Kwa nini waathirika wa unyanyasaji majumbani hawaondoki
-
0:01 - 0:04Leo niko hapa kuongea kuhusu swala nyeti,
-
0:04 - 0:08ambalo lina jibu tatanishi.
-
0:08 - 0:11Swala langu ni zile siri za ugomvi nyumbani,
-
0:11 - 0:14na swali nitakalokabiliana nalo
-
0:14 - 0:18ni lile swali moja kila mmoja huliuliza kila mara:
-
0:18 - 0:19Kwa nini muathirika hubakia?
-
0:19 - 0:23Kwa nini mtu yeyote abaki na mume ampigaye?
-
0:23 - 0:26Mie si daktari wa akili, mfanyakazi wa ustawi wa jamii
-
0:26 - 0:29au mtaalam wa ugomvi wa nyumbani.
-
0:29 - 0:32Mimi ni mwanamke mwenye hadithi ya kusimulia.
-
0:32 - 0:36Nilikuwa na umri wa miaka ishirini na miwili. Nilikuwa nimehitimu tu kutoka chuo cha Harvard.
-
0:36 - 0:39Nilikuwa nimehamia mjini New York kwa ajili ya kazi yangu ya kwanza
-
0:39 - 0:42kama mwandishi na mhariri wa gazeti la Seventeen.
-
0:42 - 0:44Nilikuwa na nyumba yangu ya kwanza,
-
0:44 - 0:48kadi yangu ya kwanza ya American Express,
-
0:48 - 0:51na nilikuwa na siri moja kubwa sana.
-
0:51 - 0:54Siri yangu ilikuwa kwamba kulikuwa na bunduki
-
0:54 - 0:58iliyojaa risasi iliyoelekezwa kichwani mwangu
-
0:58 - 1:00na mwanamme niliyefikiria alikuwa mpenzi wangu,
-
1:00 - 1:04mara kadhaa.
-
1:04 - 1:07Mwanamme huyu niliyempenda kuliko yeyote duniani
-
1:07 - 1:11alielekeza bunduki kichwani mwangu na kutishia kuniua
-
1:11 - 1:15mara nyingi kuliko zile ningeweza kukumbuka.
-
1:15 - 1:17Niko hapa kuwapa hadithi ya upendo wa kupindukia,
-
1:17 - 1:20mtego wa kisaikolojia uliofichwa kama mapenzi,
-
1:20 - 1:23ambao mamilioni ya wanawake na hata wanaume wengine
-
1:23 - 1:26hutumbukia kila mwaka.
-
1:26 - 1:28Inaweza hata kuwa hadithi yako.
-
1:28 - 1:32Sionekani kama mtu niliyenusurika na ugomvi katika mahusiano.
-
1:32 - 1:34Nina shahada ya sanaa katika Kiigereza kutoka chuo cha Harvard,
-
1:34 - 1:36na shahada ya juu katika mauzo kutoka kwa chuo cha biashara cha Wharton.
-
1:36 - 1:39Nimetumia muda mrefu maishani nikifanya kazi kwenye kampuni bora duniani
-
1:39 - 1:44zikiwemo Johnson & Johnson, Leo Burnett na The Washington Post.
-
1:44 - 1:48Nimeolewa takriban miaka ishirini kwa mme wangu wa pili
-
1:48 - 1:50na tuna wana watatu pamoja
-
1:50 - 1:55Mbwa wangu ni mweusi, na mie huendesha gari ndogo la Honda Odyssey.
-
1:55 - 1:57(Kicheko)
-
1:57 - 2:00Kwa hivyo ujumbe wangu wa kwanza kwenu ni kwamba ugomvi wa nyumbani
-
2:00 - 2:02humtokea yeyote--
-
2:02 - 2:06kila jamii,dini, kila kipato na ngazi ya kimasomo.
-
2:06 - 2:08Iko kila mahali.
