[Script Info] Title: [Events] Format: Layer, Start, End, Style, Name, MarginL, MarginR, MarginV, Effect, Text Dialogue: 0,0:00:00.68,0:00:03.97,Default,,0000,0000,0000,,Leo niko hapa kuongea kuhusu swala nyeti, Dialogue: 0,0:00:03.97,0:00:07.67,Default,,0000,0000,0000,,ambalo lina jibu tatanishi. Dialogue: 0,0:00:07.67,0:00:11.27,Default,,0000,0000,0000,,Swala langu ni zile siri za ugomvi nyumbani, Dialogue: 0,0:00:11.27,0:00:13.60,Default,,0000,0000,0000,,na swali nitakalokabiliana nalo Dialogue: 0,0:00:13.60,0:00:17.68,Default,,0000,0000,0000,,ni lile swali moja kila mmoja huliuliza kila mara: Dialogue: 0,0:00:17.68,0:00:19.30,Default,,0000,0000,0000,,Kwa nini muathirika hubakia? Dialogue: 0,0:00:19.30,0:00:23.29,Default,,0000,0000,0000,,Kwa nini mtu yeyote abaki na mume ampigaye? Dialogue: 0,0:00:23.29,0:00:26.27,Default,,0000,0000,0000,,Mie si daktari wa akili, mfanyakazi wa ustawi wa jamii Dialogue: 0,0:00:26.27,0:00:28.60,Default,,0000,0000,0000,,au mtaalam wa ugomvi wa nyumbani. Dialogue: 0,0:00:28.60,0:00:31.80,Default,,0000,0000,0000,,Mimi ni mwanamke mwenye hadithi ya kusimulia. Dialogue: 0,0:00:31.80,0:00:36.32,Default,,0000,0000,0000,,Nilikuwa na umri wa miaka ishirini na miwili. Nilikuwa nimehitimu tu kutoka chuo cha Harvard. Dialogue: 0,0:00:36.32,0:00:38.79,Default,,0000,0000,0000,,Nilikuwa nimehamia mjini New York kwa ajili ya kazi yangu ya kwanza Dialogue: 0,0:00:38.79,0:00:42.08,Default,,0000,0000,0000,,kama mwandishi na mhariri wa gazeti la Seventeen. Dialogue: 0,0:00:42.08,0:00:44.32,Default,,0000,0000,0000,,Nilikuwa na nyumba yangu ya kwanza, Dialogue: 0,0:00:44.32,0:00:47.52,Default,,0000,0000,0000,,kadi yangu ya kwanza ya American Express, Dialogue: 0,0:00:47.52,0:00:50.55,Default,,0000,0000,0000,,na nilikuwa na siri moja kubwa sana. Dialogue: 0,0:00:50.55,0:00:54.25,Default,,0000,0000,0000,,Siri yangu ilikuwa kwamba kulikuwa na bunduki Dialogue: 0,0:00:54.25,0:00:57.69,Default,,0000,0000,0000,,iliyojaa risasi iliyoelekezwa kichwani mwangu Dialogue: 0,0:00:57.69,0:01:00.25,Default,,0000,0000,0000,,na mwanamme niliyefikiria alikuwa mpenzi wangu, Dialogue: 0,0:01:00.25,0:01:03.74,Default,,0000,0000,0000,,mara kadhaa. Dialogue: 0,0:01:03.74,0:01:07.30,Default,,0000,0000,0000,,Mwanamme huyu niliyempenda kuliko yeyote duniani Dialogue: 0,0:01:07.30,0:01:11.38,Default,,0000,0000,0000,,alielekeza bunduki kichwani mwangu na kutishia kuniua Dialogue: 0,0:01:11.38,0:01:14.56,Default,,0000,0000,0000,,mara nyingi kuliko zile ningeweza kukumbuka. Dialogue: 0,0:01:14.56,0:01:17.30,Default,,0000,0000,0000,,Niko hapa kuwapa hadithi ya upendo wa kupindukia, Dialogue: 0,0:01:17.30,0:01:20.49,Default,,0000,0000,0000,,mtego wa kisaikolojia uliofichwa kama mapenzi, Dialogue: 0,0:01:20.49,0:01:23.34,Default,,0000,0000,0000,,ambao mamilioni ya wanawake na hata wanaume wengine Dialogue: 0,0:01:23.34,0:01:25.72,Default,,0000,0000,0000,,hutumbukia kila mwaka. Dialogue: 0,0:01:25.72,0:01:28.47,Default,,0000,0000,0000,,Inaweza hata kuwa hadithi yako. Dialogue: 0,0:01:28.47,0:01:31.51,Default,,0000,0000,0000,,Sionekani kama mtu niliyenusurika na ugomvi katika mahusiano. Dialogue: 0,0:01:31.51,0:01:33.82,Default,,0000,0000,0000,,Nina shahada ya sanaa katika Kiigereza kutoka chuo cha Harvard, Dialogue: 0,0:01:33.82,0:01:36.18,Default,,0000,0000,0000,,na shahada ya juu katika mauzo kutoka kwa chuo cha biashara cha Wharton. Dialogue: 0,0:01:36.18,0:01:39.47,Default,,0000,0000,0000,,Nimetumia muda mrefu maishani nikifanya kazi kwenye kampuni bora duniani Dialogue: 0,0:01:39.47,0:01:43.74,Default,,0000,0000,0000,,zikiwemo Johnson & Johnson, Leo Burnett na The Washington Post. Dialogue: 0,0:01:43.74,0:01:47.54,Default,,0000,0000,0000,,Nimeolewa takriban miaka ishirini kwa mme wangu wa pili Dialogue: 0,0:01:47.54,0:01:50.33,Default,,0000,0000,0000,,na