1 00:00:00,785 --> 00:00:03,840 Njiani kufika hapa, 2 00:00:03,840 --> 00:00:07,542 nilikuwa na mazungumzo mazuri na mtu aliyekuwa anakaa pembeni yangu kwenye 3 00:00:07,542 --> 00:00:10,562 ndege. Alinambia 4 00:00:10,562 --> 00:00:13,805 "Hamna kazi tena USA, 5 00:00:13,805 --> 00:00:16,073 yaani sasa wamebuni kazi mpya: 6 00:00:16,083 --> 00:00:21,373 mwanasaikolojia wa paka, mzungumzaji wa mbwa,msasi wa kimbunga." 7 00:00:21,373 --> 00:00:24,453 Punde, aliniuliza, 8 00:00:24,453 --> 00:00:27,132 "Kwani wewe unafanya kazi gani?" 9 00:00:27,132 --> 00:00:29,722 Nikamjibu, "Mjenzi wa usalama?" 10 00:00:29,722 --> 00:00:33,025 (Vicheko) 11 00:00:34,355 --> 00:00:38,985 Kila siku, nafanya bidii kuwazidishia wanawake sauti 12 00:00:39,445 --> 00:00:42,925 na kuoneysha maisha yao na michango yao 13 00:00:42,925 --> 00:00:45,722 katika hatua za kutafuta usalama na kutatua migogoro, 14 00:00:47,652 --> 00:00:52,989 na kwa sababu ya kazi zangu, natambua kwamba njia ya pekee 15 00:00:53,259 --> 00:00:55,338 kwa kuhakikisha ushirikiano kamili 16 00:00:55,338 --> 00:00:58,928 wa wanawake duniani ni kuchukua tena dini mikononi mwetu. 17 00:00:59,398 --> 00:01:03,104 Sasa, jambo hilo ni muhimu sana kwangu. 18 00:01:03,164 --> 00:01:06,914 Kama muislamu na mwanamke kijana, ninaijali dini yangu sana. 19 00:01:07,974 --> 00:01:12,095 Inanipa nguvu na msimamo katika kazi zangu kila siku. 20 00:01:12,095 --> 00:01:15,435 Ndiyo sababu inayoniwezesha kusimama hapa leo mbele yenu. 21 00:01:15,965 --> 00:01:20,199 Lakini siwezi kutojali hasara kubwa zilizofanyika kwa kutumia jina la dini, 22 00:01:21,393 --> 00:01:24,843 si dini yangu tu, lakini dini zote kubwa za dunia. 23 00:01:25,243 --> 00:01:30,401 Kuyatumia vibaya na kuyageuza maandiko ya kidini 24 00:01:30,744 --> 00:01:34,034 kumebadilisha desturi zetu za kijamii na kitamaduni, 25 00:01:34,074 --> 00:01:36,570 sheria zetu, kila siku zetu, 26 00:01:36,570 --> 00:01:39,910 hadi kumefikia tusipoweza kupagundua. 27 00:01:39,910 --> 00:01:45,280 Wazazi wangu walihama Libya, Afrika ya Kaskazini kwenda Kanada 28 00:01:45,280 --> 00:01:47,340 mwanzoni mwa miaka 1980, 29 00:01:47,340 --> 00:01:50,994 na mimi niko katikati ya watoto 11. 30 00:01:51,251 --> 00:01:53,211 Ehee, 11. 31 00:01:53,721 --> 00:01:55,115 Lakini katika kukulia kwangu, 32 00:01:55,115 --> 00:01:59,635 niliwaona wazazi wangu, wote wacha Mungu na waumini wa Akhera, wakisali na 33 00:01:59,645 --> 00:02:01,925 kumshukuru kwa baraka zao, 34 00:02:01,975 --> 00:02:05,915 kama mimi, lakini zinginezo pia. (Vicheko) 35 00:02:07,015 --> 00:02:10,105 Walikuwa na huruma, wenye kuchekesha, na wenye subira, 36 00:02:10,105 --> 00:02:15,285 subira kubwa, aina inayofunzwa kwa kuwalea watoto 11. 37 00:02:16,021 --> 00:02:17,651 Pia walifanya haki. 38 00:02:18,421 --> 00:02:21,971 Sikuwahi kupaswa kuijua dini kwa mtazamo wa kitamaduni tu. 39 00:02:22,741 --> 00:02:25,071 Nilitendewa sawasawa na kaka zangu, na sisi sote 40 00:02:25,071 --> 00:02:27,441 tulikuwa tunatarijiwa kufanya sawasawa. 