-
2:08 - 2:11Na ujumbe wangu wa pili ni kwamba kila mtu hufikiri
-
2:11 - 2:13ugomvi wa nyumbani huwaathiri wanawake,
-
2:13 - 2:15ati ni swala la wanawake.
-
2:15 - 2:17Si sahihi.
-
2:17 - 2:21Zaidi ya asili mia 85 ya wanyanyasaji ni wanaume, na ugomvi wa nyumbani
-
2:21 - 2:27hutokea haswa katika mahusiano ya undani, ya kutegemeana na yale ya muda mrefu,
-
2:27 - 2:30yaani, katika familia,
-
2:30 - 2:33mahali tusipotaka au kutarajia kupata ugomvi,
-
2:33 - 2:38ndio sababu tuhuma za kinyumbani ni tatanishi hivi.
-
2:38 - 2:41Ningekuambia kwamba ningekuwa mtu wa mwisho duniani
-
2:41 - 2:44kukaa na mwanaume anayenipiga,
-
2:44 - 2:47lakini kusema kweli nilikuwa mwathirika kwa sababu ya umri wangu.
-
2:47 - 2:51Nilikuwa mwenye umri wa miaka ishirini na mbili na Marekani,
-
2:51 - 2:54wanawake wenye umri kati ya miaka kumi na sita hadi ishirini na nne wana uwezekano wa mara tatu zaidi
-
2:54 - 2:57kuwa waathirika wa ugomvi wa nyumbani
-
2:57 - 3:00ikilinganishwa na wanawake wa umri mwingine,
-
3:00 - 3:03vilevile zaidi ya wanawake mia tano na wasichana wa umri huu
-
3:03 - 3:07huuawa kila mwaka na wapenzi wanyanyasaji,
-
3:07 - 3:11wapenzi, na waume zao Marekani.
-
3:11 - 3:15Nilikuwa muathirika kwa sababu sikujua chochote
-
3:15 - 3:19kuhusu ugomvi wa nyumbani, maonyo yake ama mifano yake.
-
3:19 - 3:24Nilikutana na Conor usiku mmoja wenye baridi na mvua, mwezi wa Januari.
-
3:24 - 3:27Alikaa kando yangu kwenye treni katika mji wa New York,
-
3:27 - 3:29na alianza kuniongelesha.
-
3:29 - 3:31Aliniambia mambo mawili.
-
3:31 - 3:35La kwanza kuwa, yeye pia, alikuwa amehitimu kutoka kwa kati ya zile shule bora zaidi Marekani,
-
3:35 - 3:39na kwamba alifanya kazi kwenye benki moja ya kuvutia sana huko Wall Street.
-
3:39 - 3:43Lakini kile kilichonivutia zaidi siku hiyo
-
3:43 - 3:46ni kuwa alikuwa mwerevu na mcheshi
-
3:46 - 3:48na alionekana kuwa kijana wa mashambani.
-
3:48 - 3:50Alikuwa na haya mashavu makubwa, haya mashavu makubwa ya waridi
-
3:50 - 3:52na hii nywele za rangi kama ya ngano,
-
3:52 - 3:55na alionekana kuwa mwema sana.
-
3:55 - 3:59Jambo moja la busara Conor alilofanya, kutoka mwanzoni,
-
3:59 - 4:04lilikuwa kufanya kana kwamba nilikuwa mwenye ushawishi mkubwa katika huo uhusiano.
-
4:04 - 4:07Alifanya hivi haswa hapo mwanzo
-
4:07 - 4:09kwa kunihusudu.
-
4:09 - 4:13Tukaanza kutoka pamoja, na alipenda kila kitu kunihusu,
-
4:13 - 4:14ati nilikuwa mwerevu, ati nilisomea chuo cha Harvard,
-
4:14 - 4:17ati nilikuwa mwenye shauku kusaidia wasichana wadogo, na kazi yangu.
-
4:17 - 4:20Alitaka kujua kila kitu kuhusu familia yangu
-
4:20 - 4:23na utoto wangu na matarajio na ndoto zangu.
