Nitaanza leo kwa kuigawana shairi iliyoandikiwa na rafiki yangu mmalawi, Eileen Piri. Eileen ana miaka 13 tu, lakini tulipoangalia diwani ya ushairi tuliyoandika, Niliona shairi yake ilinivuta sana, ilitia motisha sana. Basi nitakusomeeni. Ameiita shairi yake "Nitaolewa ninapotaka" (Kicheko) "Nitaolewa ninapotaka. Mama yangu hatonilazimisha kuolewa. Baba yangu hatonilazimisha kuolewa. Mjomba, Shangazi, Kaka au dada, Hawawezi kunilazimisha. Hakuna mtu duniani awezaye kunilazimisha kuolewa. Nitaolewa ninapotaka. Hata ukinipiga, hata ukinifukuza hata ukinifanya vibaya, Nitaolewa ninapotaka. Nitaolewa ninapotaka, lakini sio kabla sijapata elimu nzuri na sio kabla sijakua mtu mzima Nitaolewa ninapotaka." Shairi inaonekana isiyo ya kawaida kuandikwa na msichana wa miaka 13, lakini tunapotoka mimi na Eileen, shairi hiyo, niliyoikusomeeni, ni sauti ya shujaa. Ninatoka Malawi. Malawi ni nchi ya maskini, maskini sana, ambapo usawa wa kijinsi sio hakika. Kukua katika nchi ile, Sikuweza kujichagulia katika maisha. Sikuweza hata kuzichungua nafasi za kibinafsi katika maisha yangu. Nitakuambieni hadithi ya wasichana wawili tofauti, wasichana wawili warembo. Hawa wasichana walikua chini ya paa moja. Walikula chakula sawa sawa. Wakati wengine, wangezigawana nguo, na hata viatu. Lakini maisha zao ziliishia tofauti, kwa njia mbili tofauti. Yule msichana mwengine ni dada yangu mdogo. Dada yangu alikuwa na miaka 11 alipopata mimba. Ni jambo la kuumiza. Si kama ilimwumiza pekee, lakini mimi pia. Nilikuwa na wakati wa tafrani pia. Kwa sasa katika utamaduni wangu, ukifika ubalehe, inabidi uende makambi ya kuanzisha. Katika makambi haya, unafundishwa vipi umfurahishe mwanamume kwa kijinsia. Kuna siku maalum, wanayoiita "Siku maalum sana" ambapo mwanamume anaajiriwa na jamii anakuja kambini na anafanya mapenzi na watoto wadogo. Wazeni kiwewe wasichana hawa wanachokisikia kila siku. Wasichana wengi wanapata mimba. Na hata wanashikwa na ukimwi na magonjwa mengine ya zinaa. Kwa dadangu mdogo, alipata mimba. Leo, ana miaka 16 na ana watoto watatu. Ndoa yake ya kwanza haijaishi, wala ndoa yake ya pili. Kwa upande wengine, kuna msichana huyo. Anashangaza. (Kicheko) (Makofi) Nasema anashangaza kwa sababu ni kweli. Ni zaidi ya mzuri. Msichana yule ni mimi. (Kicheko) Nilipokuwa na miaka 13, Niliambiwa, umekua mzima, sasa umebalehe, inadhaniwa uende kambi la kuanzisha. Nilisema, "Nini? Siendi kwa yale makambi ya kuanzisha." Unajua nini mwanamke yule aliniambia? "Wewe ni mpumbavu. Mkaidi. Huziheshimu desturi za jamii yetu, za jumuia yetu." Nilikataa kwa sababu nilijua wapi nilipokwenda. Nilijua nilivyotaka katika maisha yangu. Nilikuwa na matumaini mengi nilipokuwa mtoto. Nilitaka kupata elimu nzuri Kutafuta kazi nzuri wakati wa badae. Nilikuwa najifikiria kama mwanasheria, kukaa katika kiti kile kikubwa. Yale yalikuwa mawazo yaliokuwa katika akili yangu kila siku. Na nilijua kwamba siku moja Ningesaidia kupa kitu, kitu kidogo kwa jumuia yangu. Lakini kila siku baada ya kukataa, wanawake wangeniambia, "Jitazama, umekua mtu mzima. Dadako mdogo amepata mtoto. Vipi wewe?" Ile ilikuwa muziki niliyoisikia kila siku, na ile ni muziki wasichana wanayoisikia kila siku wasipolifanya jambo ambalo jumuia inawatakia wafanye. Nilipozilinganisha hadithi hizo mbili kati ya mimi na dadangu, Nilisema, "Mbona nisiweze kufanya kitu?" Kwa nini nisiweze kubadilisha jambo lililotokea kwa muda mrefu katika jamii yetu?" Wakati ule niliwaita wasichana wengine kama dadangu, ambao wamepata watoto, waliokwenda darasani lakini wamesahau kusoma na kuandika. Nilisema "Njoo, tukumbushane je kusoma na