Unaweza kujua kweli kama mtoto anadanganya?
-
0:01 - 0:02Habari
-
0:02 - 0:05Ngoja niiulize hadhira swali:
-
0:05 - 0:07Ulishawahi kudanganya ukiwa mtoto?
-
0:07 - 0:10Kama uliwahi, unaweza
kunyanyua mkono tafadhali? -
0:11 - 0:15Wow! hili ni kundi la watu wakweli
kuliko wote niliowahi kukutana nao. -
0:15 - 0:17(Kicheko)
-
0:17 - 0:18Hadi sasa kwa miaka 20 iliyopita,
-
0:18 - 0:22Nimekuwa nikisoma
jinsi watoto wanavyojifunza kudanganya. -
0:22 - 0:24Na leo, nitawashirikisha
-
0:24 - 0:26baadhi ya ugunduzi tulioupata.
-
0:27 - 0:32Ila kwa kuanza, nitawaambia
hadithi kutoka kwa Bwana Richard Messina, -
0:32 - 0:35ambaye ni rafiki yangu na mkuu wa
shule ya msingi. -
0:35 - 0:37Alipokea simu siku moja.
-
0:39 - 0:40Aliyepiga akasema,
-
0:40 - 0:44"Bwana Messina, mtoto wangu Johnny
hatakuja shuleni leo -
0:44 - 0:46kwasababu anaumwa."
-
0:46 - 0:48Bwana Messina akauliza,
-
0:48 - 0:50"Naongea na nani, tafadhali?"
-
0:51 - 0:52Na aliyepiga akasema,
-
0:52 - 0:54"Mimi ni baba yangu."
-
0:54 - 0:57(Kicheko)
-
0:58 - 1:00Sasa hadithi hii --
-
1:00 - 1:01(Vicheko)
-
1:01 - 1:06inajumlisha vizuri sana
imani tatu zilizo zoeleka tulizonazo -
1:06 - 1:08kuhusu watoto na kudanganya.
-
1:08 - 1:13Moja, watoto huja tu kusema uongo
-
1:13 - 1:15baada ya kuingia shule ya msingi.
-
1:16 - 1:18Mbili, watoto hawadanganyi vizuri.
-
1:18 - 1:21Watu wazima twaweza kugundua uwongo wao.
-
1:21 - 1:25Na tatu, kama watoto watadanganya
katika umri mdogo sana, -
1:25 - 1:28lazima watakuwa na makosa
kitabia, -
1:28 - 1:32na watakuja kuwa
wagonjwa wa kudanganya maishani. -
1:33 - 1:35Hivyo inaonekana kwamba
-
1:35 - 1:37imani zote tatu hazikuwa sahihi.
-
1:39 - 1:41Tumekuwa tukifanya mchezo wa kukisia
-
1:41 - 1:43na watoto dunia nzima.
-
1:43 - 1:45Huu ni mfano
-
1:45 - 1:49Hivyo katika mchezo huu, tunauliza watoto
kukisia namba kwenye kadi. -
1:50 - 1:53Na tunawaambia wakishinda mchezo,
-
1:53 - 1:55watapata zawadi kubwa.
-
1:56 - 1:57Lakini katikati ya mchezo,
-
1:57 - 2:00tunatoa udhuru na kutoka kwenye chumba.
-
2:02 - 2:04Na kabla ya kutoka kwenye chumba,
-
2:04 - 2:07tunawaambia wasichungulie kwenye kadi.
-
2:08 - 2:09Bila shaka,
-
2:09 - 2:11tuna kamera zilizofichwa katika chumba
-
2:11 - 2:13kuangalia kila hatua yao.
-
2:14 - 2:18Kwasababu haja ya kushinda
mchezo ni kubwa sana, -
2:18 - 2:21zaidi ya asilimia 90 ya watoto
watachungulia -
2:21 - 2:23mara tutakapotoka chumbani.
-
2:23 - 2:25(Kicheko)
-
2:25 - 2:27Swali la msingi ni:
-
2:27 - 2:30Tutakaporudi na kuuliza watoto
-
2:30 - 2:32Kama wamechungulia au la,
-
2:32 - 2:35watoto waliochungulia watakiri
-
2:35 - 2:38au watadanganya kuhusu makosa yao?
