1 00:00:00,000 --> 00:00:04,336 Simulizi za Afrika inayokua zinapata changamoto 2 00:00:04,360 --> 00:00:08,816 Karibia miaka 10 iliyopita Niliongea kuhusu Afrika, 3 00:00:08,840 --> 00:00:11,536 Afrika yenye matumaini na fursa, 4 00:00:11,560 --> 00:00:13,496 Afrika ya wajasiriamali, 5 00:00:13,520 --> 00:00:16,976 Afrika tofauti kabisa na Afrika ambayo umezoaea kusikia 6 00:00:17,000 --> 00:00:19,776 ya vifo, umaskini na magonjwa. 7 00:00:19,800 --> 00:00:21,856 Na kile nilichokiongelea, 8 00:00:21,880 --> 00:00:27,336 ikawa sehemu ya kile kinachojulikana sasa kama hadithi ya Afrika inayokua. 9 00:00:27,360 --> 00:00:30,696 Nataka niwaambie hadithi mbili kuhusu hii Afrika inayokua. 10 00:00:30,720 --> 00:00:32,496 Ya kwanza inaihusisha Rwanda, 11 00:00:32,520 --> 00:00:35,936 nchi ambayo imepitia majaribu mengi na dhiki. 12 00:00:35,960 --> 00:00:40,456 Na Rwanda ikaamua kuwa kitovu cha teknolojia, au kitovu cha teknolojia 13 00:00:40,480 --> 00:00:41,816 kwenye bara la Afrika. 14 00:00:41,840 --> 00:00:44,856 Ni nchi yenye milima na ardhi ya eneo lenye vilima, 15 00:00:44,880 --> 00:00:46,096 kidogo kama hapa, 16 00:00:46,120 --> 00:00:49,296 hivyo ni vigumu sana kupeleka huduma kwa watu. 17 00:00:49,320 --> 00:00:51,016 Hivyo Rwanda imesema nini? 18 00:00:51,040 --> 00:00:54,696 Ili kuweza kuokoa maisha, itajaribu kutumia ndege zisizo na rubani 19 00:00:54,720 --> 00:00:57,936 kupeleka madawa ya kuokoa maisha, chanjo na damu 20 00:00:57,960 --> 00:00:59,976 kwa watu katika sehemu zisizo fikika 21 00:01:00,000 --> 00:01:02,496 wakishirikiana na kampuni inayoitwa Zipline, 22 00:01:02,520 --> 00:01:07,056 pamoja na UPS, na pia Gavi shirika la kimataifa la chanjo. 23 00:01:07,080 --> 00:01:09,456 Katika kufanya hivi, itaokoa maisha. 24 00:01:09,480 --> 00:01:14,776 Hii ni sehemu ya ubunifu tunayotaka kuona katika Afrika inayokua. 25 00:01:14,800 --> 00:01:17,336 Hadithi ya pili inahusiana na jambo 26 00:01:17,360 --> 00:01:20,376 ambalo ninauhakika wengi wenu mmeona au mtakumbuka. 27 00:01:20,400 --> 00:01:24,296 Mara nyingi, nchi za Afrika zimeteseka na ukame na mafuriko, 28 00:01:24,320 --> 00:01:28,016 na inaongezeka zaidi kwasababu ya athari za mabadiliko ya tabia nchi. 29 00:01:28,040 --> 00:01:33,736 Wakati haya yanapotokea, kawaida husubiri nchi za kimataifa kuchanga fedha. 30 00:01:33,760 --> 00:01:37,136 Unaona picha za watoto wakiwa na nzi kwenye nyuso zao 31 00:01:37,160 --> 00:01:39,656 mizoga ya wanyama waliokufa na kadhalika. 32 00:01:39,680 --> 00:01:42,696 Sasa nchi hizi, nchi 32, zilikutana pamoja 33 00:01:42,720 --> 00:01:45,176 chini ya mwamvuli wa Umoja wa Afrika 34 00:01:45,200 --> 00:01:50,216 na kuamua kuunda shirika linaloitwa Africa Risk Capacity. 