Simulizi za Afrika inayokua
zinapata changamoto
Karibia miaka 10 iliyopita
Niliongea kuhusu Afrika,
Afrika yenye matumaini na fursa,
Afrika ya wajasiriamali,
Afrika tofauti kabisa na Afrika
ambayo umezoaea kusikia
ya vifo, umaskini na magonjwa.
Na kile nilichokiongelea,
ikawa sehemu ya kile kinachojulikana sasa
kama hadithi ya Afrika inayokua.
Nataka niwaambie hadithi mbili
kuhusu hii Afrika inayokua.
Ya kwanza inaihusisha Rwanda,
nchi ambayo imepitia majaribu mengi
na dhiki.
Na Rwanda ikaamua kuwa kitovu
cha teknolojia, au kitovu cha teknolojia
kwenye bara la Afrika.
Ni nchi yenye milima na ardhi ya eneo
lenye vilima,
kidogo kama hapa,
hivyo ni vigumu sana
kupeleka huduma kwa watu.
Hivyo Rwanda imesema nini?
Ili kuweza kuokoa maisha,
itajaribu kutumia ndege zisizo na rubani
kupeleka madawa ya kuokoa maisha,
chanjo na damu
kwa watu katika sehemu zisizo fikika
wakishirikiana na
kampuni inayoitwa Zipline,
pamoja na UPS, na pia Gavi
shirika la kimataifa la chanjo.
Katika kufanya hivi, itaokoa maisha.
Hii ni sehemu ya ubunifu
tunayotaka kuona katika Afrika inayokua.
Hadithi ya pili inahusiana na jambo
ambalo ninauhakika wengi wenu
mmeona au mtakumbuka.
Mara nyingi, nchi za Afrika
zimeteseka na ukame na mafuriko,
na inaongezeka zaidi kwasababu
ya athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Wakati haya yanapotokea, kawaida
husubiri nchi za kimataifa kuchanga fedha.
Unaona picha za watoto
wakiwa na nzi kwenye nyuso zao
mizoga ya wanyama waliokufa na kadhalika.
Sasa nchi hizi,
nchi 32, zilikutana pamoja
chini ya mwamvuli wa Umoja wa Afrika
na kuamua kuunda shirika
linaloitwa Africa Risk Capacity.
Linafanya nini?
Ni wakala wa bima wa hali ya hewa
na nchi hizi zinachofanya
ni kulipa bima kila mwaka,
karibia dola milioni 3 kwa mwaka
kutoka kwenye rasilimali zao,
ili kwamba endapo wanakumbwa
na hali ya ukame mgumu au mafuriko,
fedha hizi zitalipwa kuwasaidia
ambazo wanaweza kuzitumia
kuwatunza wananchi wao
badala ya kusubiri msaada kuja.
Shirika la African Risk Capacity
mwaka jana lilipa dola milioni 26
kwa Mauritania, Senegal na Niger.
Hii iliwawezesha kuwatunza
watu milioni 1.3 walioathirika na ukame.
Waliweza kurudisha tena maisha yao,
kununua majani ya n'gombe
kulisha watoto mashuleni
kuwafanya wananchi wabaki nyumbani
badala ya kuhama nje ya eneo.
Hivyo hizi ni aina za hadithi
za Afrika iliyotayari
kuchukua majikumu yake yenyewe,
na kutafuta suluhisho
kwa matatizo yake yenyewe.
Ila simulizi hizo zinapata changamoto sasa
kwasababu bara letu halijafanya vema
kwa miaka miwili iliyopita.
Ilikuwa inakua kwa kiwango
cha asilimia 5 kwa mwaka
kwa muongo mmoja na nusu uliopita
lakini utabiri wa mwaka huu
ulikuwa asilimia tatu. Kwanini?
kwa mazingira ya ulimwengu yanavyobadilika
bei za bidhaa zimeshuka.
Uchumi wa nchi nyingi
bado unaendeshwa na bidhaa,
na hivyo utendaji wake
umeteleza
Na sasa suala la kujitoa kwa Uingereza
haifanyi iwe rahisi
Sikujua kama Uingereza ingejitoa
na hilo lingekuwa moja ya vitu ambavyo
vingeleta kutokuwa na uhakika ulimwenguni
kama tulivyo.
Hivyo sasa tuna hii hali
na ninafikiri ni wakati wakuangalia
na kusema ni vitu gani ambavyo
nchi za Afrika zilifanya sahihi?
Kipi walikosea?
Tutajengaje kwenye haya yote
na kujifunza
ili kwamba tuendeleze Afrika inayokua?
Hivyo ngoja niongelee kuhusu mambo sita
ninayofikiri tulifanya sahihi.
