WEBVTT 00:00:00.681 --> 00:00:03.969 Leo niko hapa kuongea kuhusu swala nyeti, 00:00:03.969 --> 00:00:07.667 ambalo lina jibu tatanishi. 00:00:07.667 --> 00:00:11.269 Swala langu ni zile siri za ugomvi nyumbani, 00:00:11.269 --> 00:00:13.603 na swali nitakalokabiliana nalo 00:00:13.603 --> 00:00:17.684 ni lile swali moja kila mmoja huliuliza kila mara: 00:00:17.684 --> 00:00:19.296 Kwa nini muathirika hubakia? 00:00:19.296 --> 00:00:23.292 Kwa nini mtu yeyote abaki na mume ampigaye? 00:00:23.292 --> 00:00:26.269 Mie si daktari wa akili, mfanyakazi wa ustawi wa jamii 00:00:26.269 --> 00:00:28.604 au mtaalam wa ugomvi wa nyumbani. 00:00:28.604 --> 00:00:31.803 Mimi ni mwanamke mwenye hadithi ya kusimulia. NOTE Paragraph 00:00:31.803 --> 00:00:36.316 Nilikuwa na umri wa miaka ishirini na miwili. Nilikuwa nimehitimu tu kutoka chuo cha Harvard. 00:00:36.316 --> 00:00:38.788 Nilikuwa nimehamia mjini New York kwa ajili ya kazi yangu ya kwanza 00:00:38.788 --> 00:00:42.084 kama mwandishi na mhariri wa gazeti la Seventeen. 00:00:42.084 --> 00:00:44.324 Nilikuwa na nyumba yangu ya kwanza, 00:00:44.324 --> 00:00:47.524 kadi yangu ya kwanza ya American Express, 00:00:47.524 --> 00:00:50.552 na nilikuwa na siri moja kubwa sana. 00:00:50.552 --> 00:00:54.251 Siri yangu ilikuwa kwamba kulikuwa na bunduki 00:00:54.251 --> 00:00:57.689 iliyojaa risasi iliyoelekezwa kichwani mwangu 00:00:57.689 --> 00:01:00.252 na mwanamme niliyefikiria alikuwa mpenzi wangu, 00:01:00.252 --> 00:01:03.737 mara kadhaa. 00:01:03.737 --> 00:01:07.297 Mwanamme huyu niliyempenda kuliko yeyote duniani 00:01:07.297 --> 00:01:11.376 alielekeza bunduki kichwani mwangu na kutishia kuniua 00:01:11.376 --> 00:01:14.561 mara nyingi kuliko zile ningeweza kukumbuka. 00:01:14.561 --> 00:01:17.304 Niko hapa kuwapa hadithi ya upendo wa kupindukia, 00:01:17.304 --> 00:01:20.488 mtego wa kisaikolojia uliofichwa kama mapenzi, 00:01:20.488 --> 00:01:23.340 ambao mamilioni ya wanawake na hata wanaume wengine 00:01:23.340 --> 00:01:25.721 hutumbukia kila mwaka. 00:01:25.721 --> 00:01:28.470 Inaweza hata kuwa hadithi yako. NOTE Paragraph 00:01:28.470 --> 00:01:31.513 Sionekani kama mtu niliyenusurika na ugomvi katika mahusiano. 00:01:31.513 --> 00:01:33.819 Nina shahada ya sanaa katika Kiigereza kutoka chuo cha Harvard, 00:01:33.819 --> 00:01:36.181 na shahada ya juu katika mauzo kutoka kwa chuo cha biashara cha Wharton. 00:01:36.181 --> 00:01:39.473 Nimetumia muda mrefu maishani nikifanya kazi kwenye kampuni bora duniani 00:01:39.473 --> 00:01:43.745 zikiwemo Johnson & Johnson, Leo Burnett na The Washington Post. 00:01:43.745 --> 00:01:47.541 Nimeolewa takriban miaka ishirini kwa mme wangu wa pili 00:01:47.541 --> 00:01:50.330 na tuna wana watatu pamoja 00:01:50.330 --> 00:01:54.559 Mbwa wangu ni mweusi, na mie huendesha gari ndogo la Honda Odyssey. 