0:00:00.520,0:00:02.096 Siku. 0:00:02.120,0:00:03.496 Damu. 0:00:03.520,0:00:04.720 Hedhi. 0:00:05.440,0:00:07.016 Uchafu. 0:00:07.040,0:00:08.656 Siri. 0:00:08.680,0:00:09.880 Kuficha. 0:00:10.400,0:00:11.600 Kwanini? 0:00:12.760,0:00:14.656 Utaratibu asilia kibaolojia 0:00:14.680,0:00:18.496 ambao kila msichana na mwanamke[br]anapitia kila mwezi 0:00:18.520,0:00:20.696 kwa karibia nusu ya maisha yake. 0:00:20.720,0:00:23.416 Jambo ambalo ni la umuhimu mkubwa sana 0:00:23.440,0:00:27.640 kiasi kwamba kupona na uenezwaji[br]wa spishi zetu unautegemea. 0:00:28.480,0:00:30.320 Bado tunauchukulia kama mwiko. 0:00:31.160,0:00:34.040 Tunajisikia ugumu[br]na fedheha kuliongelea. 0:00:35.840,0:00:37.656 Nilipopata siku zangu mara ya kwanza, 0:00:37.680,0:00:40.040 Niliambiwa nifanye iwe[br]siri nisiwaambie wengine-- 0:00:40.760,0:00:42.640 hata kwa baba yangu au kaka. 0:00:43.640,0:00:46.256 Baadaye wakati hili somo[br]limejitokeza vitabuni mwetu, 0:00:46.280,0:00:48.616 mwalimu wetu wa baolojia aliiruka mada. 0:00:48.640,0:00:51.320 (Kicheko) 0:00:52.000,0:00:53.680 Nilijifunza nini kutokana na hili? 0:00:54.360,0:00:57.520 Nilijifunza kwamba[br]ni fedheha mno kuongelea jambo hili. 0:00:58.080,0:01:00.736 Nilijifunza kufedheshwa na mwili wangu. 0:01:00.760,0:01:03.816 Nilijifunza kutokufahamu siku zangu 0:01:03.840,0:01:05.800 ili kuweza kubaki na heshima. 0:01:06.440,0:01:08.256 Utafiti katika sehemu mbalimbali India 0:01:08.280,0:01:13.016 waonyesha wasichana watatu kati ya kumi[br]hawafahamu kuhusu hedhi 0:01:13.040,0:01:14.800 wakati wa siku zao za kwanza. 0:01:15.400,0:01:17.016 Na baadhi ya sehemu za Rajasthan 0:01:17.040,0:01:21.880 hii namba ni kubwa kama wasichana tisa[br]kati ya kumi kutokufahamu 0:01:22.800,0:01:24.456 Unaweza kushangazwa kujua 0:01:24.480,0:01:26.696 kwamba wasichana wengi[br]nilioongea nao, 0:01:26.720,0:01:30.536 waliokuwa hawajui kuhusu siku zao[br]wakati wa hedhi zao za kwanza 0:01:30.560,0:01:32.936 walifikiria kuwa wana saratani ya damu 0:01:32.960,0:01:34.560 na watakufa muda sio mrefu. 0:01:36.760,0:01:39.696 Usafi wa hedhi[br]ni kipengele muhimu cha hatari 0:01:39.720,0:01:42.280 kwa maambukizi wa mfumo wa via vya uzazi. 0:01:43.040,0:01:46.216 Lakini India, ni asilimia 12 tu[br]ya wasichana na wanawake 0:01:46.240,0:01:50.000 wanaweza kupata njia za usafi[br]wa kumudu siku zao. 0:01:50.840,0:01:52.336 Ukifanya mahesabu, 0:01:52.360,0:01:57.456 asilimia 88 ya wasichana na wanawake[br]hutumia njia zisizo salama kwa siku zao. 0:01:57.480,0:01:58.680 Nilikuwa mmoja wao. 0:01:59.880,0:02:02.816 Nilikulia kwenye mji mdogo[br]uitwao Garhwa, jimbo la Jharkhand, 0:02:02.840,0:02:05.960 ambako hata kununua pedi[br]ilichukuliwa kama fedheha. 0:02:06.840,0:02:08.895 Sasa nilipoanza kupata siku zangu, 0:02:08.919,0:02:10.680 Nilianza kutumia matambara. 