41 00:02:27,461 --> 00:02:31,987 Sikuwahi kuambiwa kwamba Mungu huhukumu tofauti kwa jinsia. 42 00:02:32,917 --> 00:02:39,759 Wazazi wangu walimwona Mungu kuwa Mwingi wa Rehema, Fadhila na rizki 43 00:02:39,779 --> 00:02:42,469 na mimi nilichukulia msimamo wao. 44 00:02:43,090 --> 00:02:46,380 Kwa uhakika, malezi yangu yalikuwa na faida zake. 45 00:02:46,870 --> 00:02:51,120 kuwa katikati ya watoto 11 ni kama Diplomasia 101. (Vicheko) 46 00:02:52,312 --> 00:02:55,272 Mpaka leo, watu huniuliza wapi nilipokwenda skule, 47 00:02:55,272 --> 00:02:57,648 kama, “Ulienda Skule ya Kennedy ya Serikali?" 48 00:02:57,648 --> 00:02:59,398 na mimi huwatazama na kuwambia, “Hapana, 49 00:02:59,417 --> 00:03:02,527 Nimeenda Skule ya Murabit ya Mambo ya Kimataifa.” 50 00:03:02,577 --> 00:03:07,691 Ni maalum sana. Ungeongea na Mamangu kwa kujipatia nafasi 51 00:03:08,081 --> 00:03:10,631 Lakini kwa bahati yenu, yupo leo. 52 00:03:11,971 --> 00:03:16,141 Lakini kuwa miongoni wa watoto 11, na kuwa na ndugu 10, 53 00:03:16,248 --> 00:03:19,678 kunafundisha mengi kama mifumo ya mamlaka na muungano. 54 00:03:20,148 --> 00:03:22,557 Kama kuzingatia lengo; useme haraka au 55 00:03:22,557 --> 00:03:25,877 usiseme sana, kwa sababu utadakiwa mazungumzo kila mara. 56 00:03:25,877 --> 00:03:28,317 Kunafundisha umuhimu wa kuwa mjumbe mzuri. 57 00:03:28,827 --> 00:03:32,767 Uyaulize maswali kwa mpango kwa kupata jibu unalolitaka, na 58 00:03:32,887 --> 00:03:36,047 ujue kusema 'la' kwa mpango pia kwa kufuliza usalama. 59 00:03:37,213 --> 00:03:40,694 Lakini funzo muhimu sana nililolipata kutoka utoto wangu 60 00:03:40,694 --> 00:03:44,494 lilikuwa umuhimu wa kuwa na nafasi kwenye meza. 61 00:03:44,744 --> 00:03:48,135 Taa yake ndogo mamangu ilipovunjika, alivyoipenda sana, ilinilazimu niwepo 62 00:03:48,135 --> 00:03:52,655 wakati alipochunguza ilikuwaje, ili nijitetee, 63 00:03:53,965 --> 00:03:57,175 kwa sababu kama hupo, lawama inakuangukia kwako, 64 00:03:57,175 --> 00:03:59,761 na kabla hujagundua, utakuwa umeadhibiwa. 65 00:03:59,791 --> 00:04:02,731 Kwa uhahika, sijapewa adhabu mimi mwenyewe. 66 00:04:04,278 --> 00:04:09,040 Nilipokuwa na miaka 15 mwakani 2005, nikatimiza skule ya sekondari nikahamia 67 00:04:09,060 --> 00:04:11,490 Kanada-- Saskatoon -- 68 00:04:11,550 --> 00:04:15,900 Ila Zawiya, Libya, mji wa nyumbani wa wazazi wangu, 69 00:04:16,010 --> 00:04:18,099 mji wa kidesturi sana. 70 00:04:18,099 --> 00:04:23,049 Fikiri, muda huo niliwahi kufika Libya kwa ajili ya matembezi tu, 71 00:04:23,309 --> 00:04:27,719 na kama msichana wa miaka 7, ilipendeza sana. 72 00:04:27,779 --> 00:04:32,331 Ilikuwa aiskrimu na pwani na jamaa wenye furaha. 73 00:04:33,740 --> 00:04:37,790 niligundua haiko vilevile kama msichana wa miaka 15. 74 00:04:38,248 --> 00:04:44,238 Nikakutana upesi na mambo ya dini ya kiutamaduni. 75 00:04:44,676 --> 00:04:48,946 Maneno ya "haramu" -- lenye maana ya kukatazwa kidini -- 76 00:04:48,972 --> 00:04:52,432 na "aibu" -- lenye maana ya kutofaa kimaadili -- 77 00:04:52,468 --> 00:04:54,518 yalibadilishanwa bila mpango. 