tuna wana watatu pamoja Dialogue: 0,0:01:50.33,0:01:54.56,Default,,0000,0000,0000,,Mbwa wangu ni mweusi, na mie huendesha gari ndogo la Honda Odyssey. Dialogue: 0,0:01:54.56,0:01:57.04,Default,,0000,0000,0000,,(Kicheko) Dialogue: 0,0:01:57.04,0:01:59.76,Default,,0000,0000,0000,,Kwa hivyo ujumbe wangu wa kwanza kwenu ni kwamba ugomvi wa nyumbani Dialogue: 0,0:01:59.76,0:02:02.13,Default,,0000,0000,0000,,humtokea yeyote-- Dialogue: 0,0:02:02.13,0:02:06.30,Default,,0000,0000,0000,,kila jamii,dini, kila kipato na ngazi ya kimasomo. Dialogue: 0,0:02:06.30,0:02:08.24,Default,,0000,0000,0000,,Iko kila mahali. Dialogue: 0,0:02:08.24,0:02:10.76,Default,,0000,0000,0000,,Na ujumbe wangu wa pili ni kwamba kila mtu hufikiri Dialogue: 0,0:02:10.76,0:02:12.88,Default,,0000,0000,0000,,ugomvi wa nyumbani huwaathiri wanawake, Dialogue: 0,0:02:12.88,0:02:15.15,Default,,0000,0000,0000,,ati ni swala la wanawake. Dialogue: 0,0:02:15.15,0:02:17.37,Default,,0000,0000,0000,,Si sahihi. Dialogue: 0,0:02:17.37,0:02:21.48,Default,,0000,0000,0000,,Zaidi ya asili mia 85 ya wanyanyasaji ni wanaume, na ugomvi wa nyumbani Dialogue: 0,0:02:21.48,0:02:27.40,Default,,0000,0000,0000,,hutokea haswa katika mahusiano ya undani, ya kutegemeana na yale ya muda mrefu, Dialogue: 0,0:02:27.40,0:02:29.56,Default,,0000,0000,0000,,yaani, katika familia, Dialogue: 0,0:02:29.56,0:02:33.43,Default,,0000,0000,0000,,mahali tusipotaka au kutarajia kupata ugomvi, Dialogue: 0,0:02:33.43,0:02:37.71,Default,,0000,0000,0000,,ndio sababu tuhuma za kinyumbani ni tatanishi hivi. Dialogue: 0,0:02:37.71,0:02:41.26,Default,,0000,0000,0000,,Ningekuambia kwamba ningekuwa mtu wa mwisho duniani Dialogue: 0,0:02:41.26,0:02:43.83,Default,,0000,0000,0000,,kukaa na mwanaume anayenipiga, Dialogue: 0,0:02:43.83,0:02:47.24,Default,,0000,0000,0000,,lakini kusema kweli nilikuwa mwathirika kwa sababu ya umri wangu. Dialogue: 0,0:02:47.24,0:02:50.52,Default,,0000,0000,0000,,Nilikuwa mwenye umri wa miaka ishirini na mbili na Marekani, Dialogue: 0,0:02:50.52,0:02:54.37,Default,,0000,0000,0000,,wanawake wenye umri kati ya miaka kumi na sita hadi ishirini na nne wana uwezekano wa mara tatu zaidi Dialogue: 0,0:02:54.37,0:02:57.13,Default,,0000,0000,0000,,kuwa waathirika wa ugomvi wa nyumbani Dialogue: 0,0:02:57.13,0:02:59.95,Default,,0000,0000,0000,,ikilinganishwa na wanawake wa umri mwingine, Dialogue: 0,0:02:59.95,0:03:03.25,Default,,0000,0000,0000,,vilevile zaidi ya wanawake mia tano na wasichana wa umri huu Dialogue: 0,0:03:03.25,0:03:06.82,Default,,0000,0000,0000,,huuawa kila mwaka na wapenzi wanyanyasaji, Dialogue: 0,0:03:06.82,0:03:11.46,Default,,0000,0000,0000,,wapenzi, na waume zao Marekani. Dialogue: 0,0:03:11.46,0:03:14.52,Default,,0000,0000,0000,,Nilikuwa muathirika kwa sababu sikujua chochote Dialogue: 0,0:03:14.52,0:03:19.10,Default,,0000,0000,0000,,kuhusu ugomvi wa nyumbani, maonyo yake ama mifano yake. Dialogue: 0,0:03:19.10,0:03:24.16,Default,,0000,0000,0000,,Nilikutana na Conor usiku mmoja wenye baridi na mvua, mwezi wa Januari. Dialogue: 0,0:03:24.16,0:03:27.13,Default,,0000,0000,0000,,Alikaa kando yangu kwenye treni katika mji wa New York, Dialogue: 0,0:03:27.13,0:03:29.27,Default,,0000,0000,0000,,na alianza kuniongelesha. Dialogue: 0,0:03:29.27,0:03:31.14,Default,,0000,0000,0000,,Aliniambia mambo mawili. Dialogue: 0,0:03:31.14,0:03:34.94,Default,,0000,0000,0000,,La kwanza kuwa, yeye pia, alikuwa amehitimu kutoka kwa kati ya zile shule bora zaidi Marekani, Dialogue: 0,0:03:34.94,0:03:39.29,Default,,0000,0000,0000,,na kwamba alifanya kazi kwenye benki moja ya kuvutia sana huko Wall Street. Dialogue: 0,0:03:39.29,0:03:42.95,Default,,0000,0000,0000,,Lakini kile kilichonivutia zaidi siku hiyo Dialogue: 0,0:03:42.95,0:03:46.24,Default,,0000,0000,0000,,ni kuwa alikuwa mwerevu na