1 00:00:00,960 --> 00:00:03,016 Nilikuwa na umri wa miaka 14 2 00:00:03,040 --> 00:00:04,616 nikiwa kwenye jumba la michezo, 3 00:00:04,640 --> 00:00:06,400 nikiiba kwenye mashine ya mchezo, 4 00:00:07,200 --> 00:00:08,976 na nilipokuwa nikitoka nje ya jengo 5 00:00:09,000 --> 00:00:11,380 mlinzi alikamata mkono wangu, hivyo nikakimbia. 6 00:00:11,760 --> 00:00:14,736 Nilikimbilia mtaani, na nikaruka juu ya uzio. 7 00:00:14,760 --> 00:00:16,376 Na nilipofika juu, 8 00:00:16,400 --> 00:00:18,576 uzito wa sarafu 3,000 kwenye mkoba wangu 9 00:00:18,600 --> 00:00:20,240 ulinielemea na kunivuta chini. 10 00:00:20,880 --> 00:00:23,936 Niliponyanyuka, mlinzi alikuwa amesima juu yangu, 11 00:00:23,960 --> 00:00:27,376 na akasema, "Siku nyingine nyinyi vibaka, ibeni vitu mnavyoweza kubeba." 12 00:00:27,400 --> 00:00:29,416 (Kicheko) 13 00:00:29,440 --> 00:00:31,576 Nilipelekwa kwenye mahabusu ya watoto 14 00:00:31,600 --> 00:00:34,160 na nilipoachiliwa chini ya dhamana ya mama yangu, 15 00:00:35,080 --> 00:00:38,056 maneno ya kwanza mjomba wangu alisema yalikuwa, "Ulikamatwaje?" 16 00:00:38,080 --> 00:00:40,256 Nikasema, "Mzee, mkoba ulikuwa mzito sana." 17 00:00:40,280 --> 00:00:42,660 Akasema, "Mzee, hukutakiwa kuchukua sarafu zote." 18 00:00:42,660 --> 00:00:46,056 Nikasema, "Mzee, zilikuwa ndogo. Ningefanyaje?" 19 00:00:46,080 --> 00:00:50,976 na dakika 10 baadaye, alinipeleka kuiba kwenye mashine nyingine ya mchezo. 20 00:00:51,000 --> 00:00:53,020 Tulihitaji pesa ya petroli kufika maskani. 21 00:00:53,250 --> 00:00:55,290 Hayo ndiyo yalikuwa maisha yangu. 22 00:00:55,440 --> 00:00:57,296 Nimekulia Oakland, Kalifornia, 23 00:00:57,320 --> 00:00:59,656 na mama yangu na ndugu wa karibu wa familia 24 00:00:59,680 --> 00:01:00,920 walevi wa madawa ya kulevya ya kokeini . 25 00:01:01,560 --> 00:01:06,000 Mazingira yangu yalijumuisha kuishi na familia, marafiki, 26 00:01:06,960 --> 00:01:08,560 na makazi kwa wasio-na-makazi. 27 00:01:09,040 --> 00:01:12,720 Mara nyingi, mlo wa jioni tuliupata kwenye foleni za vyakula vya msaada. 28 00:01:13,440 --> 00:01:15,296 Mjomba aliniambia hivi: 29 00:01:15,320 --> 00:01:17,296 pesa inatawala dunia 30 00:01:17,320 --> 00:01:18,536 na kila kitu ndani yake. 31 00:01:18,560 --> 00:01:20,640 Na katika hii mitaa, pesa ni Mfalme. 32 00:01:21,320 --> 00:01:22,936 Na ikiwa utafuata pesa, 33 00:01:22,960 --> 00:01:25,480 itakupeleka kwa mtu mbaya au mtu mzuri. 34 00:01:26,080 --> 00:01:28,616 Baadaye kidogo, nilifanya uhalifu wangu wa kwanza, 35 00:01:28,640 --> 00:01:31,616 na ndiyo mara ya kwanza nilipoambiwa kuwa nina kipaji 36 00:01:31,640 --> 00:01:33,790 na nikajisikia kuwa kuna mtu ananiaminia. 37 00:01:34,240 --> 00:01:36,946 Hakuna aliyewahi-niambia kuwa ningeweza kuwa mwanasheria, 38 00:01:36,946 --> 00:01:38,056 daktari au mhandisi. 39 00:01:38,080 --> 00:01:41,596 Yaani, ningewezaje kufanya hivyo? Sikuweza kusoma, kuandika wala kutahajia. 