0:00:00.681,0:00:03.969 Leo niko hapa kuongea kuhusu swala nyeti, 0:00:03.969,0:00:07.667 ambalo lina jibu tatanishi. 0:00:07.667,0:00:11.269 Swala langu ni zile siri za ugomvi nyumbani, 0:00:11.269,0:00:13.603 na swali nitakalokabiliana nalo 0:00:13.603,0:00:17.684 ni lile swali moja kila mmoja huliuliza kila mara: 0:00:17.684,0:00:19.296 Kwa nini muathirika hubakia? 0:00:19.296,0:00:23.292 Kwa nini mtu yeyote abaki na mume ampigaye? 0:00:23.292,0:00:26.269 Mie si daktari wa akili, mfanyakazi wa ustawi wa jamii 0:00:26.269,0:00:28.604 au mtaalam wa ugomvi wa nyumbani. 0:00:28.604,0:00:31.803 Mimi ni mwanamke mwenye hadithi ya kusimulia. 0:00:31.803,0:00:36.316 Nilikuwa na umri wa miaka ishirini na miwili. Nilikuwa nimehitimu tu kutoka chuo cha Harvard. 0:00:36.316,0:00:38.788 Nilikuwa nimehamia mjini New York kwa ajili ya kazi yangu ya kwanza 0:00:38.788,0:00:42.084 kama mwandishi na mhariri wa gazeti la Seventeen. 0:00:42.084,0:00:44.324 Nilikuwa na nyumba yangu ya kwanza, 0:00:44.324,0:00:47.524 kadi yangu ya kwanza ya American Express, 0:00:47.524,0:00:50.552 na nilikuwa na siri moja kubwa sana. 0:00:50.552,0:00:54.251 Siri yangu ilikuwa kwamba kulikuwa na bunduki 0:00:54.251,0:00:57.689 iliyojaa risasi iliyoelekezwa kichwani mwangu 0:00:57.689,0:01:00.252 na mwanamme niliyefikiria alikuwa mpenzi wangu, 0:01:00.252,0:01:03.737 mara kadhaa. 0:01:03.737,0:01:07.297 Mwanamme huyu niliyempenda kuliko yeyote duniani 0:01:07.297,0:01:11.376 alielekeza bunduki kichwani mwangu na kutishia kuniua 0:01:11.376,0:01:14.561 mara nyingi kuliko zile ningeweza kukumbuka. 0:01:14.561,0:01:17.304 Niko hapa kuwapa hadithi ya upendo wa kupindukia, 0:01:17.304,0:01:20.488 mtego wa kisaikolojia uliofichwa kama mapenzi, 0:01:20.488,0:01:23.340 ambao mamilioni ya wanawake na hata wanaume wengine 0:01:23.340,0:01:25.721 hutumbukia kila mwaka. 0:01:25.721,0:01:28.470 Inaweza hata kuwa hadithi yako. 0:01:28.470,0:01:31.513 Sionekani kama mtu niliyenusurika na ugomvi katika mahusiano. 0:01:31.513,0:01:33.819 Nina shahada ya sanaa katika Kiigereza kutoka chuo cha Harvard, 0:01:33.819,0:01:36.181 na shahada ya juu katika mauzo kutoka kwa chuo cha biashara cha Wharton. 0:01:36.181,0:01:39.473 Nimetumia muda mrefu maishani nikifanya kazi kwenye kampuni bora duniani 0:01:39.473,0:01:43.745 zikiwemo Johnson & Johnson, Leo Burnett na The Washington Post. 0:01:43.745,0:01:47.541 Nimeolewa takriban miaka ishirini kwa mme wangu wa pili 0:01:47.541,0:01:50.330 na tuna wana watatu pamoja 0:01:50.330,0:01:54.559 Mbwa wangu ni mweusi, na mie huendesha gari ndogo la Honda Odyssey. 0:01:54.559,0:01:57.039 (Kicheko) 0:01:57.039,0:01:59.758 Kwa hivyo ujumbe wangu wa kwanza kwenu ni kwamba ugomvi wa nyumbani 0:01:59.758,0:02:02.126 humtokea yeyote-- 0:02:02.126,0:02:06.302 kila jamii,dini, kila kipato na ngazi ya kimasomo. 