Simulizi za Afrika inayokua zinapata changamoto Karibia miaka 10 iliyopita Niliongea kuhusu Afrika, Afrika yenye matumaini na fursa, Afrika ya wajasiriamali, Afrika tofauti kabisa na Afrika ambayo umezoaea kusikia ya vifo, umaskini na magonjwa. Na kile nilichokiongelea, ikawa sehemu ya kile kinachojulikana sasa kama hadithi ya Afrika inayokua. Nataka niwaambie hadithi mbili kuhusu hii Afrika inayokua. Ya kwanza inaihusisha Rwanda, nchi ambayo imepitia majaribu mengi na dhiki. Na Rwanda ikaamua kuwa kitovu cha teknolojia, au kitovu cha teknolojia kwenye bara la Afrika. Ni nchi yenye milima na ardhi ya eneo lenye vilima, kidogo kama hapa, hivyo ni vigumu sana kupeleka huduma kwa watu. Hivyo Rwanda imesema nini? Ili kuweza kuokoa maisha, itajaribu kutumia ndege zisizo na rubani kupeleka madawa ya kuokoa maisha, chanjo na damu kwa watu katika sehemu zisizo fikika wakishirikiana na kampuni inayoitwa Zipline, pamoja na UPS, na pia Gavi shirika la kimataifa la chanjo. Katika kufanya hivi, itaokoa maisha. Hii ni sehemu ya ubunifu tunayotaka kuona katika Afrika inayokua. Hadithi ya pili inahusiana na jambo ambalo ninauhakika wengi wenu mmeona au mtakumbuka. Mara nyingi, nchi za Afrika zimeteseka na ukame na mafuriko, na inaongezeka zaidi kwasababu ya athari za mabadiliko ya tabia nchi. Wakati haya yanapotokea, kawaida husubiri nchi za kimataifa kuchanga fedha. Unaona picha za watoto wakiwa na nzi kwenye nyuso zao mizoga ya wanyama waliokufa na kadhalika. Sasa nchi hizi, nchi 32, zilikutana pamoja chini ya mwamvuli wa Umoja wa Afrika na kuamua kuunda shirika linaloitwa Africa Risk Capacity. Linafanya nini? Ni wakala wa bima wa hali ya hewa na nchi hizi zinachofanya ni kulipa bima kila mwaka, karibia dola milioni 3 kwa mwaka kutoka kwenye rasilimali zao, ili kwamba endapo wanakumbwa na hali ya ukame mgumu au mafuriko, fedha hizi zitalipwa kuwasaidia ambazo wanaweza kuzitumia kuwatunza wananchi wao badala ya kusubiri msaada kuja. Shirika la African Risk Capacity mwaka jana lilipa dola milioni 26 kwa Mauritania, Senegal na Niger. Hii iliwawezesha kuwatunza watu milioni 1.3 walioathirika na ukame. Waliweza kurudisha tena maisha yao, kununua majani ya n'gombe kulisha watoto mashuleni kuwafanya wananchi wabaki nyumbani badala ya kuhama nje ya eneo. Hivyo hizi ni aina za hadithi za Afrika iliyotayari kuchukua majikumu yake yenyewe, na kutafuta suluhisho kwa matatizo yake yenyewe. Ila simulizi hizo zinapata changamoto sasa kwasababu bara letu halijafanya vema kwa miaka miwili iliyopita. Ilikuwa inakua kwa kiwango cha asilimia 5 kwa mwaka kwa muongo mmoja na nusu uliopita lakini utabiri wa mwaka huu ulikuwa asilimia tatu. Kwanini? kwa mazingira ya ulimwengu yanavyobadilika bei za bidhaa zimeshuka. Uchumi wa nchi nyingi bado unaendeshwa na bidhaa, na hivyo utendaji wake umeteleza Na sasa suala la kujitoa kwa Uingereza haifanyi iwe rahisi Sikujua kama Uingereza ingejitoa na hilo lingekuwa moja ya vitu ambavyo vingeleta kutokuwa na uhakika ulimwenguni kama tulivyo. Hivyo sasa tuna hii hali na ninafikiri ni wakati wakuangalia na kusema ni vitu gani ambavyo nchi za Afrika zilifanya sahihi? Kipi walikosea? Tutajengaje kwenye haya yote na kujifunza ili kwamba tuendeleze Afrika inayokua? Hivyo ngoja niongelee kuhusu mambo sita ninayofikiri tulifanya sahihi. La kwanza ni