0:02:12.560,0:02:15.216 Baada ya kila matumizi[br]niliyafua na kuyatumia tena. 0:02:15.240,0:02:16.496 Lakini kuyahifadhi, 0:02:16.520,0:02:19.136 Niliyaficha na kuyaweka[br]sehemu yenye giza na unyevu 0:02:19.160,0:02:21.760 ilikwamba mtu asijue[br]kuwa niko kwenye hedhi. 0:02:22.520,0:02:25.136 Kwa kuyarudia kufua[br]matambara yalikuja kuwa magumu, 0:02:25.160,0:02:28.160 na mara nyingi nilipata upele[br]na maambukizi kwa kuyatumia. 0:02:28.880,0:02:33.160 Niliyavaa kwa muda wa miaka mitano[br]hadi nilipohama ule mji. 0:02:35.640,0:02:37.976 Suala lingine[br]ambalo siku zilileta maishani mwangu 0:02:38.000,0:02:40.296 lile la kuwekewa mipaka kijamii 0:02:40.320,0:02:44.656 iliyowekwa kwa wasichana wetu[br]na wanawake wakiwa kwenye siku zao. 0:02:44.680,0:02:46.976 Nafikiri wote lazma mtakuwa mnajua, 0:02:47.000,0:02:49.960 lakini bado nitaelezea[br]kwa wale wachache wasiojua. 0:02:50.720,0:02:53.200 Sikuruhusiwa kula au kugusa vitu vichachu. 0:02:53.840,0:02:58.696 Sikuruhusiwa kukaa kwenye sofa[br]au kitandani mwa ndugu wa familia. 0:02:58.720,0:03:01.176 Nilitakiwa kufua mashuka[br]kila baada ya siku zangu, 0:03:01.200,0:03:03.136 hata kama hazikuchafuka kwa madoa. 0:03:03.160,0:03:04.976 Nilichukuliwa kama najisi 0:03:05.000,0:03:09.800 na kukatazwa kuabudu au kugusa[br]kitu chochote chenye umuhimu kidini. 0:03:10.880,0:03:13.096 Ulikutana na matangazo nje ya misikiti 0:03:13.120,0:03:15.560 kukataza wasichana[br]na wanawake walio kwenye hedhi. 0:03:17.080,0:03:18.456 Chakuchekesha, 0:03:18.480,0:03:21.296 wakati wote ni wanawake watu wazima 0:03:21.320,0:03:25.760 ndio walioweka vizuizi hivyo[br]kwa wasichana wadogo katika familia. 0:03:26.360,0:03:30.536 hata hivyo, wamekua[br]wakikubali vizuizi hivyo kama desturi. 0:03:30.560,0:03:33.576 Na katika kukosekana kwa kuingiliwa, 0:03:33.600,0:03:35.616 ni imani potofu na kutoeleweka 0:03:35.640,0:03:38.240 kunakoenezwa[br]kizazi hata kizazi. 0:03:39.240,0:03:41.096 Kwa miaka nilyofanyia kazi [br]taaluma hii, 0:03:41.120,0:03:42.616 Nimeshakutana na hadithi 0:03:42.640,0:03:46.256 ambapo wasichana walitakiwa kula[br]na kuosha vyombo vyao kwa kutengwa. 0:03:46.280,0:03:48.616 Hawakuruhusiwa [br]kuoga wakati wa siku zao, 0:03:48.640,0:03:52.720 na katika nyumba nyingine walitengwa[br]hata na ndugu wengine wa familia. 0:03:53.720,0:03:57.256 Kiasi cha asilimia 85 za wasichana[br]na wanawake India 0:03:57.280,0:04:02.600 walifuata moja au zaidi ya masharti[br]ya mila kwenye siku zao kila mwezi. 0:04:03.320,0:04:04.856 Unafikiria hii inafanya nini 0:04:04.880,0:04:07.840 katika kujithamini[br]na kujiamini kwa msichana mdogo? 