00:01:54.559 --> 00:01:57.039 (Kicheko) NOTE Paragraph 00:01:57.039 --> 00:01:59.758 Kwa hivyo ujumbe wangu wa kwanza kwenu ni kwamba ugomvi wa nyumbani 00:01:59.758 --> 00:02:02.126 humtokea yeyote-- 00:02:02.126 --> 00:02:06.302 kila jamii,dini, kila kipato na ngazi ya kimasomo. 00:02:06.302 --> 00:02:08.241 Iko kila mahali. 00:02:08.241 --> 00:02:10.761 Na ujumbe wangu wa pili ni kwamba kila mtu hufikiri 00:02:10.761 --> 00:02:12.879 ugomvi wa nyumbani huwaathiri wanawake, 00:02:12.879 --> 00:02:15.147 ati ni swala la wanawake. 00:02:15.147 --> 00:02:17.366 Si sahihi. 00:02:17.366 --> 00:02:21.478 Zaidi ya asili mia 85 ya wanyanyasaji ni wanaume, na ugomvi wa nyumbani 00:02:21.478 --> 00:02:27.396 hutokea haswa katika mahusiano ya undani, ya kutegemeana na yale ya muda mrefu, 00:02:27.396 --> 00:02:29.565 yaani, katika familia, 00:02:29.565 --> 00:02:33.430 mahali tusipotaka au kutarajia kupata ugomvi, 00:02:33.430 --> 00:02:37.708 ndio sababu tuhuma za kinyumbani ni tatanishi hivi. NOTE Paragraph 00:02:37.708 --> 00:02:41.259 Ningekuambia kwamba ningekuwa mtu wa mwisho duniani 00:02:41.259 --> 00:02:43.831 kukaa na mwanaume anayenipiga, 00:02:43.831 --> 00:02:47.238 lakini kusema kweli nilikuwa mwathirika kwa sababu ya umri wangu. 00:02:47.238 --> 00:02:50.523 Nilikuwa mwenye umri wa miaka ishirini na mbili na Marekani, 00:02:50.523 --> 00:02:54.372 wanawake wenye umri kati ya miaka kumi na sita hadi ishirini na nne wana uwezekano wa mara tatu zaidi 00:02:54.372 --> 00:02:57.133 kuwa waathirika wa ugomvi wa nyumbani 00:02:57.133 --> 00:02:59.948 ikilinganishwa na wanawake wa umri mwingine, 00:02:59.948 --> 00:03:03.251 vilevile zaidi ya wanawake mia tano na wasichana wa umri huu 00:03:03.251 --> 00:03:06.822 huuawa kila mwaka na wapenzi wanyanyasaji, 00:03:06.822 --> 00:03:11.455 wapenzi, na waume zao Marekani. NOTE Paragraph 00:03:11.455 --> 00:03:14.515 Nilikuwa muathirika kwa sababu sikujua chochote 00:03:14.515 --> 00:03:19.100 kuhusu ugomvi wa nyumbani, maonyo yake ama mifano yake. NOTE Paragraph 00:03:19.100 --> 00:03:24.165 Nilikutana na Conor usiku mmoja wenye baridi na mvua, mwezi wa Januari. 00:03:24.165 --> 00:03:27.128 Alikaa kando yangu kwenye treni katika mji wa New York, 00:03:27.128 --> 00:03:29.267 na alianza kuniongelesha. 00:03:29.267 --> 00:03:31.135 Aliniambia mambo mawili. 00:03:31.135 --> 00:03:34.937 La kwanza kuwa, yeye pia, alikuwa amehitimu kutoka kwa kati ya zile shule bora zaidi Marekani, 00:03:34.937 --> 00:03:39.292 na kwamba alifanya kazi kwenye benki moja ya kuvutia sana huko Wall Street. 