Return to Video

Fahad Al-Attiya: Nchi isiyokuwa na maji

  • 0:01 - 0:04
    Salaam alaikum
  • 0:04 - 0:05
    Karibuni Doha.
  • 0:05 - 0:09
    Mimi ndio muhusika wa usalama wa chakula nchi hii.
  • 0:09 - 0:11
    Hii ni kazi yangu kwa miaka miwili ijayo,
  • 0:11 - 0:13
    kutengeneza mpango mkuu,
  • 0:13 - 0:17
    na kwa miaka kumi ijayo kuupendekeza
  • 0:17 - 0:19
    na watu wengine wengi,
  • 0:19 - 0:23
    Lakini kwanza,nahitaji kukuhadithia,hii ni hadithi yangu,
  • 0:23 - 0:27
    kuhusu nchi hii mliyopo leo
  • 0:27 - 0:31
    Kwa uhakika,wengi wenu mmekula milo mitatu leo,
  • 0:31 - 0:35
    nahisi mtaendelea kula tena baada ya hii shughuli.
  • 0:35 - 0:40
    Tuangalie sasa ni vipi Quatar ilikuwa katika mwaka 1940?
  • 0:40 - 0:44
    Tulikuwa watu kama 11,000 tunaoishi hapa.
  • 0:44 - 0:51
    Hakukuwa na maji.Hakukuwa an nishati,mafuta,magari,vyote hivo havikuwepo.
  • 0:51 - 0:52
    Watu wengi walioishi hapa
  • 0:52 - 0:55
    waliishi vijiji vya pwani,kuvua,
  • 0:55 - 1:01
    au walikuwa watu wa kuhamahama ambao walitembea kutafuta maji.
  • 1:01 - 1:04
    Uzuri wote huu unauona haukuwepo.
  • 1:04 - 1:09
    Hakukuwa na jiji kama uonavyo leo Doha au Dubai au Abu Dhabi au Kuwait au Riyadh.
  • 1:09 - 1:12
    Haikuwa kwamba walishidwa kuendeleza miji.
  • 1:12 - 1:14
    Malighafi hazikuwepo kuweza kuendeleza.
  • 1:14 - 1:17
    Na unaweza kuona muda wa watu kuishi ulikuwa mfupi.
  • 1:17 - 1:19
    Watu wengi walifariki katika miaka 50
  • 1:19 - 1:23
    Twende sasa ukurasa wa pili:wakati wa mafuta.
  • 1:23 - 1:26
    1939,hapo ndipo mafuta yaligundulika.
  • 1:26 - 1:31
    Kwa bahati mbaya,hayakutumika vya kutosha kibiashara
  • 1:31 - 1:33
    mpaka vita ya pili ya dunia.
  • 1:33 - 1:35
    Ilifanya nini?
  • 1:35 - 1:38
    Ilibadilisha muonekano wa nchi,kama unavyoona na kushuhudia.
  • 1:38 - 1:42
    Na ilifanya wale watu wote waliokuwa wakizunguka jangwa..
  • 1:42 - 1:45
    kutafuta maji,kutafuta chakula,
  • 1:45 - 1:50
    wakijaribu kuwatunza wanyama wao..wakaepata maendeleo
  • 1:50 - 1:52
    Unaweza kuona ni ajabu,
  • 1:52 - 1:55
    lakini katika familia yangu tuna lafudhi tofauti.
  • 1:55 - 1:59
    Mama yangu ana asili ambayo ni tofauti na baba yangu,
  • 1:59 - 2:04
    wote tupo idadi inayofikia watu 300,000 tunaoishi katika nchi moja.
  • 2:04 - 2:08
    Kuna lafudhi kama tano au sita katika nchi hii ninapoongea mpaka sasa.
  • 2:08 - 2:12
    Kuna mtu husema"Kivipi?Inawezekanaje kutokea?
  • 2:12 - 2:14
    Kwa kuwa tuliishi tukiwa tumetawanyika.
  • 2:14 - 2:19
    Hatukuishi katika sehemu ya pamoja sana kwa sababu hatukuwa na malighafi.
  • 2:19 - 2:22
    Na malighafi zilipokuja,mafuta,
  • 2:22 - 2:26
    tukaanza kutengeneza teknolojia ya hali ya juu
  • 2:26 - 2:29
    na kuwaleta watu pamoja kwa sababu tulihitaji kukusanyika.
  • 2:29 - 2:32
    Watu walianza kufahamiana.
  • 2:32 - 2:36
    Na tukagundua kulikuwa na tofauti ya asili.
  • 2:36 - 2:38
    Hiyo ilikuwa ukurasa wa pili:wakati wa mafuta.
  • 2:38 - 2:41
    Tuangalie leo.
  • 2:41 - 2:45
    Inawezekana hiki ndicho wengi mnachojua kuhusu Doha.
  • 2:45 - 2:47
    Idadi ya watu ikoje leo?
  • 2:47 - 2:49
    ni watu milioni moja na laki saba.
  • 2:49 - 2:52
    Hiyo ni katika kipindi kisichozidi miaka 60.
  • 2:52 - 2:58
    Wastani wa ukuaji w uchumi wetu ni asilimia 15 katika miaka mitano iliyopita.