kusimamia uchumi wa nchi zetu vizuri Miaka ya 80 na 90 ni miongo iliyopotea, wakati Afrika haikuwa ikifanya vizuri, na baadhi yenu mtakumbuka ukurasa wa mbele wa gazeti la "Economist" lililosema, "Bara lililopotea" Ila miaka ya 2000 watunga sera walijifunza kwamba wanahitaji kusimamia mazingira ya uchumi vizuri zaidi, kuhakikisha uthabiti, kushusha mfumuko wa bei kufika tarakimu moja, kushusha nakisi ya bajeti, chini ya asilimia tatu ya Pato la Taifa, wape wawekezaji, wote wa ndani na wageni, aina ya uthabiti ili wawe na imani ya kuwekeza kwenye chumi hizi. Hivyo hiyo ilikuwa namba moja. Mbili, deni. Mwaka 1994, urari wa deni la Pato la taifa wa nchi za Kiafrila ulikuwa asilimia 130, na hawakuwa na nafasi ya fedha nakisi Hawakuweza kutumia rasilimali zao kuwekeza kwenye maendeleo yao kwakuwa walikuwa wanalipa deni kwaweza kuwa na baadhi yenu humu ndani mliofanyakazi kusaidia nchi za Afrika kupata unafuu wa madeni. Hivyo wadai binafsi, wa pande mbalimbali na pande mbili waliunganika na kuamua kuanzisha mpango wa Nchi Fukara zenye Mzigo wa madeni na kutoa unafuu wa madeni. Hivyo unafuu huu wa madeni mwaka 2005 ulifanya urari wa deni kwa Pato la taifa kushuka hadi takriban asilimia 30, na kulikuwa na rasilimali za kutosha kujaribu na kuwekeza upya. Kitu cha tatu kilikuwa makampuni yaliyopata hasara Serikali zilishiriki katika biashara ambazo hawakupaswa kuzifanya. Na walikuwa wanaendesha biashara, walikuwa wanapata hasara. Hivyo baadhi ya makampuni haya yaliundwa upya, kuwa kibiashara,kubinafsishwa au kufungwa, na kupunguza mzigo mkubwa kwa serikali. Kitu cha nne kilikuwa kitu cha kuvutia sana Mapinduzi ya makampuni ya simu yakaja, na nchi za Kiafrika zikarukia. Mwaka 2000, laini za simu zilikuwa milioni 11 Leo, tuna takriban laini milioni 687 za simu za mkononi barani. Na hi imetuwezesha kwenda na kusonga mbele na teknolojia ya simu za mkononi ambapo Afrika hakika inaongoza. Nchini Kenya, maendeleo ya kutuma fedha kwa simu M-Pesa, ambayo nyote mmesikia habari zake-- ilichukua muda kwa dunia kuona kwamba Afrika ipo mbele katika hii teknolojia. na hii kutuma pesa kwa simu za mkononi pia inatoa jukwaa kwa upatikanaji wa nishati mbadala Unajua, watu wanaoweza sasa kulipia sola kwa njia wanayotumia kulipia kwa kadi kwenye simu zao. Hivyo haya yalikuwa maendeleo mazuri sana kitu ambacho kilikwenda sahihi. Tuliwekeza zaidi kwenye elimu na afya, isivyo vyakutosha, lakini kulikuwa na maboresho. Watoto milioni 25 walipata chanjo katika muogo mmoja nanusu uliopita. Kitu kingine ilikuwa kwamba migogoro ilipungua. Kulikuwa na migogoro mingi barani. Wengi wenu mnafahamu hilo. Lakini ilipungua, na viongozi wetu waliweza hata kufifiza mapinduzi. Aina mpya ya migogoro imeibuka, na nitaielezea hiyo baadaye. Hivyo kutokana na yote haya, pia kuna baadhi ya utofautishaji barani ambao nataka muufahamu, kwasababu pamoja na kuwa kuna baadhi ya nchi-- Cote d'Ivoire, Kenya, Ethiopia Tanzania na Senegal zinafanya vizuri kwa sasa Lakini tulikosea wapi? Ngoja nitaje mambo nane. Unapaswa kuwa umekosea zaidi kuliko kupatia. (Kicheko) Hivyo kuna mambo nane tulikosea. La kwanza ilikuwa pamoja na kukua hatukutengeneza ajira za kutosha. Hatukutengeneza ajira kwa vijana wetu. Ukosefu wa ajira kwa vijana barani ni karibia asilimia 15, na upungufu wa ajira ni tatizo kubwa. Jambo la pili