35 00:01:50,240 --> 00:01:51,456 Linafanya nini? 36 00:01:51,480 --> 00:01:53,576 Ni wakala wa bima wa hali ya hewa 37 00:01:53,600 --> 00:01:57,976 na nchi hizi zinachofanya ni kulipa bima kila mwaka, 38 00:01:58,000 --> 00:02:00,936 karibia dola milioni 3 kwa mwaka kutoka kwenye rasilimali zao, 39 00:02:00,960 --> 00:02:05,776 ili kwamba endapo wanakumbwa na hali ya ukame mgumu au mafuriko, 40 00:02:05,800 --> 00:02:08,416 fedha hizi zitalipwa kuwasaidia 41 00:02:08,440 --> 00:02:11,176 ambazo wanaweza kuzitumia kuwatunza wananchi wao 42 00:02:11,200 --> 00:02:13,976 badala ya kusubiri msaada kuja. 43 00:02:14,000 --> 00:02:18,216 Shirika la African Risk Capacity mwaka jana lilipa dola milioni 26 44 00:02:18,240 --> 00:02:20,736 kwa Mauritania, Senegal na Niger. 45 00:02:20,760 --> 00:02:26,216 Hii iliwawezesha kuwatunza watu milioni 1.3 walioathirika na ukame. 46 00:02:26,240 --> 00:02:28,576 Waliweza kurudisha tena maisha yao, 47 00:02:28,600 --> 00:02:31,296 kununua majani ya n'gombe kulisha watoto mashuleni 48 00:02:31,320 --> 00:02:37,096 kuwafanya wananchi wabaki nyumbani badala ya kuhama nje ya eneo. 49 00:02:37,120 --> 00:02:38,976 Hivyo hizi ni aina za hadithi 50 00:02:39,000 --> 00:02:42,616 za Afrika iliyotayari kuchukua majikumu yake yenyewe, 51 00:02:42,640 --> 00:02:45,816 na kutafuta suluhisho kwa matatizo yake yenyewe. 52 00:02:45,840 --> 00:02:48,336 Ila simulizi hizo zinapata changamoto sasa 53 00:02:48,360 --> 00:02:53,176 kwasababu bara letu halijafanya vema kwa miaka miwili iliyopita. 54 00:02:53,200 --> 00:02:56,136 Ilikuwa inakua kwa kiwango cha asilimia 5 kwa mwaka 55 00:02:56,160 --> 00:02:58,096 kwa muongo mmoja na nusu uliopita 56 00:02:58,120 --> 00:03:00,896 lakini utabiri wa mwaka huu ulikuwa asilimia tatu. Kwanini? 57 00:03:00,920 --> 00:03:05,096 kwa mazingira ya ulimwengu yanavyobadilika bei za bidhaa zimeshuka. 58 00:03:05,120 --> 00:03:08,296 Uchumi wa nchi nyingi bado unaendeshwa na bidhaa, 59 00:03:08,320 --> 00:03:10,880 na hivyo utendaji wake umeteleza 60 00:03:11,480 --> 00:03:15,456 Na sasa suala la kujitoa kwa Uingereza haifanyi iwe rahisi 61 00:03:15,480 --> 00:03:19,096 Sikujua kama Uingereza ingejitoa 62 00:03:19,120 --> 00:03:23,256 na hilo lingekuwa moja ya vitu ambavyo vingeleta kutokuwa na uhakika ulimwenguni 63 00:03:23,280 --> 00:03:24,576 kama tulivyo. 64 00:03:24,600 --> 00:03:26,776 Hivyo sasa tuna hii hali 65 00:03:26,800 --> 00:03:29,656 na ninafikiri ni wakati wakuangalia 66 00:03:29,680 --> 00:03:34,536 na kusema ni vitu gani ambavyo nchi za Afrika zilifanya sahihi? 67 00:03:34,560 --> 00:03:36,200 Kipi walikosea? 68 00:03:36,840 --> 00:03:39,296 Tutajengaje kwenye haya yote na kujifunza 69 00:03:39,320 --> 00:03:42,120 ili kwamba tuendeleze Afrika inayokua? 70 00:03:42,720 --> 00:03:46,080 Hivyo ngoja niongelee kuhusu mambo sita ninayofikiri tulifanya sahihi. 