La kwanza ni kusimamia
uchumi wa nchi zetu vizuri
Miaka ya 80 na 90 ni miongo iliyopotea,
wakati Afrika haikuwa ikifanya vizuri,
na baadhi yenu mtakumbuka ukurasa
wa mbele wa gazeti la "Economist"
lililosema, "Bara lililopotea"
Ila miaka ya 2000 watunga sera walijifunza
kwamba wanahitaji kusimamia
mazingira ya uchumi vizuri zaidi,
kuhakikisha uthabiti,
kushusha mfumuko wa bei kufika
tarakimu moja,
kushusha nakisi ya bajeti, chini ya
asilimia tatu ya Pato la Taifa,
wape wawekezaji, wote wa ndani na wageni,
aina ya uthabiti ili wawe na imani ya
kuwekeza kwenye chumi hizi.
Hivyo hiyo ilikuwa namba moja.
Mbili, deni.
Mwaka 1994, urari wa deni la Pato la taifa
wa nchi za Kiafrila ulikuwa asilimia 130,
na hawakuwa na nafasi ya fedha nakisi
Hawakuweza kutumia rasilimali zao
kuwekeza kwenye maendeleo yao
kwakuwa walikuwa wanalipa deni
kwaweza kuwa na baadhi yenu humu ndani
mliofanyakazi kusaidia nchi za Afrika
kupata unafuu wa madeni.
Hivyo wadai binafsi, wa pande mbalimbali
na pande mbili waliunganika
na kuamua kuanzisha mpango wa
Nchi Fukara zenye Mzigo wa madeni
na kutoa unafuu wa madeni.
Hivyo unafuu huu wa madeni mwaka 2005
ulifanya urari wa deni kwa Pato la taifa
kushuka hadi takriban asilimia 30,
na kulikuwa na rasilimali za kutosha
kujaribu na kuwekeza upya.
Kitu cha tatu kilikuwa
makampuni yaliyopata hasara
Serikali zilishiriki katika biashara
ambazo hawakupaswa kuzifanya.
Na walikuwa wanaendesha biashara,
walikuwa wanapata hasara.
Hivyo baadhi ya makampuni haya
yaliundwa upya,
kuwa kibiashara,kubinafsishwa au kufungwa,
na kupunguza mzigo mkubwa
kwa serikali.
Kitu cha nne kilikuwa
kitu cha kuvutia sana
Mapinduzi ya makampuni ya simu yakaja,
na nchi za Kiafrika zikarukia.
Mwaka 2000, laini za simu zilikuwa
milioni 11
Leo, tuna takriban laini milioni 687
za simu za mkononi barani.
Na hi imetuwezesha
kwenda na kusonga mbele
na teknolojia ya simu za mkononi
ambapo Afrika hakika inaongoza.
Nchini Kenya, maendeleo ya kutuma
fedha kwa simu
M-Pesa, ambayo nyote
mmesikia habari zake--
ilichukua muda kwa dunia
kuona kwamba Afrika ipo mbele
katika hii teknolojia.
na hii kutuma pesa kwa simu za mkononi
pia inatoa jukwaa
kwa upatikanaji wa nishati mbadala
Unajua, watu wanaoweza sasa kulipia sola
kwa njia wanayotumia kulipia
kwa kadi kwenye simu zao.
Hivyo haya yalikuwa maendeleo mazuri sana
kitu ambacho kilikwenda sahihi.
Tuliwekeza zaidi kwenye elimu
na afya, isivyo vyakutosha,
lakini kulikuwa na maboresho.
Watoto milioni 25 walipata chanjo
katika muogo mmoja nanusu uliopita.
Kitu kingine ilikuwa
kwamba migogoro ilipungua.
Kulikuwa na migogoro mingi
barani.
Wengi wenu mnafahamu hilo.
Lakini ilipungua, na viongozi wetu
waliweza hata kufifiza mapinduzi.
Aina mpya ya migogoro imeibuka,
na nitaielezea hiyo baadaye.
Hivyo kutokana na yote haya, pia
kuna baadhi ya utofautishaji barani
ambao nataka muufahamu,
kwasababu pamoja na kuwa
kuna baadhi ya nchi--
Cote d'Ivoire, Kenya, Ethiopia
Tanzania na Senegal
zinafanya vizuri kwa sasa
Lakini tulikosea wapi?
Ngoja nitaje mambo nane.
Unapaswa kuwa umekosea zaidi
kuliko kupatia.
(Kicheko)
Hivyo kuna mambo nane tulikosea.
La kwanza ilikuwa pamoja na kukua
hatukutengeneza ajira za kutosha.
Hatukutengeneza ajira kwa vijana wetu.
Ukosefu wa ajira kwa vijana barani
ni karibia asilimia 15,
na upungufu wa ajira ni tatizo kubwa.