kuandika tena, kuikamata kalamu vipi, kusomaje, kuzuia kitabu." Ilikuwa wakati nzuri sana nao. Sio kwamba nilifundishwa kidogo kuhusu wale, lakini pia waliweza kuniambia hadithi zao za kibinafsi, waliyokabiliana kila siku kama mama wadogo. Wakati ule nilidhani, "Kwa nini tusiweze kuangalia mambo hayo yanayotuathiri na kuyaonesha na kuwaambia mama zao, viongozi wetu wa jadi, kwamba mambo hayo ni maovu?" Ilikuwa jambo la hofu, kwa sababu viongozi hawa wa jadi, wameshayazoea mambo yaliyokuwepo kwa muda mrefu. Ni jambo ambalo ni ngumu kubadilisha, lakini nzuri kujitahidi. Kwa hiyo tulijitahidi. Ilikuwa ngumu sana, lakini tulivumulia. Na mimi nipo kwa kusema kwamba katika jumuia yangu, ilikuwa jumuia ya kwanza baada ya wasichana walijitahidi sana kumthibitishia kiongozi wa jadi wetu, na kiongozi wetu alitutetea na akasema hakuna msichana alazimishwaye kuolewa kabla hajafika miaka 18. (Makofi) Katika jumuia yangu Ilikuwa mara ya kwanza kwa jumuia, ilibidi watazame sheria ndogo, ya kwanza iliyowalinda wasichana katika jumuia yetu. Hatukumaliza na hivyo. Tuliendelea. Tulikusudia kuwapigania wasichana sio katika jamii yangu tu lakini kwenye jamii nyingine. Wakati muswada wa ndoa za watoto iliwasilishwa mwezi wa pili tulikuwepo kwenye mahakama ya bunge. Kila siku, wakati wabunge walipoingia, tulikuwa tukiwaambia, "Tafadhali uitegemee muswada hii?" Na hatuna teknolojia nyingi kama huku, lakini tunazo simu zetu ndogo. Kwa hiyo tulisema, "Mbona tusiweze kupata namba zao na kuwatumia text?" Kwa hiyo tulifanya hivyo. Na ilikuwa jambo zuri (Makofi) Kwa hiyo muswada ilipokubalika, tuliwajibia na text, "Asante kwa kutegemea muswada." (Kicheko) Na muswada iliposajilika na Rais, kwa kuifanya kuwa sheria, ilikuwa ziada. Sasa, katika Malawi, miaka 18 ni umri wa kisheria kuolewa, kutoka 15 hadi 18. (Makofi) Ni jambo zuri kulijua kwamba muswada imakubalika, lakini nikuambieni: Kuna nchi ambako miaka 18 ni umri wa kisheria kuolewa, lakini sio tunasikia kilio za wanawake na wasichana kila siku? Kila siku, maisha ya wasichana yanashuka thamani. Ni wakati muhimu kwa viongozi waiheshimu ahadi yao. Kwa kuiheshimu ahadi hiyo, inamaanisha kuyaweka maswala ya wasichana moyoni kila mara. Tusitiishiwe kama duni, lakini wajue kwamba wanawake, kama sisi chumbani humu, sisi sio wanawake tu, sisi sio wasichana tu, sisi ni wa ajabu. Tunaweza kufanya zaidi. Na kitu chengine kwa Malawi, na si kwa Malawi pekee lakini nchi nyingine pia: Sheria zinazowepo, mnajua sheria sio sheria mpaka inatekeleza? Sheria iliyokubalika juzi na sheria ambazo katika nchi nyingine zimekuwepo, zinahitajika kutangazwa kwa njia za kienyeji, katika jamii, ambako maswala ya wasichana yako wazi. Wasichana wanakabiliana na maswala, maswala magumu, katika jamii zao kila siku. Kwa hiyo ikiwa wajue kwamba kuna sheria ziwalindazo, wataweza kusimama na kujilinda kwa sababu watajua kwamba kuna sheria ziwalindazo. Na kitu chengine nisemacho ni kwamba sauti za wasichana na wanawake ni nzuri sana, na zipo, lakini hatuwezi kufanya peke yetu. watetezi wa kiume, washirikiana, wajihusishe na tufanye kazi pamoja. ni kazi ya umoja. Tunavyohitaji ni vile vihitajikavyo na wasichana wa sehemu zote: elimu nzuri, na juu ya yote, ni kutoolewa wakiwa na miaka 11. Na zaidi ya hayo, Najua kwamba pamoja, tunaweza kubadilisha mifumo ya kisheria, kiutamaduni na kisiasa inayozikanusha haki za wasichana. Nasimama hapa leo na kutangaza kwamba tunaweza kuisha ndoa za watoto katika kizazi kimoja. Sasa ni wakati ambapo msichana na msichana, na millioni za wasichana duniani, wataweza kusema, "Nitolewa ninapotaka." (Makofi) Asante. (Makofi)