71 00:03:46,720 --> 00:03:50,016 La kwanza ni kusimamia uchumi wa nchi zetu vizuri 72 00:03:50,040 --> 00:03:54,296 Miaka ya 80 na 90 ni miongo iliyopotea, wakati Afrika haikuwa ikifanya vizuri, 73 00:03:54,320 --> 00:03:57,936 na baadhi yenu mtakumbuka ukurasa wa mbele wa gazeti la "Economist" 74 00:03:57,960 --> 00:03:59,976 lililosema, "Bara lililopotea" 75 00:04:00,000 --> 00:04:04,096 Ila miaka ya 2000 watunga sera walijifunza 76 00:04:04,120 --> 00:04:08,376 kwamba wanahitaji kusimamia mazingira ya uchumi vizuri zaidi, 77 00:04:08,400 --> 00:04:09,936 kuhakikisha uthabiti, 78 00:04:09,960 --> 00:04:12,576 kushusha mfumuko wa bei kufika tarakimu moja, 79 00:04:12,600 --> 00:04:18,176 kushusha nakisi ya bajeti, chini ya asilimia tatu ya Pato la Taifa, 80 00:04:18,200 --> 00:04:22,096 wape wawekezaji, wote wa ndani na wageni, 81 00:04:22,120 --> 00:04:25,936 aina ya uthabiti ili wawe na imani ya kuwekeza kwenye chumi hizi. 82 00:04:25,960 --> 00:04:27,456 Hivyo hiyo ilikuwa namba moja. 83 00:04:27,480 --> 00:04:28,816 Mbili, deni. 84 00:04:28,840 --> 00:04:34,536 Mwaka 1994, urari wa deni la Pato la taifa wa nchi za Kiafrila ulikuwa asilimia 130, 85 00:04:34,560 --> 00:04:36,816 na hawakuwa na nafasi ya fedha nakisi 86 00:04:36,840 --> 00:04:39,856 Hawakuweza kutumia rasilimali zao kuwekeza kwenye maendeleo yao 87 00:04:39,880 --> 00:04:41,336 kwakuwa walikuwa wanalipa deni 88 00:04:41,360 --> 00:04:46,096 kwaweza kuwa na baadhi yenu humu ndani mliofanyakazi kusaidia nchi za Afrika 89 00:04:46,120 --> 00:04:47,416 kupata unafuu wa madeni. 90 00:04:47,440 --> 00:04:51,896 Hivyo wadai binafsi, wa pande mbalimbali na pande mbili waliunganika 91 00:04:51,920 --> 00:04:55,536 na kuamua kuanzisha mpango wa Nchi Fukara zenye Mzigo wa madeni 92 00:04:55,560 --> 00:04:56,816 na kutoa unafuu wa madeni. 93 00:04:56,840 --> 00:04:58,936 Hivyo unafuu huu wa madeni mwaka 2005 94 00:04:58,960 --> 00:05:02,896 ulifanya urari wa deni kwa Pato la taifa kushuka hadi takriban asilimia 30, 95 00:05:02,920 --> 00:05:06,816 na kulikuwa na rasilimali za kutosha kujaribu na kuwekeza upya. 96 00:05:06,840 --> 00:05:09,296 Kitu cha tatu kilikuwa makampuni yaliyopata hasara 97 00:05:09,320 --> 00:05:11,376 Serikali zilishiriki katika biashara 98 00:05:11,400 --> 00:05:13,656 ambazo hawakupaswa kuzifanya. 99 00:05:13,680 --> 00:05:16,776 Na walikuwa wanaendesha biashara, walikuwa wanapata hasara. 100 00:05:16,800 --> 00:05:19,536 Hivyo baadhi ya makampuni haya yaliundwa upya, 101 00:05:19,560 --> 00:05:21,976 kuwa kibiashara,kubinafsishwa au kufungwa, 102 00:05:22,000 --> 00:05:25,200 na kupunguza mzigo mkubwa kwa serikali. 103 00:05:26,080 --> 00:05:28,480 Kitu cha nne kilikuwa kitu cha kuvutia sana 104 00:05:29,200 --> 00:05:31,496 Mapinduzi ya makampuni ya simu yakaja, 105 00:05:31,520 --> 00:05:34,096 na nchi za Kiafrika zikarukia. 106 00:05:34,120 --> 00:05:36,736 Mwaka 2000, laini za simu zilikuwa milioni 11 107 00:05:36,760 --> 00:05:42,096 Leo, tuna takriban laini milioni 687 za simu za mkononi barani. 