40 00:01:41,596 --> 00:01:42,736 Sikuwa mtu aliyesoma. 41 00:01:42,760 --> 00:01:45,880 Kwahiyo, mara zote nilifikiri uhalifu ndio njia ya kwenda. 42 00:01:47,480 --> 00:01:49,176 Na kisha siku moja 43 00:01:49,200 --> 00:01:50,456 Nilikuwa naongea na mtu 44 00:01:50,480 --> 00:01:54,080 na alikuwa ananiambia juu ya huu wizi ambao tungeweza fanya. 45 00:01:54,760 --> 00:01:55,960 Na tukaufanya. 46 00:01:57,080 --> 00:01:58,896 Ukweli ni kwamba nilikuwa nakulia 47 00:01:58,920 --> 00:02:01,296 kwenye nchi yenye uwezo mkubwa wa kifedha duniani, 48 00:02:01,296 --> 00:02:03,016 Marekani, 49 00:02:03,040 --> 00:02:07,120 huku nikiangalia mama yangu, akisimama kwenye foleni ya benki ya damu 50 00:02:08,680 --> 00:02:12,360 kuuza damu yake kwa Dola 40 kujaribu tu kulisha wanae. 51 00:02:13,320 --> 00:02:16,640 Bado ana alama za sindano mikononi mwake leo kudhihirisha hilo. 52 00:02:17,480 --> 00:02:19,216 Kwa hiyo sikuijali jumuiya yangu, 53 00:02:19,240 --> 00:02:20,736 Hawakujali maisha yangu. 54 00:02:20,760 --> 00:02:24,176 Kila mtu pale alifanya anachotaka fanya kupata alichotaka, 55 00:02:24,200 --> 00:02:26,376 wauza mihadarati, wezi, benki ya damu. 56 00:02:26,400 --> 00:02:28,016 Kila mtu alichukua fedha ya damu. 57 00:02:28,040 --> 00:02:30,196 Hivyo nilipata yangu kwa njia yoyote ile. 58 00:02:30,196 --> 00:02:31,556 Nilipata yangu. 59 00:02:31,556 --> 00:02:33,680 Elimu ya fedha kweli ilitawala dunia, 60 00:02:34,680 --> 00:02:36,656 na nilikuwa mtoto mtumwa kwake 61 00:02:36,680 --> 00:02:37,920 nikifuata mtu mbaya. 62 00:02:40,280 --> 00:02:43,456 Nikiwa na miaka 17, nilikamatwa kwa wizi na mauaji 63 00:02:43,480 --> 00:02:47,456 na punde nikajifunza kuwa fedha jela zinatawala zaidi ya zilivyo mitaani, 64 00:02:47,480 --> 00:02:48,680 Hivyo nilitaka kuingia. 65 00:02:49,600 --> 00:02:52,656 Siku moja, nilikurupuka kushika ukurasa wa michezo katika gazeti 66 00:02:52,680 --> 00:02:54,496 ili mfungwa mwenzangu anisomee, 67 00:02:54,520 --> 00:02:56,936 na kwa bahati mbaya nikachukua sehemu ya biashara. 68 00:02:56,960 --> 00:03:00,216 Na huyu mzee akasema, "Hey, kijana, umechukua hisa?" 69 00:03:00,240 --> 00:03:01,496 Na nikasema, "Ndio nini hicho?" 70 00:03:01,520 --> 00:03:04,756 Akasema, "Hiyo ndiyo sehemu ambayo watu weupe huweka pesa yao yote." 71 00:03:04,756 --> 00:03:05,936 (Kicheko) 72 00:03:05,960 --> 00:03:09,816 Na ilikuwa ndiyo mara ya kwanza nilipata ono fupi la tumaini, 73 00:03:09,840 --> 00:03:11,336 siku za baadaye. 74 00:03:11,360 --> 00:03:13,960 Alinipa maelezo mafupi ya hisa zilikuwa ni nini, 75 00:03:14,800 --> 00:03:16,340 lakini ilikuwa ni muhtasari tu. 76 00:03:18,360 --> 00:03:20,136 Yaani, ningewezaje kuifanya? 77 00:03:20,160 --> 00:03:22,210 Sikuweza kusoma, kuandika wala kutahajia. 