Nina swali:
Ni wakina nani hapa walishawahi tambua lini
watakufa?
Natambua.Nilikuwa mvulana mdogo,
na babu yangu alikuwa amefariki,
na nakumbuka siku chache baadaye nikiwa nimelala kitandani wakati wa usiku
nikijaribu kujiuliza kipi kilichotokea.
Ilimaanisha nini kwamba amekufa?
Atakuwa ameenda wapi?
Ilikuwa ni kama shimo limefunguka
na likammeza.
Na swali la kushtua likanijia:
Kama amekufa,inaweza ikanitokea na mimi?
Hilo shimo litafunguka na kunimeza?
Litafunguka chini ya kitanda changu
na kunimeza wakati nimelala?
Katika namna fulani,watoto wote wanakuja gundua kuhusu kifo.
Kinaweza kutokea katika njia nyingi tofauti,
na kawaida huja kwa hatua.
Mawazo yetu kuhusu kifo yanakua kadiri tunavyozidi kuzeeka.
Na kama ukifika katika kona za giza
za kumbukumbu yako,
utakumbuka kitu fulani kama nilichohisi mimi
wakati babu yangu alipofariki na nilipogundua
inaweza kunitokea na mimi pia,
hiyo maana iliyopo nyuma ya haya yote
ubatili unangojea.
Na haya maendeleo katika utoto
yanaakisi maendeleo ya aina yetu.
Kama kulivyokuwa na alama katika maendeleo yako
kama mtoto wakati utambuzi wako wa nafsi na muda
ulivyokuja kuchanganyika vya kutosha
kiasi cha wewe kutambua haitaishi milele,
kwa hiyo katika hali fulani ya mabadiliko yetu,
baadhi ya utambuzi wa binadamu wa nafsi na muda
ukaja jichanganya vya kutosha.
kwa wao kuja kuwa binadamu wa kwanza kutambua,
"naelekea kufa"
Kama unapenda,laana yetu.
Ni gharama tunayolipa kwa kuwa werevu wajinga.
Tunatakiwa kuishi katika maarifa
hicho ni kitu kibaya kinachoweza kutokea
siku moja kwa uhakika,
mwisho wa miradi yetu,
matumaini yetu,ndoto zetu,katika dunia ya kila mmoja.
Tunaishi katika kivuli cha
kuwaza mwisho wa dunia.
Na inaogopesha.Na kutisha.
Kwa hiyo tunatafuta njia ya kujinasua.
Kwa upande wangu,nilipokuwa na miaka mitano,
hii ilimaanisha kumuuliza mama yangu.
Sasa nilipoanza kuuliza
kipi kinatokea tukifarikia,
watu wazima waliokuwa wananizunguka wakati huo
walijibu katika mchanganyiko wa kiingereza na ulio mgumu kuelewa.
na mkristo mwenye nusu moyo,
na kipande cha sentensi ninachosikia mara nyingi
ilikuwa kwamba babu kwa sasa
"yuko juu akituangalia sisi"
na kama nikifa pia,
na mimi pia nitaenda juu,
hiki kinafanya kifo kionekane kama
lifti isiyoonekana kwa macho lakini inafanya kazi.
Lakini hii haikuonekana kama ina ukweli sana.
Nilizoea kuangalia habari za watoto wakati huo,
na huu ulikuwa wakati wa kujifunza kuhusu unajimu.
Kulikuwa na roketi zinakwenda juu angani,
zinakwenda huko.
Hamna mnajimu ambaye alirudi
na akasema kwamba amekutana na babu yangu
au mtu yoyote aliyekufa.
Lakini nilikuwa naogopa,
wazo la kupanda lifti ya kifo
kumuona babu yangu
naona ni bora zaidi kuliko kwenda kumezwa
wakati nimelala.
na nikaamini,
pamoja haikuleta maana sana.
Na hili wazo nililokuwa nalo
wakati nikiwa mtoto,nimekuwa nalo kwa muda sana
hadi nikiwa mtu mzima,
ni zao ambalo wanasaikolojia wanaita
upendeleo.
Sasa upendeleo ni njia ambayo
hufanya vitu kimakosa,
njia ambazo tunakosea kukokotoa,kutoa maamuzi,
kuharibu uhalisia,au kuona tunachotaka kuona,
na upendeleo ninaoongelea
unafanya kazi kama hivi:
Kumfata mtu na ukweli
kwamba atakufa
na wataamini kuhusu hadithi yoyote
ambayo inawaambia sio kweli
na badala yake,wanaweza kuishi milele,
hata kama inamaanisha watapanda lifti.