mcheshi Dialogue: 0,0:03:46.24,0:03:47.64,Default,,0000,0000,0000,,na alionekana kuwa kijana wa mashambani. Dialogue: 0,0:03:47.64,0:03:49.99,Default,,0000,0000,0000,,Alikuwa na haya mashavu makubwa, haya mashavu makubwa ya waridi Dialogue: 0,0:03:49.99,0:03:51.67,Default,,0000,0000,0000,,na hii nywele za rangi kama ya ngano, Dialogue: 0,0:03:51.67,0:03:54.96,Default,,0000,0000,0000,,na alionekana kuwa mwema sana. Dialogue: 0,0:03:54.96,0:03:58.74,Default,,0000,0000,0000,,Jambo moja la busara Conor alilofanya, kutoka mwanzoni, Dialogue: 0,0:03:58.74,0:04:04.32,Default,,0000,0000,0000,,lilikuwa kufanya kana kwamba nilikuwa mwenye ushawishi mkubwa katika huo uhusiano. Dialogue: 0,0:04:04.32,0:04:06.52,Default,,0000,0000,0000,,Alifanya hivi haswa hapo mwanzo Dialogue: 0,0:04:06.52,0:04:09.38,Default,,0000,0000,0000,,kwa kunihusudu. Dialogue: 0,0:04:09.38,0:04:12.67,Default,,0000,0000,0000,,Tukaanza kutoka pamoja, na alipenda kila kitu kunihusu, Dialogue: 0,0:04:12.67,0:04:14.35,Default,,0000,0000,0000,,ati nilikuwa mwerevu, ati nilisomea chuo cha Harvard, Dialogue: 0,0:04:14.35,0:04:17.38,Default,,0000,0000,0000,,ati nilikuwa mwenye shauku kusaidia wasichana wadogo, na kazi yangu. Dialogue: 0,0:04:17.38,0:04:19.92,Default,,0000,0000,0000,,Alitaka kujua kila kitu kuhusu familia yangu Dialogue: 0,0:04:19.92,0:04:22.53,Default,,0000,0000,0000,,na utoto wangu na matarajio na ndoto zangu. Dialogue: 0,0:04:22.53,0:04:26.16,Default,,0000,0000,0000,,Conor alikuwa na imani nami, kama mwandishi na mwanamke, Dialogue: 0,0:04:26.16,0:04:29.84,Default,,0000,0000,0000,,kwa njia ambayo yeyote mwengine alikuwa hajawahi. Dialogue: 0,0:04:29.84,0:04:34.17,Default,,0000,0000,0000,,Na alileta uaminifu kati yetu Dialogue: 0,0:04:34.17,0:04:36.69,Default,,0000,0000,0000,,kwa kunieleza siri yake, Dialogue: 0,0:04:36.69,0:04:41.17,Default,,0000,0000,0000,,ambayo ilikuwa, alipokuwa mvulana mdogo sana akiwa na umri wa miaka minne Dialogue: 0,0:04:41.17,0:04:44.08,Default,,0000,0000,0000,,alipigwa vibaya sana mara kwa mara Dialogue: 0,0:04:44.08,0:04:45.77,Default,,0000,0000,0000,,na babake wa kambo, Dialogue: 0,0:04:45.77,0:04:49.71,Default,,0000,0000,0000,,na unyanyasaji ulizidi kuwa mbaya zaidi hadi ikambidi aache shule akiwa daraja la nane, Dialogue: 0,0:04:49.71,0:04:52.32,Default,,0000,0000,0000,,ingawa alikuwa mwerevu sana, Dialogue: 0,0:04:52.32,0:04:55.58,Default,,0000,0000,0000,,na kwamba alitumia takriban miaka ishirini kujenga maisha yake upya. Dialogue: 0,0:04:55.58,0:04:58.74,Default,,0000,0000,0000,,Ndiyo sababu hiyo shahada yake kutoka zile shule bora zaidi Marekani, Dialogue: 0,0:04:58.74,0:05:01.55,Default,,0000,0000,0000,,na kazi yake Wall Street na maisha yake mazuri siku za usoni Dialogue: 0,0:05:01.55,0:05:04.12,Default,,0000,0000,0000,,zilikuwa za umuhimu mkubwa sana kwake. Dialogue: 0,0:05:04.12,0:05:06.26,Default,,0000,0000,0000,,Kama ungeniuliza Dialogue: 0,0:05:06.26,0:05:11.63,Default,,0000,0000,0000,,kama huyu mwanamme mwerevu, mcheshi na mwenye kujali aliyenipenda sana Dialogue: 0,0:05:11.63,0:05:16.01,Default,,0000,0000,0000,,angekuja kuniamulia kama ningejipamba au la, Dialogue: 0,0:05:16.01,0:05:18.06,Default,,0000,0000,0000,,ufupi wa sketi zangu, Dialogue: 0,0:05:18.06,0:05:19.99,Default,,0000,0000,0000,,mahali ningeishi, kazi gani ningefanya, Dialogue: 0,0:05:19.99,0:05:23.36,Default,,0000,0000,0000,,marafiki zangu wangekuwa wepi na pale ningekulia Krisimasi Dialogue: 0,0:05:23.36,0:05:25.30,Default,,0000,0000,0000,,ningekucheka, Dialogue: 0,0:05:25.30,0:05:28.35,Default,,0000,0000,0000,,kwa sababu hakukuwa na ushahidi wowote wa tuhuma au uthibiti Dialogue: 0,0:05:28.35,0:05:31.84,Default,,0000,0000,0000,,au hasira kutoka kwa Conor hapo mwanzoni. Dialogue: 0,0:05:31.84,0:05:34.96,Default,,0000,0000,0000,,Sikujua kwamba