0:02:06.302,0:02:08.241 Iko kila mahali. 0:02:08.241,0:02:10.761 Na ujumbe wangu wa pili ni kwamba kila mtu hufikiri 0:02:10.761,0:02:12.879 ugomvi wa nyumbani huwaathiri wanawake, 0:02:12.879,0:02:15.147 ati ni swala la wanawake. 0:02:15.147,0:02:17.366 Si sahihi. 0:02:17.366,0:02:21.478 Zaidi ya asili mia 85 ya wanyanyasaji ni wanaume, na ugomvi wa nyumbani 0:02:21.478,0:02:27.396 hutokea haswa katika mahusiano ya undani, ya kutegemeana na yale ya muda mrefu, 0:02:27.396,0:02:29.565 yaani, katika familia, 0:02:29.565,0:02:33.430 mahali tusipotaka au kutarajia kupata ugomvi, 0:02:33.430,0:02:37.708 ndio sababu tuhuma za kinyumbani ni tatanishi hivi. 0:02:37.708,0:02:41.259 Ningekuambia kwamba ningekuwa mtu wa mwisho duniani 0:02:41.259,0:02:43.831 kukaa na mwanaume anayenipiga, 0:02:43.831,0:02:47.238 lakini kusema kweli nilikuwa mwathirika kwa sababu ya umri wangu. 0:02:47.238,0:02:50.523 Nilikuwa mwenye umri wa miaka ishirini na mbili na Marekani, 0:02:50.523,0:02:54.372 wanawake wenye umri kati ya miaka kumi na sita hadi ishirini na nne wana uwezekano wa mara tatu zaidi 0:02:54.372,0:02:57.133 kuwa waathirika wa ugomvi wa nyumbani 0:02:57.133,0:02:59.948 ikilinganishwa na wanawake wa umri mwingine, 0:02:59.948,0:03:03.251 vilevile zaidi ya wanawake mia tano na wasichana wa umri huu 0:03:03.251,0:03:06.822 huuawa kila mwaka na wapenzi wanyanyasaji, 0:03:06.822,0:03:11.455 wapenzi, na waume zao Marekani. 0:03:11.455,0:03:14.515 Nilikuwa muathirika kwa sababu sikujua chochote 0:03:14.515,0:03:19.100 kuhusu ugomvi wa nyumbani, maonyo yake ama mifano yake. 0:03:19.100,0:03:24.165 Nilikutana na Conor usiku mmoja wenye baridi na mvua, mwezi wa Januari. 0:03:24.165,0:03:27.128 Alikaa kando yangu kwenye treni katika mji wa New York, 0:03:27.128,0:03:29.267 na alianza kuniongelesha. 0:03:29.267,0:03:31.135 Aliniambia mambo mawili. 0:03:31.135,0:03:34.937 La kwanza kuwa, yeye pia, alikuwa amehitimu kutoka kwa kati ya zile shule bora zaidi Marekani, 0:03:34.937,0:03:39.292 na kwamba alifanya kazi kwenye benki moja ya kuvutia sana huko Wall Street. 0:03:39.292,0:03:42.952 Lakini kile kilichonivutia zaidi siku hiyo 0:03:42.952,0:03:46.240 ni kuwa alikuwa mwerevu na mcheshi 0:03:46.240,0:03:47.640 na alionekana kuwa kijana wa mashambani. 0:03:47.640,0:03:49.987 Alikuwa na haya mashavu makubwa, haya mashavu makubwa ya waridi 0:03:49.987,0:03:51.672 na hii nywele za rangi kama ya ngano, 0:03:51.672,0:03:54.959 na alionekana kuwa mwema sana. 0:03:54.959,0:03:58.743 Jambo moja la busara Conor alilofanya, kutoka mwanzoni, 0:03:58.743,0:04:04.317 lilikuwa kufanya kana kwamba nilikuwa mwenye ushawishi mkubwa katika huo uhusiano. 0:04:04.317,0:04:06.518 Alifanya hivi haswa hapo mwanzo 0:04:06.518,0:04:09.384 kwa kunihusudu. 