78 00:03:22,600 --> 00:03:25,216 Ujuzi niliokuwa nimeukuza kuficha kutokusoma kwangu 79 00:03:25,240 --> 00:03:27,296 haukufanya kazi tena katika mazingira haya. 80 00:03:27,296 --> 00:03:30,336 Nilikuwa nimenaswa kwenye kizimba mateka kati ya watekaji, 81 00:03:30,360 --> 00:03:32,256 nikipigania uhuru ambao sijawahi kuwa nao. 82 00:03:32,280 --> 00:03:34,456 Nilikuwa nimepotea, nimechoka, 83 00:03:34,480 --> 00:03:35,840 na sikuwa na machaguzi. 84 00:03:37,000 --> 00:03:38,776 Kwa hiyo nikiwa na miaka 20, 85 00:03:38,800 --> 00:03:42,130 nilifanya kitu kigumu kuliko vyote nilivyowahi kufanya maishani mwangu. 86 00:03:42,160 --> 00:03:43,360 Nilichukua kitabu, 87 00:03:45,400 --> 00:03:47,880 na ilikuwa ni kipindi kigumu sana maishani mwangu. 88 00:03:49,320 --> 00:03:51,136 kujaribu kujifunza jinsi ya kusoma, 89 00:03:51,160 --> 00:03:53,776 kutengana na familia yangu, 90 00:03:53,800 --> 00:03:55,000 na rafiki zangu. 91 00:03:56,280 --> 00:03:57,736 Ilikuwa shida, mzee. 92 00:03:57,760 --> 00:03:59,136 Ilikuwa ni mahangaiko. 93 00:03:59,160 --> 00:04:00,856 Lakini sikufahamu japo kidogo kuwa 94 00:04:00,880 --> 00:04:04,296 nilikuwa napata zawadi kubwa kuliko zote nilizowahi kuziota, 95 00:04:04,320 --> 00:04:05,520 kujithamini, 96 00:04:06,320 --> 00:04:08,160 maarifa, nidhamu. 97 00:04:09,000 --> 00:04:12,696 Nilisisimka mno kusoma, kiasi kwamba nilisoma kila kitu nilichokitia mkononi: 98 00:04:12,720 --> 00:04:16,055 makaratasi ya pipi, nembo za nguo, alama za barabarani, kila kitu. 99 00:04:16,079 --> 00:04:17,326 Nilikuwa nikisoma tu vitu! 100 00:04:17,326 --> 00:04:18,336 (Makofi na Vifijo) 101 00:04:18,360 --> 00:04:19,560 kusoma tu vitu. 102 00:04:21,360 --> 00:04:24,560 Nilisisimka sana kujua jinsi ya kusoma na kujua jinsi ya kutahajia. 103 00:04:24,720 --> 00:04:27,006 Rafiki alikuja, akaniuliza, "Mzee, unakula nini?" 104 00:04:27,006 --> 00:04:28,736 Nikasema, "P-I-P-I, pipi." 105 00:04:28,760 --> 00:04:31,016 (Kicheko) 106 00:04:31,040 --> 00:04:33,656 Akasema, "Nipe kidogo." Nikasema, "L-A. La." 107 00:04:33,656 --> 00:04:34,776 (Kicheko) 108 00:04:34,800 --> 00:04:36,216 Ilikuwa babukubwa. 109 00:04:36,240 --> 00:04:39,416 Yaani, sasa naweza, kwa mara ya kwanza katika maisha yangu, kusoma. 110 00:04:39,440 --> 00:04:41,480 Hisia niliyoipata, ni ya kustaajabu sana. 111 00:04:43,240 --> 00:04:45,840 Kisha, nikiwa na miaka 22, nikijisikia mwenyewe, 112 00:04:46,800 --> 00:04:48,536 nikijiamini, 113 00:04:48,560 --> 00:04:50,400 Nilikumbuka kile yule mzee aliniambia. 114 00:04:51,760 --> 00:04:55,496 Kwa hiyo nilichukua kurasa za biashara za gazeti. 115 00:04:55,520 --> 00:04:57,456 Nilitaka kuwatafuta hawa matajiri weupe. 116 00:04:57,480 --> 00:04:59,080 (Kicheko) 117 00:05:00,520 --> 00:05:02,440 Kwa hiyo nilitafuta ule muhtasari. 118 00:05:03,480 --> 00:05:05,096 Nilipokuwa nikijiendeleza kikazi 119 00:05:05,120 --> 00:05:08,976 nikifundisha wengine namna ya kusimamia fedha na kuwekeza, 120 00:05:09,000 --> 00:05:12,336 punde nikajifunza kuwa nilihitaji kuwajibika kwa matendo yangu. 