78 00:04:55,228 --> 00:04:58,838 kama yalikuwa na maana moja na adhabu moja vilevile. 79 00:04:59,618 --> 00:05:04,238 Nikajikuta sana katika mazungumzo na wenzangu wa skule 80 00:05:04,238 --> 00:05:07,584 na wa kazi, profesa, rafiki zangu na hata jamaa zangu, 81 00:05:07,594 --> 00:05:11,644 nikaanza kujiuliza kuhusu desturi zangu na malengo yangu. 82 00:05:12,304 --> 00:05:16,164 Na hata na msingi mzuri niliopokea kutoka wazazi wangu, 83 00:05:16,200 --> 00:05:19,850 Nilijikuta nikajiuliza kuhusu nafasi ya mwanamke katika dini yangu. 84 00:05:21,710 --> 00:05:24,413 Kule kwenye Skule ya Murabit ya Mambo ya Kimataifa, 85 00:05:24,437 --> 00:05:27,307 tunapenda sana kufanya mjadala, 86 00:05:27,307 --> 00:05:32,637 na sheria ya kwanza ni fanya utafiti wako, na hivyo ndivyo nilivyofanya mimi, 87 00:05:32,647 --> 00:05:36,247 Ikanishangaza sana vipi ilikuwa rahisi 88 00:05:36,247 --> 00:05:40,275 kuwagundua wanawake katika Uislamu waliokuwa viongozi, 89 00:05:40,275 --> 00:05:43,765 wavumbuzi, wenye nguvu -- 90 00:05:43,765 --> 00:05:46,774 za kisiasa, za kiuchumi hata za kijeshi. 91 00:05:47,014 --> 00:05:50,777 Khadija aliziendesha fedha za harakati za Kiislamu 92 00:05:50,787 --> 00:05:52,657 katika siku zake za mwanzo. 93 00:05:52,657 --> 00:05:54,997 Tusingekuwepo hapa leo bila michango yake. 94 00:05:55,924 --> 00:05:58,124 Kwa nini tusifundishwe kisa chake? 95 00:05:58,144 --> 00:06:01,234 Kwa nini tusifundishwe visa vya hao wanawake? 96 00:06:01,254 --> 00:06:03,624 Kwa nini wanawake wapewe vyeo vilivyotoka 97 00:06:03,626 --> 00:06:06,636 zama zilizotangulia mafunzo ya dini yetu? 98 00:06:06,636 --> 00:06:09,286 Na kwa nini, kama sisi sote tuko sawasawa machoni mwa Mungu, 99 00:06:09,296 --> 00:06:11,966 hatuko sawasawa machoni mwa binadamu? 100 00:06:12,693 --> 00:06:17,043 Hayo yalinipeleka kufikiria mafunzo yangu ya utotoni. 101 00:06:18,232 --> 00:06:22,052 Anayeamua, na kuwa na mamlaka juu ya ujumbe, 102 00:06:22,082 --> 00:06:24,702 anayo nafasi kwenye meza, 103 00:06:24,722 --> 00:06:29,484 na kwa bahati mbaya, katika dini zote za kidunia, 104 00:06:29,494 --> 00:06:31,092 hao si wanawake. 105 00:06:32,462 --> 00:06:35,212 Taasisi za kidini zinatawaliwa na wanaume 106 00:06:35,242 --> 00:06:37,222 na kuendeshwa na viongozi vya kiume, 107 00:06:37,242 --> 00:06:40,542 na wanabuni sera zinazowafaa wanaume tu, 108 00:06:40,623 --> 00:06:45,339 na ila tunaweza kubadilisha mfumo huo kabisa, kwa kweli hatuwezi 109 00:06:45,339 --> 00:06:47,759 kutarajia wanawake kushiriki kwa ukamilifu 110 00:06:47,759 --> 00:06:50,089 katika uchumi au siasa. 111 00:06:51,576 --> 00:06:53,876 Msingi wetu umevunjika. 112 00:06:55,636 --> 00:06:59,816 Mamangu husema, "huwezi kujenga nyumba nzima juu ya msingi mbovu". 113 00:07:02,976 --> 00:07:08,988 Mwakani 2011, Mapinduzi ya Libya yaliripuka na aila yangu walikuwepo mistari ya mbele. 114 00:07:09,554 --> 00:07:12,854 Kuna jambo moja la kushangaza linalojitokeza katika vita, 115 00:07:12,903 --> 00:07:15,473 kama mageuzo ya kiutamaduni, kwa muda mfupi tu. 116 00:07:16,133 --> 00:07:18,743 Kwa mara ya kwanza nilijisikia ilikubaliwa, au hata 117 00:07:18,743 --> 00:07:21,651 ilisisitizwa kwa mimi kujihusisha na mambo. 