Sasa tunaweza kuona huu ni upendeleo kupita wote.
Imeelezew katika zaidi ya masomo 400
ya undani.
masomo haya ni ya werevu,lakini ni rahisi.
Yanafanya kazi kama hivi.
Unachukua makundi mawili ya watu
ambao wako sawasawa katika kila kitu,
na unawaambia kundi moja kwamba watafariki
wengine huwaambii,unalinganisha tabia zao.
Kwa hiyo unaangalia jinsi gani unafanya tabia zao kuwa
watu wanapoanza kugundua kuhusu vifo vyao.
Na kila wakati,unapata matokeo yaleyale:
Watu ambao tayari washatambua kuhusu vifo vyao
wako tayari kuamini hadithi
ambazo zinawaambia wanaweza kukwepa kifo
na kuishi milele.
Huu ni mfano:Tafiti moja ya hivi karibuni
ilichukua makundi mawili ya wapagani,
hao ni watu ambao hawana maamuzi
katika kuamini dini.
Sasa,kundi moja liliambiwa kufikiria kuhusu kufa.
Kundi lingine likaambiwa kufikiria kuhusu
kuwa mpweke.
Waliulizwa tena kuhusu imani zao za kidini.
Wale walioambiwa kufikiria kuhusu kifo
walikuwa wakielezea mara mbili zaidi hisia zao
kuhusu Mungu na Yesu.
Mara mbili zaidi.
Pamoja na kwamba wote walikuwa wapagani.
Lakini weka uoga wa kifo ndani yao,
watakimbila kwa Yesu.
Sasa,hii inaonesha kwamba kuwakumbusha watu kuhusu kifo
inawachochea kuamini,bila kujali ukweli,
na sio kwa dini tu,
katika imani yoyote ile
ambayo inaeleza kifo katika njia tofauti tofauti,
haijalishi kama inakuwa maarufu
au kuwa na watoto
au utaifa,
ambayo inasema utaishi siku zote.
Huu ni upendeleo uliotengeneza umbile
na historia y binadamu.
Sasa,fikra iliyopo katika upendeleo huu
katika tafiti 400
inaitwa fikra ya usimamizi wa uoga,
na wazo ni rahisi.Ni hivi.
Tunakuza mawazo yetu kuhusu dunia,
hivyo,hadithi tunazoambia nafsi zetu
kuhusu dunia na sehemu yetu
ili kusaidia kusimamia
hofu ya kifo.
Na hizi hadithi za kifo
zina maelfu ya shuhuda tofauti tofauti,
lakini naamini nyuma ya utofauti uliopo
kuna aina nne za muhimu
ambazo hizi hadithi za vifo zinahusiana.
Na tunaweza kuona zinajirudia
katika historia,na utofauti mdogo sana
kuakisi msamiati wa siku.
Sasa nitatoa muhtasari wa hizi aina nne
kuu za hadithi za kifo,
na ninataka kujaribu kukuonesha maana
ni jinsi gani vinaelezewa kwa kuirudia katika kila utamaduni
au kizazi
kwa kutumia msamiati wa siku.
Sasa,hadithi ya kwanza ni rahisi sana.
Tunataka kukwepa kifo,
na ndoto ya kufanya hicho katika mwili huu
katika hii dunia milele
ni hadithi ya kwanza na rahisi ya kifo,
na inaweza kuonekana isiyo na maana kwa mara ya kwanza,
lakini kiukweli,karibia kila tamaduni katika historia ya binadamu
ilikuwa na mzimu au kiongozi mkongwe
wa kutupa maisha au kurudisha wazee katika ujana
au kitu kinachotuahidi sisi kuendelea mbele
milele.
Wahenga wa Kimisri walikuwa na huo mzimu,
Wahenga wa Babylon,wa India.
Katika historia ya ulaya,tunawaona katika kazi ya wanakemia wa kizamani,
na mpaka leo tunaamini,
tunahdithia hizi hadithi kwa kutumia msamiati
wa sayansi.
Miaka 100 iliyopita,
homoni zilikuwa zimegunduliwa,
na watu wakatumaini kwamba matibabu ya homoni
yatatibu uzee na magonjwa,
na sasa tunaweka matumaini yetu katika kiini shina
uhandisi wa gene,na teknolojia ya nano.