108 00:05:42,120 --> 00:05:43,936 Na hi imetuwezesha 109 00:05:43,960 --> 00:05:46,616 kwenda na kusonga mbele na teknolojia ya simu za mkononi 110 00:05:46,640 --> 00:05:49,256 ambapo Afrika hakika inaongoza. 111 00:05:49,280 --> 00:05:51,816 Nchini Kenya, maendeleo ya kutuma fedha kwa simu 112 00:05:51,840 --> 00:05:54,616 M-Pesa, ambayo nyote mmesikia habari zake-- 113 00:05:54,640 --> 00:05:58,096 ilichukua muda kwa dunia kuona kwamba Afrika ipo mbele 114 00:05:58,120 --> 00:05:59,656 katika hii teknolojia. 115 00:05:59,680 --> 00:06:02,896 na hii kutuma pesa kwa simu za mkononi pia inatoa jukwaa 116 00:06:02,920 --> 00:06:05,376 kwa upatikanaji wa nishati mbadala 117 00:06:05,400 --> 00:06:08,896 Unajua, watu wanaoweza sasa kulipia sola 118 00:06:08,920 --> 00:06:13,136 kwa njia wanayotumia kulipia kwa kadi kwenye simu zao. 119 00:06:13,160 --> 00:06:17,680 Hivyo haya yalikuwa maendeleo mazuri sana kitu ambacho kilikwenda sahihi. 120 00:06:18,240 --> 00:06:22,736 Tuliwekeza zaidi kwenye elimu na afya, isivyo vyakutosha, 121 00:06:22,760 --> 00:06:24,416 lakini kulikuwa na maboresho. 122 00:06:24,440 --> 00:06:29,960 Watoto milioni 25 walipata chanjo katika muogo mmoja nanusu uliopita. 123 00:06:30,520 --> 00:06:33,896 Kitu kingine ilikuwa kwamba migogoro ilipungua. 124 00:06:33,920 --> 00:06:35,976 Kulikuwa na migogoro mingi barani. 125 00:06:36,000 --> 00:06:37,456 Wengi wenu mnafahamu hilo. 126 00:06:37,480 --> 00:06:42,296 Lakini ilipungua, na viongozi wetu waliweza hata kufifiza mapinduzi. 127 00:06:42,320 --> 00:06:46,376 Aina mpya ya migogoro imeibuka, na nitaielezea hiyo baadaye. 128 00:06:46,400 --> 00:06:50,016 Hivyo kutokana na yote haya, pia kuna baadhi ya utofautishaji barani 129 00:06:50,040 --> 00:06:51,496 ambao nataka muufahamu, 130 00:06:51,520 --> 00:06:54,016 kwasababu pamoja na kuwa 131 00:06:54,040 --> 00:06:58,016 kuna baadhi ya nchi-- Cote d'Ivoire, Kenya, Ethiopia 132 00:06:58,148 --> 00:07:01,148 Tanzania na Senegal zinafanya vizuri kwa sasa 133 00:07:03,120 --> 00:07:05,256 Lakini tulikosea wapi? 134 00:07:05,280 --> 00:07:06,656 Ngoja nitaje mambo nane. 135 00:07:06,680 --> 00:07:08,856 Unapaswa kuwa umekosea zaidi kuliko kupatia. 136 00:07:08,880 --> 00:07:10,336 (Kicheko) 137 00:07:10,360 --> 00:07:12,736 Hivyo kuna mambo nane tulikosea. 138 00:07:12,760 --> 00:07:16,280 La kwanza ilikuwa pamoja na kukua hatukutengeneza ajira za kutosha. 139 00:07:16,800 --> 00:07:18,696 Hatukutengeneza ajira kwa vijana wetu. 140 00:07:18,720 --> 00:07:21,656 Ukosefu wa ajira kwa vijana barani ni karibia asilimia 15, 141 00:07:21,680 --> 00:07:24,720 na upungufu wa ajira ni tatizo kubwa. 142 00:07:25,400 --> 00:07:30,936 Jambo la pili tulichofanya ni kuwa kiwango cha ukuaji hakikuwa kizuri vyakutosha 143 00:07:30,960 --> 00:07:34,496 Hata ajira zilizoundwa zilikuwa ni ajira zenye tija ndogo sana, 144 00:07:34,520 --> 00:07:38,016 hivyo tulihamisha watu kutoka kilimo duni kisicho na tija 145 00:07:38,040 --> 00:07:41,976 kwenda biashara zisizo na tija na kufanyia kazi sekta isiyo rasmi 146 00:07:42,000 --> 00:07:43,720 katika maeneo ya mijini. 