00:03:39.292 --> 00:03:42.952 Lakini kile kilichonivutia zaidi siku hiyo 00:03:42.952 --> 00:03:46.240 ni kuwa alikuwa mwerevu na mcheshi 00:03:46.240 --> 00:03:47.640 na alionekana kuwa kijana wa mashambani. 00:03:47.640 --> 00:03:49.987 Alikuwa na haya mashavu makubwa, haya mashavu makubwa ya waridi 00:03:49.987 --> 00:03:51.672 na hii nywele za rangi kama ya ngano, 00:03:51.672 --> 00:03:54.959 na alionekana kuwa mwema sana. NOTE Paragraph 00:03:54.959 --> 00:03:58.743 Jambo moja la busara Conor alilofanya, kutoka mwanzoni, 00:03:58.743 --> 00:04:04.317 lilikuwa kufanya kana kwamba nilikuwa mwenye ushawishi mkubwa katika huo uhusiano. 00:04:04.317 --> 00:04:06.518 Alifanya hivi haswa hapo mwanzo 00:04:06.518 --> 00:04:09.384 kwa kunihusudu. 00:04:09.384 --> 00:04:12.670 Tukaanza kutoka pamoja, na alipenda kila kitu kunihusu, 00:04:12.670 --> 00:04:14.354 ati nilikuwa mwerevu, ati nilisomea chuo cha Harvard, 00:04:14.354 --> 00:04:17.384 ati nilikuwa mwenye shauku kusaidia wasichana wadogo, na kazi yangu. 00:04:17.384 --> 00:04:19.915 Alitaka kujua kila kitu kuhusu familia yangu 00:04:19.915 --> 00:04:22.531 na utoto wangu na matarajio na ndoto zangu. 00:04:22.531 --> 00:04:26.165 Conor alikuwa na imani nami, kama mwandishi na mwanamke, 00:04:26.165 --> 00:04:29.844 kwa njia ambayo yeyote mwengine alikuwa hajawahi. 00:04:29.844 --> 00:04:34.169 Na alileta uaminifu kati yetu 00:04:34.169 --> 00:04:36.689 kwa kunieleza siri yake, 00:04:36.689 --> 00:04:41.169 ambayo ilikuwa, alipokuwa mvulana mdogo sana akiwa na umri wa miaka minne 00:04:41.169 --> 00:04:44.080 alipigwa vibaya sana mara kwa mara 00:04:44.080 --> 00:04:45.766 na babake wa kambo, 00:04:45.766 --> 00:04:49.706 na unyanyasaji ulizidi kuwa mbaya zaidi hadi ikambidi aache shule akiwa daraja la nane, 00:04:49.706 --> 00:04:52.325 ingawa alikuwa mwerevu sana, 00:04:52.325 --> 00:04:55.581 na kwamba alitumia takriban miaka ishirini kujenga maisha yake upya. 00:04:55.581 --> 00:04:58.737 Ndiyo sababu hiyo shahada yake kutoka zile shule bora zaidi Marekani, 00:04:58.737 --> 00:05:01.550 na kazi yake Wall Street na maisha yake mazuri siku za usoni 00:05:01.550 --> 00:05:04.121 zilikuwa za umuhimu mkubwa sana kwake. 00:05:04.121 --> 00:05:06.265 Kama ungeniuliza 00:05:06.265 --> 00:05:11.629 kama huyu mwanamme mwerevu, mcheshi na mwenye kujali aliyenipenda sana 00:05:11.629 --> 00:05:16.012 angekuja kuniamulia kama ningejipamba au la, 00:05:16.012 --> 00:05:18.062 ufupi wa sketi zangu, 00:05:18.062 --> 00:05:19.992 mahali ningeishi, kazi gani ningefanya, 00:05:19.992 --> 00:05:23.356 marafiki zangu wangekuwa wepi na pale ningekulia Krisimasi 00:05:23.356 --> 00:05:25.304 ningekucheka, 00:05:25.304 --> 00:05:28.352 kwa sababu hakukuwa na ushahidi wowote wa tuhuma au uthibiti 00:05:28.352 --> 00:05:31.836 au hasira kutoka kwa Conor hapo mwanzoni. 