Njiani kufika hapa,
nilikuwa na mazungumzo mazuri na
mtu aliyekuwa anakaa pembeni yangu kwenye
ndege. Alinambia
"Hamna kazi tena USA,
yaani sasa wamebuni kazi mpya:
mwanasaikolojia wa paka,
mzungumzaji wa mbwa,msasi wa kimbunga."
Punde, aliniuliza,
"Kwani wewe unafanya kazi gani?"
Nikamjibu, "Mjenzi wa usalama?"
(Vicheko)
Kila siku, nafanya bidii
kuwazidishia wanawake sauti
na kuoneysha maisha yao na michango yao
katika hatua za kutafuta usalama
na kutatua migogoro,
na kwa sababu ya kazi zangu,
natambua kwamba njia ya pekee
kwa kuhakikisha ushirikiano kamili
wa wanawake duniani
ni kuchukua tena dini mikononi mwetu.
Sasa, jambo hilo ni muhimu sana kwangu.
Kama muislamu na mwanamke kijana,
ninaijali dini yangu sana.
Inanipa nguvu na msimamo katika
kazi zangu kila siku.
Ndiyo sababu inayoniwezesha
kusimama hapa leo mbele yenu.
Lakini siwezi kutojali hasara kubwa
zilizofanyika kwa kutumia jina la dini,
si dini yangu tu, lakini
dini zote kubwa za dunia.
Kuyatumia vibaya na
kuyageuza maandiko ya kidini
kumebadilisha desturi zetu
za kijamii na kitamaduni,
sheria zetu, kila siku zetu,
hadi kumefikia tusipoweza
kupagundua.
Wazazi wangu walihama Libya,
Afrika ya Kaskazini kwenda Kanada
mwanzoni mwa miaka 1980,
na mimi niko katikati ya watoto 11.
Ehee, 11.
Lakini katika kukulia kwangu,
niliwaona wazazi wangu, wote wacha Mungu
na waumini wa Akhera, wakisali na
kumshukuru kwa baraka zao,
kama mimi, lakini zinginezo pia.
(Vicheko)
Walikuwa na huruma, wenye kuchekesha,
na wenye subira,
subira kubwa, aina inayofunzwa
kwa kuwalea watoto 11.
Pia walifanya haki.
Sikuwahi kupaswa kuijua dini kwa
mtazamo wa kitamaduni tu.
Nilitendewa sawasawa na kaka zangu,
na sisi sote
tulikuwa tunatarijiwa
kufanya sawasawa.
Sikuwahi kuambiwa kwamba Mungu
huhukumu tofauti kwa jinsia.
Wazazi wangu walimwona Mungu kuwa
Mwingi wa Rehema, Fadhila na rizki
na mimi nilichukulia
msimamo wao.
Kwa uhakika, malezi yangu yalikuwa
na faida zake.
kuwa katikati ya watoto 11
ni kama Diplomasia 101. (Vicheko)
Mpaka leo, watu huniuliza wapi
nilipokwenda skule,
kama, “Ulienda Skule ya
Kennedy ya Serikali?"
na mimi huwatazama na
kuwambia, “Hapana,
Nimeenda Skule ya Murabit ya
Mambo ya Kimataifa.”
Ni maalum sana. Ungeongea na
Mamangu kwa kujipatia nafasi
Lakini kwa bahati yenu, yupo leo.
Lakini kuwa miongoni wa watoto 11,
na kuwa na ndugu 10,
kunafundisha mengi kama
mifumo ya mamlaka na muungano.
Kama kuzingatia lengo;
useme haraka au
usiseme sana, kwa sababu
utadakiwa mazungumzo kila mara.
Kunafundisha umuhimu wa kuwa
mjumbe mzuri.
Uyaulize maswali kwa mpango kwa
kupata jibu unalolitaka, na
ujue kusema 'la' kwa mpango pia
kwa kufuliza usalama.
Lakini funzo muhimu sana
nililolipata kutoka utoto wangu
lilikuwa umuhimu wa kuwa na nafasi kwenye
meza.
Taa yake ndogo mamangu ilipovunjika,
alivyoipenda sana, ilinilazimu niwepo
wakati alipochunguza ilikuwaje,
ili nijitetee,
kwa sababu kama hupo,
lawama inakuangukia kwako,
na kabla hujagundua, utakuwa umeadhibiwa.
