WEBVTT 00:00:00.960 --> 00:00:03.016 Nilikuwa na umri wa miaka 14 00:00:03.040 --> 00:00:04.616 nikiwa kwenye jumba la michezo, 00:00:04.640 --> 00:00:06.400 nikiiba kwenye mashine ya mchezo, 00:00:07.200 --> 00:00:08.976 na nilipokuwa nikitoka nje ya jengo 00:00:09.000 --> 00:00:11.380 mlinzi alikamata mkono wangu, hivyo nikakimbia. 00:00:11.760 --> 00:00:14.736 Nilikimbilia mtaani, na nikaruka juu ya uzio. 00:00:14.760 --> 00:00:16.376 Na nilipofika juu, 00:00:16.400 --> 00:00:18.576 uzito wa sarafu 3,000 kwenye mkoba wangu 00:00:18.600 --> 00:00:20.240 ulinielemea na kunivuta chini. 00:00:20.880 --> 00:00:23.936 Niliponyanyuka, mlinzi alikuwa amesima juu yangu, 00:00:23.960 --> 00:00:27.376 na akasema, "Siku nyingine nyinyi vibaka, ibeni vitu mnavyoweza kubeba." NOTE Paragraph 00:00:27.400 --> 00:00:29.416 (Kicheko) NOTE Paragraph 00:00:29.440 --> 00:00:31.576 Nilipelekwa kwenye mahabusu ya watoto 00:00:31.600 --> 00:00:34.160 na nilipoachiliwa chini ya dhamana ya mama yangu, 00:00:35.080 --> 00:00:38.056 maneno ya kwanza mjomba wangu alisema yalikuwa, "Ulikamatwaje?" 00:00:38.080 --> 00:00:40.256 Nikasema, "Mzee, mkoba ulikuwa mzito sana." 00:00:40.280 --> 00:00:42.660 Akasema, "Mzee, hukutakiwa kuchukua sarafu zote." 00:00:42.660 --> 00:00:46.056 Nikasema, "Mzee, zilikuwa ndogo. Ningefanyaje?" 00:00:46.080 --> 00:00:50.976 na dakika 10 baadaye, alinipeleka kuiba kwenye mashine nyingine ya mchezo. 00:00:51.000 --> 00:00:53.020 Tulihitaji pesa ya petroli kufika maskani. 00:00:53.250 --> 00:00:55.290 Hayo ndiyo yalikuwa maisha yangu. NOTE Paragraph 00:00:55.440 --> 00:00:57.296 Nimekulia Oakland, Kalifornia, 00:00:57.320 --> 00:00:59.656 na mama yangu na ndugu wa karibu wa familia 00:00:59.680 --> 00:01:00.920 walevi wa madawa ya kulevya ya kokeini . 00:01:01.560 --> 00:01:06.000 Mazingira yangu yalijumuisha kuishi na familia, marafiki, 00:01:06.960 --> 00:01:08.560 na makazi kwa wasio-na-makazi. 00:01:09.040 --> 00:01:12.720 Mara nyingi, mlo wa jioni tuliupata kwenye foleni za vyakula vya msaada. 00:01:13.440 --> 00:01:15.296 Mjomba aliniambia hivi: 00:01:15.320 --> 00:01:17.296 pesa inatawala dunia 00:01:17.320 --> 00:01:18.536 na kila kitu ndani yake. 00:01:18.560 --> 00:01:20.640 Na katika hii mitaa, pesa ni Mfalme. 00:01:21.320 --> 00:01:22.936 Na ikiwa utafuata pesa, 00:01:22.960 --> 00:01:25.480 itakupeleka kwa mtu mbaya au mtu mzuri. NOTE Paragraph 00:01:26.080 --> 00:01:28.616 Baadaye kidogo, nilifanya uhalifu wangu wa kwanza, 00:01:28.640 --> 00:01:31.616 na ndiyo mara ya kwanza nilipoambiwa kuwa nina kipaji 00:01:31.640 --> 00:01:33.790 na nikajisikia kuwa kuna mtu ananiaminia. 00:01:34.240 --> 00:01:36.946 Hakuna aliyewahi-niambia kuwa ningeweza kuwa mwanasheria, 00:01:36.946 --> 00:01:38.056 daktari au mhandisi. 00:01:38.080 --> 00:01:41.596 Yaani, ningewezaje kufanya hivyo? Sikuweza kusoma, kuandika wala kutahajia. 