daraja la kwanza Dialogue: 0,0:05:34.96,0:05:37.34,Default,,0000,0000,0000,,katika uhusiano wowote wenye ugomvi Dialogue: 0,0:05:37.34,0:05:40.99,Default,,0000,0000,0000,,ni kumvuta na kumpumbaza mwathirika Dialogue: 0,0:05:40.99,0:05:45.75,Default,,0000,0000,0000,,Pia sikujua kuwa daraja ya pili ni kumtenga mwathirika. Dialogue: 0,0:05:45.75,0:05:49.90,Default,,0000,0000,0000,,Conor hakuja nyumbani siku moja na kutangaza, Dialogue: 0,0:05:49.90,0:05:53.04,Default,,0000,0000,0000,,"Unajua huu uhusiano wetu kama wa Romeo na Julieti umekuwa mtamu, Dialogue: 0,0:05:53.04,0:05:55.04,Default,,0000,0000,0000,,lakini nataka kwenda katika hatua inayofuata Dialogue: 0,0:05:55.04,0:05:59.22,Default,,0000,0000,0000,,ambapo nitakutenga na kukunyanyasa" - (Kicheko) - Dialogue: 0,0:05:59.22,0:06:00.58,Default,,0000,0000,0000,,"kwa hivyo nataka kukuhamisha kutoka nyumba hii Dialogue: 0,0:06:00.58,0:06:02.22,Default,,0000,0000,0000,,ambapo majirani wanawezakusikia ukipiga mayowe Dialogue: 0,0:06:02.22,0:06:04.69,Default,,0000,0000,0000,,na kukupeleka nje ya mji huu ambapo una marafiki na familia Dialogue: 0,0:06:04.69,0:06:07.100,Default,,0000,0000,0000,,na wafanyakazi wenzako wanaoweza kuona hiyo michubuko." Dialogue: 0,0:06:07.100,0:06:12.22,Default,,0000,0000,0000,,Badala yake, Conor alikuja nyumbani jioni ya Ijumaa moja Dialogue: 0,0:06:12.22,0:06:14.95,Default,,0000,0000,0000,,na akaniambia kuwa alikuwa ameacha kazi siku hiyo, Dialogue: 0,0:06:14.95,0:06:17.41,Default,,0000,0000,0000,,kazi ya ndoto zake, Dialogue: 0,0:06:17.41,0:06:21.55,Default,,0000,0000,0000,,na akasema kwamba alikuwa ameacha kazi hiyo kwa sababu yangu, Dialogue: 0,0:06:21.55,0:06:24.73,Default,,0000,0000,0000,,kwa sababu nilimfanya ahisi usalama na kupendwa Dialogue: 0,0:06:24.73,0:06:27.85,Default,,0000,0000,0000,,ati hakuhitaji tena kujithibitisha huko Wall Street, Dialogue: 0,0:06:27.85,0:06:30.37,Default,,0000,0000,0000,,na alitaka tu kutoka mjini Dialogue: 0,0:06:30.37,0:06:33.35,Default,,0000,0000,0000,,na kukaa mbali na familia yake iliyomnyanyasa. Dialogue: 0,0:06:33.35,0:06:36.47,Default,,0000,0000,0000,,na kuhamia mji mdogo wa New England Dialogue: 0,0:06:36.47,0:06:40.04,Default,,0000,0000,0000,,ambapo angeweza kuanza upya maisha yake nikiwa kando yake. Dialogue: 0,0:06:40.04,0:06:43.91,Default,,0000,0000,0000,,Sikutaka kamwe kuhama kutoka New York, Dialogue: 0,0:06:43.91,0:06:47.52,Default,,0000,0000,0000,,na kuacha kazi ya ndoto zangu, Dialogue: 0,0:06:47.52,0:06:50.10,Default,,0000,0000,0000,,lakini nilifikiria mtu hujitoa muhanga kwa mpenzi wake, Dialogue: 0,0:06:50.10,0:06:53.56,Default,,0000,0000,0000,,kwa hivyo nikakubali na nikaacha kazi yangu, Dialogue: 0,0:06:53.56,0:06:56.19,Default,,0000,0000,0000,,na Conor na mimi tukaondoka Manhattan pamoja. Dialogue: 0,0:06:56.19,0:07:00.56,Default,,0000,0000,0000,,Sikuwai kufikiria kwamba penzi nililokuwa nalo halikuwa la kawaida, Dialogue: 0,0:07:00.56,0:07:04.19,Default,,0000,0000,0000,,na kwamba nilikuwa nikitembea bila habari ndani ya Dialogue: 0,0:07:04.19,0:07:09.17,Default,,0000,0000,0000,,mtego mzuri wa kimwili, kifedha na kiakili Dialogue: 0,0:07:09.17,0:07:11.49,Default,,0000,0000,0000,,Daraja ya pili katika ugomvi wa kimahusiano Dialogue: 0,0:07:11.49,0:07:15.77,Default,,0000,0000,0000,,ni kuleta tishio la vurugu Dialogue: 0,0:07:15.77,0:07:17.97,Default,,0000,0000,0000,,na kuangalia vile linavyomgusa. Dialogue: 0,0:07:17.97,0:07:20.68,Default,,0000,0000,0000,,Na hapa ndipo bunduki zinapoingia. Dialogue: 0,0:07:20.68,0:07:23.60,Default,,0000,0000,0000,,Muda tu tulipohamia New England--unajua, Dialogue: 0,0:07:23.60,0:07:26.34,Default,,0000,0000,0000,,mahali Connor aliposema pangemfanya ajisikie salama-- Dialogue: 0,0:07:26.34,0:07:28.75,Default,,0000,0000,0000,,alinunua bunduki tatu. Dialogue: 