Kwa uhahika, sijapewa
adhabu mimi mwenyewe.
Nilipokuwa na miaka 15 mwakani 2005,
nikatimiza skule ya sekondari nikahamia
Kanada-- Saskatoon --
Ila Zawiya, Libya,
mji wa nyumbani wa wazazi wangu,
mji wa kidesturi sana.
Fikiri, muda huo niliwahi kufika
Libya kwa ajili ya matembezi tu,
na kama msichana wa miaka 7,
ilipendeza sana.
Ilikuwa aiskrimu na pwani na jamaa
wenye furaha.
niligundua haiko vilevile kama
msichana wa miaka 15.
Nikakutana upesi na mambo ya dini ya
kiutamaduni.
Maneno ya "haramu" --
lenye maana ya kukatazwa kidini --
na "aibu" -- lenye maana ya kutofaa
kimaadili --
yalibadilishanwa bila mpango.
kama yalikuwa na maana moja na
adhabu moja vilevile.
Nikajikuta sana katika mazungumzo na
wenzangu wa skule
na wa kazi, profesa, rafiki zangu na hata
jamaa zangu,
nikaanza kujiuliza kuhusu desturi zangu
na malengo yangu.
Na hata na msingi mzuri niliopokea
kutoka wazazi wangu,
Nilijikuta nikajiuliza kuhusu nafasi
ya mwanamke katika dini yangu.
Kule kwenye Skule ya Murabit ya Mambo
ya Kimataifa,
tunapenda sana kufanya mjadala,
na sheria ya kwanza ni fanya utafiti wako,
na hivyo ndivyo nilivyofanya mimi,
Ikanishangaza sana vipi ilikuwa rahisi
kuwagundua wanawake katika Uislamu
waliokuwa viongozi,
wavumbuzi, wenye nguvu --
za kisiasa, za kiuchumi hata za kijeshi.
Khadija aliziendesha fedha za
harakati za Kiislamu
katika siku zake za mwanzo.
Tusingekuwepo hapa leo bila michango yake.
Kwa nini tusifundishwe kisa chake?
Kwa nini tusifundishwe
visa vya hao wanawake?
Kwa nini wanawake wapewe vyeo
vilivyotoka
zama zilizotangulia mafunzo ya dini yetu?
Na kwa nini, kama sisi sote tuko sawasawa
machoni mwa Mungu,
hatuko sawasawa machoni mwa binadamu?
Hayo yalinipeleka kufikiria mafunzo
yangu ya utotoni.
Anayeamua, na kuwa na mamlaka
juu ya ujumbe,
anayo nafasi kwenye meza,
na kwa bahati mbaya, katika dini zote
za kidunia,
hao si wanawake.
Taasisi za kidini
zinatawaliwa na wanaume
na kuendeshwa na viongozi vya kiume,
na wanabuni sera zinazowafaa wanaume tu,
na ila tunaweza kubadilisha mfumo huo
kabisa, kwa kweli hatuwezi
kutarajia wanawake kushiriki
kwa ukamilifu
katika uchumi au siasa.
Msingi wetu umevunjika.
Mamangu husema, "huwezi kujenga nyumba
nzima juu ya msingi mbovu".
Mwakani 2011, Mapinduzi ya Libya yaliripuka
na aila yangu walikuwepo mistari ya mbele.
Kuna jambo moja la kushangaza
linalojitokeza katika vita,
kama mageuzo ya kiutamaduni,
kwa muda mfupi tu.
Kwa mara ya kwanza nilijisikia
ilikubaliwa, au hata
ilisisitizwa kwa mimi kujihusisha
na mambo.
Ilihitajika.
Mimi na wanawake wengine walipewa nafasi
kwenye meza.
Hatukuwa wasaidizi wa wanaume tu.
Tulichangia katika uamuzi.
Tulichangia katika kutoa taarifa.
Tulikuwa muhimu sana.
Na mimi nilitaka, nilihitaji mageuzo hayo
kutoondoka.
Lakini niligundua si rahisi
kuwa nilivyotaka.
Ilichukua wiki chache tu kabla hao
wanawake niliowafanya nao kazi
walikuwa wanarejea katika kazi zao za
zamani,
na wengi walipewa maneno ya
kusisitizwa
kutoka kwa viongozi wa kidini na
vya kisiasa, wengi wao
walijaribu kuthibitisha hoja
zao kwa maandishi ya kidini.