00:01:41.596 --> 00:01:42.736 Sikuwa mtu aliyesoma. 00:01:42.760 --> 00:01:45.880 Kwahiyo, mara zote nilifikiri uhalifu ndio njia ya kwenda. NOTE Paragraph 00:01:47.480 --> 00:01:49.176 Na kisha siku moja 00:01:49.200 --> 00:01:50.456 Nilikuwa naongea na mtu 00:01:50.480 --> 00:01:54.080 na alikuwa ananiambia juu ya huu wizi ambao tungeweza fanya. 00:01:54.760 --> 00:01:55.960 Na tukaufanya. NOTE Paragraph 00:01:57.080 --> 00:01:58.896 Ukweli ni kwamba nilikuwa nakulia 00:01:58.920 --> 00:02:01.296 kwenye nchi yenye uwezo mkubwa wa kifedha duniani, 00:02:01.296 --> 00:02:03.016 Marekani, 00:02:03.040 --> 00:02:07.120 huku nikiangalia mama yangu, akisimama kwenye foleni ya benki ya damu 00:02:08.680 --> 00:02:12.360 kuuza damu yake kwa Dola 40 kujaribu tu kulisha wanae. 00:02:13.320 --> 00:02:16.640 Bado ana alama za sindano mikononi mwake leo kudhihirisha hilo. NOTE Paragraph 00:02:17.480 --> 00:02:19.216 Kwa hiyo sikuijali jumuiya yangu, 00:02:19.240 --> 00:02:20.736 Hawakujali maisha yangu. 00:02:20.760 --> 00:02:24.176 Kila mtu pale alifanya anachotaka fanya kupata alichotaka, 00:02:24.200 --> 00:02:26.376 wauza mihadarati, wezi, benki ya damu. 00:02:26.400 --> 00:02:28.016 Kila mtu alichukua fedha ya damu. 00:02:28.040 --> 00:02:30.196 Hivyo nilipata yangu kwa njia yoyote ile. 00:02:30.196 --> 00:02:31.556 Nilipata yangu. 00:02:31.556 --> 00:02:33.680 Elimu ya fedha kweli ilitawala dunia, 00:02:34.680 --> 00:02:36.656 na nilikuwa mtoto mtumwa kwake 00:02:36.680 --> 00:02:37.920 nikifuata mtu mbaya. NOTE Paragraph 00:02:40.280 --> 00:02:43.456 Nikiwa na miaka 17, nilikamatwa kwa wizi na mauaji 00:02:43.480 --> 00:02:47.456 na punde nikajifunza kuwa fedha jela zinatawala zaidi ya zilivyo mitaani, 00:02:47.480 --> 00:02:48.680 Hivyo nilitaka kuingia. 00:02:49.600 --> 00:02:52.656 Siku moja, nilikurupuka kushika ukurasa wa michezo katika gazeti 00:02:52.680 --> 00:02:54.496 ili mfungwa mwenzangu anisomee, 00:02:54.520 --> 00:02:56.936 na kwa bahati mbaya nikachukua sehemu ya biashara. 00:02:56.960 --> 00:03:00.216 Na huyu mzee akasema, "Hey, kijana, umechukua hisa?" 00:03:00.240 --> 00:03:01.496 Na nikasema, "Ndio nini hicho?" 00:03:01.520 --> 00:03:04.756 Akasema, "Hiyo ndiyo sehemu ambayo watu weupe huweka pesa yao yote." NOTE Paragraph 00:03:04.756 --> 00:03:05.936 (Kicheko) NOTE Paragraph 00:03:05.960 --> 00:03:09.816 Na ilikuwa ndiyo mara ya kwanza nilipata ono fupi la tumaini, 00:03:09.840 --> 00:03:11.336 siku za baadaye. 00:03:11.360 --> 00:03:13.960 Alinipa maelezo mafupi ya hisa zilikuwa ni nini, 00:03:14.800 --> 00:03:16.340 lakini ilikuwa ni muhtasari tu. 00:03:18.360 --> 00:03:20.136 Yaani, ningewezaje kuifanya? 00:03:20.160 --> 00:03:22.210 Sikuweza kusoma, kuandika wala kutahajia. 