-
4:23 - 4:26Conor alikuwa na imani nami, kama mwandishi na mwanamke,
-
4:26 - 4:30kwa njia ambayo yeyote mwengine alikuwa hajawahi.
-
4:30 - 4:34Na alileta uaminifu kati yetu
-
4:34 - 4:37kwa kunieleza siri yake,
-
4:37 - 4:41ambayo ilikuwa, alipokuwa mvulana mdogo sana akiwa na umri wa miaka minne
-
4:41 - 4:44alipigwa vibaya sana mara kwa mara
-
4:44 - 4:46na babake wa kambo,
-
4:46 - 4:50na unyanyasaji ulizidi kuwa mbaya zaidi hadi ikambidi aache shule akiwa daraja la nane,
-
4:50 - 4:52ingawa alikuwa mwerevu sana,
-
4:52 - 4:56na kwamba alitumia takriban miaka ishirini kujenga maisha yake upya.
-
4:56 - 4:59Ndiyo sababu hiyo shahada yake kutoka zile shule bora zaidi Marekani,
-
4:59 - 5:02na kazi yake Wall Street na maisha yake mazuri siku za usoni
-
5:02 - 5:04zilikuwa za umuhimu mkubwa sana kwake.
-
5:04 - 5:06Kama ungeniuliza
-
5:06 - 5:12kama huyu mwanamme mwerevu, mcheshi na mwenye kujali aliyenipenda sana
-
5:12 - 5:16angekuja kuniamulia kama ningejipamba au la,
-
5:16 - 5:18ufupi wa sketi zangu,
-
5:18 - 5:20mahali ningeishi, kazi gani ningefanya,
-
5:20 - 5:23marafiki zangu wangekuwa wepi na pale ningekulia Krisimasi
-
5:23 - 5:25ningekucheka,
-
5:25 - 5:28kwa sababu hakukuwa na ushahidi wowote wa tuhuma au uthibiti
-
5:28 - 5:32au hasira kutoka kwa Conor hapo mwanzoni.
-
5:32 - 5:35Sikujua kwamba daraja la kwanza
-
5:35 - 5:37katika uhusiano wowote wenye ugomvi
-
5:37 - 5:41ni kumvuta na kumpumbaza mwathirika
-
5:41 - 5:46Pia sikujua kuwa daraja ya pili ni kumtenga mwathirika.
-
5:46 - 5:50Conor hakuja nyumbani siku moja na kutangaza,
-
5:50 - 5:53"Unajua huu uhusiano wetu kama wa Romeo na Julieti umekuwa mtamu,
-
5:53 - 5:55lakini nataka kwenda katika hatua inayofuata
-
5:55 - 5:59ambapo nitakutenga na kukunyanyasa" - (Kicheko) -
-
5:59 - 6:01"kwa hivyo nataka kukuhamisha kutoka nyumba hii
-
6:01 - 6:02ambapo majirani wanawezakusikia ukipiga mayowe
-
6:02 - 6:05na kukupeleka nje ya mji huu ambapo una marafiki na familia
-
6:05 - 6:08na wafanyakazi wenzako wanaoweza kuona hiyo michubuko."
-
6:08 - 6:12Badala yake, Conor alikuja nyumbani jioni ya Ijumaa moja
-
6:12 - 6:15na akaniambia kuwa alikuwa ameacha kazi siku hiyo,
-
6:15 - 6:17kazi ya ndoto zake,
-
6:17 - 6:22na akasema kwamba alikuwa ameacha kazi hiyo kwa sababu yangu,
-
6:22 - 6:25kwa sababu nilimfanya ahisi usalama na kupendwa
-
6:25 - 6:28ati hakuhitaji tena kujithibitisha huko Wall Street,
-
6:28 - 6:30na alitaka tu kutoka mjini
-
6:30 - 6:33na kukaa mbali na familia yake iliyomnyanyasa.
