 - 4:25
    na muhimu zaidi,kutunza taarifa
  • 4:25 - 4:28
    ili tuweze kujifunza
  • 4:28 - 4:32
    na baadae tukatumia mfumo
  • 4:32 - 4:36
    ambao uliruhusu kufanya majaribio na taarifa
  • 4:36 - 4:38
    kw awakati huo huo ili kuona kilichokuwa kinatokea,
  • 4:38 - 4:42
    ili tuweze kujua wakati mambo yanapobadilika.
  • 4:42 - 4:46
    katika mbio za magari, tuna kuwa tumejaa matumaini
  • 4:46 - 4:49
    na wakati mwingine kujivuna kiasi,
  • 4:49 - 4:52
    kwa hiyo tukaamua kuangalia watoto
  • 4:52 - 4:55
    walipokuwa wanapelekwa katika wodi ya watu mahututi.
  • 4:55 - 4:57
    Kwa nini tusubiri mpaka wanapowasili katika hospitali
  • 4:57 - 4:59
    kabla ya kuanza kuangalia?
  • 4:59 - 5:02
    Kwa hiyo tukaweka kiunganishi cha wakati huo huo
  • 5:02 - 5:05
    kati ya gari ya wagonjwa na hospitali,
  • 5:05 - 5:09
    na kwa kutumia mfumo wa simu wa 3G kutuma taarifa
  • 5:09 - 5:11
    Kwa hiyo gari ya wagonjwa likawa ni kitanda cha ziada
  • 5:11 - 5:14
    katika wodi ya wagonjwa mahututi.
  • 5:14 - 5:18
    Na baadae tukaanza kuangalia taarifa.
  • 5:18 - 5:21
    Mistari yote hii juu,rangi zote,
  • 5:21 - 5:24
    Ni taarifa za kawaida kuziona katika kirusha picha
  • 5:24 - 5:28
    mapigo ya moyo,oksijeni katika damu,
  • 5:28 - 5:31
    na kupumua.
  • 5:31 - 5:33
    Mistari hapo chini, ya bluu na myekundu
  • 5:33 - 5:35
    hii ni ya kustaajabisha.
  • 5:35 - 5:38
    Mstari mwekundu unaonyesha mfumo wa moja kwa moja
  • 5:38 - 5:39
    wa maonyo ya mapema
  • 5:39 - 5:42
    ambayo yalikuwa yanaendeshwa na hospitali ya watoto ya birmingham
  • 5:42 - 5:44
    Walikuwa wanaiendesha toka 2008,
  • 5:44 - 5:47
    na tayari imesimamamisha mistuko ya moyo
  • 5:47 - 5:49
    na msongo wa mawazo hospitalini
  • 5:49 - 5:52
    Mstari wa bluu ni kiashiria
  • 5:52 - 5:54
    cha mwenendo unapoanza kubadilika,
  • 5:54 - 5:57
    na haraka,kabla hata ya kuanza
  • 5:57 - 5:58
    na kuweka utafsiri wa kitabibu
  • 5:58 - 6:01
    tunaweza kuona taarifa zikuzungumza nasi.
  • 6:01 - 6:05
    zinatuambia kuwa kitu si sawa.
  • 6:05 - 6:09
    mistari ya rangi nyekundu na kijani
  • 6:09 - 6:11
    hii inaonyesha kitu kingine
  • 6:11 - 6:14
    kuhusu taarifa.
  • 6:14 - 6:18
    Kijani inaonyesha kilicho sawa kwa mtoto
  • 6:18 - 6:20
    tunaiita kuwa ni wingu la kawaida.
  • 6:20 - 6:23
    na mambo yanapobadilika,
  • 6:23 - 6:25
    na hali kuwa mbaya
  • 6:25 - 6:27
    tunaenda katika mstari mwekundu.
  • 6:27 - 6:29
    Hakuna kitu cha ajabu hapa.
  • 6:29 - 6:33
    inaonyesha taarifa ambazo zipo katika njia nyingine,
  • 6:33 - 6:37
    kuwaonyesha madaktari
  • 6:37 - 6:39
    na manesi, ili wajue kinachoendelea.
  • 6:39 - 6:42
    sawa sawa na jinsi dereva wa mbio za magari
  • 6:42 - 6:46
    anavyotegemea kama kuna foleni ili ajue wakati wa kupiga breki,
  • 6:46 - 6:48
    wakati wa kukata kona,
  • 6:48 - 6:51
    tunahitaji kuwasaidia madaktari na manesi wetu
  • 6:51 - 6:54
    kuona ni wakati gani mambo yanapoanza kuharibika,
  • 6:54 - 6:57
    kwa hiyo tuna mpango wa kutia matumaini.
  • 6:57 - 7:02
    Tunaamini mbio zinaenda kufanya kitu tofauti.
  • 7:02 - 7:05
    Tunawaza mbali, ni kitu sahihi kabisa kufanyika,
  • 7:05 - 7:08
    tuna njia ambayo kama itafanikiwa,
  • 7:08 - 7:11
    hakuna sababu ibaki hospitalini tu.
  • 7:11 - 7:13
    inaweza kwenda zaidi ya hapo.
  • 7:13 - 7:15
    na mawasiliano ya bila waya ya siku hizi,
  • 7:15 - 7:18
    hakuna sababu wagonjwa,daktari na nesi
  • 7:18 - 7:20
    ya kuwafanya wawe sehemu moja
  • 7:20 - 7:22
    kwa wakati mmoja
  • 7:22 - 7:26
    na wakati huo huo,tutachukua mtoto wetu wa miezi mitatu,
  • 7:26 - 7:30
    tutaendelea kumpeleka uwanjani salama,
  • 7:30 - 7:33
    na kuifanya kuwa ya haraka na nzuri zaidi.
  • 7:33 - 7:34
    Asante Sana.
  • 7:34 - 7:39
    (Makofi)
Title:
Jinsi mbio za magari zinavyoweza kuwasaidia watoto wachanga?
Speaker:
Peter van Manen
Description:

Wakati wa mbio za magari za Formula 1, gari linatuma mamia ya mamilioni ya taarifa mbalimbali karakana yake kwa ajili ya uchunguzi na upashanaji taarifa kwa wakati huo huo. Kwa hiyo kwa nini tusitumie mfumo huu wa taarifa sehemu nyingine, kama ... katika hospitali za watoto? Peter Van Manen anatueleza zaidi

more » « less
Video Language:
English
Team:
closed TED
Project:
TEDTalks
Duration:
07:56

Swahili subtitles

Revisions Compare revisions