147 00:07:44,240 --> 00:07:48,040 Jambo la tatu ni kwamba kukosekana kwa usawa kuliongezeka. 148 00:07:48,600 --> 00:07:53,576 Hivyo tuliunda mabilionea zaidi. 149 00:07:53,600 --> 00:07:56,296 mabilionea 50 wenye thamani ya dola bilioni 96 150 00:07:56,320 --> 00:08:01,160 wanamiliki utajiri zaidi kuliko watu milioni 75 wa chini barani. 151 00:08:01,920 --> 00:08:03,496 Umaskini, 152 00:08:03,520 --> 00:08:07,896 uwiano wa watu katika umaskini-- hilo ni jambo la nne--ulipungua 153 00:08:07,920 --> 00:08:12,016 lakini namba halisi hazikupungua kwasababu ya ongezeko la idadi ya watu. 154 00:08:12,040 --> 00:08:14,616 Na ongezeko la idadi ya watu ni jambo 155 00:08:14,640 --> 00:08:18,056 ambalo hatujafanyia mazungumzo ya kutosha barani. 156 00:08:18,080 --> 00:08:21,216 Na ninafikiri tutahitaji kulielewa na kulifanyia kazi 157 00:08:21,240 --> 00:08:24,496 haswa jinsi ya kuelimisha wasichana. 158 00:08:24,520 --> 00:08:29,160 Hiyo ndio njia haswa kufanyia kazi hasusan kwenye suala hili. 159 00:08:29,880 --> 00:08:36,696 Jambo la tano ni kwamba hatukuwekeza vya kutosha kwenye miundombinu. 160 00:08:36,720 --> 00:08:38,816 Tulikuwa na uwekezaji kutoka kwa Wachina. 161 00:08:38,840 --> 00:08:42,056 Ambao ulisaidia baadhi ya nchi, lakini haitoshi. 162 00:08:42,080 --> 00:08:45,416 Utumiaji wa umeme barani Afrika 163 00:08:45,440 --> 00:08:49,016 Kusini mwa jangwa la Sahara Afrika ni sawasawa na Hispania. 164 00:08:49,040 --> 00:08:52,496 Utumiaji kwa ujumla ni sawasawa na ule wa Hispania 165 00:08:52,520 --> 00:08:55,176 Hivyo watu wengi wanaishi gizani, 166 00:08:55,200 --> 00:08:58,776 na kama Rais wa Benki ya Maendeleo Afrika alivyosema hivi karibuni, 167 00:08:58,800 --> 00:09:01,080 Afrika haiwezi kuendelea gizani. 168 00:09:02,120 --> 00:09:04,256 Kitu kingine ambacho hatujafanya 169 00:09:04,280 --> 00:09:09,696 ni kwamba chumi zetu zimeshikilia muundo uliofanana 170 00:09:09,720 --> 00:09:11,336 ambao tumekuwa nao kwa miongo. 171 00:09:11,360 --> 00:09:13,016 Hivyo pamoja na kwamba tumekua 172 00:09:13,040 --> 00:09:15,736 muundo wa chumi zetu haujabadilika kwa kiasi kikubwa. 173 00:09:15,760 --> 00:09:18,336 Bado tunauza bidhaa nchi za nje 174 00:09:18,360 --> 00:09:22,216 na kuuza bidhaa nchi za nje ni nini? kuuza ajira nchi za nje. 175 00:09:22,240 --> 00:09:25,536 Ongezeko la thamani ya uzalishaji wetu ni asilimia 11 tu 176 00:09:25,560 --> 00:09:30,096 Hatuundi ajira za kutosha kwenye uzalishaji kwa vijana wetu, 177 00:09:30,120 --> 00:09:32,736 na biashara kati yetu ni kidogo. 