-
6:33 - 6:36na kuhamia mji mdogo wa New England
-
6:36 - 6:40ambapo angeweza kuanza upya maisha yake nikiwa kando yake.
-
6:40 - 6:44Sikutaka kamwe kuhama kutoka New York,
-
6:44 - 6:48na kuacha kazi ya ndoto zangu,
-
6:48 - 6:50lakini nilifikiria mtu hujitoa muhanga kwa mpenzi wake,
-
6:50 - 6:54kwa hivyo nikakubali na nikaacha kazi yangu,
-
6:54 - 6:56na Conor na mimi tukaondoka Manhattan pamoja.
-
6:56 - 7:01Sikuwai kufikiria kwamba penzi nililokuwa nalo halikuwa la kawaida,
-
7:01 - 7:04na kwamba nilikuwa nikitembea bila habari ndani ya
-
7:04 - 7:09mtego mzuri wa kimwili, kifedha na kiakili
-
7:09 - 7:11Daraja ya pili katika ugomvi wa kimahusiano
-
7:11 - 7:16ni kuleta tishio la vurugu
-
7:16 - 7:18na kuangalia vile linavyomgusa.
-
7:18 - 7:21Na hapa ndipo bunduki zinapoingia.
-
7:21 - 7:24Muda tu tulipohamia New England--unajua,
-
7:24 - 7:26mahali Connor aliposema pangemfanya ajisikie salama--
-
7:26 - 7:29alinunua bunduki tatu.
-
7:29 - 7:32Aliweka moja garini.
-
7:32 - 7:35Aliweka moja chini ya mto kitandani mwetu,
-
7:35 - 7:38na ya tatu alitembea nayo mfukoni nyakati zote.
-
7:38 - 7:40Na alisema alihitaji bunduki hizo
-
7:40 - 7:43kwa sababu ya uchungu aliopitia akiwa mchanga.
-
7:43 - 7:46Alizihitaji kujisikia salama.
-
7:46 - 7:49Lakini bunduki hizo zilikuwa ujumbe kwangu,
-
7:49 - 7:51na ingawa hakuwai kuninyoshea mkono,
-
7:51 - 7:57maisha yangu tayari yalikuwa hatarini kila dakika ya kila siku.
-
7:57 - 8:01Kwanza Conor alinishambulia
-
8:01 - 8:03siku tano kabla ya harusi yetu.
-
8:03 - 8:08Ilikuwa saa moja asubuhi na bado nilikuwa nimevalia vazi la kulala
-
8:08 - 8:12Nilikuwa nafanya kazi kweny kompyuta yangu nikijaribu kumaliza kazi fulani ya uandishi,
-
8:12 - 8:14na nilikuwa nimekasirika,
-
8:14 - 8:17na Conor akatumia hasira zangu kama kisingizio
-
8:17 - 8:20kunikaba koo
-
8:20 - 8:24na kuikaza hadi sikuweza kupumua au kupiga kelele,
-
8:24 - 8:26na alitumia mkazo huo
-
8:26 - 8:30kugonga kichwa changu mara kadhaa kwenye ukuta.
-
8:30 - 8:35Siku tano baadaye, ile michubuko kumi shingoni mwangu ilipotea
-
8:35 - 8:38na nikavaa nguo ya mama yangu ya harusi,
-
8:38 - 8:40na nikafunga ndoa naye.
-
8:40 - 8:42Licha ya yaliyotokea,
-
8:42 - 8:46nilikuwa na hakika tungeishi maisha ya raha milele,
-
8:46 - 8:50kwa sababu nilimpenda, na alinipenda sana.
-
8:50 - 8:53Na aliniomba msamaha.
-
8:53 - 8:57Alikuwa amechoshwa sana na mipango ya harusi yetu
-
8:57 - 8:59na kwa kuwa kitu kimoja na mimi.