Jambo la pili tulichofanya ni kuwa kiwango
cha ukuaji hakikuwa kizuri vyakutosha
Hata ajira zilizoundwa
zilikuwa ni ajira zenye tija ndogo sana,
hivyo tulihamisha watu
kutoka kilimo duni kisicho na tija
kwenda biashara zisizo na tija
na kufanyia kazi sekta isiyo rasmi
katika maeneo ya mijini.
Jambo la tatu ni kwamba
kukosekana kwa usawa kuliongezeka.
Hivyo tuliunda mabilionea zaidi.
mabilionea 50 wenye thamani ya dola
bilioni 96
wanamiliki utajiri zaidi kuliko watu
milioni 75 wa chini barani.
Umaskini,
uwiano wa watu katika umaskini--
hilo ni jambo la nne--ulipungua
lakini namba halisi hazikupungua
kwasababu ya ongezeko la idadi ya watu.
Na ongezeko la idadi ya watu ni jambo
ambalo hatujafanyia
mazungumzo ya kutosha barani.
Na ninafikiri tutahitaji
kulielewa na kulifanyia kazi
haswa jinsi ya kuelimisha wasichana.
Hiyo ndio njia haswa kufanyia kazi
hasusan kwenye suala hili.
Jambo la tano ni kwamba hatukuwekeza
vya kutosha kwenye miundombinu.
Tulikuwa na uwekezaji kutoka kwa Wachina.
Ambao ulisaidia baadhi ya nchi,
lakini haitoshi.
Utumiaji wa umeme
barani Afrika
Kusini mwa jangwa la Sahara Afrika
ni sawasawa na Hispania.
Utumiaji kwa ujumla
ni sawasawa na ule wa Hispania
Hivyo watu wengi wanaishi gizani,
na kama Rais wa Benki ya Maendeleo
Afrika alivyosema hivi karibuni,
Afrika haiwezi kuendelea gizani.
Kitu kingine ambacho hatujafanya
ni kwamba chumi zetu
zimeshikilia muundo uliofanana
ambao tumekuwa nao kwa miongo.
Hivyo pamoja na kwamba tumekua
muundo wa chumi zetu
haujabadilika kwa kiasi kikubwa.
Bado tunauza bidhaa nchi za nje
na kuuza bidhaa nchi za nje ni nini?
kuuza ajira nchi za nje.
Ongezeko la thamani ya uzalishaji wetu
ni asilimia 11 tu
Hatuundi ajira za kutosha kwenye
uzalishaji kwa vijana wetu,
na biashara kati yetu ni kidogo.
Takriban asilimi 12 tu ya biashara
kati yetu sisi wenyewe
Hivyo hilo ni tatizo lingine zito sana.
Kisha utawala bora.
Utawala bora ni suala zito.
Tuna taasisi dhaifu,
na wakati mwingine taasisi hewa,
ninafikiri hii inaleta mwanya wa rushwa.
Rushwa ni suala ambalo bado
hatujalimudu kiasi cha kutosha,
na tunatakuwa kupambana kufa na kupona,
hiyo na ongezeko la uwazi katika
jinsi tunavyosimamia chumi zetu
na jinsi tunavyosimamia fedha zetu.
Tunahitaji pia kujihadhari na migogoro
mipya,
aina mpya ya migogoro,
kama tuliyonayo na Boko Haram
katika nchi yangu, Nigeria,
Na Al-Shabaab nchini Kenya.
Tunahitaji kushirikiana na
washiriki wa kimataifa,
nchi zilizoendelea,
kupambana juu ya hili pamoja.
Ama sivyo, tunaunda ukweli mpya
ambao sio aina tunayotaka
kwa Afrika inayokua.
Na mwisho, ni suala la elimu.
Mifumo yetu ya elimu
katika nchi nyingi imevunjika.
Hatuundi aina ya stadi
zinazohitajika kwa siku za usoni
Hivyo tunatakiwa tutafute njia
ya kutoa elimu kwa ubora.
Hivyo hayo ni mambo ambayo
hatufanyi kwa usahihi.
Sasa, tunaenda wapi kutokea hapo?
Ninaamini njia ya kusongambele
ni kujifunza kusimamia mafanikio.
Mara nyingi, watu wanapofanikiwa
au nchi zinapofanikiwa
husahau kullichowafanya wafanikiwe.
Kujifunza kile unachoweza kufanikiwa,
kukisimamia na kukitunza
ni jambo muhimu kwetu.
Hivyo vitu vyote nilivyosema
tulifanya sahihi,
tunatakiwa kujifunza kuvifanya kwa usahihi
tena, na kuviendeleza.
Kusimamia uchumi wakati
unaunda ustawi ni muhimu,
kupata bei sahihi
na sera thabiti.
Mara nyingi hatuna uthabiti
Mfumo wa utawala mmoja ukitoka
unaingia mwingine
na wanatupa mbali hata sera zilizokuwa
zinafanyakazi vizuri awali
Hii inafanya nini?
