1 00:00:00,520 --> 00:00:02,096 Siku. 2 00:00:02,120 --> 00:00:03,496 Damu. 3 00:00:03,520 --> 00:00:04,720 Hedhi. 4 00:00:05,440 --> 00:00:07,016 Uchafu. 5 00:00:07,040 --> 00:00:08,656 Siri. 6 00:00:08,680 --> 00:00:09,880 Kuficha. 7 00:00:10,400 --> 00:00:11,600 Kwanini? 8 00:00:12,760 --> 00:00:14,656 Utaratibu asilia kibaolojia 9 00:00:14,680 --> 00:00:18,496 ambao kila msichana na mwanamke anapitia kila mwezi 10 00:00:18,520 --> 00:00:20,696 kwa karibia nusu ya maisha yake. 11 00:00:20,720 --> 00:00:23,416 Jambo ambalo ni la umuhimu mkubwa sana 12 00:00:23,440 --> 00:00:27,640 kiasi kwamba kupona na uenezwaji wa spishi zetu unautegemea. 13 00:00:28,480 --> 00:00:30,320 Bado tunauchukulia kama mwiko. 14 00:00:31,160 --> 00:00:34,040 Tunajisikia ugumu na fedheha kuliongelea. 15 00:00:35,840 --> 00:00:37,656 Nilipopata siku zangu mara ya kwanza, 16 00:00:37,680 --> 00:00:40,040 Niliambiwa nifanye iwe siri nisiwaambie wengine-- 17 00:00:40,760 --> 00:00:42,640 hata kwa baba yangu au kaka. 18 00:00:43,640 --> 00:00:46,256 Baadaye wakati hili somo limejitokeza vitabuni mwetu, 19 00:00:46,280 --> 00:00:48,616 mwalimu wetu wa baolojia aliiruka mada. 20 00:00:48,640 --> 00:00:51,320 (Kicheko) 21 00:00:52,000 --> 00:00:53,680 Nilijifunza nini kutokana na hili? 22 00:00:54,360 --> 00:00:57,520 Nilijifunza kwamba ni fedheha mno kuongelea jambo hili. 23 00:00:58,080 --> 00:01:00,736 Nilijifunza kufedheshwa na mwili wangu. 24 00:01:00,760 --> 00:01:03,816 Nilijifunza kutokufahamu siku zangu 25 00:01:03,840 --> 00:01:05,800 ili kuweza kubaki na heshima. 26 00:01:06,440 --> 00:01:08,256 Utafiti katika sehemu mbalimbali India 27 00:01:08,280 --> 00:01:13,016 waonyesha wasichana watatu kati ya kumi hawafahamu kuhusu hedhi 28 00:01:13,040 --> 00:01:14,800 wakati wa siku zao za kwanza. 29 00:01:15,400 --> 00:01:17,016 Na baadhi ya sehemu za Rajasthan 30 00:01:17,040 --> 00:01:21,880 hii namba ni kubwa kama wasichana tisa kati ya kumi kutokufahamu 31 00:01:22,800 --> 00:01:24,456 Unaweza kushangazwa kujua 32 00:01:24,480 --> 00:01:26,696 kwamba wasichana wengi nilioongea nao, 33 00:01:26,720 --> 00:01:30,536 waliokuwa hawajui kuhusu siku zao wakati wa hedhi zao za kwanza 34 00:01:30,560 --> 00:01:32,936 walifikiria kuwa wana saratani ya damu 35 00:01:32,960 --> 00:01:34,560 na watakufa muda sio mrefu. 36 00:01:36,760 --> 00:01:39,696 Usafi wa hedhi ni kipengele muhimu cha hatari 37 00:01:39,720 --> 00:01:42,280 kwa maambukizi wa mfumo wa via vya uzazi. 