0,0:07:28.75,0:07:32.19,Default,,0000,0000,0000,,Aliweka moja garini. Dialogue: 0,0:07:32.19,0:07:34.85,Default,,0000,0000,0000,,Aliweka moja chini ya mto kitandani mwetu, Dialogue: 0,0:07:34.85,0:07:38.01,Default,,0000,0000,0000,,na ya tatu alitembea nayo mfukoni nyakati zote. Dialogue: 0,0:07:38.01,0:07:40.33,Default,,0000,0000,0000,,Na alisema alihitaji bunduki hizo Dialogue: 0,0:07:40.33,0:07:43.12,Default,,0000,0000,0000,,kwa sababu ya uchungu aliopitia akiwa mchanga. Dialogue: 0,0:07:43.12,0:07:45.61,Default,,0000,0000,0000,,Alizihitaji kujisikia salama. Dialogue: 0,0:07:45.61,0:07:48.52,Default,,0000,0000,0000,,Lakini bunduki hizo zilikuwa ujumbe kwangu, Dialogue: 0,0:07:48.52,0:07:51.22,Default,,0000,0000,0000,,na ingawa hakuwai kuninyoshea mkono, Dialogue: 0,0:07:51.22,0:07:57.02,Default,,0000,0000,0000,,maisha yangu tayari yalikuwa hatarini kila dakika ya kila siku. Dialogue: 0,0:07:57.02,0:08:00.59,Default,,0000,0000,0000,,Kwanza Conor alinishambulia Dialogue: 0,0:08:00.59,0:08:03.42,Default,,0000,0000,0000,,siku tano kabla ya harusi yetu. Dialogue: 0,0:08:03.42,0:08:07.61,Default,,0000,0000,0000,,Ilikuwa saa moja asubuhi na bado nilikuwa nimevalia vazi la kulala Dialogue: 0,0:08:07.61,0:08:11.85,Default,,0000,0000,0000,,Nilikuwa nafanya kazi kweny kompyuta yangu nikijaribu kumaliza kazi fulani ya uandishi, Dialogue: 0,0:08:11.85,0:08:13.66,Default,,0000,0000,0000,,na nilikuwa nimekasirika, Dialogue: 0,0:08:13.66,0:08:16.75,Default,,0000,0000,0000,,na Conor akatumia hasira zangu kama kisingizio Dialogue: 0,0:08:16.75,0:08:19.90,Default,,0000,0000,0000,,kunikaba koo Dialogue: 0,0:08:19.90,0:08:23.72,Default,,0000,0000,0000,,na kuikaza hadi sikuweza kupumua au kupiga kelele, Dialogue: 0,0:08:23.72,0:08:25.55,Default,,0000,0000,0000,,na alitumia mkazo huo Dialogue: 0,0:08:25.55,0:08:29.97,Default,,0000,0000,0000,,kugonga kichwa changu mara kadhaa kwenye ukuta. Dialogue: 0,0:08:29.97,0:08:35.29,Default,,0000,0000,0000,,Siku tano baadaye, ile michubuko kumi shingoni mwangu ilipotea Dialogue: 0,0:08:35.29,0:08:37.77,Default,,0000,0000,0000,,na nikavaa nguo ya mama yangu ya harusi, Dialogue: 0,0:08:37.77,0:08:40.08,Default,,0000,0000,0000,,na nikafunga ndoa naye. Dialogue: 0,0:08:40.08,0:08:42.36,Default,,0000,0000,0000,,Licha ya yaliyotokea, Dialogue: 0,0:08:42.36,0:08:45.88,Default,,0000,0000,0000,,nilikuwa na hakika tungeishi maisha ya raha milele, Dialogue: 0,0:08:45.88,0:08:49.96,Default,,0000,0000,0000,,kwa sababu nilimpenda, na alinipenda sana. Dialogue: 0,0:08:49.96,0:08:53.34,Default,,0000,0000,0000,,Na aliniomba msamaha. Dialogue: 0,0:08:53.34,0:08:56.51,Default,,0000,0000,0000,,Alikuwa amechoshwa sana na mipango ya harusi yetu Dialogue: 0,0:08:56.51,0:08:58.71,Default,,0000,0000,0000,,na kwa kuwa kitu kimoja na mimi. Dialogue: 0,0:08:58.71,0:09:00.43,Default,,0000,0000,0000,,Halikuwa jambo la kawaida Dialogue: 0,0:09:00.43,0:09:04.02,Default,,0000,0000,0000,,na asingeniumiza tena. Dialogue: 0,0:09:04.02,0:09:06.60,Default,,0000,0000,0000,,Ilitokea mara mbili katika fungate. Dialogue: 0,0:09:06.60,0:09:09.69,Default,,0000,0000,0000,,Mara ya kwanza, nilikuwa naendesha gari kutafuta ufukwe wa siri Dialogue: 0,0:09:09.69,0:09:12.39,Default,,0000,0000,0000,,na nikapotea, Dialogue: 0,0:09:12.39,0:09:15.36,Default,,0000,0000,0000,,na akanipiga ngumi nzito kwenye upande wa kichwa changu Dialogue: 0,0:09:15.36,0:09:17.51,Default,,0000,0000,0000,,hata ule upande mwengine wa kichwa changu ukagonga Dialogue: 0,0:09:17.51,0:09:19.91,Default,,0000,0000,0000,,dirisha lililo kando ya dereva mara kadhaa. Dialogue: 0,0:09:19.91,0:09:23.28,Default,,0000,0000,0000,,Alafu tena siku chache baadaye, tukielekea nyumbani baada ya likizo ya harusi, Dialogue: 0,0:09:23.28,0:09:25.56,Default,,0000,0000,0000,,alikasirishwa na