0:04:09.384,0:04:12.670 Tukaanza kutoka pamoja, na alipenda kila kitu kunihusu, 0:04:12.670,0:04:14.354 ati nilikuwa mwerevu, ati nilisomea chuo cha Harvard, 0:04:14.354,0:04:17.384 ati nilikuwa mwenye shauku kusaidia wasichana wadogo, na kazi yangu. 0:04:17.384,0:04:19.915 Alitaka kujua kila kitu kuhusu familia yangu 0:04:19.915,0:04:22.531 na utoto wangu na matarajio na ndoto zangu. 0:04:22.531,0:04:26.165 Conor alikuwa na imani nami, kama mwandishi na mwanamke, 0:04:26.165,0:04:29.844 kwa njia ambayo yeyote mwengine alikuwa hajawahi. 0:04:29.844,0:04:34.169 Na alileta uaminifu kati yetu 0:04:34.169,0:04:36.689 kwa kunieleza siri yake, 0:04:36.689,0:04:41.169 ambayo ilikuwa, alipokuwa mvulana mdogo sana akiwa na umri wa miaka minne 0:04:41.169,0:04:44.080 alipigwa vibaya sana mara kwa mara 0:04:44.080,0:04:45.766 na babake wa kambo, 0:04:45.766,0:04:49.706 na unyanyasaji ulizidi kuwa mbaya zaidi hadi ikambidi aache shule akiwa daraja la nane, 0:04:49.706,0:04:52.325 ingawa alikuwa mwerevu sana, 0:04:52.325,0:04:55.581 na kwamba alitumia takriban miaka ishirini kujenga maisha yake upya. 0:04:55.581,0:04:58.737 Ndiyo sababu hiyo shahada yake kutoka zile shule bora zaidi Marekani, 0:04:58.737,0:05:01.550 na kazi yake Wall Street na maisha yake mazuri siku za usoni 0:05:01.550,0:05:04.121 zilikuwa za umuhimu mkubwa sana kwake. 0:05:04.121,0:05:06.265 Kama ungeniuliza 0:05:06.265,0:05:11.629 kama huyu mwanamme mwerevu, mcheshi na mwenye kujali aliyenipenda sana 0:05:11.629,0:05:16.012 angekuja kuniamulia kama ningejipamba au la, 0:05:16.012,0:05:18.062 ufupi wa sketi zangu, 0:05:18.062,0:05:19.992 mahali ningeishi, kazi gani ningefanya, 0:05:19.992,0:05:23.356 marafiki zangu wangekuwa wepi na pale ningekulia Krisimasi 0:05:23.356,0:05:25.304 ningekucheka, 0:05:25.304,0:05:28.352 kwa sababu hakukuwa na ushahidi wowote wa tuhuma au uthibiti 0:05:28.352,0:05:31.836 au hasira kutoka kwa Conor hapo mwanzoni. 0:05:31.836,0:05:34.961 Sikujua kwamba daraja la kwanza 0:05:34.961,0:05:37.336 katika uhusiano wowote wenye ugomvi 0:05:37.336,0:05:40.988 ni kumvuta na kumpumbaza mwathirika 0:05:40.988,0:05:45.748 Pia sikujua kuwa daraja ya pili ni kumtenga mwathirika. 0:05:45.748,0:05:49.902 Conor hakuja nyumbani siku moja na kutangaza, 0:05:49.902,0:05:53.036 "Unajua huu uhusiano wetu kama wa Romeo na Julieti umekuwa mtamu, 0:05:53.036,0:05:55.041 lakini nataka kwenda katika hatua inayofuata 0:05:55.041,0:05:59.220 ambapo nitakutenga na kukunyanyasa" - (Kicheko) - 0:05:59.220,0:06:00.575 "kwa hivyo nataka kukuhamisha kutoka nyumba hii 0:06:00.575,0:06:02.216 ambapo majirani wanawezakusikia ukipiga mayowe 0:06:02.216,0:06:04.689 na kukupeleka nje ya mji huu ambapo una marafiki na familia 0:06:04.689,0:06:07.995 na wafanyakazi wenzako wanaoweza kuona hiyo michubuko." 