38 00:01:43,040 --> 00:01:46,216 Lakini India, ni asilimia 12 tu ya wasichana na wanawake 39 00:01:46,240 --> 00:01:50,000 wanaweza kupata njia za usafi wa kumudu siku zao. 40 00:01:50,840 --> 00:01:52,336 Ukifanya mahesabu, 41 00:01:52,360 --> 00:01:57,456 asilimia 88 ya wasichana na wanawake hutumia njia zisizo salama kwa siku zao. 42 00:01:57,480 --> 00:01:58,680 Nilikuwa mmoja wao. 43 00:01:59,880 --> 00:02:02,816 Nilikulia kwenye mji mdogo uitwao Garhwa, jimbo la Jharkhand, 44 00:02:02,840 --> 00:02:05,960 ambako hata kununua pedi ilichukuliwa kama fedheha. 45 00:02:06,840 --> 00:02:08,895 Sasa nilipoanza kupata siku zangu, 46 00:02:08,919 --> 00:02:10,680 Nilianza kutumia matambara. 47 00:02:12,560 --> 00:02:15,216 Baada ya kila matumizi niliyafua na kuyatumia tena. 48 00:02:15,240 --> 00:02:16,496 Lakini kuyahifadhi, 49 00:02:16,520 --> 00:02:19,136 Niliyaficha na kuyaweka sehemu yenye giza na unyevu 50 00:02:19,160 --> 00:02:21,760 ilikwamba mtu asijue kuwa niko kwenye hedhi. 51 00:02:22,520 --> 00:02:25,136 Kwa kuyarudia kufua matambara yalikuja kuwa magumu, 52 00:02:25,160 --> 00:02:28,160 na mara nyingi nilipata upele na maambukizi kwa kuyatumia. 53 00:02:28,880 --> 00:02:33,160 Niliyavaa kwa muda wa miaka mitano hadi nilipohama ule mji. 54 00:02:35,640 --> 00:02:37,976 Suala lingine ambalo siku zilileta maishani mwangu 55 00:02:38,000 --> 00:02:40,296 lile la kuwekewa mipaka kijamii 56 00:02:40,320 --> 00:02:44,656 iliyowekwa kwa wasichana wetu na wanawake wakiwa kwenye siku zao. 57 00:02:44,680 --> 00:02:46,976 Nafikiri wote lazma mtakuwa mnajua, 58 00:02:47,000 --> 00:02:49,960 lakini bado nitaelezea kwa wale wachache wasiojua. 59 00:02:50,720 --> 00:02:53,200 Sikuruhusiwa kula au kugusa vitu vichachu. 60 00:02:53,840 --> 00:02:58,696 Sikuruhusiwa kukaa kwenye sofa au kitandani mwa ndugu wa familia. 61 00:02:58,720 --> 00:03:01,176 Nilitakiwa kufua mashuka kila baada ya siku zangu, 62 00:03:01,200 --> 00:03:03,136 hata kama hazikuchafuka kwa madoa. 63 00:03:03,160 --> 00:03:04,976 Nilichukuliwa kama najisi 64 00:03:05,000 --> 00:03:09,800 na kukatazwa kuabudu au kugusa kitu chochote chenye umuhimu kidini. 65 00:03:10,880 --> 00:03:13,096 Ulikutana na matangazo nje ya misikiti 66 00:03:13,120 --> 00:03:15,560 kukataza wasichana na wanawake walio kwenye hedhi. 67 00:03:17,080 --> 00:03:18,456 Chakuchekesha, 68 00:03:18,480 --> 00:03:21,296 wakati wote ni wanawake watu wazima 69 00:03:21,320 --> 00:03:25,760 ndio walioweka vizuizi hivyo kwa wasichana wadogo katika familia. 70 00:03:26,360 --> 00:03:30,536 hata hivyo, wamekua wakikubali vizuizi hivyo kama desturi. 71 00:03:30,560 --> 00:03:33,576 Na katika kukosekana kwa kuingiliwa, 72 00:03:33,600 --> 00:03:35,616 ni imani potofu na kutoeleweka 73 00:03:35,640 --> 00:03:38,240 kunakoenezwa kizazi hata kizazi. 