00:05:31.836 --> 00:05:34.961 Sikujua kwamba daraja la kwanza 00:05:34.961 --> 00:05:37.336 katika uhusiano wowote wenye ugomvi 00:05:37.336 --> 00:05:40.988 ni kumvuta na kumpumbaza mwathirika NOTE Paragraph 00:05:40.988 --> 00:05:45.748 Pia sikujua kuwa daraja ya pili ni kumtenga mwathirika. 00:05:45.748 --> 00:05:49.902 Conor hakuja nyumbani siku moja na kutangaza, 00:05:49.902 --> 00:05:53.036 "Unajua huu uhusiano wetu kama wa Romeo na Julieti umekuwa mtamu, 00:05:53.036 --> 00:05:55.041 lakini nataka kwenda katika hatua inayofuata 00:05:55.041 --> 00:05:59.220 ambapo nitakutenga na kukunyanyasa" - (Kicheko) - 00:05:59.220 --> 00:06:00.575 "kwa hivyo nataka kukuhamisha kutoka nyumba hii 00:06:00.575 --> 00:06:02.216 ambapo majirani wanawezakusikia ukipiga mayowe 00:06:02.216 --> 00:06:04.689 na kukupeleka nje ya mji huu ambapo una marafiki na familia 00:06:04.689 --> 00:06:07.995 na wafanyakazi wenzako wanaoweza kuona hiyo michubuko." 00:06:07.995 --> 00:06:12.216 Badala yake, Conor alikuja nyumbani jioni ya Ijumaa moja 00:06:12.216 --> 00:06:14.947 na akaniambia kuwa alikuwa ameacha kazi siku hiyo, 00:06:14.947 --> 00:06:17.412 kazi ya ndoto zake, 00:06:17.412 --> 00:06:21.553 na akasema kwamba alikuwa ameacha kazi hiyo kwa sababu yangu, 00:06:21.553 --> 00:06:24.731 kwa sababu nilimfanya ahisi usalama na kupendwa 00:06:24.731 --> 00:06:27.854 ati hakuhitaji tena kujithibitisha huko Wall Street, 00:06:27.854 --> 00:06:30.369 na alitaka tu kutoka mjini 00:06:30.369 --> 00:06:33.347 na kukaa mbali na familia yake iliyomnyanyasa. 00:06:33.347 --> 00:06:36.469 na kuhamia mji mdogo wa New England 00:06:36.469 --> 00:06:40.042 ambapo angeweza kuanza upya maisha yake nikiwa kando yake. 00:06:40.042 --> 00:06:43.908 Sikutaka kamwe kuhama kutoka New York, 00:06:43.908 --> 00:06:47.515 na kuacha kazi ya ndoto zangu, 00:06:47.515 --> 00:06:50.098 lakini nilifikiria mtu hujitoa muhanga kwa mpenzi wake, 00:06:50.098 --> 00:06:53.562 kwa hivyo nikakubali na nikaacha kazi yangu, 00:06:53.562 --> 00:06:56.193 na Conor na mimi tukaondoka Manhattan pamoja. 00:06:56.193 --> 00:07:00.559 Sikuwai kufikiria kwamba penzi nililokuwa nalo halikuwa la kawaida, 00:07:00.559 --> 00:07:04.191 na kwamba nilikuwa nikitembea bila habari ndani ya 00:07:04.191 --> 00:07:09.171 mtego mzuri wa kimwili, kifedha na kiakili NOTE Paragraph 00:07:09.171 --> 00:07:11.491 Daraja ya pili katika ugomvi wa kimahusiano 00:07:11.491 --> 00:07:15.773 ni kuleta tishio la vurugu 00:07:15.773 --> 00:07:17.972 na kuangalia vile linavyomgusa. 00:07:17.972 --> 00:07:20.681 Na hapa ndipo bunduki zinapoingia. 00:07:20.681 --> 00:07:23.599 Muda tu tulipohamia New England--unajua, 00:07:23.599 --> 00:07:26.337 mahali Connor aliposema pangemfanya ajisikie salama-- 00:07:26.337 --> 00:07:28.753 alinunua bunduki tatu. 00:07:28.753 --> 00:07:32.193 Aliweka moja garini. 