Inaleta sintofahamu kwa watu,
kaya
sintofahamu kwa biashara
Hawajui jinsi na wakati wa kuwekeza.
Deni: tunatakiwa tusimamie' mafanikio
tuliyopata katika kupunguza deni letu,
lakini sasa nchi zimerudia
katika kukopa tena,
na tumeona urari wa deni kwa Pato la taifa
unaanza kupanda tena,
na katika baadhi ya nchi,
deni linakuwa ni tatizo,
hivyo tunatakiwa tuliepuke.
Hivyo usimamizi wa mafanikio
Kinachofuata
ni kuwa makini sana
na yale mambo ambayo
hatukufanya vizuri.
Kitu cha kwanza kabisa ni miundombinu
Ndio, nchi nyingi sasa zinatambua
zinahitaji kuwekeza kwenye hili,
na zinajaribu kufanya
kadiri ziwezavyo kufanya hivyo.
Lazima.
Kitu muhimu sana ni umeme.
Huwezi kuendelea katika giza.
Na kisha utawala bora na rushwa:
tunatakiwa tupambane.
Tunatakiwa kuendesha nchi zetu kwa uwazi.
Pamoja na yote hayo, lazima
tuwashirikishe vijana.
Tuna ubunifu katika vijana wetu
Ninauona kila siku.
Ndio kinachoniamsha asubuhi
na kujisikia tayari kwenda.
Tunatakiwa tusibanie ubunifu
katika vijana wetu,
tusiwazibie njia,
tuwaunge mkono kuunda na ugunduzi
na kuongoza njia.
Na ninajua kwamba watatuongoza
katika mwelekeo sahihi.
Na wanawake wetu, na wasichana wetu:
tunatakiwa tutambue kwamba
wanawake na wasichana ni zawadi.
Wana nguvu,
na tunatakiwa tusiwabanie hiyo nguvu
ili waweze kutoa mchango
wao barani.
Nina amini kwa nguvu
kwamba tukifanya hayo yote,
tutakuta kwamba simulizi za Afrika
inayokua
sio ubabaishaji.
ni harakati.
Ni harakati, na tukiendelea,
tusipowabania vijana wetu,
tusipowabania wanawake wetu,
wakati mwingine tunaweza kurudi nyuma,
tunaweza pia kukaa pembezoni,
lakini harakati ziko wazi.
Afrika itaendelea kukua.
Na ninawaambia wafanyabiashara
mliopo kwenye hadhira hii,
uwekezaji Afrika sio kwa ajili ya leo,
sio kwa ajili ya kesho,
sio kitu cha muda mfupi,
ni kitu cha muda mrefu.
Lakini ikiwa hamtawekeza Afrika,
basi mtakuwa mnakosa
mojawapo ya fursa zinazoibuka
duniani.
Asante.
(Makofi)
Kelly Stoetzel: Umegusia rushwa
katika mazungumzo yako
na unafahamika vizuri
kuwa mpambanaji thabiti wa rushwa.
Lakini hiyo ilikuwa na matokeo yake.
Watu walijibu mashambulizi,
na mama yako alitekwa nyara.
Umewezaje kulimudu hili?
Ngozi Okonjo-Iweala:
Imekuwa ngumu sana.
Asante kwa kugusia
suala la kutekwa nyara mama yangu
Ni mada ngumu sana.
Lakini inachomaanisha
ni kwamba unapopambana na rushwa,
unapogusa mifuko ya watu
wanaoiba pesa,
hawanyamazi kimya tu.
Watajibu mashambulizi, na suala kubwa
ni wanapojaribu kutumia vitisho
unakata tamaa, au unaendeleza mapambano?
Unatafuta njia ya kubakia
na kujibu mashambulizi?
Na jibu nililokuwa nalo
nikiwa na timu zilizofanya nazo kazi
ni kuendeleza mapambano
Tunatakiwa kuunda hizo taasisi.
Tunatakiwa kutafuta njia ya kuwazuia
hawa watu
waache kuchukua urithi
wa baadaye.
Na hicho ndicho tulichofanya.
Na hata nje ya serikali,
tuliendelea kuweka msisitizo.
Katika nchi zetu, hakuna,
hakuna atakaye pambana na rushwa
isipokuwa sisi wenyewe.
kwa hiyo,
hilo linakuja na matokeo,
na tunatakiwa kufanya kadiri tuwezavyo.
Lakini nakushukuru na kuwashukuru TED
kutupa sauti
kuwaambia hao watu, hamtashinda,
na hatutatishika
Asante.
(Makofi)
Kelly Stoetzel: Asante sana
kwa mazungumzo yako mazuri na kazi muhimu.
(Makofi)