118 00:07:21,651 --> 00:07:23,591 Ilihitajika. 119 00:07:24,510 --> 00:07:27,340 Mimi na wanawake wengine walipewa nafasi kwenye meza. 120 00:07:27,350 --> 00:07:30,570 Hatukuwa wasaidizi wa wanaume tu. 121 00:07:30,580 --> 00:07:32,427 Tulichangia katika uamuzi. 122 00:07:32,427 --> 00:07:35,547 Tulichangia katika kutoa taarifa. Tulikuwa muhimu sana. 123 00:07:35,880 --> 00:07:39,640 Na mimi nilitaka, nilihitaji mageuzo hayo kutoondoka. 124 00:07:42,550 --> 00:07:45,368 Lakini niligundua si rahisi kuwa nilivyotaka. 125 00:07:45,368 --> 00:07:49,170 Ilichukua wiki chache tu kabla hao wanawake niliowafanya nao kazi 126 00:07:49,170 --> 00:07:51,720 walikuwa wanarejea katika kazi zao za zamani, 127 00:07:52,130 --> 00:07:56,437 na wengi walipewa maneno ya kusisitizwa 128 00:07:56,437 --> 00:07:58,891 kutoka kwa viongozi wa kidini na vya kisiasa, wengi wao 129 00:07:58,891 --> 00:08:02,151 walijaribu kuthibitisha hoja zao kwa maandishi ya kidini. 130 00:08:02,151 --> 00:08:05,631 Ndivyo walivyojipatia mikono ya watu katika hoja zao. 131 00:08:06,951 --> 00:08:12,141 Mwanzoni, nilizingatia kuwapa wanawake nguvu katika siasa na uchumi. 132 00:08:12,141 --> 00:08:15,437 Nikafikiri ingeliongoza mabadiliko ya kiutamaduni na kijamii. 133 00:08:15,765 --> 00:08:19,565 Niligundua, ilifanikiwa kidogo tu, lakini sio sana. 134 00:08:20,325 --> 00:08:24,205 Nikaamua kuitumia njia yao wale viongozi wa kidini 135 00:08:24,480 --> 00:08:28,260 nikaanza kuthibitisha hoja zangu kwa maandishi ya kiislamu pia. 136 00:08:29,320 --> 00:08:33,221 Katika miaka 2012 na 2013, shirika langu liliongoza kampeni ya pekee iliyokuwa 137 00:08:33,221 --> 00:08:36,231 kubwa na pana kuliko zote Libya. 138 00:08:36,881 --> 00:08:40,371 Tulipenyeza nyumbani, skuleni na vyuoni, hata misikitni. 139 00:08:41,101 --> 00:08:44,301 Tulizungumza na watu 50,000 uso kwa uso, na mamia ya maelfu zaidi 140 00:08:44,731 --> 00:08:46,613 kwa njia za matangazo ya kubandika, 141 00:08:46,613 --> 00:08:49,163 matangazo kwenye tv na kwenye radio. 142 00:08:50,803 --> 00:08:53,173 Labda mnajiuliza, shirika la haki za wanawake 143 00:08:53,210 --> 00:08:56,646 waliweza kufanya hivyo vipi katika jamii ilyopingana na sisi 144 00:08:56,646 --> 00:08:58,196 kabisa mwanzoni. 145 00:08:59,436 --> 00:09:01,556 Niliyatumia maandishi ya kiislamu. 146 00:09:02,070 --> 00:09:05,870 Nilitumia aya za Korani na misemo ya Mtume Mohammed, 147 00:09:06,810 --> 00:09:11,340 Hadithi zake, misemo yake ambayo ni, kwa mfano, 148 00:09:11,780 --> 00:09:14,865 "Mtu bora ndiye anayefanya wema kwa familia yake." 149 00:09:14,875 --> 00:09:18,008 "Usimruhusu mtu kumdhulumu mwingine." 150 00:09:19,148 --> 00:09:24,068 Kwa mara ya kwanza, hotuba za Ijumaa kutoka kwa imamu wa kienyeji 151 00:09:24,128 --> 00:09:26,338 zilitangaza haki za wanawake. 152 00:09:26,338 --> 00:09:29,506 zilizungumzia masuala yasiyo kawaida, kama vurugu ya nyumbani. 