74 00:03:39,240 --> 00:03:41,096 Kwa miaka nilyofanyia kazi taaluma hii, 75 00:03:41,120 --> 00:03:42,616 Nimeshakutana na hadithi 76 00:03:42,640 --> 00:03:46,256 ambapo wasichana walitakiwa kula na kuosha vyombo vyao kwa kutengwa. 77 00:03:46,280 --> 00:03:48,616 Hawakuruhusiwa kuoga wakati wa siku zao, 78 00:03:48,640 --> 00:03:52,720 na katika nyumba nyingine walitengwa hata na ndugu wengine wa familia. 79 00:03:53,720 --> 00:03:57,256 Kiasi cha asilimia 85 za wasichana na wanawake India 80 00:03:57,280 --> 00:04:02,600 walifuata moja au zaidi ya masharti ya mila kwenye siku zao kila mwezi. 81 00:04:03,320 --> 00:04:04,856 Unafikiria hii inafanya nini 82 00:04:04,880 --> 00:04:07,840 katika kujithamini na kujiamini kwa msichana mdogo? 83 00:04:08,720 --> 00:04:11,456 Kiwewe cha kisaikolojia ambacho hili huumiza, 84 00:04:11,480 --> 00:04:14,056 kuathiri haiba yake, 85 00:04:14,080 --> 00:04:15,816 utendaji wake kimasomo 86 00:04:15,840 --> 00:04:20,480 na kila kipengele cha ukuaji katika miaka ya awali ya uumbaji wake? 87 00:04:21,760 --> 00:04:25,800 Nilifuata kwa bidii masharti haya yote ya kimila kwa miaka 13, 88 00:04:26,400 --> 00:04:28,776 hadi mjadala na mshirika mwenzangu, Tuhin, 89 00:04:28,800 --> 00:04:31,360 ulipobadilisha mtazamo wangu kuhusu hedhi milele. 90 00:04:32,280 --> 00:04:37,736 Mwaka 2009, mimi na Tuhin tulikuwa tunasoma stashada katika ubunifu. 91 00:04:37,760 --> 00:04:39,416 Tukapendana 92 00:04:39,440 --> 00:04:41,880 na nilikuwa huru kujadiliana naye kuhusu siku zangu. 93 00:04:42,640 --> 00:04:44,560 Tuhin alijua kidogo kuhusu siku. 94 00:04:45,520 --> 00:04:47,800 (Kicheko) 95 00:04:51,800 --> 00:04:55,416 Alishangazwa kujua kwamba wasichana hupata maumivu makali 96 00:04:55,440 --> 00:04:56,856 na hutokwa damu kila mwezi. 97 00:04:56,880 --> 00:04:58,976 (Kicheko) 98 00:04:59,000 --> 00:05:00,496 Ndio. 99 00:05:00,520 --> 00:05:02,296 Alishtushwa kabisa kujua 100 00:05:02,320 --> 00:05:07,496 kuhusu vizuizi vinavyowekwa kwa wasichana na wanawake walio kwenye hedhi 101 00:05:07,520 --> 00:05:10,096 na familia pamoja na jamii zao wenyewe. 102 00:05:10,120 --> 00:05:12,176 Ili kuweza kunisaidia na maumivu yangu, 103 00:05:12,200 --> 00:05:16,000 alikwenda kwenye mtandao wa intaneti kujifunza kuhusu hedhi. 