00:07:32.193 --> 00:07:34.849 Aliweka moja chini ya mto kitandani mwetu, 00:07:34.849 --> 00:07:38.011 na ya tatu alitembea nayo mfukoni nyakati zote. 00:07:38.011 --> 00:07:40.329 Na alisema alihitaji bunduki hizo 00:07:40.329 --> 00:07:43.125 kwa sababu ya uchungu aliopitia akiwa mchanga. 00:07:43.125 --> 00:07:45.609 Alizihitaji kujisikia salama. 00:07:45.609 --> 00:07:48.521 Lakini bunduki hizo zilikuwa ujumbe kwangu, 00:07:48.521 --> 00:07:51.215 na ingawa hakuwai kuninyoshea mkono, 00:07:51.215 --> 00:07:57.021 maisha yangu tayari yalikuwa hatarini kila dakika ya kila siku. NOTE Paragraph 00:07:57.021 --> 00:08:00.594 Kwanza Conor alinishambulia 00:08:00.594 --> 00:08:03.419 siku tano kabla ya harusi yetu. 00:08:03.419 --> 00:08:07.611 Ilikuwa saa moja asubuhi na bado nilikuwa nimevalia vazi la kulala 00:08:07.611 --> 00:08:11.851 Nilikuwa nafanya kazi kweny kompyuta yangu nikijaribu kumaliza kazi fulani ya uandishi, 00:08:11.851 --> 00:08:13.665 na nilikuwa nimekasirika, 00:08:13.665 --> 00:08:16.752 na Conor akatumia hasira zangu kama kisingizio 00:08:16.752 --> 00:08:19.903 kunikaba koo 00:08:19.903 --> 00:08:23.723 na kuikaza hadi sikuweza kupumua au kupiga kelele, 00:08:23.723 --> 00:08:25.547 na alitumia mkazo huo 00:08:25.547 --> 00:08:29.973 kugonga kichwa changu mara kadhaa kwenye ukuta. 00:08:29.973 --> 00:08:35.291 Siku tano baadaye, ile michubuko kumi shingoni mwangu ilipotea 00:08:35.291 --> 00:08:37.766 na nikavaa nguo ya mama yangu ya harusi, 00:08:37.766 --> 00:08:40.083 na nikafunga ndoa naye. NOTE Paragraph 00:08:40.083 --> 00:08:42.364 Licha ya yaliyotokea, 00:08:42.364 --> 00:08:45.883 nilikuwa na hakika tungeishi maisha ya raha milele, 00:08:45.883 --> 00:08:49.964 kwa sababu nilimpenda, na alinipenda sana. 00:08:49.964 --> 00:08:53.336 Na aliniomba msamaha. 00:08:53.336 --> 00:08:56.509 Alikuwa amechoshwa sana na mipango ya harusi yetu 00:08:56.509 --> 00:08:58.706 na kwa kuwa kitu kimoja na mimi. 00:08:58.706 --> 00:09:00.427 Halikuwa jambo la kawaida 00:09:00.427 --> 00:09:04.023 na asingeniumiza tena. NOTE Paragraph 00:09:04.023 --> 00:09:06.603 Ilitokea mara mbili katika fungate. 00:09:06.603 --> 00:09:09.690 Mara ya kwanza, nilikuwa naendesha gari kutafuta ufukwe wa siri 00:09:09.690 --> 00:09:12.392 na nikapotea, 00:09:12.392 --> 00:09:15.362 na akanipiga ngumi nzito kwenye upande wa kichwa changu 00:09:15.362 --> 00:09:17.506 hata ule upande mwengine wa kichwa changu ukagonga 00:09:17.506 --> 00:09:19.913 dirisha lililo kando ya dereva mara kadhaa. 