-
8:59 - 9:00Halikuwa jambo la kawaida
-
9:00 - 9:04na asingeniumiza tena.
-
9:04 - 9:07Ilitokea mara mbili katika fungate.
-
9:07 - 9:10Mara ya kwanza, nilikuwa naendesha gari kutafuta ufukwe wa siri
-
9:10 - 9:12na nikapotea,
-
9:12 - 9:15na akanipiga ngumi nzito kwenye upande wa kichwa changu
-
9:15 - 9:18hata ule upande mwengine wa kichwa changu ukagonga
-
9:18 - 9:20dirisha lililo kando ya dereva mara kadhaa.
-
9:20 - 9:23Alafu tena siku chache baadaye, tukielekea nyumbani baada ya likizo ya harusi,
-
9:23 - 9:26alikasirishwa na trafiki,
-
9:26 - 9:29na akarusha Big Mac baridi usoni mwangu.
-
9:29 - 9:32Conor aliendelea kunipiga mara moja au mbili kwa wiki
-
9:32 - 9:35kwa miaka miwili na nusu ya ndoa yetu.
-
9:35 - 9:38Nilifanya makosa kufikiria nilikuwa wa kipekee
-
9:38 - 9:41na peke yangu katika hali hii.
-
9:41 - 9:43Mmoja kati ya wanawake watatu wakiAmerika
-
9:43 - 9:47hupitia ugomvi wa nyumbani ama kufuatwa fuatwa wakati mmoja maishani mwake,
-
9:47 - 9:51na CDC inaripoti kwamba watoto milioni kumi na tano
-
9:51 - 9:54wananyanyaswa kila mwaka, milioni kumi na tano.
-
9:54 - 9:59Hivyo basi, nilikuwa kwenye ushirika mzuri sana.
-
9:59 - 10:01Kurudia swali langu:
-
10:01 - 10:03Kwa nini nilibaki?
-
10:03 - 10:06Jibu lenyewe ni rahisi.
-
10:06 - 10:09Sikujua alikuwa akininyanyasa.
-
10:09 - 10:13Hata ingawa alielekeza bunduki zilizo na risasi kichwani mwangu,
-
10:13 - 10:15akanisukuma ngazini,
-
10:15 - 10:16akatishia kuua mbwa wetu,
-
10:16 - 10:20akatoa ufunguo wa gari nikiendesha barabarani,
-
10:20 - 10:23akamwaga maganda ya kahawa kichwani mwangu
-
10:23 - 10:25nikijitayarisha kwa mahojiano ya kazi,
-
10:25 - 10:29SIkuwai hata mara moja kujihisi kuwa mke anayenyanyaswa.
-
10:29 - 10:33Badala yake, nilikuwa mwanamke mwenye nguvu
-
10:33 - 10:35alimpenda sana mwanaume aliyekuwa na shida,
-
10:35 - 10:37na nilikuwa mtu wa pekee duniani
-
10:37 - 10:41ambaye angeweza kumsaidia Conor kukabiliana na mashetani yake.
-
10:41 - 10:45Swali lingine kila mtu huuliza ni,
-
10:45 - 10:47kwa nini hatoki tu?
-
10:47 - 10:51Kwa nini sikuondoka? Ningeweza kuondoka wakati wowote.
-
10:51 - 10:56Kwangu mimi, hili ndilo swali chungu na la kuhuzunisha zaidi ambalo watu huniuliza,
-
10:56 - 10:59kwa sababu sisi waathiriwa tunajua jambo nyinyi msilojua:
-
10:59 - 11:03Ni jambo la hatari sana kumtoroka mnyanyasaji.
-
11:03 - 11:06Kwa sababu daraja ya mwisho katika tuhuma za kinyumbani
-
11:06 - 11:09ni kumuua.