  • 2:58 - 3:00
    Tegemeo la kuishi limeongezeka hadi miaka 78.
  • 3:00 - 3:05
    Matumizi ya maji yameongezeka hadi lita 430.
  • 3:05 - 3:09
    Na hii ndo takwimu kubwa duniani.
  • 3:09 - 3:11
    Kutoka kutokuwa na maji
  • 3:11 - 3:16
    mpaka kutumia maji katika kiwango kikubwa duniani,kikubwa kuliko taifa lolote.
  • 3:16 - 3:20
    Sijui kama hii ni matokeo ya ukosefu wa maji.
  • 3:20 - 3:26
    Lakini ni kipi kinachonifurahisha kwenye hadithi niliyosimulia?
  • 3:26 - 3:29
    Kinachofurahisha ni kwamba tunaendelea kukua
  • 3:29 - 3:36
    asilimia 15 kila mwaka kwa miaka mitano bila maji.
  • 3:36 - 3:41
    Sasa hiyo ni historia.Haijawahi tokea kabla ya historia.
  • 3:41 - 3:45
    Miji yote iliharibika kwa sababu ya ukoseu wa maji.
  • 3:45 - 3:47
    Hii ni historia iliyotengenezwa katika eneo hili.
  • 3:47 - 3:49
    Sio miji tu ndo tunajenga,
  • 3:49 - 3:54
    lakini miji yenye maono na watu ambao wanatamani kuwa wanasayansi,madaktari.
  • 3:54 - 3:58
    Kujenga nyumba nzuri,kuwaleta wasanifu majengo,kutengeneza nyumba yangu.
  • 3:58 - 4:04
    Hawa watu wanaamini kwamba sehemu hii unaweza kuishi wakati ilipokuwa haiwezekani.
  • 4:04 - 4:06
    Lakini kwa sababu ya teknolojia.
  • 4:06 - 4:12
    Brazil ina kiasi cha mvua kwa milimita 1782 kwa mwaka.
  • 4:12 - 4:15
    Quatar ina 74,na tuna ukuaji kiasi hicho.
  • 4:15 - 4:17
    Swali ni kivipi?
  • 4:17 - 4:20
    Tunawezaje kuendela hivi?
  • 4:20 - 4:22
    Hatuna maji kabisa.
  • 4:22 - 4:29
    kwa sababu ya mashine kubwa ya kutoa chumvi kwenye maji.
  • 4:29 - 4:33
    Nishati ni kitu kikubwa hapa.Imebadilisha kila kitu.
  • 4:33 - 4:37
    Ni ambacho kinakitoa toka ardhini,tunaunguza tani na tani,
  • 4:37 - 4:40
    wengi wenu mmekitumia kuja Doha.
  • 4:40 - 4:43
    Hilo ni ziwa letu,kama unaweza kuona.
  • 4:43 - 4:45
    Huo ni mto wetu.
  • 4:45 - 4:51
    Hivyo ndivyo inavotokea mpaka kutumia na kufaidi maji.
  • 4:51 - 4:57
    Hii ni teknolojia nzuri sana ambayo eneo hili linayo,kuondoa chumvi katika maji
  • 4:57 - 4:59
    Je,hatari ni zipi?
  • 4:59 - 5:01
    Unaogopa sana?
  • 5:01 - 5:05
    Naweza kusema,ukiangalia ukweli kiujumla,
  • 5:05 - 5:08
    utagundua,unatakiwa kuwa na mashaka.
  • 5:08 - 5:10
    Kuna hitaji la kukua,ukuaji wa idadi ya watu.
  • 5:10 - 5:13
    Tumekuwa bilioni saba miezi michache iliyopita.
  • 5:13 - 5:17
    Na hiyo idadi pia inahitaji chakula.
  • 5:17 - 5:20
    Na kuna makisio kwamba tutakuwa bilioni tisa kwa mwaka 2050.
  • 5:20 - 5:23
    Kwa hiyo nchi ambayo haina maji
  • 5:23 - 5:26
    inakuwa na wasiwasi kipi kitachotokea nje ya mipaka yake.
  • 5:26 - 5:29
    Kuna kubadilisha ulaji.
  • 5:29 - 5:33
    Kwa kuongezeka katika hali ya juu ya maisha,
  • 5:33 - 5:35
    pia wanabadilisha ulaji wao.
  • 5:35 - 5:38
    Wanaanza kula kula sana nyama na vinginevyo.
  • 5:38 - 5:40
    Kwa upande mwingine,uzalishaji unaporomoka
  • 5:40 - 5:43
    kwa sababu ya mabadiliko ya tabia ya nchi na sababu nyinginezo.
  • 5:43 - 5:48
    Na inatakiwa mtu atambue lini hili tatizo litakuja kutokea.
  • 5:48 - 5:52
    Hii ni hali hapa Quatar,kwa wale wasiojua.
  • 5:52 - 5:55
    Tuna siku mbili tu za utunzaji maji.
  • 5:55 - 5:58
    Tunaagiza asilimia 90 ya chakula chetu,
  • 5:58 - 6:01
    na tunalima chini ya asilimia moja ya ardhi yetu.
  • 6:01 - 6:04