0:06:07.995,0:06:12.216 Badala yake, Conor alikuja nyumbani jioni ya Ijumaa moja 0:06:12.216,0:06:14.947 na akaniambia kuwa alikuwa ameacha kazi siku hiyo, 0:06:14.947,0:06:17.412 kazi ya ndoto zake, 0:06:17.412,0:06:21.553 na akasema kwamba alikuwa ameacha kazi hiyo kwa sababu yangu, 0:06:21.553,0:06:24.731 kwa sababu nilimfanya ahisi usalama na kupendwa 0:06:24.731,0:06:27.854 ati hakuhitaji tena kujithibitisha huko Wall Street, 0:06:27.854,0:06:30.369 na alitaka tu kutoka mjini 0:06:30.369,0:06:33.347 na kukaa mbali na familia yake iliyomnyanyasa. 0:06:33.347,0:06:36.469 na kuhamia mji mdogo wa New England 0:06:36.469,0:06:40.042 ambapo angeweza kuanza upya maisha yake nikiwa kando yake. 0:06:40.042,0:06:43.908 Sikutaka kamwe kuhama kutoka New York, 0:06:43.908,0:06:47.515 na kuacha kazi ya ndoto zangu, 0:06:47.515,0:06:50.098 lakini nilifikiria mtu hujitoa muhanga kwa mpenzi wake, 0:06:50.098,0:06:53.562 kwa hivyo nikakubali na nikaacha kazi yangu, 0:06:53.562,0:06:56.193 na Conor na mimi tukaondoka Manhattan pamoja. 0:06:56.193,0:07:00.559 Sikuwai kufikiria kwamba penzi nililokuwa nalo halikuwa la kawaida, 0:07:00.559,0:07:04.191 na kwamba nilikuwa nikitembea bila habari ndani ya 0:07:04.191,0:07:09.171 mtego mzuri wa kimwili, kifedha na kiakili 0:07:09.171,0:07:11.491 Daraja ya pili katika ugomvi wa kimahusiano 0:07:11.491,0:07:15.773 ni kuleta tishio la vurugu 0:07:15.773,0:07:17.972 na kuangalia vile linavyomgusa. 0:07:17.972,0:07:20.681 Na hapa ndipo bunduki zinapoingia. 0:07:20.681,0:07:23.599 Muda tu tulipohamia New England--unajua, 0:07:23.599,0:07:26.337 mahali Connor aliposema pangemfanya ajisikie salama-- 0:07:26.337,0:07:28.753 alinunua bunduki tatu. 0:07:28.753,0:07:32.193 Aliweka moja garini. 0:07:32.193,0:07:34.849 Aliweka moja chini ya mto kitandani mwetu, 0:07:34.849,0:07:38.011 na ya tatu alitembea nayo mfukoni nyakati zote. 0:07:38.011,0:07:40.329 Na alisema alihitaji bunduki hizo 0:07:40.329,0:07:43.125 kwa sababu ya uchungu aliopitia akiwa mchanga. 0:07:43.125,0:07:45.609 Alizihitaji kujisikia salama. 0:07:45.609,0:07:48.521 Lakini bunduki hizo zilikuwa ujumbe kwangu, 0:07:48.521,0:07:51.215 na ingawa hakuwai kuninyoshea mkono, 0:07:51.215,0:07:57.021 maisha yangu tayari yalikuwa hatarini kila dakika ya kila siku. 0:07:57.021,0:08:00.594 Kwanza Conor alinishambulia 0:08:00.594,0:08:03.419 siku tano kabla ya harusi yetu. 0:08:03.419,0:08:07.611 Ilikuwa saa moja asubuhi na bado nilikuwa nimevalia vazi la kulala 0:08:07.611,0:08:11.851 Nilikuwa nafanya kazi kweny kompyuta yangu nikijaribu kumaliza kazi fulani ya uandishi, 0:08:11.851,0:08:13.665 na nilikuwa nimekasirika, 0:08:13.665,0:08:16.752 na Conor akatumia hasira zangu kama kisingizio 0:08:16.752,0:08:19.903 kunikaba koo 0:08:19.903,0:08:23.723 na kuikaza hadi sikuweza kupumua au kupiga kelele, 0:08:23.723,0:08:25.547 na alitumia mkazo huo 0:08:25.547,0:08:29.973 kugonga kichwa changu mara kadhaa kwenye ukuta. 