178 00:09:32,760 --> 00:09:36,256 Takriban asilimi 12 tu ya biashara kati yetu sisi wenyewe 179 00:09:36,280 --> 00:09:38,976 Hivyo hilo ni tatizo lingine zito sana. 180 00:09:39,000 --> 00:09:41,096 Kisha utawala bora. 181 00:09:41,120 --> 00:09:43,536 Utawala bora ni suala zito. 182 00:09:43,560 --> 00:09:45,776 Tuna taasisi dhaifu, 183 00:09:45,800 --> 00:09:50,816 na wakati mwingine taasisi hewa, ninafikiri hii inaleta mwanya wa rushwa. 184 00:09:50,840 --> 00:09:56,056 Rushwa ni suala ambalo bado hatujalimudu kiasi cha kutosha, 185 00:09:56,080 --> 00:09:58,696 na tunatakuwa kupambana kufa na kupona, 186 00:09:58,720 --> 00:10:02,296 hiyo na ongezeko la uwazi katika jinsi tunavyosimamia chumi zetu 187 00:10:02,320 --> 00:10:04,776 na jinsi tunavyosimamia fedha zetu. 188 00:10:04,800 --> 00:10:09,536 Tunahitaji pia kujihadhari na migogoro mipya, 189 00:10:09,560 --> 00:10:11,496 aina mpya ya migogoro, 190 00:10:11,520 --> 00:10:14,736 kama tuliyonayo na Boko Haram katika nchi yangu, Nigeria, 191 00:10:14,760 --> 00:10:16,816 Na Al-Shabaab nchini Kenya. 192 00:10:16,840 --> 00:10:20,176 Tunahitaji kushirikiana na washiriki wa kimataifa, 193 00:10:20,200 --> 00:10:23,056 nchi zilizoendelea, kupambana juu ya hili pamoja. 194 00:10:23,080 --> 00:10:24,976 Ama sivyo, tunaunda ukweli mpya 195 00:10:25,000 --> 00:10:28,256 ambao sio aina tunayotaka kwa Afrika inayokua. 196 00:10:28,280 --> 00:10:31,816 Na mwisho, ni suala la elimu. 197 00:10:31,840 --> 00:10:35,136 Mifumo yetu ya elimu katika nchi nyingi imevunjika. 198 00:10:35,160 --> 00:10:39,696 Hatuundi aina ya stadi zinazohitajika kwa siku za usoni 199 00:10:39,720 --> 00:10:42,360 Hivyo tunatakiwa tutafute njia ya kutoa elimu kwa ubora. 200 00:10:42,920 --> 00:10:45,640 Hivyo hayo ni mambo ambayo hatufanyi kwa usahihi. 201 00:10:46,240 --> 00:10:48,640 Sasa, tunaenda wapi kutokea hapo? 202 00:10:49,240 --> 00:10:53,936 Ninaamini njia ya kusongambele ni kujifunza kusimamia mafanikio. 203 00:10:53,960 --> 00:10:57,696 Mara nyingi, watu wanapofanikiwa au nchi zinapofanikiwa 204 00:10:57,720 --> 00:10:59,920 husahau kullichowafanya wafanikiwe. 205 00:11:00,680 --> 00:11:03,216 Kujifunza kile unachoweza kufanikiwa, 206 00:11:03,240 --> 00:11:05,656 kukisimamia na kukitunza ni jambo muhimu kwetu. 207 00:11:05,680 --> 00:11:07,896 Hivyo vitu vyote nilivyosema tulifanya sahihi, 208 00:11:07,920 --> 00:11:11,816 tunatakiwa kujifunza kuvifanya kwa usahihi tena, na kuviendeleza. 209 00:11:11,840 --> 00:11:15,416 Kusimamia uchumi wakati unaunda ustawi ni muhimu, 210 00:11:15,440 --> 00:11:18,936 kupata bei sahihi na sera thabiti. 211 00:11:18,960 --> 00:11:21,336 Mara nyingi hatuna uthabiti 212 00:11:21,360 --> 00:11:23,616 Mfumo wa utawala mmoja ukitoka unaingia mwingine 213 00:11:23,640 --> 00:11:27,096 na wanatupa mbali hata sera zilizokuwa zinafanyakazi vizuri awali 214 00:11:27,120 --> 00:11:28,376 Hii inafanya nini? 215 00:11:28,400 --> 00:11:30,776 Inaleta sintofahamu kwa watu, kaya 216 00:11:30,800 --> 00:11:32,176 sintofahamu kwa biashara 217 00:11:32,200 --> 00:11:34,896 Hawajui jinsi na wakati wa kuwekeza. 