Ndivyo walivyojipatia mikono ya
watu katika hoja zao.
Mwanzoni, nilizingatia kuwapa
wanawake nguvu katika siasa na uchumi.
Nikafikiri ingeliongoza
mabadiliko ya kiutamaduni na kijamii.
Niligundua, ilifanikiwa kidogo tu, lakini
sio sana.
Nikaamua kuitumia njia yao wale
viongozi wa kidini
nikaanza kuthibitisha hoja zangu kwa
maandishi ya kiislamu pia.
Katika miaka 2012 na 2013, shirika langu
liliongoza kampeni ya pekee iliyokuwa
kubwa na pana kuliko zote Libya.
Tulipenyeza nyumbani, skuleni na
vyuoni, hata misikitni.
Tulizungumza na watu 50,000
uso kwa uso, na mamia ya maelfu zaidi
kwa njia za
matangazo ya kubandika,
matangazo kwenye tv na kwenye radio.
Labda mnajiuliza, shirika la
haki za wanawake
waliweza kufanya hivyo vipi katika jamii
ilyopingana na sisi
kabisa mwanzoni.
Niliyatumia maandishi ya kiislamu.
Nilitumia aya za Korani na misemo ya
Mtume Mohammed,
Hadithi zake, misemo yake ambayo ni,
kwa mfano,
"Mtu bora ndiye anayefanya
wema kwa familia yake."
"Usimruhusu mtu kumdhulumu mwingine."
Kwa mara ya kwanza, hotuba za Ijumaa
kutoka kwa imamu wa kienyeji
zilitangaza haki za wanawake.
zilizungumzia masuala yasiyo kawaida, kama
vurugu ya nyumbani.
Sera zilibadilishwa.
Katika jamii fulani, ilitubidi
kusema lile Azimio
la Kimataifa la Haki ya Wanadamu
mlilopingana nayo
kwa sababu haikuandikwi na watalaamu
wa kidini,
eti, misingi yote ile imo kitabu chetu.
Yaani, Shirika la Umoja wa Mataifa
lilituiga tu.
Kwa kuubadilisha ujumbe wenyewe,
tuliweza kuitoa
sura mpya iliyotangaza haki za wanawake
Libya.
Ni jambo ambalo sasa limeigwa duniani,
na sisemi ni rahisi--- niamini,
si rahisi kabisa.
'Liberals' watasema unaitumia dini
na kukuita 'conservative' mbaya.
na 'conservatives' watakupa
matusi mengi.
Mimi mwenyewe nimeyapata mengi, kama
"Wazazi wako hawaaibiki na wewe?" --
sio kweli;
wao wananipenda kuliko wote --
au "Hutoishi kuona siku
yako ya kuzaliwa tena" --
tena sio kweli, nimeshaiona.
Na bado, ninaamini kabisa
kwamba haki za wanawake
na dini zinaweza kuendana.
Lakini lazima tupewe nafasi kwenye meza.
Tusiache kupigania
nafasi yetu, kwa sababu
kwa kukaa kimya, tunaruhusu mateso na
dhuluma za wanawake duniani kuendelea.
Kwa kudai tutapigania haki za wanawake
na kupigania ugaidi kwa kutumia
mabomu na vita,
tunaharibu jamii za kienyeji zinazohitaji
kuyashughulikia masuala hayo
ili yawezekane kuendelea.
Sio rahisi, kushindana na taarifa za dini
za kupotosha.
Utapata vyako vya matusi na dhihaka na
vitisho.
Lakini ni lazima ifanyike.
Hatuna budi ila kuuchukua tena
ujumbe wa haki za binadamu,
maadili ya dini yetu, si kwa ajili yetu,
na si kwa ajili ya
wanawake wenu tu,
si kwa ajili ya
wanawake humu leo,
hata si kwa ajili ya
wanawake kule nje,
bali kwa ajili ya jamii ambazo
zingebadilika kuwa nzuri
kwa mashirikiano ya wanawake.
Na jinsi ya pekee sisi tunavyoweza
kufanya hivyo,
njia yetu moja tu,
ni kupata nafasi na kukaa daima,
kwenye meza.
Asante.
(Makofi)