121 00:05:12,360 --> 00:05:15,376 Kweli, nilikulia kwenye mazingira tata sana, 122 00:05:15,400 --> 00:05:17,336 lakini nilichagua kufanya uhalifu, 123 00:05:17,360 --> 00:05:19,136 na nilipaswa kukiri hilo. 124 00:05:19,160 --> 00:05:21,776 Nilipaswa kuwajibika kwa hilo, na nilifanya hivyo. 125 00:05:21,800 --> 00:05:24,696 Nilikuwa nikiunda mtaala ambao ungeweza kuwafundisha wafungwa 126 00:05:24,720 --> 00:05:27,110 namna ya kusimamia fedha kupitia ajira za gerezani. 127 00:05:28,720 --> 00:05:31,896 Kutiisha mtindo wetu wa maisha kungeweza kutoa zana zihamishikazo 128 00:05:31,920 --> 00:05:35,256 ambazo tunaweza kuzitumia kusimamia fedha tunapoirudi kwenye jamii, 129 00:05:35,280 --> 00:05:38,536 kama watu wengi walivyofanya ambao hawakufanya uhalifu. 130 00:05:38,560 --> 00:05:39,760 Kisha niligundua 131 00:05:40,680 --> 00:05:42,736 kulingana takwimu ya MarketWatch, 132 00:05:42,760 --> 00:05:45,296 zaidi ya asilimia 60 ya wakazi wa Marekani 133 00:05:45,320 --> 00:05:47,440 wana chini ya Dola 1,000 katika akiba. 134 00:05:48,200 --> 00:05:51,416 Michezo ilielezea kwamba zaidi ya asilimia 60 ya wachezaji wa NBA 135 00:05:51,440 --> 00:05:52,976 na wachezaji wa NFL hufilisika. 136 00:05:53,000 --> 00:05:56,040 Asilimia 40 ya matatizo ya ndoa hutokana na masuala ya kifedha. 137 00:05:57,080 --> 00:05:58,296 Balaa gani? 138 00:05:58,320 --> 00:06:00,456 (Kicheko) 139 00:06:00,480 --> 00:06:03,176 Unataka kuniambia, watu wamefanya kazi maisha yao yote, 140 00:06:03,200 --> 00:06:05,776 wakinunua magari, nguo, nyumba na vitu mbalimbali 141 00:06:05,800 --> 00:06:08,016 lakini walikuwa waliishi hundi kwa hundi? 142 00:06:08,040 --> 00:06:12,376 Ni namna gani duniani wanajamii wangekwenda kuwasaidia wafungwa 143 00:06:12,400 --> 00:06:13,616 kurudi kwenye jamii 144 00:06:13,640 --> 00:06:15,830 ikiwa hawakuweza kusimamia mambo yao wenyewe? 145 00:06:16,160 --> 00:06:17,416 Tumevurugwa. 146 00:06:17,440 --> 00:06:19,176 (Kicheko) 147 00:06:19,200 --> 00:06:20,600 Nahitaji mpango mzuri zaidi. 148 00:06:22,520 --> 00:06:24,640 Hii haitakwenda kufanya kazi vizuri. 149 00:06:25,040 --> 00:06:26,240 Hivyo ... 150 00:06:27,880 --> 00:06:29,080 Nilifikiria. 151 00:06:31,800 --> 00:06:35,020 Sasa nilikuwa na wajibu kukutana na wale waliokuwa kwenye mkondo huo 152 00:06:36,360 --> 00:06:37,576 na kuwasaidia, 153 00:06:37,600 --> 00:06:40,856 na ilikuwa ni ajabu sababu sasa nilijali jumuiya yangu 154 00:06:40,880 --> 00:06:43,240 Lo, hebu fikiria. Nilijali kuhusu jumuiya yangu. 155 00:06:44,640 --> 00:06:46,936 Ujinga juu ya Fedha ni ugonjwa 156 00:06:46,960 --> 00:06:49,976 ambao umedhohofisha wachache na walio chini katika jamii yetu 157 00:06:50,000 --> 00:06:52,136 kwa vizazi na vizazi, 158 00:06:52,160 --> 00:06:54,656 na tunapaswa kukasirika juu ya hilo. 159 00:06:54,680 --> 00:06:56,256 Ebu jiulize: 160 00:06:56,280 --> 00:06:59,536 Inawezekanaje asilimia 50 ya wakazi wa Marekani 161 00:06:59,560 --> 00:07:03,520 wasiwe na elimu ya fedha katika nchi inayoendeshwa kwa ustawi wa kifedha? 