-
2:40 - 2:44Tuligundua kwamba bila kujali
jinsia, nchi, au dini, -
2:45 - 2:47katika umri wa miaka miwili,
-
2:47 - 2:49asilimia 30 hudanganya,
-
2:49 - 2:53asilimia 70 husema ukweli
kuhusu makosa yao. -
2:53 - 2:55Katika umri wa miaka mitatu,
-
2:55 - 2:59asilimia 50 hudanganya na asilimia 50
husema kweli. -
2:59 - 3:01Katika umri wa miaka minne,
-
3:01 - 3:03zaidi ya asilimia 80 hudanganya.
-
3:04 - 3:07Na baada ya miaka minne,
-
3:07 - 3:08watoto wengi hudanganya.
-
3:09 - 3:11Hivyo unaweza kuona,
-
3:11 - 3:14kudanganya ni sehemu halisi
ya kuendelea. -
3:14 - 3:17Na baadhi ya watoto huanza kusema uwongo
-
3:17 - 3:19wakiwa na umri mdogo wa miaka miwili.
-
3:20 - 3:24Hivyo sasa, tuangalie kwa ukaribu
watoto wadogo. -
3:25 - 3:29Kwanini baadhi na sio wote
watoto wadogo hudanganya? -
3:30 - 3:34Katika mapishi unahitaji viungo vizuri
-
3:34 - 3:35kupika chakula kizuri.
-
3:36 - 3:40Na uongo mzuri unahitaji
viungo viwili vikuu. -
3:41 - 3:45Kiungo kikuu cha kwanza
ni nadharia ya akili, -
3:45 - 3:47au uwezo wa kusoma- akili.
-
3:48 - 3:50Kusoma akili ni uwezo wa kujua
-
3:50 - 3:54kwamba watu tofauti wana
ufahamu tofauti kuhusu hali fulani -
3:55 - 3:58na uwezo wa kutofautisha
kati ya ninachojua -
3:58 - 4:00na kile unachojua
-
4:00 - 4:02Kusoma akili ni muhimu kwa kudanganya
-
4:02 - 4:06kwasababu ya msingi wa kudanganya ni najua
-
4:06 - 4:07hujui
-
4:07 - 4:08ninachojua.
-
4:08 - 4:10Hivyo, naweza kukudanganya.
-
4:11 - 4:16Kiungo cha pili muhimu
-
4:16 - 4:20Ni uwezo wa kudhibiti maneno yako,
kuonyesha hisia usoni -
4:20 - 4:22na lugha ya mwili,
-
4:22 - 4:24ili kwamba unaweza kusema uongo thabiti.
-
4:25 - 4:29Na tulikuta kwamba wale watoto wadogo
-
4:29 - 4:34walio na uwezo mkubwa wa kusoma akili
na uwezo wa kujidhibiti -
4:34 - 4:36husema uwongo mapema
-
4:36 - 4:38na ni waongo wa kisasa.
-
4:40 - 4:46Kama inavyokuwa, uwezo huu wa aina mbili
ni muhimu pia kwetu sote -
4:46 - 4:48kuweza kufanya kazi katika jamii yetu.
-
4:49 - 4:53Ki ukweli, kushindwa kusoma akili
na uwezo wa kujidhibiti -
4:53 - 4:57vinahusianishwa na matatizo makubwa
ya ukuaji, -
4:57 - 5:00kama ADHD na usonji.
-
5:02 - 5:07Hivyo ukigundua mtoto wako wa miaka miwili
anakudanganya kwa mara ya kwanza, -
5:07 - 5:09badala ya kushtushwa,
-
5:09 - 5:11unatakiwa usherehekee--
-
5:11 - 5:12(Kicheko)
-
5:12 - 5:18kwasababu inaashiria kwamba mtoto wako
amefikia hatua mpya -
5:18 - 5:20ya ukuaji wa kawaida.
-
5:21 - 5:24Sasa, watoto hawadanganyi vizuri?
-
5:25 - 5:28Unafikiri unaweza kugundua
udanganyifu wao kirahisi? -
5:29 - 5:30Ungependa kujaribu?
-
5:31 - 5:32Ndio? Sawa.
-
5:32 - 5:35Sasa nitakuonyesha video mbili
-
5:35 - 5:36Kwenye video,
-
5:36 - 5:39watoto watajibu maswali ya
utafiti, -
5:39 - 5:41"Ulichungulia?"
-
5:41 - 5:42Sasa jaribu kuniambia
-
5:42 - 5:44mtoto yupi anadanganya
-
5:44 - 5:46na mtoto yupi anasema ukweli.
-
5:46 - 5:48Huyu ni mtoto namba moja.