0:04:08.720,0:04:11.456 Kiwewe cha kisaikolojia[br]ambacho hili huumiza, 0:04:11.480,0:04:14.056 kuathiri haiba yake, 0:04:14.080,0:04:15.816 utendaji wake kimasomo 0:04:15.840,0:04:20.480 na kila kipengele cha ukuaji[br]katika miaka ya awali ya uumbaji wake? 0:04:21.760,0:04:25.800 Nilifuata kwa bidii masharti haya yote[br]ya kimila kwa miaka 13, 0:04:26.400,0:04:28.776 hadi mjadala na mshirika mwenzangu, Tuhin, 0:04:28.800,0:04:31.360 ulipobadilisha mtazamo wangu[br]kuhusu hedhi milele. 0:04:32.280,0:04:37.736 Mwaka 2009, mimi na Tuhin tulikuwa [br]tunasoma stashada katika ubunifu. 0:04:37.760,0:04:39.416 Tukapendana 0:04:39.440,0:04:41.880 na nilikuwa huru[br]kujadiliana naye kuhusu siku zangu. 0:04:42.640,0:04:44.560 Tuhin alijua kidogo kuhusu siku. 0:04:45.520,0:04:47.800 (Kicheko) 0:04:51.800,0:04:55.416 Alishangazwa kujua kwamba[br]wasichana hupata maumivu makali 0:04:55.440,0:04:56.856 na hutokwa damu kila mwezi. 0:04:56.880,0:04:58.976 (Kicheko) 0:04:59.000,0:05:00.496 Ndio. 0:05:00.520,0:05:02.296 Alishtushwa kabisa kujua 0:05:02.320,0:05:07.496 kuhusu vizuizi vinavyowekwa kwa[br]wasichana na wanawake walio kwenye hedhi 0:05:07.520,0:05:10.096 na familia pamoja na jamii zao wenyewe. 0:05:10.120,0:05:12.176 Ili kuweza kunisaidia na maumivu yangu, 0:05:12.200,0:05:16.000 alikwenda kwenye mtandao wa intaneti[br]kujifunza kuhusu hedhi. 0:05:16.600,0:05:18.336 Aliponielezea alichojifunza, 0:05:18.360,0:05:21.360 Niligundua ufahamu mdogo[br]nilionao kuhusu hedhi, 0:05:21.960,0:05:25.080 na vitu vingi nilivyoamini[br]vilikuja kuwa ni imani potofu, 0:05:26.360,0:05:27.896 Ndipo nilipojiuliza: 0:05:27.920,0:05:30.256 kama sisi, tumesoma vizuri hivi, 0:05:30.280,0:05:32.376 tumefundishwa vibaya kuhusu hedhi, 0:05:32.400,0:05:36.400 kutakuwa na mamilioni ya wasichana huko [br]nje waliofundishwa vibaya, pia. 0:05:37.760,0:05:38.976 Kusoma-- 0:05:39.000,0:05:40.776 kuelewa tatizo vizuri, 0:05:40.800,0:05:45.416 Nilifanya utafiti wa mwaka mmoja kujifunza[br]ukosefu wa ufahamu kuhusu hedhi 0:05:45.440,0:05:47.040 na chanzo chake nyuma yake. 0:05:47.960,0:05:49.696 Wakati kiujumla inaaminika 0:05:49.720,0:05:55.696 kwamba kutokufahamu hedhi na[br]kuelewa vibaya ni tatizo la vijijini, 0:05:55.720,0:05:56.936 katika utafiti wangu, 0:05:56.960,0:05:59.936 Niligundua kwamba[br]ni tatizo la mijini pia. 0:05:59.960,0:06:04.320 Na lipo kwa daraja la walioelimika[br]mijini, pia. 0:06:05.280,0:06:07.776 Wakati naongea na wazazi wengi[br]pamoja na waalimu, 0:06:07.800,0:06:13.096 Niligundua kuwa wengi wao walitaka[br]kuelimisha wasichana kuhusu siku zao 0:06:13.120,0:06:15.760 kabla hawajaanza[br]kupata mzunguko wao wa hedhi. 0:06:16.840,0:06:18.056 Na-- 0:06:18.080,0:06:21.616 lakini wenyewe walikosa[br]njia stahiki. 