00:09:19.913 --> 00:09:23.279 Alafu tena siku chache baadaye, tukielekea nyumbani baada ya likizo ya harusi, 00:09:23.279 --> 00:09:25.562 alikasirishwa na trafiki, 00:09:25.562 --> 00:09:28.994 na akarusha Big Mac baridi usoni mwangu. 00:09:28.994 --> 00:09:31.602 Conor aliendelea kunipiga mara moja au mbili kwa wiki 00:09:31.602 --> 00:09:35.019 kwa miaka miwili na nusu ya ndoa yetu. NOTE Paragraph 00:09:35.019 --> 00:09:38.144 Nilifanya makosa kufikiria nilikuwa wa kipekee 00:09:38.144 --> 00:09:40.787 na peke yangu katika hali hii. 00:09:40.787 --> 00:09:42.978 Mmoja kati ya wanawake watatu wakiAmerika 00:09:42.978 --> 00:09:47.130 hupitia ugomvi wa nyumbani ama kufuatwa fuatwa wakati mmoja maishani mwake, 00:09:47.130 --> 00:09:50.771 na CDC inaripoti kwamba watoto milioni kumi na tano 00:09:50.771 --> 00:09:54.181 wananyanyaswa kila mwaka, milioni kumi na tano. 00:09:54.181 --> 00:09:58.554 Hivyo basi, nilikuwa kwenye ushirika mzuri sana. NOTE Paragraph 00:09:58.554 --> 00:10:00.970 Kurudia swali langu: 00:10:00.970 --> 00:10:03.465 Kwa nini nilibaki? 00:10:03.465 --> 00:10:06.203 Jibu lenyewe ni rahisi. 00:10:06.203 --> 00:10:08.891 Sikujua alikuwa akininyanyasa. 00:10:08.891 --> 00:10:12.739 Hata ingawa alielekeza bunduki zilizo na risasi kichwani mwangu, 00:10:12.739 --> 00:10:14.962 akanisukuma ngazini, 00:10:14.962 --> 00:10:16.343 akatishia kuua mbwa wetu, 00:10:16.343 --> 00:10:20.266 akatoa ufunguo wa gari nikiendesha barabarani, 00:10:20.266 --> 00:10:22.783 akamwaga maganda ya kahawa kichwani mwangu 00:10:22.783 --> 00:10:25.099 nikijitayarisha kwa mahojiano ya kazi, 00:10:25.099 --> 00:10:29.469 SIkuwai hata mara moja kujihisi kuwa mke anayenyanyaswa. 00:10:29.469 --> 00:10:33.046 Badala yake, nilikuwa mwanamke mwenye nguvu 00:10:33.046 --> 00:10:35.298 alimpenda sana mwanaume aliyekuwa na shida, 00:10:35.298 --> 00:10:37.355 na nilikuwa mtu wa pekee duniani 00:10:37.355 --> 00:10:40.795 ambaye angeweza kumsaidia Conor kukabiliana na mashetani yake. NOTE Paragraph 00:10:40.795 --> 00:10:44.506 Swali lingine kila mtu huuliza ni, 00:10:44.506 --> 00:10:46.923 kwa nini hatoki tu? 00:10:46.923 --> 00:10:50.874 Kwa nini sikuondoka? Ningeweza kuondoka wakati wowote. 00:10:50.874 --> 00:10:55.586 Kwangu mimi, hili ndilo swali chungu na la kuhuzunisha zaidi ambalo watu huniuliza, 00:10:55.586 --> 00:10:58.677 kwa sababu sisi waathiriwa tunajua jambo nyinyi msilojua: 00:10:58.677 --> 00:11:03.070 Ni jambo la hatari sana kumtoroka mnyanyasaji. 00:11:03.070 --> 00:11:06.389 Kwa sababu daraja ya mwisho katika tuhuma za kinyumbani 00:11:06.389 --> 00:11:09.284 ni kumuua. 00:11:09.284 --> 00:11:11.825 Zaidi ya asilimia sabini ya vifo vinavyosababishwa na tuhuma za kinyumbani 00:11:11.825 --> 00:11:15.893 hutokea baada ya mwathiriwa kukatiza uhusiano huo, 00:11:15.893 --> 00:11:17.786 baada ya kutoka, 00:11:17.786 --> 00:11:21.037 kwa sababu wakati huo mnyanyasaji hana chochote cha kupoteza. 