00:03:22.600 --> 00:03:25.216 Ujuzi niliokuwa nimeukuza kuficha kutokusoma kwangu 00:03:25.240 --> 00:03:27.296 haukufanya kazi tena katika mazingira haya. 00:03:27.296 --> 00:03:30.336 Nilikuwa nimenaswa kwenye kizimba mateka kati ya watekaji, 00:03:30.360 --> 00:03:32.256 nikipigania uhuru ambao sijawahi kuwa nao. 00:03:32.280 --> 00:03:34.456 Nilikuwa nimepotea, nimechoka, 00:03:34.480 --> 00:03:35.840 na sikuwa na machaguzi. NOTE Paragraph 00:03:37.000 --> 00:03:38.776 Kwa hiyo nikiwa na miaka 20, 00:03:38.800 --> 00:03:42.130 nilifanya kitu kigumu kuliko vyote nilivyowahi kufanya maishani mwangu. 00:03:42.160 --> 00:03:43.360 Nilichukua kitabu, 00:03:45.400 --> 00:03:47.880 na ilikuwa ni kipindi kigumu sana maishani mwangu. 00:03:49.320 --> 00:03:51.136 kujaribu kujifunza jinsi ya kusoma, 00:03:51.160 --> 00:03:53.776 kutengana na familia yangu, 00:03:53.800 --> 00:03:55.000 na rafiki zangu. 00:03:56.280 --> 00:03:57.736 Ilikuwa shida, mzee. 00:03:57.760 --> 00:03:59.136 Ilikuwa ni mahangaiko. 00:03:59.160 --> 00:04:00.856 Lakini sikufahamu japo kidogo kuwa 00:04:00.880 --> 00:04:04.296 nilikuwa napata zawadi kubwa kuliko zote nilizowahi kuziota, 00:04:04.320 --> 00:04:05.520 kujithamini, 00:04:06.320 --> 00:04:08.160 maarifa, nidhamu. 00:04:09.000 --> 00:04:12.696 Nilisisimka mno kusoma, kiasi kwamba nilisoma kila kitu nilichokitia mkononi: 00:04:12.720 --> 00:04:16.055 makaratasi ya pipi, nembo za nguo, alama za barabarani, kila kitu. 00:04:16.079 --> 00:04:17.326 Nilikuwa nikisoma tu vitu! NOTE Paragraph 00:04:17.326 --> 00:04:18.336 (Makofi na Vifijo) NOTE Paragraph 00:04:18.360 --> 00:04:19.560 kusoma tu vitu. 00:04:21.360 --> 00:04:24.560 Nilisisimka sana kujua jinsi ya kusoma na kujua jinsi ya kutahajia. 00:04:24.720 --> 00:04:27.006 Rafiki alikuja, akaniuliza, "Mzee, unakula nini?" 00:04:27.006 --> 00:04:28.736 Nikasema, "P-I-P-I, pipi." NOTE Paragraph 00:04:28.760 --> 00:04:31.016 (Kicheko) NOTE Paragraph 00:04:31.040 --> 00:04:33.656 Akasema, "Nipe kidogo." Nikasema, "L-A. La." NOTE Paragraph 00:04:33.656 --> 00:04:34.776 (Kicheko) NOTE Paragraph 00:04:34.800 --> 00:04:36.216 Ilikuwa babukubwa. 00:04:36.240 --> 00:04:39.416 Yaani, sasa naweza, kwa mara ya kwanza katika maisha yangu, kusoma. 00:04:39.440 --> 00:04:41.480 Hisia niliyoipata, ni ya kustaajabu sana. NOTE Paragraph 00:04:43.240 --> 00:04:45.840 Kisha, nikiwa na miaka 22, nikijisikia mwenyewe, 00:04:46.800 --> 00:04:48.536 nikijiamini, 00:04:48.560 --> 00:04:50.400 Nilikumbuka kile yule mzee aliniambia. 00:04:51.760 --> 00:04:55.496 Kwa hiyo nilichukua kurasa za biashara za gazeti. 00:04:55.520 --> 00:04:57.456 Nilitaka kuwatafuta hawa matajiri weupe. NOTE Paragraph 00:04:57.480 --> 00:04:59.080 (Kicheko) NOTE Paragraph 00:05:00.520 --> 00:05:02.440 Kwa hiyo nilitafuta ule muhtasari. 