0:06:21.640,0:06:22.896 Na kwavile ni mwiko, 0:06:22.920,0:06:25.960 wanajisikia kusita[br]na fedheha kuongelea jambo hilo. 0:06:26.840,0:06:31.456 Wasichana siku hizi hupata siku zao[br]wakiwa darasa la sita na la saba, 0:06:31.480,0:06:33.096 lakini mtaala wetu wa elimu 0:06:33.120,0:06:36.920 hufundisha wasichana kuhusu siku zao[br]darasa la nane na la tisa tu. 0:06:37.800,0:06:39.360 na kwa vile ni mwiko, 0:06:40.000,0:06:43.440 waalimu bado[br]wanairuka mada. 0:06:44.840,0:06:49.096 Hivyo shule haziwafundishi[br]wasichana kuhusu siku zao, 0:06:49.120,0:06:51.256 wazazi hawazungumzii jambo hilo. 0:06:51.280,0:06:52.680 Wasichana wanaenda wapi? 0:06:53.680,0:06:56.520 Miongo miwili iliyopita na sasa-- 0:06:57.120,0:06:58.400 hakuna kilichobadilika. 0:07:00.120,0:07:02.940 Nilimshirikisha Tuhin matokeo yangu[br]na tulijiuliza 0:07:02.960,0:07:04.576 Itakuwaje tukianzisha kitu 0:07:04.600,0:07:09.176 ambacho kitasaidia wasichana kuelewa[br]kuhusu hedhi wao wenyewe -- 0:07:09.200,0:07:13.416 Kitu ambacho kitawasaidia[br]wazazi na waalimu 0:07:13.440,0:07:16.360 kuongelea kuhusu siku za hedhi[br]kwa raha kwa wasichana wadogo? 0:07:17.840,0:07:19.456 Wakati wa utafiti wangu, 0:07:19.480,0:07:21.456 Nilikuwa nakusanya hadithi nyingi. 0:07:21.480,0:07:26.160 Hizi ni hadithi za mambo waliyopitia[br]wasichana kipindi cha siku zao. 0:07:26.800,0:07:30.056 Hadithi hizi zitawafanya wasichana[br]wawe wadadisi na kuvutiwa 0:07:30.080,0:07:34.016 katika kuongea kuhusu hedhi[br]ndani ya watu wao wa karibu. 0:07:34.040,0:07:35.496 Hicho ndio tulichotaka. 0:07:35.520,0:07:38.856 Tulitaka kitu ambacho[br]kingewafanya wasichana wawe wadadisi 0:07:38.880,0:07:41.056 na kuwasukuma kujifunza. 0:07:41.080,0:07:44.240 Tulitaka kutumia hadithi hizi[br]kufundisha wasichana kuhusu siku zao. 0:07:45.360,0:07:48.456 Hivyo tukaamua kutengeneza kitabu[br]cha vikatuni 0:07:48.480,0:07:51.736 ambapo wahusika wa katuni[br]wataigiza hadithi hizi 0:07:51.760,0:07:55.640 na kuwaelimisha wasichana kuhusu hedhi[br]kwa njia ya kufurahisha na kuwashirikisha. 0:07:56.360,0:07:59.376 Kuwasilisha wasichana[br]katika hatua zao tofauti za kubalehe, 0:07:59.400,0:08:01.040 tunao wahusika watatu. 0:08:01.560,0:08:04.736 Pinki, ambaye hajapata siku zake bado, 0:08:04.760,0:08:08.256 Jiya anayepata siku zake[br]wakati wa simulizi za kitabu 0:08:08.280,0:08:11.536 na Mira ambaye tayari[br]amekuwa akipata siku zake. 0:08:11.560,0:08:13.976 Kuna mhusika wa nne, Priya Didi. 0:08:14.000,0:08:17.536 Kupitia yeye, wasichana wanakuja kujua[br]kuhusu vipengele kadhaa vya ukuaji 0:08:17.560,0:08:19.360 na kusimamia usafi wa hedhi. 0:08:20.455,0:08:22.398 Utengenezaji kitabu,[br]ulitumia umakini 0:08:22.423,0:08:26.376 hakuna katika vielelezo ambavyo[br]vilikuwa na pingamizi lolote 0:08:26.400,0:08:28.360 na hiyo ni nyeti kitamaduni. 0:08:29.200,0:08:33.056 Wakati wa majaribio ya sampuli ya awali[br]tuligundua wasichana wakilipenda kitabu. 0:08:33.080,0:08:34.456 Walikuwa na hamu ya kukisoma 0:08:34.480,0:08:37.240 na kujua zaidi na zaidi[br]kuhusu siku zao wao wenyewe. 