tulichofanya ni kuwa kiwango cha ukuaji hakikuwa kizuri vyakutosha Hata ajira zilizoundwa zilikuwa ni ajira zenye tija ndogo sana, hivyo tulihamisha watu kutoka kilimo duni kisicho na tija kwenda biashara zisizo na tija na kufanyia kazi sekta isiyo rasmi katika maeneo ya mijini. Jambo la tatu ni kwamba kukosekana kwa usawa kuliongezeka. Hivyo tuliunda mabilionea zaidi. mabilionea 50 wenye thamani ya dola bilioni 96 wanamiliki utajiri zaidi kuliko watu milioni 75 wa chini barani. Umaskini, uwiano wa watu katika umaskini-- hilo ni jambo la nne--ulipungua lakini namba halisi hazikupungua kwasababu ya ongezeko la idadi ya watu. Na ongezeko la idadi ya watu ni jambo ambalo hatujafanyia mazungumzo ya kutosha barani. Na ninafikiri tutahitaji kulielewa na kulifanyia kazi haswa jinsi ya kuelimisha wasichana. Hiyo ndio njia haswa kufanyia kazi hasusan kwenye suala hili. Jambo la tano ni kwamba hatukuwekeza vya kutosha kwenye miundombinu. Tulikuwa na uwekezaji kutoka kwa Wachina. Ambao ulisaidia baadhi ya nchi, lakini haitoshi. Utumiaji wa umeme barani Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara Afrika ni sawasawa na Hispania. Utumiaji kwa ujumla ni sawasawa na ule wa Hispania Hivyo watu wengi wanaishi gizani, na kama Rais wa Benki ya Maendeleo Afrika alivyosema hivi karibuni, Afrika haiwezi kuendelea gizani. Kitu kingine ambacho hatujafanya ni kwamba chumi zetu zimeshikilia muundo uliofanana ambao tumekuwa nao kwa miongo. Hivyo pamoja na kwamba tumekua muundo wa chumi zetu haujabadilika kwa kiasi kikubwa. Bado tunauza bidhaa nchi za nje na kuuza bidhaa nchi za nje ni nini? kuuza ajira nchi za nje. Ongezeko la thamani ya uzalishaji wetu ni asilimia 11 tu Hatuundi ajira za kutosha kwenye uzalishaji kwa vijana wetu, na biashara kati yetu ni kidogo. Takriban asilimi 12 tu ya biashara kati yetu sisi wenyewe Hivyo hilo ni tatizo lingine zito sana. Kisha utawala bora. Utawala bora ni suala zito. Tuna taasisi dhaifu, na wakati mwingine taasisi hewa, ninafikiri hii inaleta mwanya wa rushwa. Rushwa ni suala ambalo bado hatujalimudu kiasi cha kutosha, na tunatakuwa kupambana kufa na kupona, hiyo na ongezeko la uwazi katika jinsi tunavyosimamia chumi zetu na jinsi tunavyosimamia fedha zetu. Tunahitaji pia kujihadhari na migogoro mipya, aina mpya ya migogoro, kama tuliyonayo na Boko Haram katika nchi yangu, Nigeria, Na Al-Shabaab nchini Kenya. Tunahitaji kushirikiana na washiriki wa kimataifa, nchi zilizoendelea, kupambana juu ya hili pamoja. Ama sivyo, tunaunda ukweli mpya ambao sio aina tunayotaka kwa Afrika inayokua. Na mwisho, ni suala la elimu. Mifumo yetu ya elimu katika nchi nyingi imevunjika. Hatuundi aina ya stadi zinazohitajika kwa siku za usoni Hivyo tunatakiwa tutafute njia ya kutoa elimu kwa ubora. Hivyo hayo ni mambo ambayo hatufanyi kwa usahihi. Sasa, tunaenda wapi kutokea hapo? Ninaamini njia ya kusongambele ni kujifunza kusimamia mafanikio. Mara nyingi, watu wanapofanikiwa au nchi zinapofanikiwa husahau kullichowafanya wafanikiwe. Kujifunza kile unachoweza kufanikiwa, kukisimamia na kukitunza ni jambo muhimu kwetu. Hivyo vitu vyote nilivyosema tulifanya sahihi, tunatakiwa kujifunza kuvifanya kwa usahihi tena, na kuviendeleza. Kusimamia uchumi wakati unaunda ustawi ni muhimu, kupata bei sahihi na sera thabiti. Mara nyingi hatuna uthabiti Mfumo