00:05:03.480 --> 00:05:05.096 Nilipokuwa nikijiendeleza kikazi 00:05:05.120 --> 00:05:08.976 nikifundisha wengine namna ya kusimamia fedha na kuwekeza, 00:05:09.000 --> 00:05:12.336 punde nikajifunza kuwa nilihitaji kuwajibika kwa matendo yangu. 00:05:12.360 --> 00:05:15.376 Kweli, nilikulia kwenye mazingira tata sana, 00:05:15.400 --> 00:05:17.336 lakini nilichagua kufanya uhalifu, 00:05:17.360 --> 00:05:19.136 na nilipaswa kukiri hilo. 00:05:19.160 --> 00:05:21.776 Nilipaswa kuwajibika kwa hilo, na nilifanya hivyo. 00:05:21.800 --> 00:05:24.696 Nilikuwa nikiunda mtaala ambao ungeweza kuwafundisha wafungwa 00:05:24.720 --> 00:05:27.110 namna ya kusimamia fedha kupitia ajira za gerezani. 00:05:28.720 --> 00:05:31.896 Kutiisha mtindo wetu wa maisha kungeweza kutoa zana zihamishikazo 00:05:31.920 --> 00:05:35.256 ambazo tunaweza kuzitumia kusimamia fedha tunapoirudi kwenye jamii, 00:05:35.280 --> 00:05:38.536 kama watu wengi walivyofanya ambao hawakufanya uhalifu. 00:05:38.560 --> 00:05:39.760 Kisha niligundua 00:05:40.680 --> 00:05:42.736 kulingana takwimu ya MarketWatch, 00:05:42.760 --> 00:05:45.296 zaidi ya asilimia 60 ya wakazi wa Marekani 00:05:45.320 --> 00:05:47.440 wana chini ya Dola 1,000 katika akiba. 00:05:48.200 --> 00:05:51.416 Michezo ilielezea kwamba zaidi ya asilimia 60 ya wachezaji wa NBA 00:05:51.440 --> 00:05:52.976 na wachezaji wa NFL hufilisika. 00:05:53.000 --> 00:05:56.040 Asilimia 40 ya matatizo ya ndoa hutokana na masuala ya kifedha. 00:05:57.080 --> 00:05:58.296 Balaa gani? NOTE Paragraph 00:05:58.320 --> 00:06:00.456 (Kicheko) NOTE Paragraph 00:06:00.480 --> 00:06:03.176 Unataka kuniambia, watu wamefanya kazi maisha yao yote, 00:06:03.200 --> 00:06:05.776 wakinunua magari, nguo, nyumba na vitu mbalimbali 00:06:05.800 --> 00:06:08.016 lakini walikuwa waliishi hundi kwa hundi? 00:06:08.040 --> 00:06:12.376 Ni namna gani duniani wanajamii wangekwenda kuwasaidia wafungwa 00:06:12.400 --> 00:06:13.616 kurudi kwenye jamii 00:06:13.640 --> 00:06:15.830 ikiwa hawakuweza kusimamia mambo yao wenyewe? 00:06:16.160 --> 00:06:17.416 Tumevurugwa. NOTE Paragraph 00:06:17.440 --> 00:06:19.176 (Kicheko) NOTE Paragraph 00:06:19.200 --> 00:06:20.600 Nahitaji mpango mzuri zaidi. 00:06:22.520 --> 00:06:24.640 Hii haitakwenda kufanya kazi vizuri. 00:06:25.040 --> 00:06:26.240 Hivyo ... 00:06:27.880 --> 00:06:29.080 Nilifikiria. 00:06:31.800 --> 00:06:35.020 Sasa nilikuwa na wajibu kukutana na wale waliokuwa kwenye mkondo huo 00:06:36.360 --> 00:06:37.576 na kuwasaidia, 00:06:37.600 --> 00:06:40.856 na ilikuwa ni ajabu sababu sasa nilijali jumuiya yangu 00:06:40.880 --> 00:06:43.240 Lo, hebu fikiria. Nilijali kuhusu jumuiya yangu. NOTE Paragraph 00:06:44.640 --> 00:06:46.936 Ujinga juu ya Fedha ni ugonjwa 00:06:46.960 --> 00:06:49.976 ambao umedhohofisha wachache na walio chini katika jamii yetu 00:06:50.000 --> 00:06:52.136 kwa vizazi na vizazi, 00:06:52.160 --> 00:06:54.656 na tunapaswa kukasirika juu ya hilo. 00:06:54.680 --> 00:06:56.256 Ebu jiulize: 00:06:56.280 --> 00:06:59.536 Inawezekanaje asilimia 50 ya wakazi wa Marekani 00:06:59.560 --> 00:07:03.520 wasiwe na elimu ya fedha katika nchi inayoendeshwa kwa ustawi wa kifedha? 