Lakini wazo kwamba sayansi inaweza kuponya kifo
liko sura moja mbele zaidi katika hadithi
ya maajabu ya kuweza kuishi milele,
hadithi ambayo ni ya zamani kama ulivyo ustaarabu.
Lakini kuweka mawazo yote katika kufikiria kutafuta kuishi milele
na kukaa wazima siku zote
ni mkakati wenye hatari sana.
Tukiangalia nyuma katika historia
wale waliotafuta kuishi milele huko nyuma,
kitu kimoja ambacho wote wanacho
ni kwamba wote wameshakufa.
Kwa hiyo tunahitaji mpango wa kutukomboa,na mpango huu mbadala
ni ambao aina ya pili ya kifo inaelezea,
ni kufufuka.
Na hiyo inakuwa ni wazo kwamba mimi ni huu mwili,
Ni kiumbe kamili.
Kinakubali kwamba kitakufa
lakini kinasema,pamoja na hilo,
Ninaweza amka na nikaishi tena.
Katika maneno mengine,naweza fanya kama alichofanya Yesu.
Yesu alikufa,akakaa siku tatu kaburini,
na baada ya hapo akafufuka na kuamka tena.
Na wazo ambalo tunaishi nalo ni kwamba wote sisi tunaweza fufuka na kuishi tena
hata waimani ya Orthodox wanaamini,si kwa wakristo tu
hata Wayahudi na Waislamu.
Lakini tamaa yetu katika kuamini hizi hadithi
imefungamana kiundani sana
kwamba tunaivumbua tena
kwa enzi za kisayansi,
kwa mfano,kwa kutumia wazo la kutumia mazingira ya joto dogo sana ili kuweza kutunza kiumbe kirudi katika uhai
Wazo ni kwamba ukifa,
unaweza kujigandisha mwenyewe,
na baadaye,katika namna fulani teknolojia
imekua vya kutosha,
unaweza kutengenezwa na tena kurudi katika uhai
kwa kufufuka.
Na watu wanaamini Mungu wa nguvu zote
atawafufua na wataishi tena,
na wengine wanaamini wanasayansci wenye nguvu na maarifa watawafufua nao pia.
Lakini kwa wengine,wazo zima ni kuhusu kufufuka,
kwa kutoka nje ya kaburi,
ni kama zile sinema z kutisha za zombies.
Mwili unakuwa mchafu sana,usiotamanika
kwa kuwezesha maisha ya milele,
Watu wanaweka matumaini yao katika hili swala la tatu,
hadithi ya kifo iliyokaa kiroho zaidi,
wazo kwamba tutaiacha miili yetu nyuma
na kuishi kama roho.
Sasa,watu wengi katika dunia
wanaamini wana roho,
na wazo hili ni kuu kwa dini nyingi.
Lakini hata hivyo,katika mfumo wa sasa,
katika utamaduni wake,
wazo la roho ni maarufu sana,
achilia yote hayo tunakuja tena
kuvumbua wazo hili katika nyakati za kidigitali,
kwa mfano
unaweza kuacha mwili wako nyuma
kwa kuwezesha akili yako,uhalisia wako,
wewe halisi,kwenye kompyuta,
na kuishi kama avatar.
Lakini kuna wabishi ambao wanasema
tukiangalia katika ukweli wa sayansi,
hasa sayansi ya mishipa ya fahamu,
inadokeza kwamba,akili yako
uhalisi wako,
vinategemea sana upande fulani
wa mwili wako,ambao ni ubongo.
Na aho wenye wasiwasi wanaweza pata faraja
katika aina ya nne ya hadithi ya kifo,
na huo ni urithi,
wazo kwamba unaweza ishi
mpaka kwenye mwangi unaiacha dunia,
kama mwanajeshi hodari wa Kigiriki Achilles,
aliyetoa sadaka ya maisha yake kwa Troy
ili kupata umaarufu wa kifo.
Na umaarufu ulisambaa
na ni maarufu kama ilivyokuwa zamani,
na katika nyakati hizi za kidigitali,
ni rahisi sana kufanikiwa.
Huitaji kuwa kama mwanajeshi hodari kama Achilles
au kuwa mfalme hodari au shujaa.
Unachohitaji ni mtandao wa intaneti na paka anayefurahisha(Vicheko)
Lakini watu wengi wanapendelea kuacha vile vionekanavyo,
urithi wa kibiolojia--watoto,kwa mfano.
Au wapo hivi,wana imani,kuishi
katika nafasi ya maisha yote,
taifa au familia au kabila,
gene zao.