trafiki, Dialogue: 0,0:09:25.56,0:09:28.99,Default,,0000,0000,0000,,na akarusha Big Mac baridi usoni mwangu. Dialogue: 0,0:09:28.99,0:09:31.60,Default,,0000,0000,0000,,Conor aliendelea kunipiga mara moja au mbili kwa wiki Dialogue: 0,0:09:31.60,0:09:35.02,Default,,0000,0000,0000,,kwa miaka miwili na nusu ya ndoa yetu. Dialogue: 0,0:09:35.02,0:09:38.14,Default,,0000,0000,0000,,Nilifanya makosa kufikiria nilikuwa wa kipekee Dialogue: 0,0:09:38.14,0:09:40.79,Default,,0000,0000,0000,,na peke yangu katika hali hii. Dialogue: 0,0:09:40.79,0:09:42.98,Default,,0000,0000,0000,,Mmoja kati ya wanawake watatu wakiAmerika Dialogue: 0,0:09:42.98,0:09:47.13,Default,,0000,0000,0000,,hupitia ugomvi wa nyumbani ama kufuatwa fuatwa wakati mmoja maishani mwake, Dialogue: 0,0:09:47.13,0:09:50.77,Default,,0000,0000,0000,,na CDC inaripoti kwamba watoto milioni kumi na tano Dialogue: 0,0:09:50.77,0:09:54.18,Default,,0000,0000,0000,,wananyanyaswa kila mwaka, milioni kumi na tano. Dialogue: 0,0:09:54.18,0:09:58.55,Default,,0000,0000,0000,,Hivyo basi, nilikuwa kwenye ushirika mzuri sana. Dialogue: 0,0:09:58.55,0:10:00.97,Default,,0000,0000,0000,,Kurudia swali langu: Dialogue: 0,0:10:00.97,0:10:03.46,Default,,0000,0000,0000,,Kwa nini nilibaki? Dialogue: 0,0:10:03.46,0:10:06.20,Default,,0000,0000,0000,,Jibu lenyewe ni rahisi. Dialogue: 0,0:10:06.20,0:10:08.89,Default,,0000,0000,0000,,Sikujua alikuwa akininyanyasa. Dialogue: 0,0:10:08.89,0:10:12.74,Default,,0000,0000,0000,,Hata ingawa alielekeza bunduki zilizo na risasi kichwani mwangu, Dialogue: 0,0:10:12.74,0:10:14.96,Default,,0000,0000,0000,,akanisukuma ngazini, Dialogue: 0,0:10:14.96,0:10:16.34,Default,,0000,0000,0000,,akatishia kuua mbwa wetu, Dialogue: 0,0:10:16.34,0:10:20.27,Default,,0000,0000,0000,,akatoa ufunguo wa gari nikiendesha barabarani, Dialogue: 0,0:10:20.27,0:10:22.78,Default,,0000,0000,0000,,akamwaga maganda ya kahawa kichwani mwangu Dialogue: 0,0:10:22.78,0:10:25.10,Default,,0000,0000,0000,,nikijitayarisha kwa mahojiano ya kazi, Dialogue: 0,0:10:25.10,0:10:29.47,Default,,0000,0000,0000,,SIkuwai hata mara moja kujihisi kuwa mke anayenyanyaswa. Dialogue: 0,0:10:29.47,0:10:33.05,Default,,0000,0000,0000,,Badala yake, nilikuwa mwanamke mwenye nguvu Dialogue: 0,0:10:33.05,0:10:35.30,Default,,0000,0000,0000,,alimpenda sana mwanaume aliyekuwa na shida, Dialogue: 0,0:10:35.30,0:10:37.36,Default,,0000,0000,0000,,na nilikuwa mtu wa pekee duniani Dialogue: 0,0:10:37.36,0:10:40.80,Default,,0000,0000,0000,,ambaye angeweza kumsaidia Conor kukabiliana na mashetani yake. Dialogue: 0,0:10:40.80,0:10:44.51,Default,,0000,0000,0000,,Swali lingine kila mtu huuliza ni, Dialogue: 0,0:10:44.51,0:10:46.92,Default,,0000,0000,0000,,kwa nini hatoki tu? Dialogue: 0,0:10:46.92,0:10:50.87,Default,,0000,0000,0000,,Kwa nini sikuondoka? Ningeweza kuondoka wakati wowote. Dialogue: 0,0:10:50.87,0:10:55.59,Default,,0000,0000,0000,,Kwangu mimi, hili ndilo swali chungu na la kuhuzunisha zaidi ambalo watu huniuliza, Dialogue: 0,0:10:55.59,0:10:58.68,Default,,0000,0000,0000,,kwa sababu sisi waathiriwa tunajua jambo nyinyi msilojua: Dialogue: 0,0:10:58.68,0:11:03.07,Default,,0000,0000,0000,,Ni jambo la hatari sana kumtoroka mnyanyasaji. Dialogue: 0,0:11:03.07,0:11:06.39,Default,,0000,0000,0000,,Kwa sababu daraja ya mwisho katika tuhuma za kinyumbani Dialogue: 0,0:11:06.39,0:11:09.28,Default,,0000,0000,0000,,ni kumuua. Dialogue: 0,0:11:09.28,0:11:11.82,Default,,0000,0000,0000,,Zaidi ya asilimia sabini ya vifo vinavyosababishwa na tuhuma za kinyumbani Dialogue: 0,0:11:11.82,0:11:15.89,Default,,0000,0000,0000,,hutokea baada ya mwathiriwa kukatiza uhusiano huo, Dialogue: 0,0:11:15.89,0:11:17.79,Default,,0000,0000,0000,,baada ya kutoka, Dialogue: 0,0:11:17.79,0:11:21.04,Default,,0000,0000,0000,,kwa sababu wakati huo mnyanyasaji hana