218 00:11:34,920 --> 00:11:39,256 Deni: tunatakiwa tusimamie' mafanikio tuliyopata katika kupunguza deni letu, 219 00:11:39,280 --> 00:11:41,816 lakini sasa nchi zimerudia katika kukopa tena, 220 00:11:41,840 --> 00:11:45,256 na tumeona urari wa deni kwa Pato la taifa unaanza kupanda tena, 221 00:11:45,280 --> 00:11:46,736 na katika baadhi ya nchi, 222 00:11:46,760 --> 00:11:49,256 deni linakuwa ni tatizo, hivyo tunatakiwa tuliepuke. 223 00:11:49,280 --> 00:11:50,736 Hivyo usimamizi wa mafanikio 224 00:11:50,760 --> 00:11:53,416 Kinachofuata ni kuwa makini sana 225 00:11:53,440 --> 00:11:55,296 na yale mambo ambayo hatukufanya vizuri. 226 00:11:55,320 --> 00:11:57,176 Kitu cha kwanza kabisa ni miundombinu 227 00:11:57,200 --> 00:12:00,776 Ndio, nchi nyingi sasa zinatambua zinahitaji kuwekeza kwenye hili, 228 00:12:00,800 --> 00:12:03,416 na zinajaribu kufanya kadiri ziwezavyo kufanya hivyo. 229 00:12:03,440 --> 00:12:04,656 Lazima. 230 00:12:04,680 --> 00:12:06,336 Kitu muhimu sana ni umeme. 231 00:12:06,360 --> 00:12:08,616 Huwezi kuendelea katika giza. 232 00:12:08,640 --> 00:12:10,896 Na kisha utawala bora na rushwa: 233 00:12:10,920 --> 00:12:12,136 tunatakiwa tupambane. 234 00:12:12,160 --> 00:12:14,936 Tunatakiwa kuendesha nchi zetu kwa uwazi. 235 00:12:14,960 --> 00:12:18,536 Pamoja na yote hayo, lazima tuwashirikishe vijana. 236 00:12:18,560 --> 00:12:20,776 Tuna ubunifu katika vijana wetu 237 00:12:20,800 --> 00:12:22,056 Ninauona kila siku. 238 00:12:22,080 --> 00:12:25,616 Ndio kinachoniamsha asubuhi na kujisikia tayari kwenda. 239 00:12:25,640 --> 00:12:28,016 Tunatakiwa tusibanie ubunifu katika vijana wetu, 240 00:12:28,040 --> 00:12:31,296 tusiwazibie njia, tuwaunge mkono kuunda na ugunduzi 241 00:12:31,320 --> 00:12:32,536 na kuongoza njia. 242 00:12:32,560 --> 00:12:35,256 Na ninajua kwamba watatuongoza katika mwelekeo sahihi. 243 00:12:35,280 --> 00:12:37,456 Na wanawake wetu, na wasichana wetu: 244 00:12:37,480 --> 00:12:40,536 tunatakiwa tutambue kwamba wanawake na wasichana ni zawadi. 245 00:12:40,560 --> 00:12:42,056 Wana nguvu, 246 00:12:42,080 --> 00:12:44,216 na tunatakiwa tusiwabanie hiyo nguvu 247 00:12:44,240 --> 00:12:47,176 ili waweze kutoa mchango wao barani. 248 00:12:47,200 --> 00:12:51,016 Nina amini kwa nguvu kwamba tukifanya hayo yote, 249 00:12:51,040 --> 00:12:54,256 tutakuta kwamba simulizi za Afrika inayokua 250 00:12:54,280 --> 00:12:55,856 sio ubabaishaji. 251 00:12:55,880 --> 00:12:57,120 ni harakati. 252 00:12:57,720 --> 00:13:01,536 Ni harakati, na tukiendelea, tusipowabania vijana wetu, 253 00:13:01,560 --> 00:13:02,896 tusipowabania wanawake wetu, 254 00:13:02,920 --> 00:13:04,936 wakati mwingine tunaweza kurudi nyuma, 255 00:13:04,960 --> 00:13:06,856 tunaweza pia kukaa pembezoni, 256 00:13:06,880 --> 00:13:08,496 lakini harakati ziko wazi. 257 00:13:08,520 --> 00:13:10,536 Afrika itaendelea kukua. 