00:11:21.037 --> 00:11:24.128 Matokeo mengine ni pamoja na kufuatwa fuatwa, 00:11:24.128 --> 00:11:27.080 hata baada ya mnyanyasaji kuoa tena; 00:11:27.080 --> 00:11:29.235 unyimaji wa hela; 00:11:29.235 --> 00:11:31.624 na uingiliaji wa mfumo wa mahakama za kifamilia 00:11:31.624 --> 00:11:34.447 ili kumtia wasiwasi mwathirika na wanawe, 00:11:34.447 --> 00:11:39.373 ambao mara kwa mara hushurutishwa na majaji wa mahakama za kifamilia 00:11:39.373 --> 00:11:41.342 kuwa na wakati usiosimamiwa 00:11:41.342 --> 00:11:45.013 pamoja na mtu yule aliyemtuhumu mama yao. 00:11:45.013 --> 00:11:49.188 Na bado twauliza, kwa nini hamtoroki tu? NOTE Paragraph 00:11:49.188 --> 00:11:50.942 Niliweza kuondoka, 00:11:50.942 --> 00:11:53.844 kwa sababu ya kipigo kibaya cha mwisho 00:11:53.844 --> 00:11:57.003 kilichofumbua macho yangu. 00:11:57.003 --> 00:12:00.173 Nilitambua kwamba mtu yule niliyempenda sana 00:12:00.173 --> 00:12:03.083 angekuja kuniua kama ningeendelea kumuacha hivi hivi tu. 00:12:03.083 --> 00:12:05.598 Hivyo nikavunja ukimya. 00:12:05.598 --> 00:12:08.428 Nikawaeleza watu wote: 00:12:08.428 --> 00:12:12.213 polisi, jirani zangu, 00:12:12.213 --> 00:12:16.053 marafiki zangu na familia, wageni, 00:12:16.053 --> 00:12:22.907 na niko hapa leo kwa sababu nyote mlinisaidia. NOTE Paragraph 00:12:22.907 --> 00:12:25.445 Tuna tabia ya kuwabagua waathirika 00:12:25.445 --> 00:12:28.507 kama vichwa vibaya vya habari, 00:12:28.507 --> 00:12:31.803 wanaojitakia maovu, watu walioharibika. 00:12:31.803 --> 00:12:34.806 Swali hilo, "Kwa nini haondoki?" 00:12:34.806 --> 00:12:40.442 kwa wengine ni kama kusema, "Ni makosa yake kuendela kukaa hapo," 00:12:40.442 --> 00:12:43.766 kana kwamba waathirika huchagua kusudi kupenda wanaume 00:12:43.766 --> 00:12:46.398 walio na lengo la kutumaliza. NOTE Paragraph 00:12:46.398 --> 00:12:48.902 Lakini tangu niandike kitabu "Crazy Love," 00:12:48.902 --> 00:12:52.425 nimesikia mamia ya hadithi kutoka kwa wanaume na wanawake 00:12:52.425 --> 00:12:54.870 ambao pia waliondoka, 00:12:54.870 --> 00:12:59.250 waliojifunza somo muhimu la maisha kutokana na yale yaliyotokea, 00:12:59.250 --> 00:13:03.463 na waliojenga maisha yao tena--maisha yenye furaha 00:13:03.463 --> 00:13:05.797 kama wafanyakazi, wake na kina mama, 00:13:05.797 --> 00:13:10.478 maisha yasiyo na unyanyasaji, kama yangu. 00:13:10.478 --> 00:13:14.509 Kwa sababu inaonekana kwamba mimi nilikuwa mwathirika halisi wa unyanyasaji majumbani. 00:13:14.509 --> 00:13:17.953 na msalimika wa unyanyasaji wa majumbani. 00:13:17.953 --> 00:13:21.978 Niliolewa na mtu mwema na mpole, 00:13:21.978 --> 00:13:24.314 na pamoja tuna watoto watatu. 