Nataka niwaambie kisa
kuhusu msichana mmoja.
Lakini siwezi kuwaambia jina lake halisi.
Hivyo tufanye kumuita Hadiza.
Hadiza ana miaka 20.
Ana aibu,
lakini ana tabasamu zuri
ambalo hufanya uso wake kung'aa
Lakini yuko katika maumivu wakati wote.
Na anaweza kuwa
mtu wa matibabu maisha yake yote.
Je wataka kujua kwa nini?
Hadiza ni msichana wa Chibok,
na mnamo Aprili 14, 2014, alitekwa
na magaidi wa Boko Haram.
Ingawa alijaribu kutoroka,
kwa kuruka toka kwenye gari lililokuwa limebeba wasichana.
Lakini alipotua chini, alivunjika miguu yako yote miwili,
na alihitaji kutambaa kwa tumbo kujificha kichakani.
Aliniambia aliogopa sana
kuwa Boko Haram wangeweza kumrudia.
Alikuwa mmoja wa wasichana 57 waliotoroka
kwa kuruka toka kwenye magari siku ile.
Kisa hiki, hakika, kilisambaa kama mawimbi
duniani kote.
Watu kama Michelle Obama,
Malala na wengine
walitoa sauti zao wakipinga,
na wakati huo huo --
nilikuwa nikiishi London wati huo
Nilitumwa kutoka London kwenda Abuja
kupata habari za Jukwaa la Uchumi Duniani
ambapo Naijeria ilikuwa mwenyeji
kwa mara ya kwanza
Lakini nilipofika, ilikuwa dhahiri
kwamba kulikuwa na habari moja tu mjini.
Tuliiiweka serikali kwenye shinikizo.
Tuliuliza maswali magumu
juu ya nini wanafanya
kuwarudisha wasichana hawa.
Ilieleweka hakika,
hawakuwa na furaha juu ya maswali yetu,
na tuseme tu tulipata mgao mzuri
wa "ukweli mbadala".
(Kicheko)
Wanaijeria wenye ushawishi mkubwa
walikuwa wakituambia wakati ule
kuwa tulikuwa washamba.
hatukuelewa hali ya siasa ya Naijeria.
Lakini pia walituambia
kuwa habari ya wasichana wa Chibok
illikuwa mzaha.
Cha kusikitisha ni kuwa
habari hii ya mzaha imedumu
na bado kuna watu Naijeria leo
wanaoamini
wasichana wa Chibok hawakutekwa.
Bado, nilikuwa nikiongea na watu kama hawa
wazazi wenye huzuni kubwa,
ambao walituambia
siku Boko Haram waliwateka binti zao,
walikimbia mpaka Msitu wa Sambisa
wakifukuza magari laliyobeba binti zao.
Wao walikuwa na mapanga kama silaha,
lakini walilazimika kurudi
sababu Boko Haram walikuwa na bunduki.
Kwa miaka miwili, pasipo kuepukika,
ajenda za habari zilisonga mbele,
na kwa miaka miwili,
hatukusikia sana
kuhusu wasichana wa Chibok.
Kila moja alidhania wamekwishakufa.
Lakini Aprili mwaka jana,
niliweza kupata video hii.
Hii ni picha-mnato toka kwenye video
ambayo Boko Haram walirekodi
kama ushahidi kuwa wako hai,
na kupitia chanzo kimoja,
nilipata video hii.
Lakini kabla sijaichapisha,
Nilihitaji kusafiri
kwenda kaskazini mashariki mwa Naijeria
kuzungumza na wazazi, kuihakikisha.
Sikuhitaji kusubiri sana
kupata uthibitisho.
Mmoja wa wamama,
alipoangalia hiyo video, aliniambia
kama angeweza kuifika ndani ya kompyuta
na kumvuta na kumtoa nje mtoto wake
kutoka kwenye kompyuta,
angefanya hivyo.
Kwa wale kati yenu ambao ni wazazi,
kama mimi, katika wasikilizaji.
Mnaweza tu kufikiria uchungu
ambao yule mama aliusikia
Video hii iliendelea hadi kuanzisha
mjadala wa mazungumzo na Boko Haram.
Na seneta mmoja wa Kinaijeria aliniambia
kuwa kwa sababu ya video hii
waliingia katika yale mazungumzo,
kwa sababu muda mrefu walidhani
wasichana wa Chibok walishakufa.
Wasichana 21 waliachiwa huru
mwezi Oktoba mwaka jana.
Cha kusikitisha, karibu 200 kati yao
bado hawajapatikana.
Ni lazima nikiri,
sijawa mwangalizi niliyependelea
kuzungumzia habari hii.
Nakuwa na hasira ninapofikiria
juu ya fursa zinazopotea
kuwaokoa wasichana hawa.
Nakuwa na hasira ninapofikiria
juu ya kile wazazi wameniambia,
kuwa ingekuwa mabinti hawa
ni wa matajiri na wenye nguvu,
wangepatikana mapema zaidi.
Na nina hasira
kwamba simulizi la mzaha
ambalo naamini hakika
limesababisha kuchelewa;
lilikuwa ni sehemu ya sababu
ya ucheleweshwaji wa kurudi kwao.
Hii inaonesha kwangu
hatari kubwa ya habari za uongo.
Nini twaweza kufanya juu ya hili?
Kuna watu werevu sana,
wahandisi werevu huko Google na Facebook,
wanaojaribu kutumia tekinolojia
kuzuia kusambaa kwa habari za uongo.
Lakini zaidi ya hapo, nafikiri
kila mmoja hapa -- wewe na mimi --
tuna nafasi ya kushiriki katika hilo.
Sisi ndio tunaoshirikishana maudhui
Sisi ndio tunaoshirikishana
habari mitandaoni
Nyakati za leo, sisi sote ni wachapishaji,
na tuna jukumu.
Katika kazi yangu kama mwanahabari,
Ninaangalia, ninathibitisha,
Ninaamini hisia zangu,
lakini nauliza maswali magumu.
Kwa nini huyu mtu ananiambia habari hii?
Nini atakachokipata
kwa kunishirikisha taarifa hii?
Je, ana ajenda ya siri?
Ninaamini kabisa kuwa wote tunatakiwa
kuanza kuuliza maswali magumu zaidi
kwa taarifa tunazozipata mtandaoni.
Utafiti unaonesha kwamba kati yetu
kuna wasiosoma zaidi ya vichwa vya habari
kabla ya kushirikisha habari.
Nani hapa amefanya hivyo?
Najua mimi nimefanya.
Lakini ingekuwaje kama
tungeacha kuchukua taarifa tuipatayo jinsi ionekanavyo kijuujuu?
vipi kama tutasimama na kufikiria athari
za taarifa ambazo tunazisambaza
na uwezo wake wa kuchochea vurugu na chuki?
Vipi kama tutasimama na kufikiria juu ya athari kwenye maisha halisi
za taarifa tunazoshirikishana?
Ahsanteni sana kwa kunisikiliza.
(Makofi na vifijo)