-
5:49 - 5:50Uko tayari?
-
5:51 - 5:53(Video) Mtu: Ulichungulia? Mtoto: Hapana
-
5:54 - 5:56Kang Lee: Na huyu ni mtoto namba mbili.
-
5:58 - 6:00(Video) Mtu: Ulichungulia? Mtoto: Hapana.
-
6:01 - 6:05KL: OK, kama unafikiri
mtoto namba moja anadanganya, -
6:05 - 6:07tafadhali inua mkono wako.
-
6:08 - 6:12Na kama unafikiri mtoto namba mbili
anadanganya, tafadhali inua mkono wako. -
6:14 - 6:16OK, kusema ukweli,
-
6:16 - 6:19mtoto namba moja anasema ukweli,
-
6:19 - 6:21mtoto namba mbili anadanganya.
-
6:22 - 6:25Inaonekana wengi wenu sio wagunduzi
wazuri wa uwongo wa watoto. -
6:25 - 6:28(Kicheko)
-
6:28 - 6:31Sasa, tumeshiriki kwenye michezo sawasawa
-
6:31 - 6:36na watu wazima wengi sana
kutoka sehemu zote za maisha. -
6:37 - 6:39Na tunawaonyesha video nyingi.
-
6:39 - 6:42Katika nusu ya video, watoto walidanganya.
-
6:42 - 6:45Katika nusu ya video nyingine,
watoto walisema ukweli. -
6:47 - 6:49Ngoja tuone
watu wazima hawa walifanyaje. -
6:50 - 6:54Kwasababu kuna waongo wengi
kama wasema kweli, -
6:54 - 6:57ukikisia kwa kubahatisha,
-
6:57 - 7:01kunauwezekano wa asilimia 50
ukapatia. -
7:01 - 7:04Hivyo ikiwa usahihi wako ni takriban
asilimia 50, -
7:04 - 7:08inamaanisha wewe ni mgunduzi mbaya
wa uwongo wa watoto. -
7:08 - 7:13Sasa tuanze na wanafunzi wa shahada
ya kwanza na wanafunzi wa sheria, -
7:13 - 7:17ambao kwa ujumla
hawana uzoefu na watoto. -
7:18 - 7:20Hapana hawawezi kugundua uwongo wa watoto
-
7:20 - 7:22Utendaji wao ni wa kubahatisha
-
7:22 - 7:27Sasa vipi kuhusu wafanyakazi za jamii
na walinda haki za watoto, -
7:28 - 7:30wanaofanyakazi na watoto kila siku?
-
7:30 - 7:32Wanaweza kugundua uwongo wa watoto?
-
7:34 - 7:35Hapana, hawawezi,
-
7:35 - 7:36(Kicheko)
-
7:36 - 7:37Vipi kuhusu majaji,
-
7:37 - 7:39maafisa forodha
-
7:39 - 7:41na maafisa polisi,
-
7:41 - 7:44wanaokutana na wadanganyifu kila siku?
-
7:44 - 7:46Wanaweza kugundua uwongo wa watoto?
-
7:47 - 7:48Hapana hawawezi.
-
7:48 - 7:50Vipi kuhusu wazazi?
-
7:50 - 7:53Wazazi wanaweza kugundua uwongo wa watoto
wengine? -
7:54 - 7:55Hapana, hawawezi.
-
7:56 - 7:59Inawezekana wazazi
kugundua uwongo wa watoto wao wenyewe? -
8:01 - 8:02Hapana, hawawezi.
-
8:02 - 8:06(Kicheko) (Makofi)
-
8:06 - 8:07Hivyo sasa unaweza kuuliza
-
8:09 - 8:12kwanini uwongo wa watoto
ni vigumu kuugundua. -
8:13 - 8:16Ngoja niwaonyeshe hili
na mtoto wangu mwenyewe, Nathan -
8:16 - 8:18Hii ni hisia za uso wake
-
8:18 - 8:20anapodanganya.
-
8:20 - 8:22(Kicheko)
-
8:22 - 8:23Hivyo wakati watoto wanadanganya,
-
8:23 - 8:27hisia za nyuso zao
ni za kawaida. -
8:27 - 8:31Ingawa nyuma ya hii hisia ya kawaida,
-
8:31 - 8:34mtoto kiukweli hupitia
hisia nyingi, -
8:34 - 8:38kama hofu, hatia, fedheha
-
8:38 - 8:41na pengine raha ya kudanganya kidogo.