0:08:29.973,0:08:35.291 Siku tano baadaye, ile michubuko kumi shingoni mwangu ilipotea 0:08:35.291,0:08:37.766 na nikavaa nguo ya mama yangu ya harusi, 0:08:37.766,0:08:40.083 na nikafunga ndoa naye. 0:08:40.083,0:08:42.364 Licha ya yaliyotokea, 0:08:42.364,0:08:45.883 nilikuwa na hakika tungeishi maisha ya raha milele, 0:08:45.883,0:08:49.964 kwa sababu nilimpenda, na alinipenda sana. 0:08:49.964,0:08:53.336 Na aliniomba msamaha. 0:08:53.336,0:08:56.509 Alikuwa amechoshwa sana na mipango ya harusi yetu 0:08:56.509,0:08:58.706 na kwa kuwa kitu kimoja na mimi. 0:08:58.706,0:09:00.427 Halikuwa jambo la kawaida 0:09:00.427,0:09:04.023 na asingeniumiza tena. 0:09:04.023,0:09:06.603 Ilitokea mara mbili katika fungate. 0:09:06.603,0:09:09.690 Mara ya kwanza, nilikuwa naendesha gari kutafuta ufukwe wa siri 0:09:09.690,0:09:12.392 na nikapotea, 0:09:12.392,0:09:15.362 na akanipiga ngumi nzito kwenye upande wa kichwa changu 0:09:15.362,0:09:17.506 hata ule upande mwengine wa kichwa changu ukagonga 0:09:17.506,0:09:19.913 dirisha lililo kando ya dereva mara kadhaa. 0:09:19.913,0:09:23.279 Alafu tena siku chache baadaye, tukielekea nyumbani baada ya likizo ya harusi, 0:09:23.279,0:09:25.562 alikasirishwa na trafiki, 0:09:25.562,0:09:28.994 na akarusha Big Mac baridi usoni mwangu. 0:09:28.994,0:09:31.602 Conor aliendelea kunipiga mara moja au mbili kwa wiki 0:09:31.602,0:09:35.019 kwa miaka miwili na nusu ya ndoa yetu. 0:09:35.019,0:09:38.144 Nilifanya makosa kufikiria nilikuwa wa kipekee 0:09:38.144,0:09:40.787 na peke yangu katika hali hii. 0:09:40.787,0:09:42.978 Mmoja kati ya wanawake watatu wakiAmerika 0:09:42.978,0:09:47.130 hupitia ugomvi wa nyumbani ama kufuatwa fuatwa wakati mmoja maishani mwake, 0:09:47.130,0:09:50.771 na CDC inaripoti kwamba watoto milioni kumi na tano 0:09:50.771,0:09:54.181 wananyanyaswa kila mwaka, milioni kumi na tano. 0:09:54.181,0:09:58.554 Hivyo basi, nilikuwa kwenye ushirika mzuri sana. 0:09:58.554,0:10:00.970 Kurudia swali langu: 0:10:00.970,0:10:03.465 Kwa nini nilibaki? 0:10:03.465,0:10:06.203 Jibu lenyewe ni rahisi. 0:10:06.203,0:10:08.891 Sikujua alikuwa akininyanyasa. 0:10:08.891,0:10:12.739 Hata ingawa alielekeza bunduki zilizo na risasi kichwani mwangu, 0:10:12.739,0:10:14.962 akanisukuma ngazini, 0:10:14.962,0:10:16.343 akatishia kuua mbwa wetu, 0:10:16.343,0:10:20.266 akatoa ufunguo wa gari nikiendesha barabarani, 0:10:20.266,0:10:22.783 akamwaga maganda ya kahawa kichwani mwangu 0:10:22.783,0:10:25.099 nikijitayarisha kwa mahojiano ya kazi, 0:10:25.099,0:10:29.469 SIkuwai hata mara moja kujihisi kuwa mke anayenyanyaswa. 0:10:29.469,0:10:33.046 Badala yake, nilikuwa mwanamke mwenye nguvu 0:10:33.046,0:10:35.298 alimpenda sana mwanaume aliyekuwa na shida, 0:10:35.298,0:10:37.355 na nilikuwa mtu wa pekee duniani 0:10:37.355,0:10:40.795 ambaye angeweza kumsaidia Conor kukabiliana na mashetani yake. 0:10:40.795,0:10:44.506 Swali lingine kila mtu huuliza ni, 0:10:44.506,0:10:46.923 kwa nini hatoki tu? 0:10:46.923,0:10:50.874 Kwa nini sikuondoka? Ningeweza kuondoka wakati wowote. 