-
11:09 - 11:12Zaidi ya asilimia sabini ya vifo vinavyosababishwa na tuhuma za kinyumbani
-
11:12 - 11:16hutokea baada ya mwathiriwa kukatiza uhusiano huo,
-
11:16 - 11:18baada ya kutoka,
-
11:18 - 11:21kwa sababu wakati huo mnyanyasaji hana chochote cha kupoteza.
-
11:21 - 11:24Matokeo mengine ni pamoja na kufuatwa fuatwa,
-
11:24 - 11:27hata baada ya mnyanyasaji kuoa tena;
-
11:27 - 11:29unyimaji wa hela;
-
11:29 - 11:32na uingiliaji wa mfumo wa mahakama za kifamilia
-
11:32 - 11:34ili kumtia wasiwasi mwathirika na wanawe,
-
11:34 - 11:39ambao mara kwa mara hushurutishwa na majaji wa mahakama za kifamilia
-
11:39 - 11:41kuwa na wakati usiosimamiwa
-
11:41 - 11:45pamoja na mtu yule aliyemtuhumu mama yao.
-
11:45 - 11:49Na bado twauliza, kwa nini hamtoroki tu?
-
11:49 - 11:51Niliweza kuondoka,
-
11:51 - 11:54kwa sababu ya kipigo kibaya cha mwisho
-
11:54 - 11:57kilichofumbua macho yangu.
-
11:57 - 12:00Nilitambua kwamba mtu yule niliyempenda sana
-
12:00 - 12:03angekuja kuniua kama ningeendelea kumuacha hivi hivi tu.
-
12:03 - 12:06Hivyo nikavunja ukimya.
-
12:06 - 12:08Nikawaeleza watu wote:
-
12:08 - 12:12polisi, jirani zangu,
-
12:12 - 12:16marafiki zangu na familia, wageni,
-
12:16 - 12:23na niko hapa leo kwa sababu nyote mlinisaidia.
-
12:23 - 12:25Tuna tabia ya kuwabagua waathirika
-
12:25 - 12:29kama vichwa vibaya vya habari,
-
12:29 - 12:32wanaojitakia maovu, watu walioharibika.
-
12:32 - 12:35Swali hilo, "Kwa nini haondoki?"
-
12:35 - 12:40kwa wengine ni kama kusema, "Ni makosa yake kuendela kukaa hapo,"
-
12:40 - 12:44kana kwamba waathirika huchagua kusudi kupenda wanaume
-
12:44 - 12:46walio na lengo la kutumaliza.
-
12:46 - 12:49Lakini tangu niandike kitabu "Crazy Love,"
-
12:49 - 12:52nimesikia mamia ya hadithi kutoka kwa wanaume na wanawake
-
12:52 - 12:55ambao pia waliondoka,
-
12:55 - 12:59waliojifunza somo muhimu la maisha kutokana na yale yaliyotokea,
-
12:59 - 13:03na waliojenga maisha yao tena--maisha yenye furaha
-
13:03 - 13:06kama wafanyakazi, wake na kina mama,
-
13:06 - 13:10maisha yasiyo na unyanyasaji, kama yangu.
-
13:10 - 13:15Kwa sababu inaonekana kwamba mimi nilikuwa mwathirika halisi wa unyanyasaji majumbani.
-
13:15 - 13:18na msalimika wa unyanyasaji wa majumbani.
-
13:18 - 13:22Niliolewa na mtu mwema na mpole,
-
13:22 - 13:24na pamoja tuna watoto watatu.
-
13:24 - 13:28Nina yule mbwa wangu mweusi, na nina lile gari ndogo.
-
13:28 - 13:31Kile sitawahi kuwa nacho tena,
-
13:31 - 13:34milele,
-
13:34 - 13:36ni bunduki iliyojaa risasi iliyoelekezwa kichwani mwangu
-
13:36 - 13:40na mtu anayesema eti ananipenda.
-
13:40 - 13:43Wakati huu, labda unafikiria,
-
13:43 - 13:44"Hili ni jambo la kushangaza,"
-
13:44 - 13:48ama, "Kwa nini alikuwa mjinga hivi,"
-
13:48 - 13:54lakini muda huu wote, nimekuwa haswa nikiongea juu yako.