0:08:38.039,0:08:41.056 Wazazi na waalimu walikuwa[br]hawaoni shida kuongea kuhusu siku 0:08:41.080,0:08:42.775 kwa wasichana wadogo kutumia kitabu 0:08:42.799,0:08:45.776 na wakati mwingine hata wavulana[br]walivutiwa kukisoma. 0:08:45.800,0:08:47.936 (Kicheko) 0:08:47.960,0:08:49.720 (Makofi) 0:08:51.840,0:08:55.656 Kitabu cha vikatu kilisaidia[br]katika kujenga mazingira 0:08:55.680,0:08:58.120 ambapo itasimamisha hedhi kuwa mwiko. 0:08:58.720,0:09:02.776 Wengi wa waliojitolea walichukua hii[br]sampuli ya awali kuelimisha wasichana 0:09:02.800,0:09:06.736 na kufanya warsha za kuelimisha hedhi[br]katika majimbo matano tofauti India. 0:09:06.760,0:09:10.136 na mmoja wa waliojitolea alitumia[br]sampuli hii kuelimisha watawa vijana 0:09:10.160,0:09:12.376 na aliipeleka kwenye nyumba ya utawa[br]Ladakh. 0:09:12.400,0:09:15.736 Tulitengeneza toleo la mwisho la kitabu,[br]tukakiita "Menstrupedia Comic" 0:09:15.760,0:09:18.520 na kukizindua Septemba mwaka jana. 0:09:19.120,0:09:20.496 Na mpaka sasa, 0:09:20.520,0:09:24.856 zaidi ya wasichana 4,000 wameelimika[br]kwa kutumia kitabu India na -- 0:09:24.880,0:09:27.536 (Makofi) 0:09:27.560,0:09:28.776 Asanteni. 0:09:28.800,0:09:31.120 (Makofi) 0:09:34.240,0:09:36.040 na nchi nyingine 10. 0:09:37.160,0:09:40.176 Mara kwa mara tunakitafsiri kitabu[br]katika lugha tofauti 0:09:40.200,0:09:42.936 Na kushirikiana na mashirika ya ndani[br]nchi 0:09:42.960,0:09:45.616 na kufanya hiki kitabu kipatikane[br]katika nchi tofauti. 0:09:45.640,0:09:48.576 Mashule 15 katika sehemu tofauti India 0:09:48.600,0:09:52.016 yamekifanya kitabu hiki[br]kuwa sehemu ya mtaala wa shule zao 0:09:52.040,0:09:53.816 kufundisha wasichana kuhusu hedhi. 0:09:53.840,0:09:56.240 (Makofi) 0:10:00.440,0:10:05.776 Nafurahishwa kuona jinsi wanaojitolea, 0:10:05.800,0:10:09.936 watu binafsi, wazazi[br]waalimu, wakuu wa mashule 0:10:09.960,0:10:11.456 wamekutana pamoja 0:10:11.480,0:10:15.736 na kufanya msukumo huu wa ufahamishaji[br]wa hedhi kwa jamii zao, 0:10:15.760,0:10:19.456 wamehakikisha wasichana wanajifunza[br]kuhusu siku zao katika umri sahihi 0:10:19.480,0:10:21.640 na kusaidia katika kuvunja mwiko huu 0:10:23.040,0:10:27.336 Ninaota maisha ya mbele[br]ambapo hedhi sio laana, 0:10:27.360,0:10:28.896 sio ugonjwa, 0:10:28.920,0:10:31.360 ila ni mabadiliko katika[br]maisha ya msichana. 0:10:32.120,0:10:33.336 Na ninge -- 0:10:33.360,0:10:35.480 (Makofi) 0:10:37.960,0:10:39.336 Na ningependa kumalizia hii 0:10:39.360,0:10:43.256 kwa ombi dogo[br]kwa wazazi wote hapa. 0:10:43.280,0:10:44.480 Wapendwa wazazi, 0:10:45.240,0:10:47.456 kama mtakuwa mnafedheheshwa na hedhi 0:10:47.480,0:10:49.696 na mabinti zenu watafedheheshwa, pia. 0:10:49.720,0:10:52.176 Hivyo tafadhali muwe na mtazamo chanya[br]katika siku. 0:10:52.200,0:10:53.416 (Kicheko) 0:10:53.440,0:10:54.656 Asanteni. 0:10:54.680,0:10:57.403 (Makofi)