162 00:07:05,000 --> 00:07:07,856 Kupatikana kwa haki kwetu, hadhi yetu ya kijamii, 163 00:07:07,880 --> 00:07:10,896 hali ya maisha, usafirishaji na chakula 164 00:07:10,920 --> 00:07:13,976 vyote vinategemea fedha ambayo watu wengi hawawezi kuisimamia. 165 00:07:14,000 --> 00:07:15,576 Ni ajabu! 166 00:07:15,600 --> 00:07:16,976 Ni janga 167 00:07:17,000 --> 00:07:20,000 na hatari kubwa kwa usalama wa umma kuliko suala jingine lolote. 168 00:07:21,720 --> 00:07:24,376 Kadiri ya Kitengo cha Urekebishaji cha Kalifornia, 169 00:07:24,400 --> 00:07:26,736 zaidi ya asilimia 70 ya wale waliofungwa 170 00:07:26,760 --> 00:07:30,376 wamefanya au wameshtakiwa kwa uhalifu uhusianao na fedha: 171 00:07:30,400 --> 00:07:34,920 wizi wa kutumia nguvu, kuvunja nyumba, kutapeli, uporaji, ghusubu -- 172 00:07:35,720 --> 00:07:37,040 na orodha inaendelea. 173 00:07:37,920 --> 00:07:39,136 Angalia hii: 174 00:07:39,160 --> 00:07:42,096 Mfungwa wa kawaida 175 00:07:42,120 --> 00:07:44,616 huingia katika mfumo wa gereza wa Kalifornia 176 00:07:44,640 --> 00:07:46,200 pasipo kuwa na elimu ya fedha, 177 00:07:46,840 --> 00:07:48,816 hupata ujira wa senti 30 kwa saa, 178 00:07:48,840 --> 00:07:51,056 zaidi ya Dola 800 kwa mwaka, 179 00:07:51,080 --> 00:07:53,840 bila ya kuwa na matumizi yoyote na kuweka akiba yoyote. 180 00:07:54,760 --> 00:07:59,096 Anapopewa msamaha, hupewa dola 200 pesa ya geti na kuambiwa, 181 00:07:59,120 --> 00:08:02,340 "Wee, mafanikio mema, kaa mbali na matatizo. Usirudi gerezani tena." 182 00:08:02,800 --> 00:08:06,096 Bila kuwa na maandalizi yoyote ya maana au mpango fedha wa muda mrefu, 183 00:08:06,120 --> 00:08:07,320 anafanyaje ...? 184 00:08:08,600 --> 00:08:09,800 Akiwa na miaka 60? 185 00:08:11,120 --> 00:08:12,456 Apate kazi nzuri, 186 00:08:12,480 --> 00:08:16,400 au arudi kwenye tabia ile ile ya uhalifu iliyompeleka gerezani kwanza? 187 00:08:17,400 --> 00:08:19,176 Nyinyi walipakodi, chagueni wenyewe. 188 00:08:19,200 --> 00:08:22,360 Hakika, elimu yake imeshamchagulia, pengine. 189 00:08:23,120 --> 00:08:25,480 Kwa hiyo, tunatibuje ugonjwa huu? 190 00:08:26,240 --> 00:08:27,976 Nilishiriki kuanzisha programu 191 00:08:28,000 --> 00:08:32,576 tuliyoiita Elimu Hisia ya Uwezeshaji wa Kifedha 192 00:08:32,600 --> 00:08:34,056 tunaiita FEEL 193 00:08:34,080 --> 00:08:37,256 na inafundisha namna ya kutenganisha maamuzi ya kihisia 194 00:08:37,280 --> 00:08:39,256 na maamuzi ya kifedha, 195 00:08:39,280 --> 00:08:42,696 na sheria 4 aushi za utawala fedha binafsi: 196 00:08:42,720 --> 00:08:44,280 njia sahihi ya kuweka akiba, 197 00:08:45,560 --> 00:08:47,200 kudhibiti gharama zako za maisha, 198 00:08:48,320 --> 00:08:50,096 kukopa fedha kwenye ufanisi 199 00:08:50,120 --> 00:08:53,896 kutawanya fedha yako kuruhusu fedha yako ikufanyie kazi 200 00:08:53,920 --> 00:08:55,736 badala ya wewe kuifanyia kazi. 201 00:08:55,760 --> 00:08:59,920 Wafungwa wanahitaji ujuzi huu kabla ya kuingia tena kwenye jamii. 