00:07:05.000 --> 00:07:07.856 Kupatikana kwa haki kwetu, hadhi yetu ya kijamii, 00:07:07.880 --> 00:07:10.896 hali ya maisha, usafirishaji na chakula 00:07:10.920 --> 00:07:13.976 vyote vinategemea fedha ambayo watu wengi hawawezi kuisimamia. 00:07:14.000 --> 00:07:15.576 Ni ajabu! 00:07:15.600 --> 00:07:16.976 Ni janga 00:07:17.000 --> 00:07:20.000 na hatari kubwa kwa usalama wa umma kuliko suala jingine lolote. NOTE Paragraph 00:07:21.720 --> 00:07:24.376 Kadiri ya Kitengo cha Urekebishaji cha Kalifornia, 00:07:24.400 --> 00:07:26.736 zaidi ya asilimia 70 ya wale waliofungwa 00:07:26.760 --> 00:07:30.376 wamefanya au wameshtakiwa kwa uhalifu uhusianao na fedha: 00:07:30.400 --> 00:07:34.920 wizi wa kutumia nguvu, kuvunja nyumba, kutapeli, uporaji, ghusubu -- 00:07:35.720 --> 00:07:37.040 na orodha inaendelea. 00:07:37.920 --> 00:07:39.136 Angalia hii: 00:07:39.160 --> 00:07:42.096 Mfungwa wa kawaida 00:07:42.120 --> 00:07:44.616 huingia katika mfumo wa gereza wa Kalifornia 00:07:44.640 --> 00:07:46.200 pasipo kuwa na elimu ya fedha, 00:07:46.840 --> 00:07:48.816 hupata ujira wa senti 30 kwa saa, 00:07:48.840 --> 00:07:51.056 zaidi ya Dola 800 kwa mwaka, 00:07:51.080 --> 00:07:53.840 bila ya kuwa na matumizi yoyote na kuweka akiba yoyote. 00:07:54.760 --> 00:07:59.096 Anapopewa msamaha, hupewa dola 200 pesa ya geti na kuambiwa, 00:07:59.120 --> 00:08:02.340 "Wee, mafanikio mema, kaa mbali na matatizo. Usirudi gerezani tena." 00:08:02.800 --> 00:08:06.096 Bila kuwa na maandalizi yoyote ya maana au mpango fedha wa muda mrefu, 00:08:06.120 --> 00:08:07.320 anafanyaje ...? 00:08:08.600 --> 00:08:09.800 Akiwa na miaka 60? 00:08:11.120 --> 00:08:12.456 Apate kazi nzuri, 00:08:12.480 --> 00:08:16.400 au arudi kwenye tabia ile ile ya uhalifu iliyompeleka gerezani kwanza? 00:08:17.400 --> 00:08:19.176 Nyinyi walipakodi, chagueni wenyewe. 00:08:19.200 --> 00:08:22.360 Hakika, elimu yake imeshamchagulia, pengine. NOTE Paragraph 00:08:23.120 --> 00:08:25.480 Kwa hiyo, tunatibuje ugonjwa huu? 00:08:26.240 --> 00:08:27.976 Nilishiriki kuanzisha programu 00:08:28.000 --> 00:08:32.576 tuliyoiita Elimu Hisia ya Uwezeshaji wa Kifedha 00:08:32.600 --> 00:08:34.056 tunaiita FEEL 00:08:34.080 --> 00:08:37.256 na inafundisha namna ya kutenganisha maamuzi ya kihisia 00:08:37.280 --> 00:08:39.256 na maamuzi ya kifedha, 00:08:39.280 --> 00:08:42.696 na sheria 4 aushi za utawala fedha binafsi: 00:08:42.720 --> 00:08:44.280 njia sahihi ya kuweka akiba, 00:08:45.560 --> 00:08:47.200 kudhibiti gharama zako za maisha, 00:08:48.320 --> 00:08:50.096 kukopa fedha kwenye ufanisi 00:08:50.120 --> 00:08:53.896 kutawanya fedha yako kuruhusu fedha yako ikufanyie kazi 00:08:53.920 --> 00:08:55.736 badala ya wewe kuifanyia kazi. 00:08:55.760 --> 00:08:59.920 Wafungwa wanahitaji ujuzi huu kabla ya kuingia tena kwenye jamii. 