-
8:41 - 8:44(Kicheko)
-
8:44 - 8:49Bahati mbaya, hisia za aina hiyo
ni aidha za muda mfupi au zimejificha -
8:49 - 8:52Kwahiyo, ni ambazo hazionekani kwetu.
-
8:52 - 8:53Kwa miaka mitano iliyopita,
-
8:53 - 8:57tumekuwa tukijaribu kutafuta njia
ya kuonyesha hisia hizi zilizojificha. -
8:57 - 8:58Kisha tukapata ugunduzi.
-
8:59 - 9:02Tunajua kwamba chini ya ngozi
za nyuso zetu, -
9:02 - 9:06kuna mtandao mkubwa wa mishipa ya damu.
-
9:06 - 9:08Tunapopitia hisia tofauti,
-
9:08 - 9:11msukumo wa damu usoni hubadilika
bila kujua. -
9:12 - 9:16Na mabadiliko haya huendeshwa
kwa mfumo wa autonomiki -
9:16 - 9:18ambayo ni nje ya uwezo wetu kudhibiti.
-
9:18 - 9:22Kwa kuangalia mabadiliko ya msukumo
wa damu usoni, -
9:22 - 9:25tunaweza kuonyesha hisia za watu
zilizojificha. -
9:25 - 9:30Bahati mbaya, hisia hizo zinazohusiana
na mabadiliko ya msukumo wa damu usoni -
9:30 - 9:33ni vigumu sana kugundua kwa macho yetu.
-
9:34 - 9:37Hivyo kusaidia kuonyesha
hisia za watu usoni, -
9:37 - 9:40tumeunda teknolojia mpya ya picha
-
9:40 - 9:44tunaiita "tansderaml optical imaging"
-
9:45 - 9:49Kufanya hivyo tunatumia kamera ya video
ya kawaida kurekodi watu -
9:49 - 9:52wanapokuwa na hisia mbalimbali
zilizojificha -
9:52 - 9:56Na kisha, kwa kutumia teknolojia
ya usindikaji picha, -
9:57 - 10:02tunaweza kupata picha kupitia ngozi
za mabadiliko ya msukumo wa damu usoni. -
10:04 - 10:09Kwa kuangalia video za picha
kupitia ngozi, -
10:09 - 10:11sasa tunaweza kuona kwa urahisi
-
10:12 - 10:17mabadiliko ya msukumo wa damu usoni
yanayohusiana na hisia zilizojificha. -
10:18 - 10:20Na kwa kutumia teknolojia hii,
-
10:20 - 10:24tunaweza kuonyesha hisia zilizojificha
zinazohusiana na udanganyifu, -
10:24 - 10:27na kwahiyo kugundua uwongo wa watu.
-
10:27 - 10:30tunaweza kufanya bila upasuaji,
-
10:30 - 10:32kwa mbali, na gharama nafuu
-
10:32 - 10:36kwa usahihi wa takriban asilimia 85
-
10:36 - 10:38ambayo ni bora kuliko kubahatisha.
-
10:39 - 10:43Na kwa kuongezea, tumegundua
athari za Pinikio. -
10:44 - 10:46Hapana, sio athari za Pinokio huyu.
-
10:46 - 10:47(Kicheko)
-
10:47 - 10:50Hizi ni athari za kweli za Pinokio.
-
10:50 - 10:51Wakati watu wanapodanganya,
-
10:51 - 10:55msukumo wa damu usoni
kwenye mashavu hupungua, -
10:55 - 10:58na msukumo wa damu usoni
kwenye pua huongezeka. -
10:59 - 11:03Hata hivyo, kudanganya sio tukio pekee
-
11:03 - 11:06ambalo litaamsha hisia zilizojificha.
-
11:06 - 11:08Hivyo basi tukajiuliza wenyewe,
-
11:08 - 11:10pamoja na kugundua uwongo,
-
11:10 - 11:12teknolojia yetu inaweza kutumikaje?
-
11:13 - 11:17Utumikaji wake mmoja ni kwenye elimu.
-
11:17 - 11:21Kwa mfano, kwa kutumia teknolojia hii,
tunaweza kumsaidia mwalimu huyu wa hesabu -
11:21 - 11:24kutambua wanafunzi darasani kwake
-
11:24 - 11:29wanapata woga mkubwa
kuhusu mada anayofundisha -
11:29 - 11:30ili iweze kumsaidia.