chochote cha kupoteza. Dialogue: 0,0:11:21.04,0:11:24.13,Default,,0000,0000,0000,,Matokeo mengine ni pamoja na kufuatwa fuatwa, Dialogue: 0,0:11:24.13,0:11:27.08,Default,,0000,0000,0000,,hata baada ya mnyanyasaji kuoa tena; Dialogue: 0,0:11:27.08,0:11:29.24,Default,,0000,0000,0000,,unyimaji wa hela; Dialogue: 0,0:11:29.24,0:11:31.62,Default,,0000,0000,0000,,na uingiliaji wa mfumo wa mahakama za kifamilia Dialogue: 0,0:11:31.62,0:11:34.45,Default,,0000,0000,0000,,ili kumtia wasiwasi mwathirika na wanawe, Dialogue: 0,0:11:34.45,0:11:39.37,Default,,0000,0000,0000,,ambao mara kwa mara hushurutishwa na majaji wa mahakama za kifamilia Dialogue: 0,0:11:39.37,0:11:41.34,Default,,0000,0000,0000,,kuwa na wakati usiosimamiwa Dialogue: 0,0:11:41.34,0:11:45.01,Default,,0000,0000,0000,,pamoja na mtu yule aliyemtuhumu mama yao. Dialogue: 0,0:11:45.01,0:11:49.19,Default,,0000,0000,0000,,Na bado twauliza, kwa nini hamtoroki tu? Dialogue: 0,0:11:49.19,0:11:50.94,Default,,0000,0000,0000,,Niliweza kuondoka, Dialogue: 0,0:11:50.94,0:11:53.84,Default,,0000,0000,0000,,kwa sababu ya kipigo kibaya cha mwisho Dialogue: 0,0:11:53.84,0:11:57.00,Default,,0000,0000,0000,,kilichofumbua macho yangu. Dialogue: 0,0:11:57.00,0:12:00.17,Default,,0000,0000,0000,,Nilitambua kwamba mtu yule niliyempenda sana Dialogue: 0,0:12:00.17,0:12:03.08,Default,,0000,0000,0000,,angekuja kuniua kama ningeendelea kumuacha hivi hivi tu. Dialogue: 0,0:12:03.08,0:12:05.60,Default,,0000,0000,0000,,Hivyo nikavunja ukimya. Dialogue: 0,0:12:05.60,0:12:08.43,Default,,0000,0000,0000,,Nikawaeleza watu wote: Dialogue: 0,0:12:08.43,0:12:12.21,Default,,0000,0000,0000,,polisi, jirani zangu, Dialogue: 0,0:12:12.21,0:12:16.05,Default,,0000,0000,0000,,marafiki zangu na familia, wageni, Dialogue: 0,0:12:16.05,0:12:22.91,Default,,0000,0000,0000,,na niko hapa leo kwa sababu nyote mlinisaidia. Dialogue: 0,0:12:22.91,0:12:25.44,Default,,0000,0000,0000,,Tuna tabia ya kuwabagua waathirika Dialogue: 0,0:12:25.44,0:12:28.51,Default,,0000,0000,0000,,kama vichwa vibaya vya habari, Dialogue: 0,0:12:28.51,0:12:31.80,Default,,0000,0000,0000,,wanaojitakia maovu, watu walioharibika. Dialogue: 0,0:12:31.80,0:12:34.81,Default,,0000,0000,0000,,Swali hilo, "Kwa nini haondoki?" Dialogue: 0,0:12:34.81,0:12:40.44,Default,,0000,0000,0000,,kwa wengine ni kama kusema, "Ni makosa yake kuendela kukaa hapo," Dialogue: 0,0:12:40.44,0:12:43.77,Default,,0000,0000,0000,,kana kwamba waathirika huchagua kusudi kupenda wanaume Dialogue: 0,0:12:43.77,0:12:46.40,Default,,0000,0000,0000,,walio na lengo la kutumaliza. Dialogue: 0,0:12:46.40,0:12:48.90,Default,,0000,0000,0000,,Lakini tangu niandike kitabu "Crazy Love," Dialogue: 0,0:12:48.90,0:12:52.42,Default,,0000,0000,0000,,nimesikia mamia ya hadithi kutoka kwa wanaume na wanawake Dialogue: 0,0:12:52.42,0:12:54.87,Default,,0000,0000,0000,,ambao pia waliondoka, Dialogue: 0,0:12:54.87,0:12:59.25,Default,,0000,0000,0000,,waliojifunza somo muhimu la maisha kutokana na yale yaliyotokea, Dialogue: 0,0:12:59.25,0:13:03.46,Default,,0000,0000,0000,,na waliojenga maisha yao tena--maisha yenye furaha Dialogue: 0,0:13:03.46,0:13:05.80,Default,,0000,0000,0000,,kama wafanyakazi, wake na kina mama, Dialogue: 0,0:13:05.80,0:13:10.48,Default,,0000,0000,0000,,maisha yasiyo na unyanyasaji, kama yangu. Dialogue: 0,0:13:10.48,0:13:14.51,Default,,0000,0000,0000,,Kwa sababu inaonekana kwamba mimi nilikuwa mwathirika halisi wa unyanyasaji majumbani. Dialogue: 0,0:13:14.51,0:13:17.95,Default,,0000,0000,0000,,na msalimika wa unyanyasaji wa majumbani. Dialogue: 0,0:13:17.95,0:13:21.98,Default,,0000,0000,0000,,Niliolewa na mtu mwema na mpole, Dialogue: 0,0:13:21.98,0:13:24.31,Default,,0000,0000,0000,,na pamoja tuna watoto watatu. Dialogue: 0,0:13:24.31,0:13:27.72,Default,,0000,0000,0000,,Nina yule mbwa wangu