153 00:09:31,016 --> 00:09:33,336 Sera zilibadilishwa. 154 00:09:34,305 --> 00:09:39,295 Katika jamii fulani, ilitubidi kusema lile Azimio 155 00:09:39,295 --> 00:09:42,445 la Kimataifa la Haki ya Wanadamu mlilopingana nayo 156 00:09:42,445 --> 00:09:45,082 kwa sababu haikuandikwi na watalaamu wa kidini, 157 00:09:45,082 --> 00:09:49,212 eti, misingi yote ile imo kitabu chetu. 158 00:09:49,975 --> 00:09:53,005 Yaani, Shirika la Umoja wa Mataifa lilituiga tu. 159 00:09:56,365 --> 00:09:58,936 Kwa kuubadilisha ujumbe wenyewe, tuliweza kuitoa 160 00:09:59,026 --> 00:10:02,566 sura mpya iliyotangaza haki za wanawake Libya. 161 00:10:03,414 --> 00:10:06,454 Ni jambo ambalo sasa limeigwa duniani, 162 00:10:08,554 --> 00:10:12,439 na sisemi ni rahisi--- niamini, si rahisi kabisa. 163 00:10:12,759 --> 00:10:16,560 'Liberals' watasema unaitumia dini na kukuita 'conservative' mbaya. 164 00:10:16,560 --> 00:10:19,500 na 'conservatives' watakupa matusi mengi. 165 00:10:19,994 --> 00:10:23,990 Mimi mwenyewe nimeyapata mengi, kama "Wazazi wako hawaaibiki na wewe?" -- 166 00:10:23,990 --> 00:10:26,151 sio kweli; wao wananipenda kuliko wote -- 167 00:10:26,151 --> 00:10:28,801 au "Hutoishi kuona siku yako ya kuzaliwa tena" -- 168 00:10:28,801 --> 00:10:31,031 tena sio kweli, nimeshaiona. 169 00:10:32,931 --> 00:10:36,570 Na bado, ninaamini kabisa 170 00:10:36,570 --> 00:10:40,380 kwamba haki za wanawake na dini zinaweza kuendana. 171 00:10:42,461 --> 00:10:45,561 Lakini lazima tupewe nafasi kwenye meza. 172 00:10:45,916 --> 00:10:48,606 Tusiache kupigania nafasi yetu, kwa sababu 173 00:10:48,606 --> 00:10:55,316 kwa kukaa kimya, tunaruhusu mateso na dhuluma za wanawake duniani kuendelea. 174 00:10:56,467 --> 00:10:59,007 Kwa kudai tutapigania haki za wanawake 175 00:10:59,017 --> 00:11:02,167 na kupigania ugaidi kwa kutumia mabomu na vita, 176 00:11:02,907 --> 00:11:06,947 tunaharibu jamii za kienyeji zinazohitaji kuyashughulikia masuala hayo 177 00:11:07,556 --> 00:11:10,866 ili yawezekane kuendelea. 178 00:11:11,806 --> 00:11:15,820 Sio rahisi, kushindana na taarifa za dini za kupotosha. 179 00:11:17,030 --> 00:11:21,630 Utapata vyako vya matusi na dhihaka na vitisho. 180 00:11:21,730 --> 00:11:24,126 Lakini ni lazima ifanyike. 181 00:11:24,136 --> 00:11:29,434 Hatuna budi ila kuuchukua tena ujumbe wa haki za binadamu, 182 00:11:29,434 --> 00:11:32,904 maadili ya dini yetu, si kwa ajili yetu, 183 00:11:32,904 --> 00:11:34,591 na si kwa ajili ya wanawake wenu tu, 184 00:11:34,591 --> 00:11:36,061 si kwa ajili ya wanawake humu leo, 185 00:11:36,121 --> 00:11:38,741 hata si kwa ajili ya wanawake kule nje, 186 00:11:40,101 --> 00:11:43,434 bali kwa ajili ya jamii ambazo zingebadilika kuwa nzuri 187 00:11:43,434 --> 00:11:45,849 kwa mashirikiano ya wanawake. 188 00:11:46,489 --> 00:11:48,649 Na jinsi ya pekee sisi tunavyoweza kufanya hivyo, 189 00:11:48,649 --> 00:11:50,389 njia yetu moja tu, 190 00:11:50,469 --> 00:11:53,499 ni kupata nafasi na kukaa daima, kwenye meza. 191 00:11:53,649 --> 00:11:54,799 Asante. 192 00:11:54,799 --> 00:11:58,259 (Makofi)