(Gitaa)
(wimbo)
Gari-bembea,
farasi-bembea.
Ambapo miinuko ni mbingu,
lakini maporomoko,
oh, yaweza kuwa jehanamu.
Unaweza kushika pete
unaweza kupiga hiyo kengele
safari ifikapo mwisho,
huwezi kutambua.
Watu watakwambia kitu hiki kimoja
kitafanya maisha yako yawe kamili.
Kwahiyo u-
utatoa kila kitu ulichonacho
na utaishia mtaani.
Halafu siku moja utaamka,
na watakwambia "Wewe ni Malkia",
Lakini utakuja kukuta mtu mwingine
ndiye anayevuta nyuzi.
Gari-bembea
Farasi-bembea
Ambapo miinuko ni mbingu,
lakini maporomoko,
oh, yanaweza kuwa jehanamu.
Unaweza kushika pete,
unaweza kupiga hiyo kengele,
safari ifikapo mwisho,
huwezi kutambua.
Yule umpendaye,
anakupenda --
oh ndiyo --
mpaka mwisho wa wakati.
Lakini poteza uwezo wako au poteza utulivu wako,
atakutupa kama sarafu.
Kila mmoja atakusonga
pale mali ni rafiki yako.
Bahati yako inapokwisha,
utakuwa peke yako tena.
Gari-bembea,
Farasi-bembea.
Ambapo miinuko ni mbingu
lakini maporomoko,
oh, yanaweza kuwa jehanamu.
Unaweza kushika pete,
unaweza kupiga hiyo kengele,
safari ifikapo mwisho
huwezi kujua.
Haya, labda naweza kuwa nabeza,
na maneno yote haya ni uongo,
lakini uzoefu bado unaniambia
kuwa mwenye kujihadhari ni mwenye hekima.
Lakini kujihadhari kunakufanya usite,
na ukisita umepotea,
kwa hiyo chukua fursa zako
na kamwe usihesabu hasara.
Gari-bembea,
Farasi-bembea.
Ambapo miinuko ni mbingu,
Lakini maporomoko,
oh, yanaweza kuwa jehanamu.
Unaweza kushika pete,
unaweza kupiga hiyo kengele,
safari ifikapo mwisho --
mwisho, mwisho,
huwezi kamwe, daima kutambua.
Gari-bembea,
Farasi-bembea,
Gari-bembea,
ndiyo, ndiyo, ndiyo
Farasi-bembea.
Farasi-bembea,
farasi-bembea,
farasi-bembea,
farasi-bembea,
(makofi na vifijo)
Michael Pemberton.
(makofi na vifijo)
Asanteni sana.
Asanteni.