mweusi, na nina lile gari ndogo. Dialogue: 0,0:13:27.72,0:13:31.18,Default,,0000,0000,0000,,Kile sitawahi kuwa nacho tena, Dialogue: 0,0:13:31.18,0:13:34.14,Default,,0000,0000,0000,,milele, Dialogue: 0,0:13:34.14,0:13:36.26,Default,,0000,0000,0000,,ni bunduki iliyojaa risasi iliyoelekezwa kichwani mwangu Dialogue: 0,0:13:36.26,0:13:39.91,Default,,0000,0000,0000,,na mtu anayesema eti ananipenda. Dialogue: 0,0:13:39.91,0:13:42.54,Default,,0000,0000,0000,,Wakati huu, labda unafikiria, Dialogue: 0,0:13:42.54,0:13:44.44,Default,,0000,0000,0000,,"Hili ni jambo la kushangaza," Dialogue: 0,0:13:44.44,0:13:47.57,Default,,0000,0000,0000,,ama, "Kwa nini alikuwa mjinga hivi," Dialogue: 0,0:13:47.57,0:13:53.58,Default,,0000,0000,0000,,lakini muda huu wote, nimekuwa haswa nikiongea juu yako. Dialogue: 0,0:13:53.58,0:13:57.09,Default,,0000,0000,0000,,Nakuhakikishia kuna watu kadhaa Dialogue: 0,0:13:57.09,0:13:58.84,Default,,0000,0000,0000,,wanaonisikiliza saa hii Dialogue: 0,0:13:58.84,0:14:01.85,Default,,0000,0000,0000,,ambao wananyanyaswa Dialogue: 0,0:14:01.85,0:14:04.36,Default,,0000,0000,0000,,au ambao walinyanyaswa wakiwa watoto Dialogue: 0,0:14:04.36,0:14:07.73,Default,,0000,0000,0000,,au walio wanyanyasaji wenyewe. Dialogue: 0,0:14:07.73,0:14:09.67,Default,,0000,0000,0000,,unyanyasaji unaweza kuwa unamwathiri binti yako, Dialogue: 0,0:14:09.67,0:14:14.96,Default,,0000,0000,0000,,dadako, rafiki yako wa karibu wakati huu. Dialogue: 0,0:14:14.96,0:14:18.41,Default,,0000,0000,0000,,Niliweza kumaliza hadithi yangu wazimu ya mapenzi Dialogue: 0,0:14:18.41,0:14:20.61,Default,,0000,0000,0000,,kwa kuvunja ukimya. Dialogue: 0,0:14:20.61,0:14:23.12,Default,,0000,0000,0000,,Bado naendelea kuvunja ukimya leo. Dialogue: 0,0:14:23.12,0:14:26.94,Default,,0000,0000,0000,,Ni njia yangu ya kusaidia waathirika wengine, Dialogue: 0,0:14:26.94,0:14:30.31,Default,,0000,0000,0000,,na ni ombi langu la mwisho kwenu. Dialogue: 0,0:14:30.31,0:14:33.14,Default,,0000,0000,0000,,Ongeeni kuhusu mliyosikia hapa. Dialogue: 0,0:14:33.14,0:14:36.47,Default,,0000,0000,0000,,Unyanyasaji hushamiri tu katika ukimya. Dialogue: 0,0:14:36.47,0:14:40.17,Default,,0000,0000,0000,,Una nguvu ya kumaliza unyanyasaji majumbani Dialogue: 0,0:14:40.17,0:14:43.68,Default,,0000,0000,0000,,kwa kuongea kuhusu unyanyasaji. Dialogue: 0,0:14:43.68,0:14:46.75,Default,,0000,0000,0000,,Sisi waathirika tunahitaji kila mtu. Dialogue: 0,0:14:46.75,0:14:50.82,Default,,0000,0000,0000,,Tunawahitaji nyote kuelewa Dialogue: 0,0:14:50.82,0:14:54.60,Default,,0000,0000,0000,,siri za unyanyasaji majumbani. Dialogue: 0,0:14:54.60,0:14:57.59,Default,,0000,0000,0000,,Mulikieni mwanga unyanyasaji kwa kuuongelea Dialogue: 0,0:14:57.59,0:14:59.71,Default,,0000,0000,0000,,mkiwa na watoto wenu, wafanyakazi wenzenu, Dialogue: 0,0:14:59.71,0:15:01.65,Default,,0000,0000,0000,,marafiki zenu na familia. Dialogue: 0,0:15:01.65,0:15:05.10,Default,,0000,0000,0000,,Ongeleeni waliosalimika kama watu wema na wanaopendeka Dialogue: 0,0:15:05.10,0:15:07.91,Default,,0000,0000,0000,,walio na maisha kamili kwenye siku za usoni Dialogue: 0,0:15:07.91,0:15:11.39,Default,,0000,0000,0000,,Eleweni ishara za mapema za tuhuma Dialogue: 0,0:15:11.39,0:15:14.23,Default,,0000,0000,0000,,na muingilie kati kistadi Dialogue: 0,0:15:14.23,0:15:18.39,Default,,0000,0000,0000,,malizeni na muonyeshe waathirika njia safi ya kuiepuka. Dialogue: 0,0:15:18.39,0:15:22.38,Default,,0000,0000,0000,,Pamoja tunaweza kufanya vitanda vyetu, Dialogue: 0,0:15:22.38,0:15:26.00,Default,,0000,0000,0000,,meza zetu za mlo na familia zetu Dialogue: 0,0:15:26.00,0:15:29.26,Default,,0000,0000,0000,,mahali pa amani zinavyopaswa kuwa Dialogue: 0,0:15:29.26,0:15:31.23,Default,,0000,0000,0000,,Asanteni. Dialogue: 0,0:15:31.23,0:15:38.94,Default,,0000,0000,0000,,(Mahali)