0:10:50.874,0:10:55.586 Kwangu mimi, hili ndilo swali chungu na la kuhuzunisha zaidi ambalo watu huniuliza, 0:10:55.586,0:10:58.677 kwa sababu sisi waathiriwa tunajua jambo nyinyi msilojua: 0:10:58.677,0:11:03.070 Ni jambo la hatari sana kumtoroka mnyanyasaji. 0:11:03.070,0:11:06.389 Kwa sababu daraja ya mwisho katika tuhuma za kinyumbani 0:11:06.389,0:11:09.284 ni kumuua. 0:11:09.284,0:11:11.825 Zaidi ya asilimia sabini ya vifo vinavyosababishwa na tuhuma za kinyumbani 0:11:11.825,0:11:15.893 hutokea baada ya mwathiriwa kukatiza uhusiano huo, 0:11:15.893,0:11:17.786 baada ya kutoka, 0:11:17.786,0:11:21.037 kwa sababu wakati huo mnyanyasaji hana chochote cha kupoteza. 0:11:21.037,0:11:24.128 Matokeo mengine ni pamoja na kufuatwa fuatwa, 0:11:24.128,0:11:27.080 hata baada ya mnyanyasaji kuoa tena; 0:11:27.080,0:11:29.235 unyimaji wa hela; 0:11:29.235,0:11:31.624 na uingiliaji wa mfumo wa mahakama za kifamilia 0:11:31.624,0:11:34.447 ili kumtia wasiwasi mwathirika na wanawe, 0:11:34.447,0:11:39.373 ambao mara kwa mara hushurutishwa na majaji wa mahakama za kifamilia 0:11:39.373,0:11:41.342 kuwa na wakati usiosimamiwa 0:11:41.342,0:11:45.013 pamoja na mtu yule aliyemtuhumu mama yao. 0:11:45.013,0:11:49.188 Na bado twauliza, kwa nini hamtoroki tu? 0:11:49.188,0:11:50.942 Niliweza kuondoka, 0:11:50.942,0:11:53.844 kwa sababu ya kipigo kibaya cha mwisho 0:11:53.844,0:11:57.003 kilichofumbua macho yangu. 0:11:57.003,0:12:00.173 Nilitambua kwamba mtu yule niliyempenda sana 0:12:00.173,0:12:03.083 angekuja kuniua kama ningeendelea kumuacha hivi hivi tu. 0:12:03.083,0:12:05.598 Hivyo nikavunja ukimya. 0:12:05.598,0:12:08.428 Nikawaeleza watu wote: 0:12:08.428,0:12:12.213 polisi, jirani zangu, 0:12:12.213,0:12:16.053 marafiki zangu na familia, wageni, 0:12:16.053,0:12:22.907 na niko hapa leo kwa sababu nyote mlinisaidia. 0:12:22.907,0:12:25.445 Tuna tabia ya kuwabagua waathirika 0:12:25.445,0:12:28.507 kama vichwa vibaya vya habari, 0:12:28.507,0:12:31.803 wanaojitakia maovu, watu walioharibika. 0:12:31.803,0:12:34.806 Swali hilo, "Kwa nini haondoki?" 0:12:34.806,0:12:40.442 kwa wengine ni kama kusema, "Ni makosa yake kuendela kukaa hapo," 0:12:40.442,0:12:43.766 kana kwamba waathirika huchagua kusudi kupenda wanaume 0:12:43.766,0:12:46.398 walio na lengo la kutumaliza. 0:12:46.398,0:12:48.902 Lakini tangu niandike kitabu "Crazy Love," 0:12:48.902,0:12:52.425 nimesikia mamia ya hadithi kutoka kwa wanaume na wanawake 0:12:52.425,0:12:54.870 ambao pia waliondoka, 0:12:54.870,0:12:59.250 waliojifunza somo muhimu la maisha kutokana na yale yaliyotokea, 0:12:59.250,0:13:03.463 na waliojenga maisha yao tena--maisha yenye furaha 0:13:03.463,0:13:05.797 kama wafanyakazi, wake na kina mama, 0:13:05.797,0:13:10.478 maisha yasiyo na unyanyasaji, kama yangu. 