104 00:05:16,600 --> 00:05:18,336 Aliponielezea alichojifunza, 105 00:05:18,360 --> 00:05:21,360 Niligundua ufahamu mdogo nilionao kuhusu hedhi, 106 00:05:21,960 --> 00:05:25,080 na vitu vingi nilivyoamini vilikuja kuwa ni imani potofu, 107 00:05:26,360 --> 00:05:27,896 Ndipo nilipojiuliza: 108 00:05:27,920 --> 00:05:30,256 kama sisi, tumesoma vizuri hivi, 109 00:05:30,280 --> 00:05:32,376 tumefundishwa vibaya kuhusu hedhi, 110 00:05:32,400 --> 00:05:36,400 kutakuwa na mamilioni ya wasichana huko nje waliofundishwa vibaya, pia. 111 00:05:37,760 --> 00:05:38,976 Kusoma-- 112 00:05:39,000 --> 00:05:40,776 kuelewa tatizo vizuri, 113 00:05:40,800 --> 00:05:45,416 Nilifanya utafiti wa mwaka mmoja kujifunza ukosefu wa ufahamu kuhusu hedhi 114 00:05:45,440 --> 00:05:47,040 na chanzo chake nyuma yake. 115 00:05:47,960 --> 00:05:49,696 Wakati kiujumla inaaminika 116 00:05:49,720 --> 00:05:55,696 kwamba kutokufahamu hedhi na kuelewa vibaya ni tatizo la vijijini, 117 00:05:55,720 --> 00:05:56,936 katika utafiti wangu, 118 00:05:56,960 --> 00:05:59,936 Niligundua kwamba ni tatizo la mijini pia. 119 00:05:59,960 --> 00:06:04,320 Na lipo kwa daraja la walioelimika mijini, pia. 120 00:06:05,280 --> 00:06:07,776 Wakati naongea na wazazi wengi pamoja na waalimu, 121 00:06:07,800 --> 00:06:13,096 Niligundua kuwa wengi wao walitaka kuelimisha wasichana kuhusu siku zao 122 00:06:13,120 --> 00:06:15,760 kabla hawajaanza kupata mzunguko wao wa hedhi. 123 00:06:16,840 --> 00:06:18,056 Na-- 124 00:06:18,080 --> 00:06:21,616 lakini wenyewe walikosa njia stahiki. 125 00:06:21,640 --> 00:06:22,896 Na kwavile ni mwiko, 126 00:06:22,920 --> 00:06:25,960 wanajisikia kusita na fedheha kuongelea jambo hilo. 127 00:06:26,840 --> 00:06:31,456 Wasichana siku hizi hupata siku zao wakiwa darasa la sita na la saba, 128 00:06:31,480 --> 00:06:33,096 lakini mtaala wetu wa elimu 129 00:06:33,120 --> 00:06:36,920 hufundisha wasichana kuhusu siku zao darasa la nane na la tisa tu. 130 00:06:37,800 --> 00:06:39,360 na kwa vile ni mwiko, 131 00:06:40,000 --> 00:06:43,440 waalimu bado wanairuka mada. 132 00:06:44,840 --> 00:06:49,096 Hivyo shule haziwafundishi wasichana kuhusu siku zao, 133 00:06:49,120 --> 00:06:51,256 wazazi hawazungumzii jambo hilo. 134 00:06:51,280 --> 00:06:52,680 Wasichana wanaenda wapi? 135 00:06:53,680 --> 00:06:56,520 Miongo miwili iliyopita na sasa-- 136 00:06:57,120 --> 00:06:58,400 hakuna kilichobadilika. 137 00:07:00,120 --> 00:07:02,940 Nilimshirikisha Tuhin matokeo yangu na tulijiuliza 138 00:07:02,960 --> 00:07:04,576 Itakuwaje tukianzisha kitu 139 00:07:04,600 --> 00:07:09,176 ambacho kitasaidia wasichana kuelewa kuhusu hedhi wao wenyewe -- 140 00:07:09,200 --> 00:07:13,416 Kitu ambacho kitawasaidia wazazi na waalimu 141 00:07:13,440 --> 00:07:16,360 kuongelea kuhusu siku za hedhi kwa raha kwa wasichana wadogo? 142 00:07:17,840 --> 00:07:19,456 Wakati wa utafiti wangu, 143 00:07:19,480 --> 00:07:21,456 Nilikuwa nakusanya hadithi nyingi. 