    Idadi ndogo ya wakulima ambayo tunayo
  • 6:04 - 6:07
    wameondolewa katika taratibu zao za ulimaji
  • 6:07 - 6:13
    kwa sababu ya soko huria na ushindani, n.k.
  • 6:13 - 6:16
    Kwa hiyo tunakumbana na hatari
  • 6:16 - 6:23
    Hatari hizi zimeathiri uendeleaji wa taifa hili
  • 6:23 - 6:26
    Swali ni kwamba,je kuna suluhisho?
  • 6:26 - 6:28
    Kuna ufumbuzi wa uhakika?
  • 6:28 - 6:30
    Kiukweli upo.
  • 6:30 - 6:34
    Hii inaonesha nyaraka zipatazo 1000 za kiufundi
  • 6:34 - 6:37
    ambazo tulikuwa tunafanyia kazi katika miaka miwili iliyopita.
  • 6:37 - 6:38
    Tuanze na maji.
  • 6:38 - 6:42
    Tunajua fika...niliwaonyesha mapema..kwamba tunahitaji hii nishati.
  • 6:42 - 6:45
    Kwa hiyo kama tutahitaji nishati,ni aina ipi?
  • 6:45 - 6:47
    nishati inayoisha?mafuta ghafi?
  • 6:47 - 6:50
    Au tutumie kitu kingine?
  • 6:50 - 6:53
    Tunayo faida ya kulinganisha kutumia aina nyingine ya nishati?
  • 6:53 - 6:57
    Nahisi wote mnafahamu kwamba tuna siku 300 za jua.
  • 6:57 - 7:03
    Kwa tunaweza tumia hii nishati kutupa maji tunayohitaji.
  • 7:03 - 7:08
    Kwa hiyo tunaweza kuweka 1800 megawati za umeme jua
  • 7:08 - 7:11
    kuzalisha milioni 3.5 za ujazo za maji.
  • 7:11 - 7:13
    Na hayo ni maji mengi.
  • 7:13 - 7:15
    Hayo maji yataenda kwa wakulima,
  • 7:15 - 7:17
    na wakulima wataweza kumwagilia mazao yao,
  • 7:17 - 7:21
    wataweza kuihudumia jamii kwa chakula
  • 7:21 - 7:23
    Lakini kwa ajili ya kuhimili upande huu
  • 7:23 - 7:27
    kwa sababu hii ni mipango,hii ni mipango tunayotekeleza
  • 7:27 - 7:29
    pia tunatakiwa tuendeleze upande mwingine
  • 7:29 - 7:35
    kusimamia mifumo,elimu ya hali ya juu,tafiti na maendeleo,
  • 7:35 - 7:40
    vinwanda,teknolojia,kutengeneza teknolojia kwa matumizi,na mwisho masoko.
  • 7:40 - 7:46
    Lakini kipi kinarahisha na kuwezesha,ni sheria,sera,utaratibu.
  • 7:46 - 7:48
    Bila hivi hatuwezi kufanya chochote.
  • 7:48 - 7:50
    Kwa hiyo hiki ndicho tunachopanga kufanya.
  • 7:50 - 7:53
    Ndani ya miaka miwili tunaweza kuwa tumekamilisha mipango hii
  • 7:53 - 7:55
    na kuongelea kuitekeleza.
  • 7:55 - 8:02
    Lengo letu kuu ni kuwa jiji la kimilenia,kama majiji mengine ya kimilenia
  • 8:02 - 8:09
    Instanbul,Rome,London,Paris,Damascus,Cairo.
  • 8:09 - 8:13
    Tuna miaka 60 tu,lakini tunataka kuishi milele
  • 8:13 - 8:18
    kama jiji,kuishi kwa amani.
  • 8:18 - 8:20
    Asante sana.
  • 8:20 - 8:24
    (makofi)
Title:
Fahad Al-Attiya: Nchi isiyokuwa na maji
Speaker:
Fahad Al-Attiya
Description:

Fikiri kuhusu nchi ambayo ina umeme mwingi sana -- mafuta na gesi,Mwanga wa jua,upepo(na pesa) --lakini imepungukiwa na huduma muhimu kwa ajili ya maisha: Maji. Mhandisi wa miundo mbinu Fahad Al-Attiya anaongelea njia zisizotegemewa ambazo taifa dogo la Mashariki ya Kati la Qatar linatumia kutengeneza mfumo wake wa usambazaji wa maji.

more » « less
Video Language:
English
Team:
closed TED
Project:
TEDTalks
Duration:
08:46
Joachim Mangilima approved Swahili subtitles for A country with no water
Joachim Mangilima accepted Swahili subtitles for A country with no water
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for A country with no water
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for A country with no water
Nelson Simfukwe added a translation

Swahili subtitles

Revisions