Lakini tena,wanakuwa na wasiwasi
wana wasiwasi kwamba urithi
kiuhalisia ni kuhusu kifo.
Kwa mfano,Woody Allen alisema,
"Sitaki kuishi katika mioyo ya watu wa nchi yangu.
Nataka kuishi katika nyumba yangu"
Hizo ni
aina nne kuu za hadithi za kifo,
na nimejaribu kuonesha maana
ni jinsi zinasemwa na kila jamii
na utofauti mdogo sana
kutosha fasheni ya siku.
Na ukweli kwamba zinajirudia katika hii njia,
katika mfumo uleule lakini katika aina tofauti za kuamini,
Nadhani,
tunatakiwa kuwa na wasiwasi wa ukweli
katika aina yoyote ya hadithi hizi.
Ukweli kwamba watu wanaamini
mungu mwenye nguvu atawafufua na kuishi tena
na wengine wanaamini wanasayansi wenye nguvu watawafufua na kuishi tena.
inasema kwamba hamna anayeamini hili
au nguvu ya ukweli.
ila,tunaamini hadithi hizi
kwa sababu tunachochewa kuziamini,
na tunachochewa kuziamini
kwa sababu tunaogopa kifo.
Kwa hiyo swali ni,
je,tunapotoshwa kuongoza maisha tuliyonayo
katika njia ya uoga na kupotosha ukweli?
au tunaweza kushinda huu uchochezi?
Mphilosophia wa kigiriki Epicurus
alifikiri tunaweza.
Alihoji kwamba uoga wa kifo ni kitu cha asili,
lakini sio cha mantiki.
"kifo",alisema,"si kitu kwetu,
kwa sababu tuko hapa,kifo hakipo,
na wakati kifo kikiwa hapa,na sisi tunakuwa hatupo"
Mara nyingi kauli hii huwa inanukuliwa,lakini ni vigumu
kuielewa,kiundani zaidi,
kwa sababu kiuhakika wazo hili la kuondoka
ni gumu sana kulifikiria.
Miaka 2000 baadaye,mphilosophia mwingine,
Ludwig Wittgenstein,alisema:
"Kifo sio tukio la maisha:
Hatuishi ili kuzoea kifo.
Akaongeza kwa kusema,
"katika maana hii,maisha hayana mwisho"
Kwa hiyo ilikuwa halisi kwa mimi kama mtoto
kuogopa kumezwa na shimo la kifo,
lakini haikuwa na mantiki,
kwa sababu kumezwa na shimo la kifo
sio kitu ambacho mtu yoyote kati yetu
ataishi na kukutana nacho.
Sasa,kukwepa uchochezi huu sio kitu rahisi kwa sababu
hofu ya kifo imo ndani yetu,
wakati huohuo tunaona uoga huna mantiki,
na tunapoonyesha uoga
katika njia ambazo tunachochewa bila kujitambua,
angalau tunaweza kuanza
kupunguza ule msukumo ulionao
katika maisha yetu.
Sasa,naona inasaidia kuona maisha
ykifanana na kama kitabu:
Kama kilivyozungukwa na kava,
mwanzoni na mwishoni,
kwa hiyo maisha yetu yamezungukwa kwa kuzaliwa na kifo,
na hata kama kitabu kina mipaka mwanzoni na mwishoni,
inaweza jumuisha mazingira ya mbali,
maumbile ya kusisimua,matukio mazuri sana.
Na hata kama kitabu kina mipaka mwanzoni na mwishoni,
wahusika ndani yake
hawajui mwisho wa upeo wa macho.
Wanajua nyakati zinazohusu hadithi zao,
hata kama kitabu kikifungwa.
kwa wahusika katika kitabu
hawaogopi kufika ukurasa wa mwisho.
Long John Silver hakuogopi
kumalizia nakala yako ya "Treasure Island"
na itakuwa na sisi.
Fikiria kitabu cha maisha yako,
inakava,mwanzoni na mwishoni,kuzaliwa kwako na kufa kwako.
Unaweza kujua nyakati,
zinazofanya maisha yako.
Haileti maana kwa wewe kuogopa
kilicho nje ya kava,
kama ni kabla ya kuzaliwa
au baada ya kifo chako.
Na hautakiwi kuwa na wasiwasi kitabu ni kirefu kiasi gani,
au ni cha kichekesho au kinaelezea ukubwa wa kitu.
Kitu kimoja cha msingi
ni kwamba unaifanya iwe hadithi nzuri.
Asante.
(Makofi)