(Gitaa) (wimbo) Gari-bembea, farasi-bembea. Ambapo miinuko ni mbingu, lakini maporomoko, oh, yaweza kuwa jehanamu. Unaweza kushika pete unaweza kupiga hiyo kengele safari ifikapo mwisho, huwezi kutambua. Watu watakwambia kitu hiki kimoja kitafanya maisha yako yawe kamili. Kwahiyo u- utatoa kila kitu ulichonacho na utaishia mtaani. Halafu siku moja utaamka, na watakwambia "Wewe ni Malkia", Lakini utakuja kukuta mtu mwingine ndiye anayevuta nyuzi. Gari-bembea Farasi-bembea Ambapo miinuko ni mbingu, lakini maporomoko, oh, yanaweza kuwa jehanamu. Unaweza kushika pete, unaweza kupiga hiyo kengele, safari ifikapo mwisho, huwezi kutambua. Yule umpendaye, anakupenda -- oh ndiyo -- mpaka mwisho wa wakati. Lakini poteza uwezo wako au poteza utulivu wako, atakutupa kama sarafu. Kila mmoja atakusonga pale mali ni rafiki yako. Bahati yako inapokwisha, utakuwa peke yako tena. Gari-bembea, Farasi-bembea. Ambapo miinuko ni mbingu lakini maporomoko, oh, yanaweza kuwa jehanamu. Unaweza kushika pete, unaweza kupiga hiyo kengele, safari ifikapo mwisho huwezi kujua. Haya, labda naweza kuwa nabeza, na maneno yote haya ni uongo, lakini uzoefu bado unaniambia kuwa mwenye kujihadhari ni mwenye hekima. Lakini kujihadhari kunakufanya usite, na ukisita umepotea, kwa hiyo chukua fursa zako na kamwe usihesabu hasara. Gari-bembea, Farasi-bembea. Ambapo miinuko ni mbingu, Lakini maporomoko, oh, yanaweza kuwa jehanamu. Unaweza kushika pete, unaweza kupiga hiyo kengele, safari ifikapo mwisho -- mwisho, mwisho, huwezi kamwe, daima kutambua. Gari-bembea, Farasi-bembea, Gari-bembea, ndiyo, ndiyo, ndiyo Farasi-bembea. Farasi-bembea, farasi-bembea, farasi-bembea, farasi-bembea, (makofi na vifijo) Michael Pemberton. (makofi na vifijo) Asanteni sana. Asanteni.