0:13:10.478,0:13:14.509 Kwa sababu inaonekana kwamba mimi nilikuwa mwathirika halisi wa unyanyasaji majumbani. 0:13:14.509,0:13:17.953 na msalimika wa unyanyasaji wa majumbani. 0:13:17.953,0:13:21.978 Niliolewa na mtu mwema na mpole, 0:13:21.978,0:13:24.314 na pamoja tuna watoto watatu. 0:13:24.314,0:13:27.715 Nina yule mbwa wangu mweusi, na nina lile gari ndogo. 0:13:27.715,0:13:31.181 Kile sitawahi kuwa nacho tena, 0:13:31.181,0:13:34.139 milele, 0:13:34.139,0:13:36.264 ni bunduki iliyojaa risasi iliyoelekezwa kichwani mwangu 0:13:36.264,0:13:39.907 na mtu anayesema eti ananipenda. 0:13:39.907,0:13:42.538 Wakati huu, labda unafikiria, 0:13:42.538,0:13:44.445 "Hili ni jambo la kushangaza," 0:13:44.445,0:13:47.573 ama, "Kwa nini alikuwa mjinga hivi," 0:13:47.573,0:13:53.576 lakini muda huu wote, nimekuwa haswa nikiongea juu yako. 0:13:53.576,0:13:57.093 Nakuhakikishia kuna watu kadhaa 0:13:57.093,0:13:58.835 wanaonisikiliza saa hii 0:13:58.835,0:14:01.847 ambao wananyanyaswa 0:14:01.847,0:14:04.362 au ambao walinyanyaswa wakiwa watoto 0:14:04.362,0:14:07.732 au walio wanyanyasaji wenyewe. 0:14:07.732,0:14:09.669 unyanyasaji unaweza kuwa unamwathiri binti yako, 0:14:09.669,0:14:14.962 dadako, rafiki yako wa karibu wakati huu. 0:14:14.962,0:14:18.406 Niliweza kumaliza hadithi yangu wazimu ya mapenzi 0:14:18.406,0:14:20.607 kwa kuvunja ukimya. 0:14:20.607,0:14:23.122 Bado naendelea kuvunja ukimya leo. 0:14:23.122,0:14:26.938 Ni njia yangu ya kusaidia waathirika wengine, 0:14:26.938,0:14:30.306 na ni ombi langu la mwisho kwenu. 0:14:30.306,0:14:33.138 Ongeeni kuhusu mliyosikia hapa. 0:14:33.138,0:14:36.466 Unyanyasaji hushamiri tu katika ukimya. 0:14:36.466,0:14:40.169 Una nguvu ya kumaliza unyanyasaji majumbani 0:14:40.169,0:14:43.678 kwa kuongea kuhusu unyanyasaji. 0:14:43.678,0:14:46.752 Sisi waathirika tunahitaji kila mtu. 0:14:46.752,0:14:50.825 Tunawahitaji nyote kuelewa 0:14:50.825,0:14:54.603 siri za unyanyasaji majumbani. 0:14:54.603,0:14:57.587 Mulikieni mwanga unyanyasaji kwa kuuongelea 0:14:57.587,0:14:59.714 mkiwa na watoto wenu, wafanyakazi wenzenu, 0:14:59.714,0:15:01.651 marafiki zenu na familia. 0:15:01.651,0:15:05.097 Ongeleeni waliosalimika kama watu wema na wanaopendeka 0:15:05.097,0:15:07.912 walio na maisha kamili kwenye siku za usoni 0:15:07.912,0:15:11.393 Eleweni ishara za mapema za tuhuma 0:15:11.393,0:15:14.226 na muingilie kati kistadi 0:15:14.226,0:15:18.388 malizeni na muonyeshe waathirika njia safi ya kuiepuka. 0:15:18.388,0:15:22.383 Pamoja tunaweza kufanya vitanda vyetu, 0:15:22.383,0:15:26.000 meza zetu za mlo na familia zetu 0:15:26.000,0:15:29.257 mahali pa amani zinavyopaswa kuwa 0:15:29.257,0:15:31.229 Asanteni. 0:15:31.229,0:15:38.937 (Mahali)