-
11:31 - 11:34Na pia tunaweza kuitumia katika huduma
za afya. -
11:34 - 11:37Mfano, kila siku natumia huduma ya
Skype kuwasilina na wazazi wangu, -
11:37 - 11:40wanaoishi maelfu ya maili mbali.
-
11:40 - 11:42Na kwa kutumia teknolojia hii,
-
11:42 - 11:46Sio tu najua kinachoendelea
katika maisha yao -
11:46 - 11:52lakini pia sambamba na kuangalia mapigo
yao ya moyo na kiwango cha msongo, -
11:52 - 11:55hali zao na kama wanapata
au hawapati maumivu. -
11:56 - 11:58Na pengine kwa siku za mbele,
-
11:58 - 12:01hatari za mshtuko wa moyo au
shinikizo la damu -
12:02 - 12:03Na unaweza kuuliza:
-
12:03 - 12:09Tunaweza kutumia hii pia
kuonyesha hisia za wanasiasa? -
12:09 - 12:11(Kicheko)
-
12:11 - 12:12Kwa mfano, wakati wa mijadala
-
12:13 - 12:15Kwakweli, jibu ni ndio.
-
12:15 - 12:17Kutumia kipande kinachorushwa
kwenye TV, -
12:17 - 12:21tunaweza kugundua mapigo ya moyo
ya mwanasiasa, -
12:21 - 12:23hali na msongo,
-
12:23 - 12:27na pengine katika siku za mbele.
iwe wanatudanganya au sivyo. -
12:27 - 12:30Tunaweza pia kutumia hii
katika utafiti wa masoko, -
12:31 - 12:32kwa mfano, kujua
-
12:32 - 12:37kama watu wanapenda au hawapendi
bidhaa fulani za matumizi. -
12:37 - 12:39Tunaweza hata kutumia kwenye miadi.
-
12:40 - 12:41Sasa kwa mfano
-
12:41 - 12:44Ikiwa mliyeahidiana anakuonyesha tabasamu,
-
12:44 - 12:46teknolojia hii inaweza kukusaidia kujua
-
12:47 - 12:49kama anakupenda kweli
-
12:49 - 12:51au anajaribu tu kuonyesha wema kwako.
-
12:52 - 12:54Na kwa suala hili,
-
12:54 - 12:55anajaribu kuonyesha wema kwako.
-
12:55 - 12:58(Kicheko)
-
12:59 - 13:03Hivyo teknolojia ya transdermal optical
imaging -
13:03 - 13:06iko katika hatua za mwanzo za kuendelezwa.
-
13:06 - 13:10Matumizi mengi mapya yatakuja
ambayo hatuyajui leo. -
13:10 - 13:13Ingawa, kitu kimoja ninachojua kwa uhakika
-
13:13 - 13:17ni kwamba kudanganya
hakutakuwa kama zamani tena. -
13:17 - 13:18Asanteni sana.
-
13:18 - 13:19Asanteni.
-
13:19 - 13:23(Makofi)
- Title:
- Unaweza kujua kweli kama mtoto anadanganya?
- Speaker:
- Kang Lee
- Description:
-
Je watoto hawadanganyi vizuri? Unafikiri unaweza kugundua uwongo wao kwa urahisi? Mtafiti wa maendeleo Kang Lee amechunguza nini kinatokea kisaikolojia kwa watoto wanapodanganya. Wanafanya mara nyingi kuanzia umri mdogo wa miaka miwili, na hakika wanafanya vizuri kweli. Lee anaelezea kwanini tusherehekee wakati watoto wanaanza kudanganya na kuwasilisha teknolojia mpya ya kugundua uwongo ambayo siku moja itaonyesha hisia zetu zilizojificha.
- Video Language:
- English
- Team:
- closed TED
- Project:
- TEDTalks
- Duration:
- 13:36
Joachim Mangilima approved Swahili subtitles for Can you really tell if a kid is lying? | ||
Joachim Mangilima accepted Swahili subtitles for Can you really tell if a kid is lying? | ||
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for Can you really tell if a kid is lying? | ||
Leah Ligate edited Swahili subtitles for Can you really tell if a kid is lying? | ||
Leah Ligate edited Swahili subtitles for Can you really tell if a kid is lying? | ||
Leah Ligate edited Swahili subtitles for Can you really tell if a kid is lying? | ||
Leah Ligate edited Swahili subtitles for Can you really tell if a kid is lying? | ||
Leah Ligate edited Swahili subtitles for Can you really tell if a kid is lying? |