00:13:24.314 --> 00:13:27.715 Nina yule mbwa wangu mweusi, na nina lile gari ndogo. 00:13:27.715 --> 00:13:31.181 Kile sitawahi kuwa nacho tena, 00:13:31.181 --> 00:13:34.139 milele, 00:13:34.139 --> 00:13:36.264 ni bunduki iliyojaa risasi iliyoelekezwa kichwani mwangu 00:13:36.264 --> 00:13:39.907 na mtu anayesema eti ananipenda. NOTE Paragraph 00:13:39.907 --> 00:13:42.538 Wakati huu, labda unafikiria, 00:13:42.538 --> 00:13:44.445 "Hili ni jambo la kushangaza," 00:13:44.445 --> 00:13:47.573 ama, "Kwa nini alikuwa mjinga hivi," 00:13:47.573 --> 00:13:53.576 lakini muda huu wote, nimekuwa haswa nikiongea juu yako. 00:13:53.576 --> 00:13:57.093 Nakuhakikishia kuna watu kadhaa 00:13:57.093 --> 00:13:58.835 wanaonisikiliza saa hii 00:13:58.835 --> 00:14:01.847 ambao wananyanyaswa 00:14:01.847 --> 00:14:04.362 au ambao walinyanyaswa wakiwa watoto 00:14:04.362 --> 00:14:07.732 au walio wanyanyasaji wenyewe. 00:14:07.732 --> 00:14:09.669 unyanyasaji unaweza kuwa unamwathiri binti yako, 00:14:09.669 --> 00:14:14.962 dadako, rafiki yako wa karibu wakati huu. NOTE Paragraph 00:14:14.962 --> 00:14:18.406 Niliweza kumaliza hadithi yangu wazimu ya mapenzi 00:14:18.406 --> 00:14:20.607 kwa kuvunja ukimya. 00:14:20.607 --> 00:14:23.122 Bado naendelea kuvunja ukimya leo. 00:14:23.122 --> 00:14:26.938 Ni njia yangu ya kusaidia waathirika wengine, 00:14:26.938 --> 00:14:30.306 na ni ombi langu la mwisho kwenu. 00:14:30.306 --> 00:14:33.138 Ongeeni kuhusu mliyosikia hapa. 00:14:33.138 --> 00:14:36.466 Unyanyasaji hushamiri tu katika ukimya. 00:14:36.466 --> 00:14:40.169 Una nguvu ya kumaliza unyanyasaji majumbani 00:14:40.169 --> 00:14:43.678 kwa kuongea kuhusu unyanyasaji. 00:14:43.678 --> 00:14:46.752 Sisi waathirika tunahitaji kila mtu. 00:14:46.752 --> 00:14:50.825 Tunawahitaji nyote kuelewa 00:14:50.825 --> 00:14:54.603 siri za unyanyasaji majumbani. 00:14:54.603 --> 00:14:57.587 Mulikieni mwanga unyanyasaji kwa kuuongelea 00:14:57.587 --> 00:14:59.714 mkiwa na watoto wenu, wafanyakazi wenzenu, 00:14:59.714 --> 00:15:01.651 marafiki zenu na familia. 00:15:01.651 --> 00:15:05.097 Ongeleeni waliosalimika kama watu wema na wanaopendeka 00:15:05.097 --> 00:15:07.912 walio na maisha kamili kwenye siku za usoni 00:15:07.912 --> 00:15:11.393 Eleweni ishara za mapema za tuhuma 00:15:11.393 --> 00:15:14.226 na muingilie kati kistadi 00:15:14.226 --> 00:15:18.388 malizeni na muonyeshe waathirika njia safi ya kuiepuka. 00:15:18.388 --> 00:15:22.383 Pamoja tunaweza kufanya vitanda vyetu, 00:15:22.383 --> 00:15:26.000 meza zetu za mlo na familia zetu 00:15:26.000 --> 00:15:29.257 mahali pa amani zinavyopaswa kuwa NOTE Paragraph 00:15:29.257 --> 00:15:31.229 Asanteni. NOTE Paragraph 00:15:31.229 --> 00:15:38.937 (Mahali)