144 00:07:21,480 --> 00:07:26,160 Hizi ni hadithi za mambo waliyopitia wasichana kipindi cha siku zao. 145 00:07:26,800 --> 00:07:30,056 Hadithi hizi zitawafanya wasichana wawe wadadisi na kuvutiwa 146 00:07:30,080 --> 00:07:34,016 katika kuongea kuhusu hedhi ndani ya watu wao wa karibu. 147 00:07:34,040 --> 00:07:35,496 Hicho ndio tulichotaka. 148 00:07:35,520 --> 00:07:38,856 Tulitaka kitu ambacho kingewafanya wasichana wawe wadadisi 149 00:07:38,880 --> 00:07:41,056 na kuwasukuma kujifunza. 150 00:07:41,080 --> 00:07:44,240 Tulitaka kutumia hadithi hizi kufundisha wasichana kuhusu siku zao. 151 00:07:45,360 --> 00:07:48,456 Hivyo tukaamua kutengeneza kitabu cha vikatuni 152 00:07:48,480 --> 00:07:51,736 ambapo wahusika wa katuni wataigiza hadithi hizi 153 00:07:51,760 --> 00:07:55,640 na kuwaelimisha wasichana kuhusu hedhi kwa njia ya kufurahisha na kuwashirikisha. 154 00:07:56,360 --> 00:07:59,376 Kuwasilisha wasichana katika hatua zao tofauti za kubalehe, 155 00:07:59,400 --> 00:08:01,040 tunao wahusika watatu. 156 00:08:01,560 --> 00:08:04,736 Pinki, ambaye hajapata siku zake bado, 157 00:08:04,760 --> 00:08:08,256 Jiya anayepata siku zake wakati wa simulizi za kitabu 158 00:08:08,280 --> 00:08:11,536 na Mira ambaye tayari amekuwa akipata siku zake. 159 00:08:11,560 --> 00:08:13,976 Kuna mhusika wa nne, Priya Didi. 160 00:08:14,000 --> 00:08:17,536 Kupitia yeye, wasichana wanakuja kujua kuhusu vipengele kadhaa vya ukuaji 161 00:08:17,560 --> 00:08:19,360 na kusimamia usafi wa hedhi. 162 00:08:20,455 --> 00:08:22,398 Utengenezaji kitabu, ulitumia umakini 163 00:08:22,423 --> 00:08:26,376 hakuna katika vielelezo ambavyo vilikuwa na pingamizi lolote 164 00:08:26,400 --> 00:08:28,360 na hiyo ni nyeti kitamaduni. 165 00:08:29,200 --> 00:08:33,056 Wakati wa majaribio ya sampuli ya awali tuligundua wasichana wakilipenda kitabu. 166 00:08:33,080 --> 00:08:34,456 Walikuwa na hamu ya kukisoma 167 00:08:34,480 --> 00:08:37,240 na kujua zaidi na zaidi kuhusu siku zao wao wenyewe. 168 00:08:38,039 --> 00:08:41,056 Wazazi na waalimu walikuwa hawaoni shida kuongea kuhusu siku 169 00:08:41,080 --> 00:08:42,775 kwa wasichana wadogo kutumia kitabu 170 00:08:42,799 --> 00:08:45,776 na wakati mwingine hata wavulana walivutiwa kukisoma. 171 00:08:45,800 --> 00:08:47,936 (Kicheko) 172 00:08:47,960 --> 00:08:49,720 (Makofi) 173 00:08:51,840 --> 00:08:55,656 Kitabu cha vikatu kilisaidia katika kujenga mazingira 174 00:08:55,680 --> 00:08:58,120 ambapo itasimamisha hedhi kuwa mwiko. 175 00:08:58,720 --> 00:09:02,776 Wengi wa waliojitolea walichukua hii sampuli ya awali kuelimisha wasichana 176 00:09:02,800 --> 00:09:06,736 na kufanya warsha za kuelimisha hedhi katika majimbo matano tofauti India. 