202 00:09:01,480 --> 00:09:05,376 Hatuwezi kubadilika kuwa na maisha ya kawaida bila ujuzi huu wa maisha. 203 00:09:05,400 --> 00:09:09,216 Hii dhana kuwa ni Weledi tu wanaweza kuwekeza na kusimamia fedha 204 00:09:09,240 --> 00:09:11,496 ni ya fedheha kabisa, 205 00:09:11,520 --> 00:09:13,587 na yeyote aliyewaambia hivyo anadanganya. 206 00:09:13,627 --> 00:09:18,176 (Makofi na Vifijo) 207 00:09:18,200 --> 00:09:20,616 Mweledi ni mtu 208 00:09:20,640 --> 00:09:23,136 anayejua kazi zake kuliko walio wengi, 209 00:09:23,160 --> 00:09:28,096 na hakuna mtu ajuaye kiasi gani cha fedha wahitaji, unacho, au wataka zaidi ya wewe, 210 00:09:28,120 --> 00:09:30,080 ikimaanisha kuwa wewe ni mweledi. 211 00:09:30,880 --> 00:09:35,096 Elimu ya fedha siyo stadi, mabibi na mabwana. 212 00:09:35,120 --> 00:09:36,320 Ni mtindo wa maisha. 213 00:09:37,560 --> 00:09:42,056 Uimara wa kifedha ni matokeo ya ziada ya mtindo sahihi wa maisha. 214 00:09:42,080 --> 00:09:45,880 Mfungwa mwenye elimu nzuri ya kifedha anaweza kuwa mwananchi mlipakodi, 215 00:09:46,680 --> 00:09:50,176 na mwananchi mlipakodi mwenye elimu nzuri ya kifedha anaweza kubaki hivyo. 216 00:09:50,200 --> 00:09:54,536 Hii inatuwezesha kuunda daraja kati ya wale watu tunaowashawishi: 217 00:09:54,560 --> 00:09:57,296 familia, marafiki na wale vijana 218 00:09:57,320 --> 00:10:00,240 ambao bado wanaamini kuwa uhalifu na pesa vina uhusiano. 219 00:10:01,720 --> 00:10:04,616 Kwa hiyo tupoteze uwoga na wasiwasi 220 00:10:04,640 --> 00:10:06,096 wa maneno makubwa ya kifedha 221 00:10:06,120 --> 00:10:09,696 na ujinga mwingine wote ambao mmekuwa mkisikia huko nje. 222 00:10:09,720 --> 00:10:13,576 Na tujikite kwenye kiini kilichokuwa kinadhoofisha jamii yetu 223 00:10:13,600 --> 00:10:17,960 kuanzia kutimiza wajibu wako la kuwa meneja mzuri wa maisha. 224 00:10:19,000 --> 00:10:22,336 Na tutoe mtaala mwepesi na rahisi kutumia 225 00:10:22,360 --> 00:10:24,616 ambao utaingia kwenye kiini, kiini 226 00:10:24,640 --> 00:10:28,576 cha ni nini ukweli wa uwezeshaji wa kifedha na elimu ya hisia. 227 00:10:28,600 --> 00:10:31,496 Sasa, ikiwa umekaa hapa kwa wasikilizaji na umesema, 228 00:10:31,520 --> 00:10:33,936 "Ndiyo, kweli, hiyo si mimi na sikubaliani nayo," 229 00:10:33,960 --> 00:10:35,446 basi njoo uchukue somo langu -- 230 00:10:35,446 --> 00:10:36,976 (Kicheko) 231 00:10:37,000 --> 00:10:40,680 ili nikuoneshe ni kiasi gani cha pesa inakugharimu kila unaposhikwa na hisia. 232 00:10:41,960 --> 00:10:45,120 (Makofi na Vifijo) 233 00:10:47,600 --> 00:10:49,136 Asanteni sana. Asanteni. 234 00:10:49,160 --> 00:10:50,320 (Makofi na Vifijo)