-
13:54 - 13:57Nakuhakikishia kuna watu kadhaa
-
13:57 - 13:59wanaonisikiliza saa hii
-
13:59 - 14:02ambao wananyanyaswa
-
14:02 - 14:04au ambao walinyanyaswa wakiwa watoto
-
14:04 - 14:08au walio wanyanyasaji wenyewe.
-
14:08 - 14:10unyanyasaji unaweza kuwa unamwathiri binti yako,
-
14:10 - 14:15dadako, rafiki yako wa karibu wakati huu.
-
14:15 - 14:18Niliweza kumaliza hadithi yangu wazimu ya mapenzi
-
14:18 - 14:21kwa kuvunja ukimya.
-
14:21 - 14:23Bado naendelea kuvunja ukimya leo.
-
14:23 - 14:27Ni njia yangu ya kusaidia waathirika wengine,
-
14:27 - 14:30na ni ombi langu la mwisho kwenu.
-
14:30 - 14:33Ongeeni kuhusu mliyosikia hapa.
-
14:33 - 14:36Unyanyasaji hushamiri tu katika ukimya.
-
14:36 - 14:40Una nguvu ya kumaliza unyanyasaji majumbani
-
14:40 - 14:44kwa kuongea kuhusu unyanyasaji.
-
14:44 - 14:47Sisi waathirika tunahitaji kila mtu.
-
14:47 - 14:51Tunawahitaji nyote kuelewa
-
14:51 - 14:55siri za unyanyasaji majumbani.
-
14:55 - 14:58Mulikieni mwanga unyanyasaji kwa kuuongelea
-
14:58 - 15:00mkiwa na watoto wenu, wafanyakazi wenzenu,
-
15:00 - 15:02marafiki zenu na familia.
-
15:02 - 15:05Ongeleeni waliosalimika kama watu wema na wanaopendeka
-
15:05 - 15:08walio na maisha kamili kwenye siku za usoni
-
15:08 - 15:11Eleweni ishara za mapema za tuhuma
-
15:11 - 15:14na muingilie kati kistadi
-
15:14 - 15:18malizeni na muonyeshe waathirika njia safi ya kuiepuka.
-
15:18 - 15:22Pamoja tunaweza kufanya vitanda vyetu,
-
15:22 - 15:26meza zetu za mlo na familia zetu
-
15:26 - 15:29mahali pa amani zinavyopaswa kuwa
-
15:29 - 15:31Asanteni.
-
15:31 - 15:39(Mahali)
- Title:
- Kwa nini waathirika wa unyanyasaji majumbani hawaondoki
- Speaker:
- Leslie Morgan Steiner
- Description:
-
Leslie Morgan Steiner alikuwa katika "penzi la wazimu" -- yaani, alimpenda sana mwanaume aliyemnyanyasa mara kwa mara na kumtishia maisha. Steiner anahadithia uhusiano wake, akisahihisha maoni potofu ya watu wengi kuhusiana na waathirika wa unyanyasaji wa majumbani , na kueleza vile wote tunavyoweza kumaliza kimya hicho. (Imerekodiwa katika TEDxRainier.)
- Video Language:
- English
- Team:
- closed TED
- Project:
- TEDTalks
- Duration:
- 15:59
Dimitra Papageorgiou edited Swahili subtitles for Why domestic violence victims don't leave | ||
Joachim Mangilima approved Swahili subtitles for Why domestic violence victims don't leave | ||
Joachim Mangilima accepted Swahili subtitles for Why domestic violence victims don't leave | ||
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for Why domestic violence victims don't leave | ||
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for Why domestic violence victims don't leave | ||
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for Why domestic violence victims don't leave | ||
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for Why domestic violence victims don't leave | ||
David Mvoi edited Swahili subtitles for Why domestic violence victims don't leave |