177 00:09:06,760 --> 00:09:10,136 na mmoja wa waliojitolea alitumia sampuli hii kuelimisha watawa vijana 178 00:09:10,160 --> 00:09:12,376 na aliipeleka kwenye nyumba ya utawa Ladakh. 179 00:09:12,400 --> 00:09:15,736 Tulitengeneza toleo la mwisho la kitabu, tukakiita "Menstrupedia Comic" 180 00:09:15,760 --> 00:09:18,520 na kukizindua Septemba mwaka jana. 181 00:09:19,120 --> 00:09:20,496 Na mpaka sasa, 182 00:09:20,520 --> 00:09:24,856 zaidi ya wasichana 4,000 wameelimika kwa kutumia kitabu India na -- 183 00:09:24,880 --> 00:09:27,536 (Makofi) 184 00:09:27,560 --> 00:09:28,776 Asanteni. 185 00:09:28,800 --> 00:09:31,120 (Makofi) 186 00:09:34,240 --> 00:09:36,040 na nchi nyingine 10. 187 00:09:37,160 --> 00:09:40,176 Mara kwa mara tunakitafsiri kitabu katika lugha tofauti 188 00:09:40,200 --> 00:09:42,936 Na kushirikiana na mashirika ya ndani nchi 189 00:09:42,960 --> 00:09:45,616 na kufanya hiki kitabu kipatikane katika nchi tofauti. 190 00:09:45,640 --> 00:09:48,576 Mashule 15 katika sehemu tofauti India 191 00:09:48,600 --> 00:09:52,016 yamekifanya kitabu hiki kuwa sehemu ya mtaala wa shule zao 192 00:09:52,040 --> 00:09:53,816 kufundisha wasichana kuhusu hedhi. 193 00:09:53,840 --> 00:09:56,240 (Makofi) 194 00:10:00,440 --> 00:10:05,776 Nafurahishwa kuona jinsi wanaojitolea, 195 00:10:05,800 --> 00:10:09,936 watu binafsi, wazazi waalimu, wakuu wa mashule 196 00:10:09,960 --> 00:10:11,456 wamekutana pamoja 197 00:10:11,480 --> 00:10:15,736 na kufanya msukumo huu wa ufahamishaji wa hedhi kwa jamii zao, 198 00:10:15,760 --> 00:10:19,456 wamehakikisha wasichana wanajifunza kuhusu siku zao katika umri sahihi 199 00:10:19,480 --> 00:10:21,640 na kusaidia katika kuvunja mwiko huu 200 00:10:23,040 --> 00:10:27,336 Ninaota maisha ya mbele ambapo hedhi sio laana, 201 00:10:27,360 --> 00:10:28,896 sio ugonjwa, 202 00:10:28,920 --> 00:10:31,360 ila ni mabadiliko katika maisha ya msichana. 203 00:10:32,120 --> 00:10:33,336 Na ninge -- 204 00:10:33,360 --> 00:10:35,480 (Makofi) 205 00:10:37,960 --> 00:10:39,336 Na ningependa kumalizia hii 206 00:10:39,360 --> 00:10:43,256 kwa ombi dogo kwa wazazi wote hapa. 207 00:10:43,280 --> 00:10:44,480 Wapendwa wazazi, 208 00:10:45,240 --> 00:10:47,456 kama mtakuwa mnafedheheshwa na hedhi 209 00:10:47,480 --> 00:10:49,696 na mabinti zenu watafedheheshwa, pia. 210 00:10:49,720 --> 00:10:52,176 Hivyo tafadhali muwe na mtazamo chanya katika siku. 211 00:10:52,200 --> 00:10:53,416 (Kicheko) 212 00:10:53,440 --> 00:10:54,656 Asanteni. 213 00:10:54,680 --> 00:10:57,403 (Makofi)