wa utawala mmoja ukitoka unaingia mwingine na wanatupa mbali hata sera zilizokuwa zinafanyakazi vizuri awali Hii inafanya nini? Inaleta sintofahamu kwa watu, kaya sintofahamu kwa biashara Hawajui jinsi na wakati wa kuwekeza. Deni: tunatakiwa tusimamie' mafanikio tuliyopata katika kupunguza deni letu, lakini sasa nchi zimerudia katika kukopa tena, na tumeona urari wa deni kwa Pato la taifa unaanza kupanda tena, na katika baadhi ya nchi, deni linakuwa ni tatizo, hivyo tunatakiwa tuliepuke. Hivyo usimamizi wa mafanikio Kinachofuata ni kuwa makini sana na yale mambo ambayo hatukufanya vizuri. Kitu cha kwanza kabisa ni miundombinu Ndio, nchi nyingi sasa zinatambua zinahitaji kuwekeza kwenye hili, na zinajaribu kufanya kadiri ziwezavyo kufanya hivyo. Lazima. Kitu muhimu sana ni umeme. Huwezi kuendelea katika giza. Na kisha utawala bora na rushwa: tunatakiwa tupambane. Tunatakiwa kuendesha nchi zetu kwa uwazi. Pamoja na yote hayo, lazima tuwashirikishe vijana. Tuna ubunifu katika vijana wetu Ninauona kila siku. Ndio kinachoniamsha asubuhi na kujisikia tayari kwenda. Tunatakiwa tusibanie ubunifu katika vijana wetu, tusiwazibie njia, tuwaunge mkono kuunda na ugunduzi na kuongoza njia. Na ninajua kwamba watatuongoza katika mwelekeo sahihi. Na wanawake wetu, na wasichana wetu: tunatakiwa tutambue kwamba wanawake na wasichana ni zawadi. Wana nguvu, na tunatakiwa tusiwabanie hiyo nguvu ili waweze kutoa mchango wao barani. Nina amini kwa nguvu kwamba tukifanya hayo yote, tutakuta kwamba simulizi za Afrika inayokua sio ubabaishaji. ni harakati. Ni harakati, na tukiendelea, tusipowabania vijana wetu, tusipowabania wanawake wetu, wakati mwingine tunaweza kurudi nyuma, tunaweza pia kukaa pembezoni, lakini harakati ziko wazi. Afrika itaendelea kukua. Na ninawaambia wafanyabiashara mliopo kwenye hadhira hii, uwekezaji Afrika sio kwa ajili ya leo, sio kwa ajili ya kesho, sio kitu cha muda mfupi, ni kitu cha muda mrefu. Lakini ikiwa hamtawekeza Afrika, basi mtakuwa mnakosa mojawapo ya fursa zinazoibuka duniani. Asante. (Makofi) Kelly Stoetzel: Umegusia rushwa katika mazungumzo yako na unafahamika vizuri kuwa mpambanaji thabiti wa rushwa. Lakini hiyo ilikuwa na matokeo yake. Watu walijibu mashambulizi, na mama yako alitekwa nyara. Umewezaje kulimudu hili? Ngozi Okonjo-Iweala: Imekuwa ngumu sana. Asante kwa kugusia suala la kutekwa nyara mama yangu Ni mada ngumu sana. Lakini inachomaanisha ni kwamba unapopambana na rushwa, unapogusa mifuko ya watu wanaoiba pesa, hawanyamazi kimya tu. Watajibu mashambulizi, na suala kubwa ni wanapojaribu kutumia vitisho unakata tamaa, au unaendeleza mapambano? Unatafuta njia ya kubakia na kujibu mashambulizi? Na jibu nililokuwa nalo nikiwa na timu zilizofanya nazo kazi ni kuendeleza mapambano Tunatakiwa kuunda hizo taasisi. Tunatakiwa kutafuta njia ya kuwazuia hawa watu waache kuchukua urithi wa baadaye. Na hicho ndicho tulichofanya. Na hata nje ya serikali, tuliendelea kuweka msisitizo. Katika nchi zetu, hakuna, hakuna atakaye pambana na rushwa isipokuwa sisi wenyewe. kwa hiyo, hilo linakuja na matokeo, na tunatakiwa kufanya kadiri tuwezavyo. Lakini nakushukuru na kuwashukuru TED kutupa sauti kuwaambia hao watu, hamtashinda, na hatutatishika Asante. (Makofi) Kelly Stoetzel: Asante sana kwa mazungumzo yako mazuri na kazi muhimu. (Makofi)