258 00:13:10,560 --> 00:13:14,296 Na ninawaambia wafanyabiashara mliopo kwenye hadhira hii, 259 00:13:14,320 --> 00:13:17,776 uwekezaji Afrika sio kwa ajili ya leo, sio kwa ajili ya kesho, 260 00:13:17,800 --> 00:13:21,056 sio kitu cha muda mfupi, ni kitu cha muda mrefu. 261 00:13:21,080 --> 00:13:23,496 Lakini ikiwa hamtawekeza Afrika, 262 00:13:23,520 --> 00:13:24,936 basi mtakuwa mnakosa 263 00:13:24,960 --> 00:13:29,216 mojawapo ya fursa zinazoibuka duniani. 264 00:13:29,240 --> 00:13:30,456 Asante. 265 00:13:30,480 --> 00:13:33,000 (Makofi) 266 00:13:39,227 --> 00:13:41,896 Kelly Stoetzel: Umegusia rushwa katika mazungumzo yako 267 00:13:41,920 --> 00:13:45,416 na unafahamika vizuri kuwa mpambanaji thabiti wa rushwa. 268 00:13:45,440 --> 00:13:47,976 Lakini hiyo ilikuwa na matokeo yake. 269 00:13:48,000 --> 00:13:50,936 Watu walijibu mashambulizi, na mama yako alitekwa nyara. 270 00:13:50,960 --> 00:13:52,520 Umewezaje kulimudu hili? 271 00:13:53,280 --> 00:13:55,456 Ngozi Okonjo-Iweala: Imekuwa ngumu sana. 272 00:13:55,480 --> 00:13:59,816 Asante kwa kugusia suala la kutekwa nyara mama yangu 273 00:13:59,840 --> 00:14:02,416 Ni mada ngumu sana. 274 00:14:02,440 --> 00:14:06,296 Lakini inachomaanisha ni kwamba unapopambana na rushwa, 275 00:14:06,320 --> 00:14:09,736 unapogusa mifuko ya watu wanaoiba pesa, 276 00:14:09,760 --> 00:14:11,616 hawanyamazi kimya tu. 277 00:14:11,640 --> 00:14:15,296 Watajibu mashambulizi, na suala kubwa ni wanapojaribu kutumia vitisho 278 00:14:15,320 --> 00:14:18,776 unakata tamaa, au unaendeleza mapambano? 279 00:14:18,800 --> 00:14:21,936 Unatafuta njia ya kubakia na kujibu mashambulizi? 280 00:14:21,960 --> 00:14:26,216 Na jibu nililokuwa nalo nikiwa na timu zilizofanya nazo kazi 281 00:14:26,240 --> 00:14:28,016 ni kuendeleza mapambano 282 00:14:28,040 --> 00:14:29,856 Tunatakiwa kuunda hizo taasisi. 283 00:14:29,880 --> 00:14:33,096 Tunatakiwa kutafuta njia ya kuwazuia hawa watu 284 00:14:33,120 --> 00:14:36,296 waache kuchukua urithi wa baadaye. 285 00:14:36,320 --> 00:14:38,216 Na hicho ndicho tulichofanya. 286 00:14:38,240 --> 00:14:41,856 Na hata nje ya serikali, tuliendelea kuweka msisitizo. 287 00:14:41,880 --> 00:14:45,856 Katika nchi zetu, hakuna, hakuna atakaye pambana na rushwa 288 00:14:45,880 --> 00:14:47,416 isipokuwa sisi wenyewe. 289 00:14:47,440 --> 00:14:49,656 kwa hiyo, hilo linakuja na matokeo, 290 00:14:49,680 --> 00:14:51,576 na tunatakiwa kufanya kadiri tuwezavyo. 291 00:14:51,600 --> 00:14:55,016 Lakini nakushukuru na kuwashukuru TED kutupa sauti 292 00:14:55,040 --> 00:14:58,336 kuwaambia hao watu, hamtashinda, 293 00:14:58,360 --> 00:15:00,696 na hatutatishika 294 00:15:00,720 --> 00:15:01,936 Asante. 295 00:15:01,960 --> 00:15:03,176 (Makofi) 296 00:15:03,200 --> 00:15:06,666 Kelly Stoetzel: Asante sana kwa mazungumzo yako mazuri na kazi muhimu. 297 00:15:06,690 --> 00:15:10,060 (Makofi)