00:09:01.480 --> 00:09:05.376 Hatuwezi kubadilika kuwa na maisha ya kawaida bila ujuzi huu wa maisha. 00:09:05.400 --> 00:09:09.216 Hii dhana kuwa ni Weledi tu wanaweza kuwekeza na kusimamia fedha 00:09:09.240 --> 00:09:11.496 ni ya fedheha kabisa, 00:09:11.520 --> 00:09:13.587 na yeyote aliyewaambia hivyo anadanganya. NOTE Paragraph 00:09:13.627 --> 00:09:18.176 (Makofi na Vifijo) NOTE Paragraph 00:09:18.200 --> 00:09:20.616 Mweledi ni mtu 00:09:20.640 --> 00:09:23.136 anayejua kazi zake kuliko walio wengi, 00:09:23.160 --> 00:09:28.096 na hakuna mtu ajuaye kiasi gani cha fedha wahitaji, unacho, au wataka zaidi ya wewe, 00:09:28.120 --> 00:09:30.080 ikimaanisha kuwa wewe ni mweledi. 00:09:30.880 --> 00:09:35.096 Elimu ya fedha siyo stadi, mabibi na mabwana. 00:09:35.120 --> 00:09:36.320 Ni mtindo wa maisha. 00:09:37.560 --> 00:09:42.056 Uimara wa kifedha ni matokeo ya ziada ya mtindo sahihi wa maisha. 00:09:42.080 --> 00:09:45.880 Mfungwa mwenye elimu nzuri ya kifedha anaweza kuwa mwananchi mlipakodi, 00:09:46.680 --> 00:09:50.176 na mwananchi mlipakodi mwenye elimu nzuri ya kifedha anaweza kubaki hivyo. 00:09:50.200 --> 00:09:54.536 Hii inatuwezesha kuunda daraja kati ya wale watu tunaowashawishi: 00:09:54.560 --> 00:09:57.296 familia, marafiki na wale vijana 00:09:57.320 --> 00:10:00.240 ambao bado wanaamini kuwa uhalifu na pesa vina uhusiano. 00:10:01.720 --> 00:10:04.616 Kwa hiyo tupoteze uwoga na wasiwasi 00:10:04.640 --> 00:10:06.096 wa maneno makubwa ya kifedha 00:10:06.120 --> 00:10:09.696 na ujinga mwingine wote ambao mmekuwa mkisikia huko nje. 00:10:09.720 --> 00:10:13.576 Na tujikite kwenye kiini kilichokuwa kinadhoofisha jamii yetu 00:10:13.600 --> 00:10:17.960 kuanzia kutimiza wajibu wako la kuwa meneja mzuri wa maisha. 00:10:19.000 --> 00:10:22.336 Na tutoe mtaala mwepesi na rahisi kutumia 00:10:22.360 --> 00:10:24.616 ambao utaingia kwenye kiini, kiini 00:10:24.640 --> 00:10:28.576 cha ni nini ukweli wa uwezeshaji wa kifedha na elimu ya hisia. NOTE Paragraph 00:10:28.600 --> 00:10:31.496 Sasa, ikiwa umekaa hapa kwa wasikilizaji na umesema, 00:10:31.520 --> 00:10:33.936 "Ndiyo, kweli, hiyo si mimi na sikubaliani nayo," 00:10:33.960 --> 00:10:35.446 basi njoo uchukue somo langu -- NOTE Paragraph 00:10:35.446 --> 00:10:36.976 (Kicheko) NOTE Paragraph 00:10:37.000 --> 00:10:40.680 ili nikuoneshe ni kiasi gani cha pesa inakugharimu kila unaposhikwa na hisia. NOTE Paragraph 00:10:41.960 --> 00:10:45.120 (Makofi na Vifijo) NOTE Paragraph 00:10:47.600 --> 00:10:49.136 Asanteni sana. Asanteni. NOTE Paragraph 00:10:49.160 --> 00:10:50.320 (Makofi na Vifijo)